Kuzuia habari Waraka wa Maaskofu kuripotiwa kwenye Vyombo vya Habari ni uminywaji wa kiwango cha juu sana katika utoaji habari

Matangwa

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
641
1,061
Katika awamu Hii vyombo vya habari hasa TV, Magazeti, na Radio vimebanwa hasa kupitia BAHASHA za KAKI zinazotolewa na akina napenauye.

Ishu ipo hivyo, vyombo vya habari vilivyo vingi hapa nchini ni njaa kali, kwa hii serikali ya wala rushwa na mafisadi yanayokula kwa urefu wa kamba zao wanawaambia waandishi wa habari chagua moja au ULE na sisi ukubali uwe chawa wa mama au UFE njaa na watanzania wenzako kwa kutete maslahi mapana ya TAIFA.

Waandishi wa habari walio wengi na vyombo vya habari ving vimechagua kula mapochopocho ya mafisadi ya awamu ya sita kuwa sharti moja tu. Hakuna Kuisema vibaya serikali hii.

Ndio maana waziri wa Habari nape anakuwa na jeuri ya kuvipangia vyombo vya habari, habari gani iripotiwe na habari gani isiripotiwe kwenye vyombo vya habari.

Kwa hili la WARAKA WA MAASKOFU vyombo vya habari vimejidhalilisha sana.
 
Nape"Bichwa kubwa" amekuwa mara kadhaa akijinasibu mbele ya vyombo vya ndani na nje kuwa awamu ya sita inazingatia uhuru wa vyombo vya habari sio kama awamu ya tano,ambapo si kweli.

Jana TEC(Baraza la Maaskofu Katoliki Tz) limetoa waraka wake juu ya Mkataba wa hovyo wa Bandari, kama ilivyo ada na hii sio mara ya kwanza kufanya hivyo,ilitoa Waraka kipindi cha mwenda zake na awamu zote imefanya hivyo kama sehemu ya jukumu lake la kulinda rasilimali za nchi,mdau wa maendeleo nk

Jana chombo pekee kilichoripoti waraka huo ni JF kwenye mitandao yao yote wamefanya hivyo.Heko kwa JF muishi sana.Hakuna ITV,CLOUDS,WASAFI,EFM nk

Millard Ayo alipost lakini alifuta punde baada ya kupokea simu toka mamlaka za juu "Bichwa kubwa".

Sasa ni hivi asomaye na afahamu kuwa Waraka huo wa Maaskofu utasomwa kwenye misa zote hapo kesho 20/08/2023 mbele ya waumini wao juu ya mkataba wa kimangungo wa serikali ya Samia na "Emirate of Dubai"

Serikali ya Samia acheni kibri wananchi hatuutaki huo mkataba wa kimangungo mnafosi kuwapa "Emirate of Dubai" wamewapa nini?

Lolote utakalofanya juu ya bandari zetu hauna baraka la Maaskofu(Watanzania) usiseme hukuambiwa,Sikio la kufa halisikii dawa.

Roma Locusta,Causa Finita.(Rome has spoken,the cause is closed!)
View attachment 2722558= View attachment 2722560
 

Attachments

  • Screenshot_20230819_210214_Instagram.jpg
    Screenshot_20230819_210214_Instagram.jpg
    52 KB · Views: 4
  • IMG-20230819-WA0007.jpg
    IMG-20230819-WA0007.jpg
    79 KB · Views: 4
Millardayo alipost na kufuta nikajua atakuwa alipokea maelekezo🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom