Nilimpotezea huyu mwanamke kwa hii kauli ya kishenzi

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,604
Niende moja kwa moja kwenye mada,

July 2015 asubuhi ya saa nne nikiwa nimetoka kwenye dawati langu naelekea washroom, nilikutana na binti mmoja kwenye corridor akiwa na bahasha ya kaki mkononi. Yeye ndo alianza kunisalimia na baada ya kumsalimia akaniambia "Bro samahani nimekuja kwenye interview ya legal officer sijui unaweza kunielekeza?"

Kwa sababu interview room ni office fulani ipo ndani, ilibidi nijitolee kumpeleka kwanza mapokezi halafu mimi nikaelekea washroom.

Baada ya kurudi washroom, nilimkuta akiwa kwenye bench anasubir. Inaonesha kweli kulikuwa na interview zinaendelea maana mda ule niliona tena watu wengine kama wawili wamekuja pale.

Nikaamua nijivute kwenye kiti nimuulize mawili matatu, maana alikuwa ni binti tu mzur ameumbika.

Baada ya story mbili tatu nikagundua ndo alikiwa amemaliza chuo mwaka huo huo 2015 so hapo kuna mtu tu alimpigia pande maana hata cheti alikuwa bado hana.

***

Wakati huo nilikuwa ndo nimeanza kazi kwenye moja ya bank kubwa sana hapa nchini.

Baada ya story mbili tatu akaniambia yeye amesoma UDSM na kwa sababu na mimi pia nilisoma UDSM story zikaanza kutiririka.

Mimi: Hivi, Prof Mgongo Fimbo bado yupo? Nasikia mtata sana jamaa yule...

Yeye: Hahahahahahaaaa Yupoo!!

Ikawa hivo, bla bla blaa nyingi.. Ikaishia nikachukua namba zake kwa nia kwamba nitaendelea kuwasiliana nae.

***
Bahati mbaya ile kazi aliikosa kwa kigezo cha uzoefu maana ndo kwanza alikuwa amemaliza chuo.

Kwa kipindi kifupi cha mawasiliano ya hapa na pale na kuzidi kumsoma nikagundua ni binti tu mwenye maadili na kizuri zaidi alikuwa ni msabato na alikuwa ameshika dini mno.

Mi kimoyoni nikawa namfikiria kama mke mtarajiwa maana ki ukweli yule binti ni mzuri. Alikuwa ni black girl fulani hivi baba yake ni Mnyamwezi na Mama yake ni mkurya. Guu kama lote na shape heeeeh debe halafu hee toto ameshika dini.

Nikasema hapa hata mama Mushi akileta za kuleta eti hataki mnyamwezi ningempinga kwa sauti kubwa.

**
Ki ukweli yule binti sikutaka kumtakia kwamba nampenda kwa wakati huo. Japo nilikuwa nimeshakufa na kuoza kwake.

Ili kuhakikisha hakuna Bwege anatia mguu na kumyumbisha ikabidi nimpe treatment kama mpenzi wangu. Kwa kuwa wakati huo alikuwa hajapata kazi bado so nikawa najitoa kisawasawa.

Messages na maphone ilikuwa kila wakati nikipata chance lazima nimchek. Kila mwisho wa wiki jpili ilikuwa lazima nimtoe out. Nguo, saa na vipoch vya kutosha..

Mi sielewi mambo ya kisheria sana, ila alikuwa pia akihudhuria school of law pale mawasiliano akaniambia kuna uwezekana mkubwa akamaliza mwishoni mwa mwaka huo huo na ku graduate.

****
Cut long story short,

Yule binti alikuwa amefaulu hiyo mitihani yake ya school of law. So kilichokuwa kinafuatia hapo ni kufanya sherehe ya graduation.

Mimi alinipa taarifa na kuniambia kwamba ndugu zake wote watakuwepo siku hiyo na kwamba tayar walikwisha mchangia pesa kwa ajili ya kufanya sherehe.

Maandalizi ya graduation yake yakiendelea, nakumbuka siku moja akanipigia simu asubuhi sana. Nakimbuka ilikuwa ni siku ya tarehe 29 (Siku mbili baada ya mshahara).

Note: ukweli ni kwamba japo hii siku ilikuwa ni ya mwisho wa mwezi ila mshahara wote ulioingia nilikuwa nimempa mwenye nyumba kwa kuwa ndo ulikuwa mwisho wa mkataba so nikawa nimekubaliana na mwenyenyumba kuongeza tena kama miezi 6 (Nililipa kama laki 9) . So nikawa nimebakiwa na kama laki 3 na nusu)

Maongezi ya ile simu ya asubuhi ya tareh 29 yalikuwa kama ifuatavyo.

Yeye: Mushieehh.. Umeamkaje baba! (kwa zile huduma nilikuwa nampatia
alitokea kunizoea nadhani alihisi tumeshazama kwenye mapenzi tayar wakati sikuwa nimemtamkia)

Mimi: Nimeamka poa ndo najiandaa kwenda kazini mama akee.

Yeye: Naomba uniongezee laki 3 nimepungukiwa na bajeti ya maandalizi ya sherehe. Kwakuwa nilikuwa nimebakiwa na laki 3 na nusu tu, nisingeweza kumpatia hiyo pesa (Ukweli ni kwamba laiti ningekuwa na hela ningempatia bila hata kujiuliza mara mbili) ikabidi nifunguke tu

Mimi: Daah leo nipo vibaya mama sina hiyo hela kabisa.

Yeye: UNAKOSAJE HELA NA LEO NI MWISHO WA MWEZI?

Hakika sikutegemea hili swali la kipuuzi namna hii. Nilimchukia ghafla na kumtoa moyoni ndani ya mda mfupi.

Sikutaka kumuonesha nimekasirika kwa mda ule na pia sikutaka kumjibu swali alilouliza. Ikabidi nimjibu tu

Mimi: Anyway, embu ngoja nifanya utaratibu then baadae ntakujulisha.

Nilitaka kujipa mda wa kuandaa mazingira ya kulipa kisasi cha kuulizwa swali la kipumbavu.

Kwa kuwa nilimuambia ntafanya utaratibu, mchana wake akanipigia simu ila sikupokea.

Usiku akapiga tena kama tano na sikupokea vile vile. Niliapa kukata mawasiliano once and for all.

Kesho yake vile vile akawa anapiga simu. Na mimi nikaacha kupokea vile vile.

Nikahisi hapa huyu atakuja ghetto maana haikuwa kawaida yangu kutokupokea simu zake.

Mchana wa siku ya pili nikamtext "Nimepata dharura naelekea Moshi mara moja kuna mambo ya kifamilia"

Akajaribu kupiga saa hiyo hiyo, mi sikupokea tena. Tuma message zake nyingi tu na sikumjibu.

Sikumjibu, sikumjibu, sikupokea simu zake tena, sijui ni kwa namna gani nilimuumiza moyo wake. Na ndo mwisho wa uhusiano na binti.

Mwaka jana nikikutana na binamu yake Mlimani City akaniambia 'Roselyn' anafanya kazi kwenye shirika moja kubwa ila yupo kikazi kenya.

Nilifurahi kwa kuwa ameendelea na maisha yake na amepiga hatua. Yawezekana hakuwa mtu sahihi kwangu au mimi sikuwa mtu sahihi kwake.

But yote kwa yote, swali aliloniuliza lilikuwa ni la kipuuzi.
 
Kweli hakutakiwa kuuliza swali la hivyo....najiona kuwa na maamuzi kama yako kama ningekuwa wewe

Asprin kama utahitaji summary niambie,nimeisoma yote
Muda mwingine nawaza huenda ni malaika alitengeneza mazingira. Imagie umeshamuoa mtu halafu anakuja na shombo kama hizo sijui kama ndoa ingekuwa na raha
 
Kwl kaka hata ingekuwa mm!

Kimtokacho mtu ndicho kilicho mjazaa

Ila kaka papuchi umekulaa
 
Waafrika bana! Hilo ni swali la kawaida sana, ulitakiwa kumuelewesha kuwa kodi iliisha umelipa. Labda asingekuelewa ndio kungekuwa na tatizo.

Kitendo cha kuombwa 300K wakati una 350K kilikuchanganya ukashindwa kufikiri vizuri, ndio maana hata hilo swali la kawaida ukalichukulia kivingine.

Sijaona mantiki ya kuacha kupokea sim za huyo bidada, kwani kwenye hizo sms alikuwa anakuandikia nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom