JamiiForums ni kiboko, imenipa kazi mwenzenu

Duh! 400,000 ukikatwa kodi, kisha NSSF wakachukua chao unabakiwa na nini?

Walimu na wauguzi wanaishije? Acheni kujifanya sio watanzania, huu ni ubwege. Ni kweli huo mshahara si mkubwa lkn si kweli kwamba hauwezi kuishi. Sasa hivi hana hata senti anaishije? Umbea wa kiume hauna hata mashiko. Kwa bajeti hiyo mimi enzi zangu mbona ningemiliki hata nyumba ndogo 2. Tupunguze mashauz, huyu anayeuliza hana mtoto wala mjukuu, ni yeye, sehemu zake za siri na tumbo, atashindwa vipi kuishi kama sio kutaka kuleta ujuaji hapa?

WEWE BWANA MDOGO, KAANZE KAZI WA NOTI NDEFU UTAKUKUTA HUKO HUKO UKIWA KAZINI. NDIO WAKATI WAKO WA KUJIFUNZA MAISHA NA BAJETI
 
Habari wakuu!,mi ni graduate-2011 na nimekuwa nikifuatilia matangazo ya kazi hapa JF na kutuma application zangu, nimeitwa kwenye interview 5 na sasa nimeitwa kufanya kazi kwenye kampuni 3 tofauti, zote nimepewa mikataba nimeisoma lkn sijaisaini bado, tatizo ni malipo. Yani ina-arange 380,000 mpaka 400,000. Je, kwa maisha ya Dar zinaweza kukidhi? Mi sina uzoefu na jiji hili nimekuja tu kutafuta kazi na nipo kwa ndugu maana yake nikipata kikazi hicho nitalazimika kuanza maisha yangu.

usijali mkubwa hicho kianzio si kibaya japo ni kiduchu, we tafuta uzoefu kwanza au umesahau mwenye nacho anaongezewa asiye nacho hata kile kidogo ananyang'anywa?umenisoma?
 
nenda tu mkuu hata mimi wakati namaliza chuo nilianzia huawei nikawa napewa 400000 kama miezi sita nikajenga ka cv baadae nakaitwa TTCL nikalipwa mara 4 ya ule for the same job mwanzo huwa ni mgumu ndugu
 
Wewe huna kazi umepata kazi nenda kafanye kazi ukisubiria ya mshahara mkubwa utajuuuta. Huo mshahara mkubwa utakukuta hukohuko
 
Mkuu, ni kupangilia tu, ingawaje huo mshahara sio mkubwa, lakini huwezi ku-suffer on ur way on getting perfect job for u. Binafsi, natumia about TZS 150,000/= kwa mwezi na napiga menu ya maana kabisa kuliko anayetumia 300,000/= kwa mwezi.
da! mkuu wewe ni noma, hahahahaha, nimependa summarry yako.
 
Nenda kapige kazi na upime upepo.... Maana TZ hii na mambo ya poshooooooooooooooooo hasa kwa kampuni ambazo serikali inamiliki hisa mambo yanaweza kuwa mazuri na tunakisikia baada ya mwaka umenunua gari, after 2yrs unanyumba nzuri etc. Huu ni mfano lakini ni ukweli. Nakumbuka nilipoanza kazi some yrs back rafiki yangu nilikuwa namzidi salary kama 3 times lakini baada ya 2 yrs akawa na gari, 3 yrs sasa ana nyumba kali Tabata huku mimi nikitamba na slip yenye salary kubwa bila extra income. Kumbuka sio kwamba mimi na matumizi ya anasa... NO ila toafuti ni:
  1. Kwasasa yeye akinusa tu kweye kikao job, bahasha ya laki moja
  2. Akinusa tu weekend job, ana Laki Mbili
  3. Akisafiri siku kumi tu nje ya nchi anaweza kurudi na balance hadi 10,000 US na zaidi ukizingatia sometimes anapewa allowance ya safari na huko akifika wenyeji wanagharimia kila kitu hata pesa hata ukifanyiwa full massage...... Na hapa najua numewagusa wengi.
Hiyo ndio TZzzzzzzzziiiiiiiiiii Si swala la niko kampuni fulani yenye kujulikana sana na slip nzuri wakati mtaani maisha duni.
 
Habari wakuu!,mi ni graduate-2011 na nimekuwa nikifuatilia matangazo ya kazi hapa JF na kutuma application zangu, nimeitwa kwenye interview 5 na sasa nimeitwa kufanya kazi kwenye kampuni 3 tofauti, zote nimepewa mikataba nimeisoma lkn sijaisaini bado, tatizo ni malipo. Yani ina-arange 380,000 mpaka 400,000. Je, kwa maisha ya Dar zinaweza kukidhi? Mi sina uzoefu na jiji hili nimekuja tu kutafuta kazi na nipo kwa ndugu maana yake nikipata kikazi hicho nitalazimika kuanza maisha yangu.

Huwa ninafurahi sana ninapokutana na vijana wanaoanza kazi. Three yrs back nilikua kama wewe man,napokea 450,000 net ila nilikua naishi kwa wazee. Akili ya kwamba ni save nijipange sikua nayo so nikawa nazitumbua tu. Nikipokea kamshahara ni pamba,babes na parties tu, ikifika katikati ya mwezi naomba niwekewe mafuta kwenye gari( ya mzee!). Those were the good times man, no care in the world. Akili za ku-budget zilikuja nipohama home, so from where I stand kitendo cha kwamba inakubidi uhame ukipata kazi kichukulie kama opportunity. Back to the subject. Hiyo hela inatosha, na faida nyingine ambayo unapata ni kwamba itakufunza namna ya ku-budget. im not going to give u a break down on how to spend the money, just use it wisely. Im going to tell u things ambazo unatakiwa ufanye/ usifanye:

1)Usichukue mkopo benki. Uwe wa gari, biashara au kitu nyingine. Loans zitakurudisha nyuma na ku-reduce net worth yako. Hapo ulipo unaweza ukawa tayari na HSLB loans. Gari ndio sahau kwa sasa coz sio asset ni expense.

2) Invest hela. Usianze biashara/usinunue shares or stocks. Biashara nyingi zitahitaji capital na muda, vitu hivyo huna kwa sasa. Na zina risk, and u cant afford taking risks(this applies to shares/stocks/bonds etc). Fungua investment a/c au fixed deposit a/c , ingiza hata 100,000 kwa mwezi kwa kuanzia( Ukijibana u can do this). Baada ya kuongeza kipato weka hadi kilo 3 kwa mwezi. I presume sasa utakua na umri kama wa miaka 22-24. Ukipata bank wanayotoa say 8% compound interest kwa mwaka(eg FNB), baada ya miaka 6 unakua na kama mil 150- mil 200 (kilo 2-3 kwa mwezi). Ni very few self-made ppl wana hiyo amnt by the time they are 30 hapa bongo. Masuala ya biashara yaanze baadae sana, utakapokua na uwezo wa ku-sustain loss ya millions of money.

3) I have a feeling kwamba wewe ni mwanaume sio mwanamke (from the fact kwamba u'll have to move out ukipata kazi). Relationships can be expensive in terms of money na muda, take it from me. So dont play around, u cant be a player without spending. Find urself a nice girl na umpige somo wewe ni nani na unaishi vp so awe anajua kabisa yupo na mtu wa aina gani. Sio unakua na demu ambaye baada ya miezi 6 kazini anaanza kukuuliza gari unanunua lini, utashangazwa!!. Either utachapiwa au utaanza kuishi life ambayo sio yako ili kumridhisha, either way u r f***ed. And yeah, use protection, if u r wondering whether 400,000 itakutosha ukiwa peke yako, try to imagine ukiwa na two more ppl to take care of.Kama wewe ni mwanamke, good for u; ila uwe makini na viserengeti boys vinavyochipukia and, again, use protection.

4)Usiridhike na salary ya 400,000. This means two things. Either upige mzigo wa kutosha uwe promoted hapohapo au upige mzigo wa kutosha huku unaangalia sehemu zingine. Note kwamba, kupiga mzigo wa kutosha is not an option. Maana yake ni kamba, hata kama hujaridhika na mshahara, lazima ufanye kazi kwa bidii, akili, heshima, na taadhima. Coz ukiripua, ripua halafu ukajikuta upo hapo mwaka mzima, bottomline ni kwamba u've wasted one year of your life. Kivipi? Baadae itakubidi ufanye vitu hivi: ukiandika CV useme kama ulifanya kazi hapo ->wapigiwe simu ->watoe bad reference ->ukose kazi.Au usiseme kama ulifanya kazi hapo, which means umepoteza mwaka hapo. Moreover, jiendeleze ukishajipanga na kuongeza pato.

5) Matumizi yako yasipande kadri salary inavyoongezeka. This may hard to do as we are always tempted kuongeza matumizi mshahara ukipanda. TRY!

6)Ukisha-invest for around two/three yrs nunua ardhi, trends ya ardhi bongo ina boom vibaya mno, na taxes ni very minimal so the earlie the better.

7) Hii ya mwisho, ipo arguable. In my opinion, usioe mapema. Give yourself atleast 6-7yrs from now. To me marriage means more responsibilities, emotionally, financially, etc. To others, marriage means shared responsibilities. I'm not married, so I wouldnt know about shared responsibilities. It's open for a discussion.


Muda unabana, I would have added some more. I wish JF tungekua na investments section( au ipo sijui). Ukifanya nilivyokushauri, find me 5 yrs from now( when u have alost 100M in ur savings) tuongee namna ya kuiongeza.

P.S:
1)Right now, net salary yangu imekua 5 TIMES!! na still ninaishi on less than TZS. 500,000. Tokea nilipogundua the value of money and the power of investing, nimekua an aggressive investor. Hata buku ninaiangalia twice kabla sijaitumia.

2) Ni kweli bongo life imekua ngumu, hasa ukizingatia kwamba value ya degree na value ya shillingi zote zinaporomoka but one thing we have ambayo inabidi tuichukulie advantage ni low taxes na urahisi wa kuanzisha na kuendesha biashara( faida aside! hehe). Low property taxes, low investment taxes, low real estate taxes, etc.

BON CHANCE!!
 
Sikiliza mkuu,

380,000/= na 400,000/= hakuna tofauti yoyote. Maana yangu ni kwamba, kama range ya mshahara ndio hiyo basi hapo usiangalie kigezo cha mshahara, bali angali ni kazi gani ambayo itakuuza vizuri hapo baadae. You get wht I mean?

Assume kampuni A ni benki ambayo wamekupa nafasi ya Teller na salary offer ya sh. 400,000/= na company B, nayo ni reputable company na wameku-offer post ya Marketing Officer kwa mshahara wa sh. 370,000/= ! Kwa ushauri wangu, accept offer ya marketing officer kwa 370,000/= coz' marketing officer inauzika kuliko teller.

Kama salary inatosha au haitoshi, ni kwamba huo mshahara ni mdogo lakini usiache coz' hapa town sio kwenu na umekuja kutafuta. Tatizo lenu watu kama nyinyi (yaani mliokuja Dar karibuni) mna ujinga wa kuangalia washikaji zenu wanakaa wapi badala ya kuangalia una salary kiasi gani. Utakuta mtu kamaliza UDSM, washikaji zake wanaishi Mwenge/Sinza/Ubungo (nyumbani kwao) nanyi mnataka kupanga maeneo hayo. Utaumia broda!

Mahali kama Kwa Azizi Ally, unapata chumba kwa sh.30, 000/- tena kizuri tu kwa mtafuta maisha. Mahali penyewe karibu na town, una uhakika wa kutumia 600/- tu kwa nauli; sehemu za kula bata hadi uzisumbukie..... unadhani basic ya 380,000/= haiwezi kukusogeza wakati unatafuta better post?! it can broda!

Akili za mbayumbayu, changanya na za kwako!!!

tafuta kazi ukiwa kazini...
 
Hongera kwa kupata kazi, hiyo rate unayoisema inatosha sana labda kama unaishi kwa hisia na kuiga wenzako wenye sources tofauti (ikiwemo na rushwa)

Binafsi, ninapata 350,000/= na katika hali ya kawaida inatosha maisha kiaina, chumba ninalipa 50,000/= (gharama zote za umeme, maji na usafi vimehusishwa) kwa kiwango hicho nina imani kabisa unaweza kujitegemea
 
..Fungua investment a/c au fixed deposit a/c , ingiza hata 100,000 kwa mwezi kwa kuanzia( Ukijibana u can do this). Baada ya kuongeza kipato weka hadi kilo 3 kwa mwezi. I presume sasa utakua na umri kama wa miaka 22-24. Ukipata bank wanayotoa say 8% compound interest kwa mwaka(eg FNB), baada ya miaka 6 unakua na kama mil 150- mil 200 (kilo 2-3 kwa mwezi). Ni very few self-made ppl wana hiyo amnt by the time they are 30 hapa bongo. Masuala ya biashara yaanze baadae sana, utakapokua na uwezo wa ku-sustain loss ya millions of money...

Anonimuz, ushauri wako ni mzuri mno...hata mimi nimejifunza kitu hapa.

Hata hivyo hapo kwenye investment/deposit account inabidi upaangalie tena. Kwa maoni yangu ni too optimistic/unrealistic hasa ukizingatia interest rate ya mabank yetu (umesema 8%). Hata kama ukiinvest sasa kwenye fixed deposit TZS 21,600,000 (=6x12x300,000), sioni ni vipi unaweza kuwa na TZS 150m baada ya miaka sita! (kwa compounding niijuayo mimi katika miaka hiyo sita hawezi kuwa na zaidi ya tzs 35m, labda kama rate, muda, deposits nk zibadilike kwa kwenda juu).
 
Habari wakuu!,mi ni graduate-2011 na nimekuwa nikifuatilia matangazo ya kazi hapa JF na kutuma application zangu, nimeitwa kwenye interview 5 na sasa nimeitwa kufanya kazi kwenye kampuni 3 tofauti, zote nimepewa mikataba nimeisoma lkn sijaisaini bado, tatizo ni malipo. Yani ina-arange 380,000 mpaka 400,000. Je, kwa maisha ya Dar zinaweza kukidhi? Mi sina uzoefu na jiji hili nimekuja tu kutafuta kazi na nipo kwa ndugu maana yake nikipata kikazi hicho nitalazimika kuanza maisha yangu.
Kwa kuanzia siyo mbaya.
 
Habari wakuu!,mi ni graduate-2011 na nimekuwa nikifuatilia matangazo ya kazi hapa JF na kutuma application zangu, nimeitwa kwenye interview 5 na sasa nimeitwa kufanya kazi kwenye kampuni 3 tofauti, zote nimepewa mikataba nimeisoma lkn sijaisaini bado, tatizo ni malipo. Yani ina-arange 380,000 mpaka 400,000. Je, kwa maisha ya Dar zinaweza kukidhi? Mi sina uzoefu na jiji hili nimekuja tu kutafuta kazi na nipo kwa ndugu maana yake nikipata kikazi hicho nitalazimika kuanza maisha yangu.
Kama hapo pana mkataba wowote wa kufanya kazi serikalini hata usi-arange appointment na mtu ili akupe ushauri wee saini nenda kafanye kazi, nasikia kule kuna mambo mengi kwa mfano sasa hivi kuna kuazimisha miaka hamsini ya uhuru hili halipiti bila kusainishana mihela kibao tuu, baada ya hapo utasikia kuna kamati ya kuchunguza matumizi ya hizo pesa pia zote hizo ni deal. Kuna jamaa anadai katika ofisi yao yeye hata kama serikali ikisitisha mishahara haachi kazi
 
msahahara wako wa kwanza nusu peleka kanisani
nusu lete jf ni pm tukutane nitume hqs
 
Anza kazi mara moja. Mi nilianza na mshahara wa 260000TZS, lakini nilidumu nao kwa wiki 2 nikapata kazi nyingine nikapanda hadi 391000TZS nao nikacheza nao kwa muda wa miezi 2 nipiga chini baada ya kupata offer zaidi ya 5 kutoka sehemu tofauti tofauti zenye mshahara minono! Nikachagua kazi ninayoipenda with reasonable salary, basi maisha yanasonga with challenges za hapa na pale.

Kwa hiyo ushauri wangu, anza kazi huku ukijua kuna wenzako hawana hata huo mshahara, lakini pia ukijua kuwa kuna jamaa zako pengine ulikuwa unawazidi marks darasani, lakini leo hii wanakula pesa ya kutosha zaidi yako.

Hiyo isikunyime usingizi, kwani ukianza na slope ya 90 degree tegemea kushuka muda wowote, nenda taratibu utajikuta uko nao sawa pengine utakuwa stable zaidi kutokana na hizi chellenges unazokumbana/utakazokumbana nazo.
 
Anonimuz, ushauri wako ni mzuri mno...hata mimi nimejifunza kitu hapa.

Hata hivyo hapo kwenye investment/deposit account inabidi upaangalie tena. Kwa maoni yangu ni too optimistic/unrealistic hasa ukizingatia interest rate ya mabank yetu (umesema 8%). Hata kama ukiinvest sasa kwenye fixed deposit TZS 21,600,000 (=6x12x300,000), sioni ni vipi unaweza kuwa na TZS 150m baada ya miaka sita!

I know it sounds too optimistic SMU, but it aint.
1)Hiyo uliyopiga 6*12*300,000 ni umezidisha tu 300,000 kwa miaka sita, haujaweka interest .

2)Saving a/c ya kawaida huwezi kupata 8% interest rate. That's why nikasema fungua fixed deposit a/c au investment a/c.

3) Interest rate ninayoongelea hapa ni compound interest na siyo simple interest

4) Bank nyingi huwa wana-compound monthly, which is even better.

5) Formula rahisi ya kutafuta pato kwa kutumia compound interest ni P(1+r/n)^ nt (for one-time investment)

6) Ukitaka kuelewa zaidi haya mambo cheki kitabu nime-attach hapa, a good read indeed. Soma chapter ya kwanza tu, utakua hata ukiiona fisi (TZS. 50) imezubaa zubaa unaipeleka benki, im telling u

Au ngoja nikurahisishie: 300,000 monthly, for 6 yrs at 8% compound interest, compounded annually

6x3.6M + 5x3.6Mx1.08+ 4x3.6Mx1.08^2 + 3x3.6mx1.08^3 + 2x3.6Mx1.08^4+ 1x3.6mx1.08^5 = aprox. 90M
If u compound it monthly, inaenda to 100m+ coz u deposit monthly too!!

BON CHANCE!!
 

Attachments

  • Multiple_Streams_of_Income__How_to_Generate_a_Lifetime_of_Unlimited_Wealth___Second_Edition.pdf
    5.5 MB · Views: 6,401
Hongera zako Mkuu. Hiyo ni pesa ndogo sana inabidi ujinyime kwenye baadhi ya mambo ili uweze kumudu gharama za maisha ambazo zimepanda sana.

Kila la heri.
hiyo pesa ni ndogo lablda kama ni serikalini

ni chini ya $200
 
Kama wewe ni graduate wa 2011 na uko mjini kutafuta kazi, ndo umepata kazi sasa.Wapo ma graduate toka 2008 hawajapata kazi, sasa basi; ukitaka kupata jibu lako " ULIOMBA KAZI UKAPATA KAZI, SASA ACHA KAZI UONE KAZI:A S 465:"
 
Kapige hiyo kazi, kama hujarithika endeleea kutafuta kazi wakati unafanya kazi


lL Gambino.
 
Back
Top Bottom