Jamani kama Intellectuals hebu tuweke ushabiki pembeni, tujadili haya madai ya madereva wetu

Mkuu umeongea vizuri, ila hapo kwa red naomba ufafanuzi kidogo, hiyo picha ya dereva tajiri anaitoa wapi? je anakuwa ni dereva kweli? kama kweli ni dereva, inakuwaje anampa wakati anajua utaratibu ukoje?

Pia hapo kwa blue unaposema nauli haziwezi kupanda, unaweza kutoa maelezo kidogo mtu mwenye bus moja kwa mfano atawezaje kumudu kulipa stahiki hizo bila nauli kupanda kwa abiria?

chukulia mfano wewe ni dereva.
mmiliki atachukua copy ya leseni yako pamoja na picha akaitambulishe kule.
akipewa route anamchukua binamu yake anaendesha basi.
kwa hiyo wewe utakua hauna kazi tena
 
Uko sahihi mkuu, tukipata majibu ya maswali yako, tutaweza kujua kama wamiliki wa magari wana uwezo wa kulipa hayo madai bila kuhamishia mzigo kwa abiria

Unajua hili suala la mgomo wa madereva tunalichukulia kiushabiki zaidi kuliko kiuhalisia

kikubwa kwanza ni mkataba wa kazi.
pili mishahara ukipiga hesabu kumlipa dereva 150000 ni pesa ndogo sana ukilinganisha na faida anayoipata mmiliki.halafu naona wangewekeana mikataba
kisha wakajiunga katika mfuko wa bima ya afya na pesa yake anakatwa mwisho wa mwezi kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine.
 
usomi upi unaouzungumzia...wewe.....? transportation industry is like other industries companyies....
....... sema inawendeshwa na wababaishaji......unajua why hauna air tanzania? while kenya airways, ethopian airlines na emirate zimejaa tanzani? uwe na aibu kuongea vitu usivyo na taaluma navyo....

tanzania vitu vinaendesha kibabaishaji kuliko ki taaluma .......
open ur eyes
....
.........
 
Hivi mi nauliza jamani haya madai ya madereva wetu ni sahii kung'ang'ana na serikali badala ya waajiri wao? madai yao ya msingi ni haya hapa;
1. kufuta kusoma kila lesen inapo-expire (hili limeishafutwa tayari)
2. madai ya mikataba bora ya kazi
3. posho za safari
4. mishahara inayokidhi malipo ya pango
5. bima (nadhani hapa wanamaanisha bima ya afya)
6. nauli ya kazini kwa dereva

Ila yote tisa, kumi ni kwamba haya madai yao mwisho wa siku yatapandisha nauli za mabasi na dalala halafu watu wataanza tena kulalamika. Wote tunajua mfanyabiashara habebagi hasara, sisi abiria ndo tutabeba huo mzigo kwa kupandishiwa nauli

Unachokisahau ni kwamba wakati maboss wao wanapeleka mapendekezo ya nauli kwa SUMATRA hivyo vitu tayari Viko included ila madereva hawapewi.
 
Matajiri wengi wanaendesha biashara hii kimagumashi sana, wao wanatafuta sehemu ya kupiga faida.

Kumbuka bus la kwenda na kutoka mkoani linatakiwa kufanyiwa service kila siku, sasa hawa mabosi hawafanyi hivyo. Badala ya kununua matairi mapya wanarudisha mengine yaliotumika siku zilizopita.

Na pia wafanyabiashara wengi sio wamiliki wa mabasi pekee hawana formalities. Biashara zinaenda kimagumashi tu. Wafanyakazi wengi wa tanzania ni vibarua. Hawana mkataba wa kazi, serikali inakosa mapato.
 
Wamilki wanatumia mtu mwingine kwenye kusajili gari na anaendesha mwingine asie na mkataba. Sasa Sumatra na wizara husika wakishatoa vibali hawafuatilii nani anaendesha gari gani na mkataba gani.

Deiwaka wengi ndio wanaendesha haya magari,mikataba ni ya kukatia leseni za biashara tu!

inabidi madereva waanze kutembea na leseni na pia mkataba wa kazi.kama hana gari likapaki police mpaka aje nao mkataba
 
inabidi madereva waanze kutembea na leseni na pia mkataba wa kazi.kama hana gari likapaki police mpaka aje nao mkataba

Tena mkataba uliolipiwa stamp duty, mhuri wizara ya kazi, sumatra n.k ikiwemo picha ya dreva.....pia kabla ya mikataba hiyo kuhalalishwa iwe na vipengele muhimu kama makato ya NSSF.....na nakala moja apewe dreva ili akipata tatizo mahakama za kazi iwe rahisi kutatua kero zao....
 
Dereva wa mabasi yote nchi watambuliwe na mamlaka husika,kwa maana kuwa usajiri wao ufanyike pasipo kuwashikisha waajiri wao.
Serikali iwaombe mikataba yao ya wao kupewa dhamana hiyo na waajiri wao.
Serikali iangalie mikataba kama inaendana na uhalisia wa madai yao.
Leseni zao ziwe maalumu kwa kazi hiyo na inapowezekana waajiri wao waambiwe juu ya umuhimu wa kuwatumia hao madereva pasipo shaka.
Wenye mabasi na malori watengeneza Kampuni na yadi za kudumu na waolezeshe wafanyakazi wao wote ili watambulike kisheria.
 
chukulia mfano wewe ni dereva.
mmiliki atachukua copy ya leseni yako pamoja na picha akaitambulishe kule.
akipewa route anamchukua binamu yake anaendesha basi.
kwa hiyo wewe utakua hauna kazi tena

usikute wanapewa kidogo dogo ili atoe copy ya leseni yake na picha, otherwise kwanini mimi kama dereva nikubali kitu kama hicho?
 
kikubwa kwanza ni mkataba wa kazi.
pili mishahara ukipiga hesabu kumlipa dereva 150000 ni pesa ndogo sana ukilinganisha na faida anayoipata mmiliki.halafu naona wangewekeana mikataba
kisha wakajiunga katika mfuko wa bima ya afya na pesa yake anakatwa mwisho wa mwezi kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine.

Mmmh usije kuwa umechukulia juu juu mkuu, unless uniambie una bus au daladala whotever
 
usomi upi unaouzungumzia...wewe.....? transportation industry is like other industries companyies....
....... sema inawendeshwa na wababaishaji......unajua why hauna air tanzania? while kenya airways, ethopian airlines na emirate zimejaa tanzani? uwe na aibu kuongea vitu usivyo na taaluma navyo....

tanzania vitu vinaendesha kibabaishaji kuliko ki taaluma .......
open ur eyes
....
.........

Umejuaje kama sina taaluma navyo mkuu?
 
Unachokisahau ni kwamba wakati maboss wao wanapeleka mapendekezo ya nauli kwa SUMATRA hivyo vitu tayari Viko included ila madereva hawapewi.

Vinaweza kuwa included kwa sababu tu ni requirements ya Sumatra, swali langu linabaki pale kwamba wanaweza kweli kulipa madai ya madereva bila kupandisha nauli kwa abiria?
 
Suluhisho hapo wajiunge na NSSF watajitengenezea pension zao za uzee na pia watapata matibabu bure manake mimi sasa hivi ninanufaika na hayo matibabu ya bure yanayotolewa na NSSF.
 
we ndio unataka kuchanganya mambo, utaratibu wa sasa ni kuwa, mtu ukiagiza basi, ukimalizana na tra, unakwenda wizara ya kazi na ajira, kujaza form ya mkataba wa ajira baina ya tajiri na dreva, yote mliokubaliana yanakuwa kwenye mkataba, mnasaini mbeleya afisa kazi, unabandika na picha ya dreva husika, wanaipitisha na kugonga mihuri, wanampa tajiri anazipeleka sumatra, nao wakishazikagua ndio wanatoa, kibali cha route husika. Sasa cha ajabu kinachofanyika sasa ni kuwa tajiri anakwenda wizara ya ajira na picha ya mtu anayodai kuwa ndio atakuwa ni dreva wake anagongewa mihuri na mkataba unapita kimagumashi, anaupeleka sumatra anapewa route, bila kumuona huyo dreva physically!! Sasa unaposema kuwa madai yao yataongeza nauli sio kweli, na serikali hapa sio kwamba inapanga kiwango cha mshahara wao, kila sector, ina kiwango chake cha chini cha kulipa wafanyakazi ambacho serikali ilikipanga siku nyingi, wao wanataka waajiliwe wamechoka kuwa vibarua, na sheria za kazi zipi wazi, sifa za kibarua ni zipi, sasa mtu anaefanya kazi miaka 10,bado ni kibarua!! Anakuja kwa baba yake ambaye ni serikali unamkana na kumwambia mi hayo hayanihusu kakae na boss wako, mtayamaliza!! Siku zote bepali yeye ni ku maximise profit tu, can u imagine dreva analipwa mshahara wake kwa kupitia mpesa, tg pesa?? Hapo serikali kodi inapata vipi? Matokeo yake ni kuzidi kuwaumiza hawa wafanyakazi wengine ambao wako kwenye ajira rasmi, kwani tax base, inakuwa ni ile ile miaka nenda rudi, wao wanataka ajira rasmi ambapo hataweza kufukuzwa kwa njia ya simu, na wengi wao wanalipwa posho na sio mishahara. Ila ugumu unakuwa wenye kusimamia haya mambo ndio hao hao wanyonyaji, kwani ukiwaajiri kwenye mifuko ya jamii lazima upeleke, nakufukuzana ovyo hakutakuwepo, kuhusu bima hapa wanataka bima ya maisha, na sio bina ya afya kama unavyosema wewe, wewe fanya utafiti kidogo tafuta dreva wa hata roli wa zambia, kenya au rwanda akwambie maslahi yake, wa hapa kwetu utawaonea huruma, na tajiri hamtambui tingo, wewe kama una mtaka mtafute kwa pesa yako wewe!! Utakuwa una mlipa kwa mileage yako!! Tuwe wakweli mchawi wa yote haya ni serikali,. Watu wakose haki zao eti huku wengine tutapata shida!! Wee umekula maharage ya wapi??? Mbona wenyewe kwenye escrow hawakuona kama watatuletea balaa kubwa kama hili la pesa yetu kupolomoka kiasi hiki!??? Mtu adai ujira wake halali unatwambia atakuletea balaa!! Hiyo miradi inayojengwa kila leo chini ya viwango huzioni impacts zake, we bwana vipi?!!


wamiliki wengi wa magari ni ccm ???????????????????????
 
Dereva wa mabasi yote nchi watambuliwe na mamlaka husika,kwa maana kuwa usajiri wao ufanyike pasipo kuwashikisha waajiri wao.
Serikali iwaombe mikataba yao ya wao kupewa dhamana hiyo na waajiri wao.
Serikali iangalie mikataba kama inaendana na uhalisia wa madai yao.
Leseni zao ziwe maalumu kwa kazi hiyo na inapowezekana waajiri wao waambiwe juu ya umuhimu wa kuwatumia hao madereva pasipo shaka.
Wenye mabasi na malori watengeneza Kampuni na yadi za kudumu na waolezeshe wafanyakazi wao wote ili watambulike kisheria.

Mawazo yako ni mazuri sawa na alichosema mkuu ZeMarcopolo ktk comment #19 , ila ukweli mchungu ni ule aliosema TRUVADA ktk comment #36
 
Last edited by a moderator:
In short ni kuwa madereva wanataka utaratibu wa mtu kuwa na daladala moja au mbili uondolewe.
Ili kukidhi mahitaji yao inabidi kuwe na kampuni zenye magari mengi na mfumo madhubuti wa kuwasimamia. In the end hata mapato yao yale ya magumashi yatakosa mwanya, watalalamika tena.

Mimi naona wanajikaanga wenyewe.

Kuhusu kufukuzwa kazi kiholela, sidhani kama mmiliki anaweza kumfukuza mtu anayeheshimu masharti ya kazi na kulitunza gari.

Halafu,next mgomo kwenye hili utakuwa wa mahouse girl. Hawa pia ajira yao haijadalimishwa na hawalipiwi nssf. Kwahiyo kama unaunga mkono madereva, jiandae kuunga mkono mahousegirl pia.

Uwezo wako wa kuona mambo siku zote uu finyu kabisa. Sasa unataka hii nchi watu waendelee kutegemea mapato ya kimagushi? Hapa watu wanataka ajira na mshahara kwa mujibu wa sheria na sio ''mapato ya kimagumashi. Na kuhusu ma-house girls... ndio hata wao wanatakiwa kuwa na ajira na malipo ya uhakika. Tatizo lako mfumo wa maisha wa kimagushi magushi wa Tanzania umekudumaza!
 
Watu wengi wameshindwa kuyaelewa madai ya madereva, wanataka ajira zao zirasimoshwe kama ajira zingine, ajira zenye uhakika sio unatoka lubumbashi unafika tunduma tajiri anakuambia acha gari yangu hapo hapo funguo mpe fulani, pia kibwa kuliko serikali ikusanye kodi kwao kwakia serikalo haijawai kisanya kpdi kwenye ajira ya udereva na kama imewahi basi kwa kiasi kidogo sana
 
madreva kudai haki ni sawa lakini haki ipi kwa magari yapi? ambayo kufika kwake hapa yashaoza? gari meter inasoma km mil.1 yaani mwezi sita inakuwa banda la kuku, tujiulize yako wapi mabasi makubwa fuso ingine nyuma. kuna wakati madreva wanachosha magari kwa kuwapa maday waka lena wanaalibu ingine , body, kuwa na mabas ni biashara kichaa.
 
Back
Top Bottom