JamiiForums ni kiboko, imenipa kazi mwenzenu

Tiamaji

Member
Oct 17, 2011
33
32
Habari wakuu!,mi ni graduate-2011 na nimekuwa nikifuatilia matangazo ya kazi hapa JF na kutuma application zangu, nimeitwa kwenye interview 5 na sasa nimeitwa kufanya kazi kwenye kampuni 3 tofauti, zote nimepewa mikataba nimeisoma lkn sijaisaini bado, tatizo ni malipo. Yani ina-arange 380,000 mpaka 400,000. Je, kwa maisha ya Dar zinaweza kukidhi? Mi sina uzoefu na jiji hili nimekuja tu kutafuta kazi na nipo kwa ndugu maana yake nikipata kikazi hicho nitalazimika kuanza maisha yangu.
 
Hongera kwa kupata kazi sio mbaya ukanzb na hapo then baadaye utapima kama itakufaa au la kwani kilamtu anademand zake.
 
Hongera zako Mkuu. Hiyo ni pesa ndogo sana inabidi ujinyime kwenye baadhi ya mambo ili uweze kumudu gharama za maisha ambazo zimepanda sana.

Kila la heri.
 
Sikiliza mkuu,

380,000/= na 400,000/= hakuna tofauti yoyote. Maana yangu ni kwamba, kama range ya mshahara ndio hiyo basi hapo usiangalie kigezo cha mshahara, bali angali ni kazi gani ambayo itakuuza vizuri hapo baadae. You get wht I mean?

Assume kampuni A ni benki ambayo wamekupa nafasi ya Teller na salary offer ya sh. 400,000/= na company B, nayo ni reputable company na wameku-offer post ya Marketing Officer kwa mshahara wa sh. 370,000/= ! Kwa ushauri wangu, accept offer ya marketing officer kwa 370,000/= coz' marketing officer inauzika kuliko teller.

Kama salary inatosha au haitoshi, ni kwamba huo mshahara ni mdogo lakini usiache coz' hapa town sio kwenu na umekuja kutafuta. Tatizo lenu watu kama nyinyi (yaani mliokuja Dar karibuni) mna ujinga wa kuangalia washikaji zenu wanakaa wapi badala ya kuangalia una salary kiasi gani. Utakuta mtu kamaliza UDSM, washikaji zake wanaishi Mwenge/Sinza/Ubungo (nyumbani kwao) nanyi mnataka kupanga maeneo hayo. Utaumia broda!

Mahali kama Kwa Azizi Ally, unapata chumba kwa sh.30, 000/- tena kizuri tu kwa mtafuta maisha. Mahali penyewe karibu na town, una uhakika wa kutumia 600/- tu kwa nauli; sehemu za kula bata hadi uzisumbukie..... unadhani basic ya 380,000/= haiwezi kukusogeza wakati unatafuta better post?! it can broda!

Akili za mbayumbayu, changanya na za kwako!!!
 
komaa mkuu chukua hiyo ajira, kuna wafanyakazi wa serikali wanalipwa 150,000. Hapo hapo wanakatwa NSSF na PAYE. Na maisha yao bado yanaendelea kusonga. Ukiwa kazini ni rahisi kupata kazi nyingine
 
Habari wakuu!,mi ni graduate-2011 na nimekuwa nikifuatilia matangazo ya kazi hapa JF na kutuma application zangu, nimeitwa kwenye interview 5 na sasa nimeitwa kufanya kazi kwenye kampuni 3 tofauti, zote nimepewa mikataba nimeisoma lkn sijaisaini bado, tatizo ni malipo. Yani ina-arange 380,000 mpaka 400,000. Je, kwa maisha ya Dar zinaweza kukidhi? Mi sina uzoefu na jiji hili nimekuja tu kutafuta kazi na nipo kwa ndugu maana yake nikipata kikazi hicho nitalazimika kuanza maisha yangu.

Hongera sana, we nenda kachape mzigo, mshahara mzuri unaendana na uzoefu na utendaji mzuri wa kazi, bila kusahau ujuzi na elimu. with time utapata kazi nzuri zaidi
 
Duh! 400,000 ukikatwa kodi, kisha NSSF wakachukua chao unabakiwa na nini?

Mkuu, ni kupangilia tu, ingawaje huo mshahara sio mkubwa, lakini huwezi ku-suffer on ur way on getting perfect job for u. Binafsi, natumia about TZS 150,000/= kwa mwezi na napiga menu ya maana kabisa kuliko anayetumia 300,000/= kwa mwezi.

Here is how I do (Huwa nafanya yafuatayo mara nipatapo salary yangu):

- Nanunua mchele 15 kg@ 1,500/- = TZS 22,500/-
- Nampa mshikaji wa bucha sh. 28,000/ kwa mwezi ~hapo ni nyama 0.5kg (stake) na 0.5kg(maini). Hizo ni kwa wiki, ambapo natumia 7,000/- kwa wiki na 28,000/- kwa mwezi. Nilichofanya baada ya kuhamia hapa kitaa, nikajenga mazoea na mshikaji wa bucha hadi akawa rafiki yangu na hivyo, ninapomwachia 28,000/- nina uhakika wa kwenda kuchukua nyama kila wiki bila longolongo!
- Watu wa mwambao bila nazi, msosi hauendi...na siku kuna nazi(ya tui) za bakhresa, nina shida gani!!!! Natumia pakti mbili kwa wiki @600, therefore nanunua za mwezi mzima kwa sh. 4,800/-
- Huwa nanunua mafuta ya kula tena yale yale ambayo maskini kama mimi wanayaogopa....ya alizeti kwa sh.18,000/ (lita 3) ambayo nayatumia si chini ya miezi 4 (means kwa mwezi na-spend sh 4,500/-)
- Nanunua in advance sukari 2kg @2000= TZS 4,000/- .
- Nanunua Soya 3 packets @2,000~~~~ TZS 6,000/- kwa mwezi (huwa situmii kabisa majani ya chai)
- Maharage 2kg@ 1,800/= (3,600/- kwa mwezi).... nyama peke yake huwa haipandi kwahiyo lazima nipate maharage kidogo.
- Tambi kwa ajili ya weekend 8pc @ 1000= 8,000/-
- Mafuta ya taa 6lts @ 2000 = 12,000
- Njegele 1,200/- kila weekend...napenda sana hii ki2 na tambi!= 4,800/- kwa mwezi

22,500 + 28,000+4800+4500+4000+6000+3600+8000+12,000+4,800= 98,200/=

Hapo unakuta natumia kama laki tu, lakini napata vitu vyote muhimu for my favorite meal !! Addition point ni kwamba, ninapoenda job, huwa sinywi chai asubuhi, BALI HUWA NAKULA MSOSI!!!

Nimeeleweka?

Sinywi chai; NAPIGA MSOSI! Always, ingawaje sikai mbali na town, huwa naamka saa 11 alfajiri na kuanza kupika WALIIIIIIIII......! Nikishapiga menu yangu ya adabu asubuhi, wala sihangaiki lunch time; by the way, nikishatulia kwenye kiti changu huwa sipendi usumbufu!

Eti unakuta mtoto wa kiume anasema "eti siwezi kula asubuhi.....!" mtu ukiwa na hayo mawazo then be prepared kuolewa mambo yatakapobana! Nasikitika sana kwamba hamna daladala ambazo naweza kulipa in advance, otherwise, I'd do it....sipendi stress kwenye maisha, hususani kwa vitu vya kipuuzi kama basic needs!

Try it, utakuja gundua maisha is very easy sema hatuyajulii tu!!!
 
Aisee usiache hiyo kazi, kuna watu huku JF na hata mitaani tu huwa wanataka hata kazi za kujitolea siku nenda rudi, mchana na usiku, ulipopata nenda, angalia kwenye incentives na kazi ambayo itaongeza CV yako kuwa bora zaidi, ni rahis kupata kazi nyingine ukiwa kazini, kuliko ukiwa home umekaa tu, michongo huwa yaenda makazini kaka. For the time being ikubli hiyo kazi yle searching for anaza better job.

Mwenyewe niandikae hapa nina degree na niliajiriwa mwaka jana August na nalipwa 380,000/=tshs per month na its a year na miez minne sasa toka nimeanza hii kazi, though naendelea tafuta kwingine, ila kwa kujinyima naweza fanya starehe kidogo pale napojiskia, na maendeleo yangu kidogo, pia wala sikai muhofia mtu au jigonga kwa mtu kwa kuomba hela, coz i can sustain my self with my needs, just go on and take the job suitabo for yu, utapata connections za kukuwezesha pata better job there.

ALL THE BEST
 
Kama unaona mshahara hautoshi endelea kutafta utakapo lipwa vizur (tanzania ajira zpo za kutosha)
 
Habari wakuu!,mi ni graduate-2011 na nimekuwa nikifuatilia matangazo ya kazi hapa JF na kutuma application zangu, nimeitwa kwenye interview 5 na sasa nimeitwa kufanya kazi kwenye kampuni 3 tofauti, zote nimepewa mikataba nimeisoma lkn sijaisaini bado, tatizo ni malipo. Yani ina-arange 380,000 mpaka 400,000. Je, kwa maisha ya Dar zinaweza kukidhi? Mi sina uzoefu na jiji hili nimekuja tu kutafuta kazi na nipo kwa ndugu maana yake nikipata kikazi hicho nitalazimika kuanza maisha yangu.
Hizi 380k/400k ni kabla ya makato (gross) au baada (net)? Kwa vyovyote vile kama upo peke yako (huna wategemezi) inaweza kuku sustain lakini itakubidi ujibane sana na kama ukiweza jaribu kutafuta vyanzo vingine vya mapato (vya halali). Lakini la muhimu zaidi ni wewe kufanya kazi ili upate uzoefu kwanza ambao baadae utakupa 'jeuri' ya kuchagua mshahara unaoutaka!
 
Hongera Dogo Ingia mzigoni, Mara nyingi kazi nyingine huwezi kujua maslahi ya Ziada mpaka uingie Mzigoni. Nakumbuka kazi yangu ya kwanza kufanya Maslahi ya Ziada yalikuwa makubwa kuliko Mshahara. Ingia mzigoni mambo mengine uko uko.
 
Safari moja huanzisha nyingi, grab it then open your eyes ukitafuta nyingine, put in mind kuwa unajenga CV pia. Close your eyes grab one of it
 
Habari wakuu!,mi ni graduate-2011 na nimekuwa nikifuatilia matangazo ya kazi hapa JF na kutuma application zangu, nimeitwa kwenye interview 5 na sasa nimeitwa kufanya kazi kwenye kampuni 3 tofauti, zote nimepewa mikataba nimeisoma lkn sijaisaini bado, tatizo ni malipo. Yani ina-arange 380,000 mpaka 400,000. Je, kwa maisha ya Dar zinaweza kukidhi? Mi sina uzoefu na jiji hili nimekuja tu kutafuta kazi na nipo kwa ndugu maana yake nikipata kikazi hicho nitalazimika kuanza maisha yangu.

Kuanza maisha unaanza siku uliyozaliwa. Hilo suala lako la ki-fukunyuku kuwa 380,000 zinatosha au lah, nenda kawaulize walimu wa shule za serikali. Wao wanalipwa 149,000/= wana watoto wanasoma na nyumba ndogo wanazihudumia pia. Huna adabu!
 
Mkuu naomba uelewe kuwa ck zote salary humtosha yule anayejua nini afanye kwanza, kipi akipe kipaumbele na wala usitegemee kuwa na mshahara mkubwa ndo utaweza life la DAR. Kwani wangapi wana salary kubwa but maisha yao yako ovyo.

Mimi nakushauri uanze kazi na hiyo salary inatosha sana kama utajua kipi ni kipaumbele chako na ukatekeleza kimoja baada ya kingine. Usikurupuke na maisha mambo taratibu na kuakikisha unaishi kwa amani.
 
Ninakushauri kabla ya ku sign hiyo kandarasi ya barua ulizopata ufanye analysis ya waajiri hao.

Kwanza usome kwa makini terms za hizo contracts za hao waajiri wote ili uweze kuangalia mambo muhimu kama vile benefits mbalimbali ambazo waajiri hao watazitoa kama vile medical benefits, safari za kutoka nje ya kituo chako cha kazi na kama wana utaratibu wa kulipa per diem system na benefits zinginezo.

Ninachotaka ku communicate hapa ni kwamba si kuangalia tu ile package peke yake bali usome hizo offer letters ili uone ni packages zipi zingine zinatolewa na hao waajiri ndipo ufanye maamuzi ya muajiri gani utakaye sign kandarasi yake.

Otherwise ninakupongeza sana kwa hatua hiyo ya kupata kazi zaidi sana nafasi za kazi zinazotangazwa kupitia JF.
 
Back
Top Bottom