Elections 2010 Sera ya Elimu: Wapinzani -vs- Chama Tawala

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Ndugu zangu!

Naomba tuchambue sera hizi za vyama objectively kutoka kwenye ilani zenyewe za vyama.

CCM: Ilani ya uchaguzi 2010-2015
9:[FONT=Tahoma,Bold]Majukumu ya Msingi[/FONT]
(a) Kuimarisha na kuboresha elimu.
(b) Kuandaa raslimali watu katika maarifa na mwelekeo.
(c) Kufanya mapinduzi ya kilimo, ufugaji na uvuvi.
(d) Kufanya mapinduzi ya viwanda.
(e) Kuinua matumizi ya maarifa, yaani sayansi na teknolojia katika uchumi wa nchi.
(f) Upatikanaji wa nishati yenye uhakika na nishati mbadala.
(g) Ujenzi wa miundombinu ya kisasa.

9. Elimu 2005-2010 mafanikio
15. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Serikali ya CCM imeendelea kufanya upanuzi mkubwa wa elimu katika ngazi zote. Kwa kushirikiana na wananchi na kwa kupitia programu na miradi mbalimbali kama vile MMEM, MMES na MEMKWA yamepatikana mafanikio makubwa kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi na mpaka elimu ya juu. Elimu ya Watu Wazima na elimu maalumu nayo imepewa msukumo maalumu.

(a) [FONT=Tahoma,Bold]Elimu ya Awali

(i) Idadi ya madarasa ya shule za Awali imeongezeka kutoka 18,455 mwaka 2005 hadi 28,048 mwaka 2009.
(ii) Wanafunzi wa Elimu ya awali wameongezeka kutoka 638,591 mwaka 2005 hadi 873,981 mwaka 2009, wakiwemo wanafunzi 2,146 wenye mahitaji maalumu.

(b) [FONT=Tahoma,Bold]Shule za Msingi[/FONT]
(i) Shule za msingi zimeongezeka kutoka 13,679 mwaka 2005 hadi 15,675 mwaka 2009.
(ii) Idadi ya wanafunzi wa shule za msingi imeongezeka kutoka 7,083,063 mwaka 2005 hadi kufikia 8,441,553 mwaka 2009.
(iii) Uandikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu umeongezeka kutoka 18,982 mwaka 2005 hadi 27,422 mwaka 2009.


(c) [FONT=Tahoma,Bold]Sekondari

(i) Idadi ya shule za sekondari imeongezeka kutoka 1,745 (1,202 za Serikali na 543 zisizo za Serikali) mwaka 2005 hadi shule 4,102 (3,283 za Serikali na 819 zisizo za Serikali) mwaka 2009.
(ii) Uandikishaji wa wanafunzi (kidato cha 1-4) uliongezeka kutoka 401,598 mwaka 2005 hadi 1,401,559 mwaka 2009. Hili ni ongezeko la asilimia 179.
(iii) Serikali imejenga madarasa 11,266, nyumba za walimu 986 na shule za hosteli 52 katika kata 2,575 zilizopo.
(iv) Uandikishaji wa wanafunzi wa kidato cha 5 hadi 6 uongezeka asilimia 0.6 mwaka 2005 hadi asilimia 1.5 mwaka 2009.
(v) Serikali imegharamia elimu ya sekondari kwa wanafunzi 41,211 wanaotoka katika familia zenye kipato duni ambapo jumla ya Shilingi 6,677,537,600 zilitumika katika miaka ya 2006 na 2007.

(d) [FONT=Tahoma,Bold]Vyuo vya Ufundi[/FONT]
(i) Udahili wa wanafunzi wa vyuo vya ufundi umeongezeka kutoka 40,059 mwaka 2005/2006 hadi kufikia 48,441 mwaka 2008/2009. Ongezeko hili limechangiwa na kuongezeka kwa vyuo vya ufundi kufikia 210 mwaka 2009 kutoka 183 mwaka 2005.
(ii) Pia vyuo vya ufundi stadi vimeongezeka kutoka 260 mwaka 2005 hadi 932 mwaka 2009.

(e) [FONT=Tahoma,Bold]Vyuo Vikuu[/FONT]
(i) Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka 26 mwaka 2005 hadi kufikia 32 mwaka 2009. Kati ya hivyo vipya kimoja ni cha Serikali [FONT=Tahoma,Bold]kinachojengwa Dodoma ambacho kitakapokamilika kitakuwa na wanafunzi 40,000 [/FONT]na kuwa ndicho kikubwa kuliko vyote nchini.
(ii) Wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu vilivyopo nchini waliongezeka kutoka 55,296 mwaka 2005/2006 hadi 118,000 mwaka 2009/2010.
(iii) Kati yao wanafunzi 69,250 walipata mikopo ya elimu ya juu.
(iv) Jumla ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya mikopo iliongezeka kutoka Tshs. 56.1 bilioni mwaka 2005/2006 hadi Tshs. 243 bilioni mwaka 2010.

(f) [FONT=Tahoma,Bold]Vyuo vya Ualimu[/FONT]
(i) Serikali imepanua mafunzo ya walimu na kuishirikisha sekta binafsi.
(ii) Mpaka kufikia mwaka 2009 vyuo 79 nchini vimekuwa vikitoa mafunzo ya ualimu. Kati ya vyuo hivyo 34 ni vya Serikali na 45 ni vya watu na mashirika binafsi.
(iii) Idadi ya walimu wa awali iliongezeka kutoka 11,148 mwaka 2005 na kuwa 16,597 mwaka 2009.
(iv) Walimu wa shule za msingi waliongezeka kutoka 135,013 mwaka 2005 na kufikia 154,895 mwaka 2009.
(v) Idadi ya walimu wapya wa sekondari waliohitimu katika vyuo vikuu hapa nchini imeongezeka kutoka 500 mwaka 2005 hadi 19,124 mwaka 2010 kati yao 7,004 ni wa Diploma na Digrii 12,120.

(vi) Serikali ilitoa Shilingi bilioni 22.5 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 2,501 za walimu wa shule za sekondari.

(vii) Miundombinu imeongezeka ambapo hadi mwaka 2009 nyumba za walimu 26,848, madarasa 79,102 na matundu ya vyoo 97,603vimejengwa.



(g) [FONT=Tahoma,Bold]Vitabu na Vifaa vya Kufundishia[/FONT]
Kumekuwepo na ongezeko kubwa katika bajeti ya sekta ya elimu ambalo limesaidia katika kukabiliana na tatizo la uhaba wa vitabu na vifaa vyakufundishia.











AHADI
Serikali itachukua hatua za kuboresha, kuimarisha na hata kupanua elimu ya Awali hadi ya Chuo Kikuu na kuhakikisha kwamba elimu ya ngazi zote itakayotolewa nchini tangu sasa iwe ya ubora utakaowawezesha vijana wetu kuchukua nafasi zao stahiki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na dunia kwa ujumla. Hivyo, lengo hilo litafikiwa kwa kuishirikisha sekta binafsi kwa ukamilifu katika kutekeleza yafuatayo:-


(a) [FONT=Tahoma,Bold]Elimu ya Awali[/FONT]
(i) Kuhakikisha kwamba kila shule ya msingi ina darasa la Elimu ya Awali lenye madawati yanayolingana na hali ya watoto wa elimu hiyo.
(ii) Kujenga vyoo kwa ajili ya watoto wa Elimu ya Awali ili wasiingiliane na wale wa shule za msingi.
(iii) Kuandaa walimu wengi wa Elimu ya Awali na kuwapanga katika shule zinazohusika.

(b) [FONT=Tahoma,Bold]Elimu ya Msingi[/FONT]
Kusimamia kwa ukamilifu utekekezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi awamu ya pili (MMEM II – 2007 – 2011) na kuandaa na kutekeleza awamu ya tatu (MMEM III):-
(i) Kununua na kusambaza vifaa vya kufundishia na kujifunzia katikashule zote.
(ii) Kuimarisha Vituo vya Walimu (Teacher Resource Centres) katika Kanda na Halmashauri zote ili viweze kutoa mafunzo ya walimukazini.
(iii) Kuimarisha utoaji wa mafunzo kwa walimu wa masomo ya Hisabati,Kiingereza na Sayansi.
(iv) Kuendelea kuweka msukumo katika uandikishaji wa watoto wotewa rika lengwa katika ngazi ya Elimu ya Msingi kufikia asilimia 100 mwaka 2015.
(v) Kuinua kiwango cha uandikishaji wa watoto wenye ulemavu nawenye mahitaji maalumu.
(vi) Kuendelea kuratibu na kusimamia upatikanaji wa maslahi ya walimu wa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ualimu na
kuyaboresha ili kuhakikisha kwamba mishahara itolewayo inazingatia hali halisi ya maisha na ya soko.
(vii) Kuendelea kuimarisha ukaguzi wa shule na kuhakikisha kuwa kilashule inakaguliwa angalau mara moja kwa mwaka na taarifa za ukaguzi kufanyiwa kazi.
(viii) Kuhakikisha kwamba kila shule ya msingi ina walimu, madawati, vitabu vya kiada kwa kila somo vya kutosha. Uwiano wa mwalimu mmoja kwa kila wanafunzi 60 ufanyiwe kazi.
(xv Serikali Kuu ihakikishe kwamba kila Manispaa au Halmashauri ya Wilaya inajenga vyoo vya kisasa na vya kutosha katika shule zote za msingi ambazo ziko chini yake. Sekta binafsi ishirikishwe katikautekelezaji wa mradi huu.
(x) Kuanzisha mradi kabambe wa ujenzi wa nyumba nyingi za walimuwa shule za msingi za vijijini kwa kuwashirikisha wadau wote. Utekelezaji uanzie katika Wilaya ambazo zina uhaba mkubwa wa nyumba za walimu.
(xi) Kuongeza idadi ya wanafunzi watakaochaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari kufikia asilimia 100 ifikapo mwaka 2015.
(xii) Kuimarisha uwezo wa watendaji katika usimamizi na menejimenti ya programu za elimu katika ngazi zote.

(c) [FONT=Tahoma,Bold]Elimu ya Sekondari[/FONT]
Kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimuya Sekondari awamu ya pili (MMES II – 2010 - 2014), kuandaa nakutekeleza awamu ya tatu (MMES III):-
(i) Kuendelea kutekeleza azma ya kuwa na angalau shule moja yakidato cha tano na sita kwa kila tarafa.
(ii) Kuongeza idadi ya wanafunzi wa kidato cha 4 kwenda kidato cha 5 kufikia asilimia 50 ya watoto wanaofaulu ifikapo mwaka 2015.
(iii) Kuendeleza na Kuimarisha mafanikio tuliyofikia katika ujenzi wa shule za sekondari kwa kuongeza idadi ya walimu, kununua vifaa vya maabara, vitabu, kuimarisha Maktaba na kukabiliana na jambololote litakalopunguza ufanisi wa kiwango cha elimu katika shulehizo.
(iv) Kuendelea kutekeleza mpango wa kujenga maabara ya Sayansi na ya Lugha katika kila Shule ya Sekondari ili kuboresha ufundishaji.
(v) Kuendelea kutekeleza Programu ya kufundishia na kujifunzia kwakutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Shule za Sekondari.
(vi) Kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi, Hisabati na Lugha na kuinua ufaulu wa masomo hayo.
(vii) Kuendelea na mpango wa ujenzi wa nyumba za walimu hasa sehemu za vijijini na maeneo magumu kufikika.
(viii) Kuendelea kusimamia na kuimarisha michezo shuleni.
(ix) Kupitia na kuimarisha mitaala ya elimu ya sekondari kulingana na mahitaji.
(x) Kusimamia ubora wa miundombinu ya shule za sekondari ili kuleta ufanisi katika utoaji wa elimu.
(xi) Kuimarisha uwezo wa watendaji katika usimamizi na menejimenti ya programu za elimu katika ngazi zote.
(xii) Kurudisha utaratibu wa kuzipelekea shule vitabu na vifaa ili kuhakikisha kwamba shule hazitofautiani katika upatikanaji na
utumiaji wa vifaa hivyo.
(xiii) Kuimarisha na kuboresha kwa kiwango kikubwa shule za vijana wenye vipaji maalumu ili lengo la kuzianzisha liweze kufikiwa kama lilivyokusudiwa tangu mwanzo.
(xiv) Katika shule za sekondari, uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 45 uzingatiwe kama hatua ya kuinua ubora wa elimu hiyo.


(d) [FONT=Tahoma,Bold]Elimu ya Ualimu[/FONT]
Kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo na Menejimenti ya Ualimu (Teacher Development Management Strategy - TDMS) katika utoaji wa mafunzo ya ualimu:-
(i) Kuanzisha mafunzo ya walimu wa shule za msingi watakaoandaliwa kufundisha masomo mawili tu ambayo kila mmoja anayamudu ili kuinua ubora wa elimu ya msingi.
(ii) Kuandaa na kuendeleza walimu wanaofundisha masomo ya Sayansi, Hisabati na Lugha katika Shule za Msingi na Sekondari.
(iii) Kuongeza udahili wa wanachuo katika mafunzo ya Ualimu tarajali ngazi ya Cheti na Stashahada.
(iv) Kutoa mafunzo kwa walimu kazini ili kuimarisha na kuendeleza mbinu za ufundishaji kwa walimu.
(v) Kutoa mafunzo ya TEKNOHAMA katika kufundishia na kujifunzia katika Vyuo vya Ualimu.
(vi) Kuendelea kusimamia na kuimarisha michezo katika vyuo vya ualimu.
(vii) Kuimarisha miundombinu ya vyuo vya ualimu ili kuleta ufanisi katika utoaji wa elimu.
(viii) Kuboresha maabara ya vyuo vya ualimu vyenye mchepuo wa sayansi na kuvipatia vifaa na kemikali zinazotakiwa kwa ajili ya mafunzo ya vitendo katika vyuo hivyo.
(ix) Kuandaa mitaala wa mafunzo yatakayojumuisha masomo ya mapinduzi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na viwanda ili kupata
wataalamu wa kufundisha masomo hayo. Uandishi wa vitabu vya masomo hayo yaende sambamba na maandalizi ya mtaala huo.
(x) Kuimarisha uwezo wa watendaji katika usimamizi na menejimenti ya programu za elimu katika ngazi zote.


(e) [FONT=Tahoma,Bold]Elimu ya Juu[/FONT]
Kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Juu:-
(i) Kuboresha utaratibu wa utoaji na urejeshwaji wa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu.
(ii) Kupanua wigo wa utoaji wa mikopo ili kila mwanafunzi aliye na sifa ya kuingia chuo kikuu apate mkopo.
(iii) Kukarabati, kupanua na kuimarisha miundombinu ya vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki ili iweze kuhimili ongezeko kubwa la wanafunzi watakaomaliza elimu ya sekondari.
(iv) Kuongeza udahili wa wanafunzi kwenye vyuo vya elimu ya juu.
(v) Kuongeza idadi ya wanafunzi wa kike vyuo vikuu ili ifikie angalau asilimia 40 ya wanavyuo wanaodahiliwa kila mwaka.
(vi) Kuandaa wahadhiri wa kutosha na wenye sifa za kufundisha kwenye vyuo vya elimu ya juu.
(vii) Kuunganisha vyuo vikuu na taasisi za utafiti kwenye mtandao ili kuimarisha utafiti wa pamoja, kupanua elimu kiwango cha uzamili na uzamivu.
(viii) Kuratibu na kusimamia utoaji wa Elimu ya Juu iliyo bora na kufanyika kwa utafiti ili ziweze kutatua matatizo ya kijamii na kiuchumi.
(ix) Kuimarisha mazingira ya utoaji wa Elimu ya Juu na maslahi yanayoendana nayo ili wahadhiri wavutiwe kujiunga na kubaki katika vyuo vya Elimu ya Juu na Vyuo Vikuu.
(x) Kuimarisha utoaji wa Elimu ya Juu kwa njia ya Masafa na Elimu Mtandao.
(xi) Kuimarisha uwezo wa watendaji katika usimamizi na menejimenti ya programu za elimu katika ngazi zote.


(f) [FONT=Tahoma,Bold]Mafunzo ya Ufundi[/FONT]
Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi:-
(i) Kuongeza kasi ya upanuzi wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi kwa kushirikisha sekta binafsi.
(ii) Kuanzisha vyuo vya Ufundi Stadi angalau kimoja kwa kila wilaya ifikapo mwaka 2015.
(iii) Kuendeleza mafunzo ya ufundi na kada za kati za fani mbalimbali.
(iv) Kuongeza idadi ya wahitimu wa vyuo vya ufundi stadi wenye sifa za kuendeleza progamu za elimu ya ufundi kuanzia ngazi ya ufundi sanifu hadi ngazi za juu.
(v) Kuendelea kuhamasisha wanafunzi wa kike kujiunga na Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
(vi) Kuimarisha miundombinu ya Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
(vii) Kuimarisha uwezo wa watendaji katika usimamizi na menejimenti ya programu za elimu katika ngazi zote.

(g) [FONT=Tahoma,Bold]Elimu ya Watu Wazima Yenye Manufaa[/FONT]
(i) Kuandaa na kutekeleza mpango kabambe wa Elimu ya Watu Wazima Yenye Manufaa nchini kote.
(ii) Kuimarisha Mipango ya Elimu ya kujiendeleza ikiwa ni pamoja na Elimu Masafa na Ana kwa Ana.
(iii) Kuimarisha utoaji wa Elimu Nje ya Mfumo Rasmi kupitia Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa (MEMKWA) kwa kushirikiana na wadau wengine.
(iv) Kuinua ubora wa utoaji elimu ya watu wazima kupitia Mpango wa Uwiano Kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii (MUKEJA).
(v) Kuimarisha uwezo wa watendaji katika usimamizi na menejimenti ya programu za elimu katika ngazi zote.




CHADEMA: ilani ya uchaguzi 2010-2015
FURSA KWA KILA MTOTO WA KITANZANIA KUPATA ELIMU BORA
2.1 Utangulizi
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]CHADEMA inaamini kuwa elimu ndio nguzo kuu ya maendeleo na nyenzo ya haraka na ya uhakika zaidi ya kujenga taifa la kisasa. Wananchi wasio na elimu au wenye elimu hafifu hawawezi kupata fursa za kumiliki na kuendesha uchumi, hawawezi kuiwajibisha serikali yao na hawawezi kuwajibika. Kwa hivyo kutoa fursa katika kupata elimu bora ni hatua ya kwanza na ya msingi katika kujenga taifa linalojitegemea na lenye uchumi imara na maendeleo endelevu. [/FONT]
[/FONT]2.2 Hali halisi kuhusu elimu hapa nchini
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]2.2.1 Kuna matatizo mawili ya msingi kuhusu elimu hapa nchini. Tatizo la kwanza ni uduni wa elimu inayotolewa katika shule zetu, na hasa shule za umma. Ukiwauliza CCM kuhusu elimu wanakujibu kuwa Taifa limepiga hatua kubwa ya upanuzi wa fursa za elimu hapa nchini, hasa elimu ya sekondari kufuatia kuanzishwa kwa Mpango wa Elimu ya Sekondari (MES). Hii ni kweli kwa upande mmoja. Mfano mzuri ni kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule za sekondari, hasa za kata, kutoka wanafunzi 345,441 mwaka 2003 hadi kufikia wanafunzi 1,466,402 mwaka 2009. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]2.2.2 Hata hivyo, Serikali ya CCM iliahidi kupitia Mpango wa Elimu ya Sekondari (MES) kuongeza kiwango cha kufaulu katika madaraja ya I, II na III toka asilimia 37.8 mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 70 mwaka 2009. Lakini, pamoja na kwamba Serikali ya CCM kwa msaada wa mashirika ya kimataifa imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 200 chini ya Mpango wa Elimu ya Sekondari, kiwango cha kufaulu katika madaraja haya kimeshuka. Kwa mfano, kwa mujibu wa takwimu za Baraza la Mitihani la Taifa na Kijitabu cha Takwimu cha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, idadi ya wanafunzi wanaofaulu katika madaraja ya I, II na III kimeshuka kutoka asilimia 37.8 mwaka 2004 hadi asilimia 17.8 tu mwaka 2009. Aidha, idadi ya wanafunzi wanaofeli kwa kupata Daraja la 0 (Division 0) 14 [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]imeongezeka kutoka asilimia 8.5 mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 27.49 mwaka 2009. Asilimia 54.66 ya watahiniwa wote wa Kidato cha Nne mwaka 2007 walifaulu kwa kiwango cha Daraja la IV, ambalo kimsingi ni sawa na kufeli. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]2.2.3 Chanzo kikubwa cha tatizo la uduni wa elimu yetu ni sera mbovu za elimu na uongozi legelege katika Wizara ya Elimu na Serikali ya CCM kwa ujumla. Sera za CCM kuhusu elimu ni bora elimu; kwao wingi wa mashule ndio elimu yenyewe bila kujali wanachokipata wahitimu wa mashule hiyo. Kwa miaka nenda wameendelea kutuhubiria juu ya [/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]kuboresha [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]elimu huku wakitekeleza sera ya [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]kubabaisha [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]elimu Serikali ya CHADEMA itatilia mkazo [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]elimu bora [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]na hiki ndicho kitakachokuwa kipaumbele cha kwanza katika sera ya elimu. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]2.2.4 Tatizo la pili la msingi linahusu mfumo wa elimu hapa nchini. Mfumo wetu wa elimu haumfanyi mhitimu aweze kujitegemea. Ni mfumo unaotaalumisha bila kutalaamisha. Hii inafanya vijana wanaohitimu masomo yao wasiweze kujitegemea kikamilifu nje ya mfumo rasmi wa ajira. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]2.2.5 Pamoja na matatizo haya ya msingi, kuna matatizo sita mahususi katika elimu yetu ambayo CHADEMA itakabiliana nayo mara baada ya kuunda serikali. [/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]i. Matabaka katika elimu na kutelekezwa kwa shule za umma [/FONT][/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Serikali ya CCM imezitekeleza shule za umma. Shule nyingi za serikali zimechakaa kimajengo, hazina madawati, vitabu, maabara na vifaa muhimu vya kisasa vya kufundishia na kujifunzia. Watoto wanaosoma katika shule za serikali wanasoma katika mazingira magumu sana. Kwenye shule kadha wa kadha za bweni na za kutwa lishe bado ni tatizo na ni duni. Matokeo yake wazazi wenye uwezo wanalazimika kuwapeleka watoto wao katika shule za binafsi, ambazo ni chache na ghali. Matokeo yake tumetengeneza ubaguzi katika mfumo wa elimu kati ya shule binafsi na za serikali. Hali hii ni hatari kwa mustakabali wa taifa kwa muda mrefu ujao. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]ii. [/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Kudhalilishwa kwa taaluma ya ualimu kiujira na kitaaluma: [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Walimu wa shule za serikali wametelekezwa kwa kulipwa mishara midogo na wanafanya kazi katika mazingira magumu na ya kudhalilishwa. Matokeo yake, walimu walio wengi [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]15 [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]wamekata tamaa, na wakipata mwanya wa kazi nyingine huacha ualimu mara moja. Bado walimu ndio viongozi wa awali kabisa ambao watoto wetu wanakutana nao katika makuzi yao na ni kutoka kwao ndio wanajifunza tunu mbalimbali za maisha. Kutotengeneza mazingira na mfumo mzuri wenye kujali maisha na kazi ya ualimu ni kuweka msingi mbaya kwa wanafunzi wao kujifunza kutoka kwao na kuwaiga. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]iii. [/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Watoto wa kitanzania kutojengewa msingi mzuri wa lugha ya taifa na za kimataifa hasa Kiingereza[/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]. Katika ukanda wa Afrika Mashariki (EAC) na Kusini mwa Afrika (SADC), ni watoto wa kitanzania pekee wasiofundishwa lugha ya kiingereza kwa ufasaha. Matokeo yake, ili mtoto ajifunze lugha kama ya Kiingereza vizuri ni lazima apelekwe kwenye shule binafsi za [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]international[/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]. Wale wasio na nafasi hizo wanajikuta katika hali ngumu ya kujifunza katika ngazi za juu za elimu ambazo zinahitaji ufasaha mkubwa wa lugha ya Kiingereza kuweza kuelewa na kujieleza. Kumudu lugha hii si kwa ajili ya ajira tu bali kwa ajili ya kujenga uwezo wao kuhusiana na kushirikiana katika ngazi mbalimbali za maisha na watu wengine ambao lugha inayowaunganisha ni ya Kiingereza au Kifaransa. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]iv. [/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Utoro na Watoto wa kike kuacha shule kwa sababu ya mimba [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Moja ya tatizo linaloikabili elimu yetu ni utoro wa wanafunzi. Takwimu za elimu zinaonyesha kuwa utoro wa wanafunzi wa shule za msingi umefikia kiwango cha asilimia 35.5, na baadhi ya mikoa na wilaya hadi asilimia 56.7. Takwimu zinaonyesha pia kwamba mimba za utotoni ni moja ya sababu kubwa za watoto wa kike kuacha shule, ambapo asilimia zaidi ya 15 ya watoto wote walioacha shule mwaka 2009 ilisababishwa na mimba za utotoni. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]Kinachoshangaza zaidi ni kwamba [/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Rais Kikwete[/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman], badala ya kuja na suluhu ya tatizo, [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]anawalaumu watoto wanaopata mimba kwa kuwaambia kuwa wanapata mimba kwa sababu ya ‘kiherehere chao' [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman](Nipashe, Jumatatu, 07 Juni 2010). Tunahitaji ufumbuzi wa haraka na wa kudumu wa tatizo la watoto wetu wa kike kuacha shuke kwa sababu ya mimba. 16 [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]Serikali ya CHADEMA itaweka utaratibu ili kuhakikisha kuwa wanafunzi ambao wanajikuta wanalazimika kukatisha masomo kwa sababu ya ujauzito wanaruhusiwa kuendelea na masomo mara baada ya kujifungua bila kulazimika kuhama maeneo yao kwa sababu ya unyanyapaa. Tanzania imepoteza mabinti wengi walioachishwa shule kwa sababu ya ujauzito ambao kama wangepata nafasi ya kuendelea na shule wangeweza kutoa mchango kwa taifa [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]Pamoja na hilo, Serikali ya CHADEMA itahakikisha kuwa wale wote wanaowapatia wanafunzi mimba wanawajibishwa kisheria pamoja na kulazimishwa kulipia gharama yote ya kukatisha masomo na malezi ya mtoto hadi mtoto afikapo miaka 18. Na wale ambao wanafanya vitendo hivyo kwa mabinti wa chini ya miaka 18 watashtakiwa kwa mujibu wa sheria kwa makosa ya ubakaji (statutory rape). [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]v. [/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Kufifishwa kwa shule za kitaifa [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Serikali ya CCM imeondoa shule za kitaifa ambazo zilikuwa ni muhimu katika kujenga moyo wa utaifa miongoni mwa vijana na wananchi kwa ujumla kwa kuwapokea wanafunzi kutoka sehemu kila pembe ya nchi. Matokeo yake kuna watoto wanaoanza shule katika kata na wilaya moja kuanzia shule ya awali hadi kidato cha sita na kuna baadhi wana hatari ya kusoma hadi chuo kikuu katika wilaya moja. Hii si hali nzuri kitaifa kwa sababu inawafanya vijana wawe na mawazo finyu na kutokutambua hali halisi ya nchi yao, na hivyo hubomoa mshikamano wa kitaifa. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]vi. [/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Mfumo usio wa uhakika wa kugharamia elimu ya juu. [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Serikali ya CCM imeshindwa kubuni njia endelevu za kugharamia elimu, na hasa elimu ya juu. Kukosekana kwa njia za uhakika za kugharamia elimu ya juu kumesabisha matatizo mengi katika sekta ya elimu ya juu ikiwemo: [/FONT]
[/FONT][FONT=Courier New,Courier New][FONT=Courier New,Courier New]o [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu kukabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha kunakopelekea vishindwe kutimiza majukumu yao ya msingi kikamilifu. Kwa mfano, katika mwaka wa fedha wa 2009/2010, baadhi ya vyuo vikuu vilipata asilimia 30 tu ya bajeti ilivyopangiwa. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]17 [/FONT]
[/FONT][FONT=Courier New,Courier New][FONT=Courier New,Courier New]o [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Kushindwa kwa Serikali ya CCM kugharamia tafiti zinazofanywa katika vyuo vyetu, na tafiti chache zinazofanywa zinagharamiwa na wafadhili wa nje. Ni wazi kuwa tafiti za namna hii haziwezi kuwa na ajenda endelevu ya kujibu matatizo ya nchi kwani wanaofadhili tafiti wana ajenda zao ambazo wangependa zitimizwe [/FONT]
[/FONT][FONT=Courier New,Courier New][FONT=Courier New,Courier New]o [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Kushindwa kuwa na mfumo endelevu wa kufadhili au kuwapa mikopo wanafunzi katika vyuo vikuu. Mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu inatolewa kimatabaka, kwa usumbufu mkubwa, na mara nyingine wanapata wasiotahiki na wanaostahiki hawapati. [/FONT]
[/FONT][FONT=Courier New,Courier New][FONT=Courier New,Courier New]o [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Vyuo vikuu kupoteza uhuru kamili wa kufanya kazi za kitaaluma na kitaalamu kunakosababishwa na kuingiliwa na wanasiasa. Imefika mahala hata ajira za vyuo vikuu sasa hivi zinaamuliwa na wanasiasa badala ya mabaraza ya vyuo hivyo kwa kuzingatia sifa zao za kitaalma na kimaadili. [/FONT]
[/FONT][FONT=Courier New,Courier New][FONT=Courier New,Courier New]o [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Kasi ndogo ya maendeleo katika sekta ya sayansi na teknolojia kunakosababishwa na uwekezaji mdogo katika sekta hii na kutowajali wana sayansi kimaslahi, hasa walio katika sekta ya umma. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman] [/FONT]
[/FONT]2.3 CHADEMA itafanya nini?
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]CHADEMA inaamini kuwa kuwekeza katika elimu ndio nyenzo kuu ya kukabiliana na matatizo yote yanayoikabili nchi yetu, ikiwemo umaskini. Tukifanikiwa kuwa na elimu bora tutakuwa tumejipatia silaha muhimu ya kukabiliana na maadui ujinga na maradhi na nyenzo muhimu ya kukuza uchumi imara na shirikishi. Hivyo basi, Serikali ya CHADEMA itatilia mkazo sana ubora wa elimu badala ya bora elimu. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]Katika kuinua ubora wa elimu CHADEMA inaamini kuwa [/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Elimu bora ni walimu bora. [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Hivyo basi, CHADEMA itaweka mkazo katika kuwapatia walimu mafunzo bora na ujira stahiki ili waweze kuwa na maarifa ya kutosha na kutulia mashuleni. Tutaweka mkazo katika kuwapatia watoto wa shule kiwango cha juu katika elimu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu. Mkazo utawekwa katika kuhakikisha kuwa shule na taasisi zote za elimu zinatoa elimu inayochochea fikra, udadisi, maarifa na ugunduzi na inayoibua vipaji. 18 [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]Lengo ni kuhakikisha kuwa kila hatua ya kielimu inamuwezesha mhitimu kujitegemea na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya nchi na jamii aliyomo. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]Katika kutekeleza haya, serikali ya CHADEMA itachukua hatua zifuatazo: [/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]2.3.1 Kuhusu Elimu ya Msingi na Sekondari [/FONT][/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]• [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Lengo la Serikali ya CHADEMA ni kubadili mfumo wa elimu ya msingi ili iweze kujitoshekeza kwa kuhakikisha kuwa wahitimu wanapata maarifa na stadi za maisha zitakazowawezesha kujitegemea kimaisha. Ili kufikia adhima hii, tutafanya mabadiliko yafuatayo: [/FONT]
[/FONT][FONT=Courier New,Courier New][FONT=Courier New,Courier New]o [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Muda wa elimu ya msingi utaongezwa kutoka miaka saba (7) hadi miaka kumi. Hii inamaanisha kuwa watoto watamaliza shule wakiwa na umri wa miaka 16/17, umri unaomwezesha kuanza maisha ya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na kimataifa [/FONT]
[/FONT][FONT=Courier New,Courier New][FONT=Courier New,Courier New]o [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Mtaala wa elimu ya msingi utapanuliwa kwa kuingiza muhtasari wa kidato cha kwanza na cha pili cha sasa kuwa sehemu ya elimu ya msingi [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Elimu ya Sekondari itabadilishwa kutoka miaka sita (6) hadi minne (4) kwa kuunganisha mihtasari ya kidato cha tatu,nne, tano na sita kuwa muhtasari mmoja wa elimu ya sekondari. Hii itasaidia sana kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata sifa za kujiunga na elimu ya sekondari. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Kuimarisha shule za umma ili zitoe elimu bora. Hili litafanywa kwa kuanzisha kampeni ya kujenga upya, kukarabati na kuzipatia shule zote nchini huduma muhimu za jamii hasa maji safi na umeme. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano ya utawala wa Serikali ya CHADEMA kila mtoto mwenye umri kati ya miaka 4 na 5 anahudhuria elimu ya awali kabla ya kuanza elimu ya msingi. Hii ni hatua muhimu kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa watoto waliohudhuria elimu ya awali huanza shule ya msingi wakiwa na msingi bora zaidi kuliko wale ambao hawakupitia elimu hiyo. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]19 [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Kuimarisha ufundishaji wa Lugha ya Kiingereza. Hili litafanywa kwa kuboresha mazingira mazuri ya kujifunzia lugha ya Kiingereza, ikiwemo kuzipatia shule walimu wenye ujuzi wa kufundisha lugha ya Kiingereza. Lengo likiwa ni kuhakikisha mwanafunzi anapoingia kidato cha pili anafahamu lugha ya kiingereza katika kuelewa, kuandika, kusema na kujieleza. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Kuimarisha ufundishwaji wa lugha ya Kiswahili. Pamoja na mkazo wa lugha ya Kiingereza, Serikali ya CHADEMA itaweka msisitizo wa pekee wa kuifahamu lugha ya Kiswahili pamoja na Kiingereza. Wanafunzi wa kitanzania ni lazima waimudu lugha yao ya taifa bila kujiona duni na wakati huo huo wakijiimarisha katika lugha ya Kiingereza. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Kuimarisha ufundishaji wa Sayansi na Hisabati kwa kuandaa walimu wa masomo hayo kwa uhakika, kujenga maabara za masomo hayo zenye vifaa vyote vya msingi pamoja na kemikali vinavyohitajika. Kwa upande wa somo la elimu viumbe, shule zitaweka utaratibu wa kufuga wanyama wadogo wadogo na kutunza mimea ya aina mbalimbali kwa ajili ya kufundishia. Ufundishaji wa Hisabati utaboreshwa ili uendane na misingi yake ambayo inazingatia sayansi ya kimantiki inayojengeka hatua kwa hatua ili kuondokana na tatizo la kukaririshwa, na hivyo kuinua kiwango cha kufaulu katika somo hili. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Kuinua ujira wa walimu kwa kuangalia upya viwango vyao vya mishahara na kuimarisha mazingira ya kazi na kimakazi. Katika kuboresha mishahara ya walimu, na wafanyakazi wengine wote katika sekta ya umma, tutaweka fomula ya kupandisha mishahara kwa kadri mfumuko wa bei na gharama za maisha zinavyopanda kwa kutumia mpango wa Scala Mobile, ambayo ndio inayotumika katika nchi nyingi duniani. Hii ndio kusema kila mara ambapo mfumuko wa bei utapanda na hivyo gharama za maisha kupanda, mshahara nao utapanda. Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanamudu gharama za maisha ya kawaida ili waweze kuwekeza muda na utaalamu wao katika kulitumikia taifa. Utaratibu huu pia utaondoa umuhimu wa migongano baina ya Serikali na vyama vya wafanyakazi. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]20 [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Sambamba na kuboresha mishahara ya wafanyakazi kwa ujumla, Serikali ya CHADEMA itarudisha posho ya mazingira magumu kwa walimu wanaofundisha maeneo magumu ya vijijini hasa katika mikoa inayotambulika kuwa ni ya pembezoni. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Kupitia upya mfumo na mtaala wa elimu ili: [/FONT]
[/FONT][FONT=Courier New,Courier New][FONT=Courier New,Courier New]o [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Kuhakikisha kuwa, pamoja na taaluma, wahitimu wanapata utaalamu na stadi sahihi za kujitegemea. Serikali ya CHADEMA itabadili kabisa mfumo wa sasa wa elimu ili kutoa fursa kwa vijana walio wengi wapate utaalamu na stadi za kujitegemea mapema. [/FONT]
[/FONT][FONT=Courier New,Courier New][FONT=Courier New,Courier New]o [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Kuhimiza ufundishwaji wa stadi za maisha na TEKINOHAMA kwa kuhakikisha kuwa matumizi ya teknolojia ya kisasa yanaanza mapema kwa wanafunzi wetu ili kuweza kuwaleta katika kiwango cha kimataifa cha elimu na ujuzi mapema inavyowezekana. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Kuingiza katika mitaala elimu ya uzazi na mahusiano kuwiana na umri wa wanafunzi. Ufundishwaji wa somo hili litawapatia vijana wa kike stadi za kuweza kujikinga na tatizo la kuanza ngono katika umri mdogo. Nchi nyingi zilizofanikiwa kupunguza au kumaliza tatizo la mimba utotoni ni zile zinazozingatia utolewaji wa elimu ya uzazi na mahusiano mashuleni. Elimu hii itazingatia uelewa wa kisayansi kuhusu maisha ya watu, lakini vile vile utazingatia umuhimu wa kulinda familia na maamuzi ya wazazi juu ya watoto wao kwa kuhakikisha elimu inayotolewa ni ile yenye kuzingatia heshima, kujiamini na kujilinda katika mahusiano ya kijinsia. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Elimu ya ngazi ya msingi na sekondari itagharamiwa na serikali kuu pamoja na serikali za mitaa. Lengo ni kuhakikisha kuwa elimu hii ya msingi kabisa inakuwa ni haki kwa kila mtoto wa Kitanzania na kiwango cha ubora kinalingana kwa nchi nzima. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Ili kukabiliana na wimbi la utoro na usinziaji darasani kwa sababu ya njaa miongoni mwa watoto wa shule, Serikali ya CHADEMA itarudisha utaratibu wa kutoa chakula cha mchana mashuleni, ambayo kitagharamiwa na serikali za halmashauri za miji na [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]21 [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]wilaya pamoja na serikali za mitaa na vijiji, kwani mtoto mwenye njaa au asiye na uhakika wa lishe hawezi kuzingatia elimu. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Tutazihuisha na kuanzisha shule mpya za kitaifa za bweni za sekondari. Shule hizi zitachukua wanafunzi wote waliofanya vizuri zaidi katika mitihani yao ya mwisho ya elimu ya msingi. Katika kila mkoa kutakuwa na angalau shule moja ya kitaifa itakayochukua wanafunzi kutoka katika mikoa mingine kwa lengo la kujenga utaifa na uzalendo miongoni mwa wanafunzi, na CHADEMA itarejesha utaratibu wa usafiri wa "Warrant" kwa wanafunzi hao ili kuondoa makali ya gharama za nauli kwa wazazi. Ni wazi kuwa utaratibu huu ni ghali, lakini kuua utaifa ni ghali zaidi! [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman] [/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]2.3.2 Kuhusu Elimu ya Juu na Vyuo Vikuu [/FONT][/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]CHADEMA kina lengo la kubadilisha na kuboresha sekta ya elimu ya juu ili iweze kuwa ya kisasa zaidi na inayomuandaa msomi wa Tanzania kushiriki katika kutumia elimu yake kuiletea maendeleo Tanzania na vile vile kumpa nyenzo za kisasa za kielimu kuweza kumuandaa na maisha ya ulimwengu wa kisasa. Lengo ni kuhakikisha kuwa elimu ya juu inapatikana kwa kila kijana wa Kitanzania anayetaka elimu hiyo, ni ya kisasa, na inamuandaa msomi kurudisha katika jamii ujuzi alioupata chuoni. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]Katika kupanua wigo na kuboresha elimu ya juu, Serikali ya CHADEMA itachukua hatua zifuatazo: [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Serikali ya CHADEMA itaanzisha mfuko wa elimu uitwao "Uhuru Scholarship Fund" kwa ajili ya kugharamia masomo katika chuo kikuu cha umma kwa wanafunzi wanaofaulu katika kiwango cha Daraja la I na II. Huu hautakuwa mkopo kwa kijana yeyote ila atalipiwa Chuo kwa kadiri ya kwamba anaendelea kufikia viwango vya juu vya kitaaluma kwa mujibu wa taratibu kwa muda wote atakaokuwa chuoni. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Kwa wanafunzi ambao watafaulu madaraja mengine (daraja la tatu na la nne) mfumo mpya wa kugharimia elimu ya juu utawekwa ili kuhakikisha kuwa gharama ya elimu ya juu haiwi kizuizi kwa kijana yeyote anayetaka elimu ya Chuo Kikuu. Katika [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]22 [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]kutimiza adhima hii, Serikali ya CHADEMA itahakikisha kila mkoa unaanzisha mifuko ya elimu ya Juu kwa ajili ya vijana wake, taasisi za dini na watu binafsi watawekewa utaratibu wa kisheria ili waweze kuanzisha mifuko ya elimu hasa inayotoa fedha zisizo mikopo (grants) kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kuzingatia vigezo mbalimbali. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu itavunjwa kutokana na uendeshaji mbovu, mfumo wake mbovu wa kisheria, na uongozi ambao umeshindwa kufanya elimu ya juu ipatikane kwa kila kijana na ambayo kutokana na uongozi usiofaa imeshindwa kukusanya madeni toka kwa wakopaji. Uchunguzi huru utafanyika wa fedha zote zilizotumika hadi hivi sasa na kuangalia kama waliopewa dhamana hawakutumia nafasi zao kujinufaisha. Miezi sita baada ya uchunguzi kufanyika ripoti itawekwa hadharani na mapendekezo yake kuanza kufanyiwa kazi mara moja. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Serikali ya CHADEMA itaunda chombo kipya cha utoaji na usimamizi wa mikopo ya elimu ya juu ambacho kitajulikana kama Mamlaka ya Taifa ya Kugharimia Elimu ya Juu (Tanzanian Higher Education Financing Authority - TAHEFA). Hiki ndicho kitakuwa ni chombo cha kifedha ambacho kitachukua majukumu yote ya Bodi ya Mikopo ya sasa chini ya muundo mpya na sheria mpya itakayoweka utaratibu mpya na wa kisasa kutoa mikopo ya elimu ya juu na kuhakikisha hakuna kijana wa Kitanzania anayetaka elimu ya juu ambaye ataikosa. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Vyuo vikuu vitapewa fursa ya kujiendesha, kuanzia utawala hadi kitaaluma bila kuingiliwa na serikali. Vyuo vikuu vitakuwa na fursa kamili ya kuchagua viongozi wao bila kuingiliwa na serikali. Kazi kuu ya serikali itakuwa ni kutunga sera za jumla za kuendeleza na kulinda ubora wa elimu ya juu, kuhakikisha rasilimali muhimu zinapatikana lakini uendeshaji wa vyuo vikuu utaachwa mikononi mwa mabaraza ya vyuo vikuu. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Serikali ya CHADEMA itarejesha na kuruhusu uwepo wa siasa katika vyuo vikuu vyote nchini kama shughuli ambazo ni nje ya masomo. Hii itasaidia kujenga uwanja wa demokrasia katika serikali za vyuo na vile vile itasaidia katika kuweka mazingira [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]23 [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]ambapo wasomi wetu wanaanza kujifunza mbinu na utendaji wa kisiasa katika mazingira ya elimu ili waweze kujifunza kuishi pamoja, kupingana kwa hoja na kujua jinsi ya kuvumiliana katika mazingira ya tofauti mbalimbali za kiitikadi, imani, na mtazamo. Uamuzi wa kufanya hivi utachukuliwa ndani ya siku mia moja za kwanza za utawala wa serikali ya CHADEMA. Utawekwa utaratibu mzuri ili shughuli za kisiasa zisiingiliane na zile za kitaaluma. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Ili kuchochea ubunifu na kuviweka vyuo vyetu vikuu katika Nyanja za kimataifa, Serikali ya CHADEMA itaanzisha [/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Baraza la Taifa la Utafiti (National Research Council) [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]ambalo pamoja na jukumu lake la kuratibu na kusimamia tafiti mbalimbali za kisayansi na teknolojia, kazi yake mojawapo itakuwa ni kutoa fedha kwa vyuo vikuu kwa njia ya kuvipatia uwezo vyuo hivyo kufanya tafiti mbalimbali ambazo matokeo yake yanakoleza matumizi ya sayansi na teknolojia nchini. Vile vile baraza hilo litasimamia mashindano ya changamoto za kisayansi ili kuchochea utafiti na ubunifu. Kila mwaka zawadi nono ya fedha taslimu itatolewa kwa Chuo Kikuu na wabunifu mbalimbali wa vitu ambavyo havijabuniwa sehemu nyingine duniani. Uundwaji wa baraza hili utaenda sambamba na uunganishwaji wa baadhi ya taasisi mbalimbali za utafiti nchini chini ya baraza hili moja huku zikiendelea kuwa huru kiutendaji, lakini zikiweza kushirikiana na kutegemeana katika kufanya utafiti na kusimamia matumizi ya tafiti hizo. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Ili kuchochea kasi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia, Serikali ya CHADEMA itabadilisha vyuo viwili vya sasa ili viwe viwe vyuo vikuu vya Teknolojia. Vyuo hivyo ni Mbeya Instute of Science and Techonology ili kiwe Mbeya University of Science and Technology – MUST pamoja na Chuo cha Ufundi Tanga kuwa Chuo Kikuu Kishiri cha MUST. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Pamoja na kutoa elimu ya Chuo Kikuu na Shahada, Serikali ya CHADEMA itaanzisha utaratibu wa kuwa na Vyuo Vya Kati vya Jumuiya ambavyo vitatoa elimu sawa na inayotolewa katika miaka miwili ya kwanza ya Chuo Kikuu. Lengo ni kuanza kutengeneza kundi la wasomi wa elimu ya kati ambao kutokana na sababu mbalimbali wasingeweza kupata elimu kamili ya chuo Kikuu. Vyuo hivi vya Jumuiya [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]24 [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman](Community Colleges) vitakuwa ni kiunganisha kati ya elimu ya Sekondari na Elimu ya Vyuo Vikuu na vitakuwa na uwezo wa kutoa Shahada Shirikishi (Associate Degrees). Mwanafunzi anayemaliza vyuo hivyo akitaka baadaye anaweza kuendelea na Elimu ya Chuo Kikuu katika taaluma yake kwa kuendeleza pale alipoachia na siyo kuanza kama mwanafunzi wa mwaka wa kwanza. Baadhi ya vyuo mbalimbali vya jamii vilivyopo sasa vitapandishwa ngazi na kuwa Vyuo Vikuu vya Jumuiya. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Serikali ya CHADEMA itafufua Huduma ya Maktaba kwa kuhakikisha kuwa kila Halmashauri ya Mji inakuwa na mfumo wa Huduma ya Maktaba. Maktaba hizi zitatakiwa kuwa ziwe kwenye bajeti zote za kwanza za Serikali ya CHADEMA na ufikapo mwaka wa pili asilimia 50 ya Halmashauri zote nchini ziwe zimekamilisha ujenzi wa Maktaba za kisasa. Utakapofika mwisho wa ngwe ya kwanza ya serikali ya CHADEMA, asilimia 100 ya Halmashauri zote ziwe na mtandao wa Huduma za kisasa za Maktaba. Viongozi wa kisiasa na jamii watahimizwa kuonesha mfano wa kupenda kujisomea ili kuchochea moyo wa kujisomea kwa vijana na watoto wetu. Ili kuonesha mfano na umuhimu wa kujisomea Rais Dr. Slaa atakuwa na utaratibu wa kusoma na watoto wetu katika mojawapo ya maktaba nchini mara kwa mara. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Ili kurudisha mori wa utumishi miongoni mwa wahadhiri wa vyuo vikuu, Serikali ya CHADEMA itahakikisha kuwa katika bajeti yake ya kwanza, madeni yote ya wanataaluma ya posho ya pango kwa wanaostahili yanalipwa na mpango wa kuboresha mafao ya uzeeni unatekelezwa kikamilifu. Tunataka wasomi wetu wasiwe na hofu ya maisha ya kila siku na wajikite kweli katika kutoa elimu, utafiti na ushauri wa kitaalam. [/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]• Ili kuendelea kutumia utaalamu na uzoefu wa maprofesa hapa nchini katika kuwanoa vijana wetu vyuo vikuu, Serikali ya CHADEMA itajadiliana na wanataaluma pamoja na Mabaraza ya Chuo na Senate zao kuona uwezekano wa kuongeza umri wa kustaafu kwa maprofesa kamili kutoka miaka 60 70, maadamu chuo husika kitakuwa kimejiridhisha kuwa maprofesa husika bado ni wataaluma kikamilifu. [/FONT]
[/FONT]


CUF: Ilani 2010-2015


ELIMU
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Kukua kwa uchumi wa kisasa wenye uwezo wa kuboresha maisha ya wananchi kunategemea wafanyakazi wenye ujuzi na maarifa. Kwa hakika utafiti unaonyesha kuwa kukua kwa uchumi wa taifa lolote kunashabihiana kwa karibu na kiwango cha kuwekeza katika sekta ya elimu. Hivi sasa dunia inashuhudia mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) ambayo yanaleta mageuzi makubwa ya uchumi na biashara ya kimataifa. Ni dhahiri hatutaweza kushindana kiuchumi na kibiashara katika ulimwengu tulionao leo iwapo hatutachukua hatua za makusudi kuhakikisha kuwa watu wetu wengi na hasa wanafunzi na vijana wote wanapata fursa kujifunza taaluma hii. [/FONT]
[/FONT]Elimu ya Chekechea
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Serikali ya CUF itawahamasisha wananchi-ikiwa ni pamoja na watu binafsi, taasisi za kidini, na mashirika yasiyo ya kiserikali kuwekeza kwenye nyanja hii chini ya utaratibu ufuatao: [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]- Serikali itashughulika na kuweka viwango vinavyotakiwa na usajili. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]- Serikali itawasaidia wananchi wenye nia ya kuanzisha shule za chekechea kwa kuwapatia viwanja vinavyotosheleza mahitaji kwa ajili ya kuzingatia viwango wakati wa ujenzi. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]- Kwa kuwa hivi sasa hakuna utaratibu wa kuwaandaa walimu wa chekechea kwenye vyuo vyetu, Serikali ya CUF itauanzisha ili watakaowekeza kwenye shule za chekechea wasiwe na shida ya kupata waalimu wenye sifa. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]- Shule za chekechea hazitatozwa kodi. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Elimu ya msingi [/FONT][/FONT]
Pamoja na kwamba Elimu yetu kwa ujumla imeendelea kukumbwa na matatizo mengi, lakini hali ni afadhali kidogo hivi sasa kuliko ilivyokuwa mwaka 2000. Mwaka 2000 kulikuwa na wastani wa watoto milioni nane (8.07) waliokuwa wanapaswa kuwa katika shule za msingi, lakini katika hao ilikuwa ni watoto milioni nne (4.37) tu ndio waliokuwa wanasoma katika shule zilizokuwepo, na waliobaki milioni tatu (3.69) hawakuwa wakisoma kwa sababu mbalimbali. Aidha ilikisiwa kuwa mpaka kufikia mwisho wa mwaka huo kungejitokeza kiasi cha watoto yatima laki nane (800,000) kutokana na wazazi wao kufariki kwa ugonjwa wa Ukimwi, na hivyo kuzidisha uwezekano wa ongezeko la watoto ambao wangekosa shule ya msingi.
Katika kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 CUF ililivalia njuga tatizo hili na kuifanya CCM ije juu na kudai kuwa CUF ilikuwa inasema uongo. Hata hivyo pamoja na kuja juu, baada ya chama hicho kurudi madarakani kilizikubali hoja za CUF, ikiwemo ya kufuta ada na michango yote mashuleni, na kuanzisha operesheni kubwa ya kupunguza idadi ya watoto wenye umri wa kwenda shule ambao walikuwa mitaani.
Pamoja na mafanikio haya kiasi yaliyokwisha patikana, sehemu kubwa ya watoto ambao wako mashuleni wanasoma katika mazingira magumu yenye matatizo makubwa matatu ikiwemo Msongamano kwenye madarasa, Njaa, na uhaba mkubwa wa waalimu na vifaa vya kufundishia. Kutokana na matatizo haya na mengine, uwezo wa darasani wa wanafunzi umeendelea kuwa wa chini.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Hali ilivyo sasa katika Sekta ya Elimu nchini; [/FONT][/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Ukosefu wa mipango ya kisera tangu mwaka 1961; [/FONT][/FONT]
Pamekuwepo utamaduni wa kutokuchukua hatua muafaka kwa wakati muafaka katika kukabiliana na changamoto nyingi zinazoikabili sekta hii ya elimu nchini. Ukosefu wa mipango ya kisera tangu awali hivi sasa taifa limejikuta likihitaji kufanya marekebisho makubwa katika elimu ya msingi ili kurejesha hali ya kawaida katika ngazi hiyo ya elimu.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Ubora wa kiwango cha elimu; [/FONT][/FONT]
Bado kiwango cha ubora ya elimu ya msingi inayotolewa nchini ni cha chini mno. Kwa wastani kila mwaka, zaidi ya nusu ya wanafunzi wote hawapati alama za kufaulu.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Watoto wenye njaa ni vigumu kufundishika; [/FONT][/FONT]
Tangu mwaka 2000 na kurejea tena mwaka 2005 Chama cha CUF imekuwa mstari wa mbele kusisitiza kuwa lazima uwepo utaratibu wa kuhakikisha kuwa watoto mashuleni wanapatiwa alau mlo mmoja kwa siku. Uzoefu unaonyesha wazi kuwa mototo mwenye njaa ni vigumu kufundishika. Lakini suala hili halikupewa umuhimu unaostahiki kutokana na ama kutofahamu au kutokuwa na dhamira ya dhati katika kupambana na adui ujinga, maradhi na umasikini,

na kumkomboa mtoto wa Tanzania kielimu. Wilaya zote zilizojaribu zimeshindwa kuendelea na kutoa chakula kwa wananfunzi kutokana na njaa kubwa inayolikabili taifa kila kukicha na maeneo mengine utaratibu huo umekuwa kero kubwa kwa wazazi/walezi wa watoto wasio na uwezo wa kumudu kuchangia madebe ya nafaka mashuleni.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Kazi ya ualimu ni ya kitaalamu; [/FONT][/FONT]
Mbali ya mwalimu kufundisha darasa zima katika ujumla wake, anatakiwa pia kumfuatilia kwa karibu mwanafunzi mmoja mmoja ili aweze kutoa msaada wa ziada kwa wale wenye kasi ndogo ya kujifunza (slow learners). Maslahi duni kwa walimu yamesababisha walimu wengi walazimike kujikita zaidi katika kuhangaikia kujikimu kuliko kuzingatia kanuni za ufundishaji. Pia malimbikizo ya mishahara kwa muda mrefu ni hali inayowamaliza walimu kwani wanajikuta wanapaswa kukaanga vitumbua na maandazi ili kujikimu na ukata mkubwa.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Elimu ya chekechea; [/FONT][/FONT]
Serikali haijawekeza kuhakikisha kuwa elimu ya chekechea inatolewa kwa watoto wote nchini. Mathalan, vyuo vya ualimu vya Serikali havina utaratibu wa kuandaa walimu wa chekechea na hivyo kusababisha waalimu wengi wa shule zilizopo kutokuwa na taaluma ipasayo. Aidha Serikali haitoi msaada wowote, mathalan wa viwanja vya ujenzi wa shule hizo kwa wananchi wenye nia ya kuanzisha mashule hayo, pamoja na kwamba inakataa kuzisajili nyingi ya shule zilizopo kwa kisingizio kuwa nyingi ziko katika majengo ya nyumba za kawaida za kuishi na hivyo kutofikia viwango vinavyotakiwa.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• [/FONT][/FONT][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Watoto wanaohitimu elimu ya msingi wengi kati yao hawajui kusoma na kuandika kiingereza na hata kiswahili japokuwa wanapelekwa sekondari; [/FONT][/FONT]
Lugha ya kufundishia imekuwa ni tatizo kubwa sana.Vigogo wa CCM wanawapeleka watoto wao shule za msingi zinazofundisha kwa kiingereza huku kiswahili kikiwa ni kama somo la kujitegemea. Watoto wa makabwela (mahohehahe) wanapelekwa katika shule zinatumia kiswahili kufundisha. Wakati haya yanatokea CCM wanajua kabisa kuwa mtoto yule anayepewa elimu ya msingi kwa kutumia kiswahili atapaswa kupewa elimu kwa kutumia kiingereza katika hatua zote za elimu zinazofuata ikiwa ni sekondari, vyuo na vyuo vikuu. Wanachofanya ni kuwadanganya watanzania kuwa wanakienzi kiswahili huku wao wakiwaandaa watoto wao kukabiliana na elimu za ngazi zinazofuata huku mtoto wa mtanzania wa kawaida akianza kujifunza upya kiingereza wakati akiwa na akili isiyokomaa na isiyoweza kujifunza vizuri lugha ngeni-ndiyo maana Taifa linaendelea kuzalisha wasomi wenye vyeti vya juu huku walikariri kila kitu darasani bila kuelewa kutokana na kutoielewa vizuri lugha ya kufundishia waliyobadilishiwa ghafla walipofika sekondari na ambayo hawakuanzishiwa mapema walipokuwa shule za msingi.
• Walimu wa shule za msingi wamezidi kuwa masikini wa kutupwa, misharaha yao inalingana na pesa ya posho ya siku moja anayopewa mbunge, walimu wamekuwa hawana hata nyumba za kuishi na hii inapelekea wakae maeneo ya mbali na shule na hivyo kuondoa ufanisi wa kazi zao shuleni. CCM waliahidi katika ilani yao ya uchaguzi ya mwaka 2005 kuwa chini ya mpango wa MKUKUTA awamu ya kwanza ambao unakamilika mwaka huu, kuwa ifikapo mwaka 2010 itajenga nyumba za walimu 22,000. mpaka sasa kuna nyumba kama 360 zilizojengwa kwa kiwango duni kabisa ambazo ni sawa na alilimia 1.6 ya asilimia 100 iliyoahidiwa.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Elimu kwa watoto wa kike(wasichana); [/FONT][/FONT]
Ukimuelimisha mwanamke ndio umeielimisha jamii nzima. Hili linatokana na ukweli kuwa wanawake wanajukumu la msingi la kimaumbile la ulezi wa familia. Kuporomoka kwa maadili

ya Taifa na ukosefu wa heshima na nidhamu na kujiingiza katika vitendo hatarishi kama utumiaji wa madawa ya kulevya, uhasherati, ukahaba, nakadharika kunatokana na kukosekana kwa kiasi kikubwa msingi wa awali wa malezi ya watoto. Watoto wa kike ndio walezi wa familia watarajiwa wenye nafasi ya kipekee katika familia. Kutokana na ugumu wa maisha wasichana walio wengi wamejikuta hawamalizi elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya juu kutokana na kupata ujauzito kutokana na ‘MAFATAKI' wakiwa mashuleni na hivyo kushindwa kuendelea na masomo. Sera ya kuwataka wasichana wanaopata mimba kuendelea na masomo na wenzao wengine darasa bado ni suala lenye utata linalohitaji umakini na uchambuzi wa kina kuangalia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na hilo.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Dira ya Mabadiliko ya CUF; [/FONT][/FONT]
Serikali ya CUF itachukua hatua zifuatazo kuhakikisha kuwa sekta ya elimu katika ngazi za msingi na chekechea inaboreshwa:
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Asilimia 25 ya Bajeti kila mwaka kutumika katika sekta ya ELIMU; [/FONT][/FONT]
Itatumia si chini ya asilimia 25 ya bajeti yake kila mwaka kuboresha sekta ya elimu kwa ujumla. Asilimia 50 ya bajeti yote ya elimu itaelekezwa kwenye kupanua na kuboresha elimu ya msingi. Hili litasaidia kukamilisha marekebisho yanayotakiwa katika ngazi hii ya elimu katika muda wa miaka mitano.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Kuhamasisha Ujenzi wa Shule binafsi na kufuta kodi katika vifaa vya elimu; [/FONT][/FONT]
Serikali itafanya juhudi kubwa kuwahamasisha watu binafsi, mashirika ya dini na mengine yasiyokuwa ya serikali, na makampuni ya biashara kujenga mashule zaidi ya msingi. Ili wananchi walio wengi waweze kumudu gharama za kusomeshea watoto wao kwenye mashule haya, Serikali haitayatoza kodi yeyote na itadhibiti viwango vya karo na michango vinavyotozwa. Aidha Serikali itavifanyia marekebisho makubwa viwango vya kodi zote zinatozwa kwenye vifaa vya elimu ili sekta ya elimu kwa ujumla inufaike na punguzo la gharama.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Marekebisho ya Mitaala; [/FONT][/FONT]
Serikali ya CUF itafanya marekebisho ya mitaala kwa kuzingatia zaidi umuhimu (Relevance) wa maudhui, muda wa kila somo, uwezo wa wanafunzi, na faida ya somo lenyewe:
- Mitaala italenga kukuza lugha ya kiingereza na hivyo kuwaongezea wanafunzi uwezo wa kumudu vizuri masomo ya sekondari.
- Shule zisizomilikiwa na serikali zitakuwa na uhuru wa kufundisha masomo ya ziada kama itakavyokubaliwa na bodi za shule zinazohusika.
- Itakuwa ni marufuku kwa wanafunzi wa shule za msingi kutumiwa kwa ajili ya maandamano ya aina yoyote zaidi ya yale yanayohusu siku ya mtoto duniani. Hii ina maana kwamba watoto wa shule za msingi hawatahusishwa na vitu kama mbio za mwenge, mapokezi ya wanasiasa, au kutumika katika shughuli za kuwachezea ngoma na kuwatumbuiza wanasiasa hao.
- Itakuwa ni marufuku kwa wanafunzi kujihusisha na aina yoyote ile ya biashara kwenye maeneo ya shule.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Matumizi ya kompyuta mashuleni; [/FONT][/FONT]
Serikali ya CUF itahakikisha kuwa Serikali inajiunga na mpango wa kimataifa wenye lengo la kumpatia kila mwanafunzi kompyuta (laptop) moja ya bei nafuu. Hatua kwa hatua shule

za msingi na sekondari zitaunganishwa na mtandao wa intaneti wanafunzi waanze mapema kutumia kompyuta na mtandao wa mawasiliano (internet).
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Lishe kwa wanafunzi; [/FONT][/FONT]
Utafiti unaonyesha kuwa watoto wenye njaa hawafundishiki, na huu ndio msimamo na mtazamo wa CUF siku zote. Serikali ya CUF kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya na kamati za shule itahakikisha kwamba watoto wote wa shule za msingi wanapata walau mlo mmoja kamili wa chakula kikuu kinachopatikana katika eneo husika, wakati wanapokuwa shuleni.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Elimu itatolewa bure na kupiga marufuku michango ya aina zote; [/FONT][/FONT]
Hili ni eneo ambalo limekuwa likilalamikiwa sana na wazazi. Michango ambayo haitabiriki imekuwa ni mingi na inavyoonekana siyo yote ambayo inachangishwa kwa nia njema. Serikali ya CUF itahakikisha kuwa huduma zote zinazotakiwa katika elimu ya msingi zitakuwa ni jukumu la serikali na kwa hivyo basi zitakuwa zinatolewa bure, mzazi atapaswa kumnunulia mtoto wake nguo za shule na madaftari tu. Vitabu na na vifaa vingine vitagharamiwa na serikali. Kamati za shule na mabaraza ya kata hayataruhusiwa kuirejeshe michango ya aina yoyote ile kwa mlango wa nyuma. Chini ya serikali ya CUF mchango wowote ule utakuwa ni suala la hiyari la muhusika.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Huduma za ukaguzi; [/FONT][/FONT]
Huduma za ukaguzi ambazo hivi sasa zimedorora kwa kiasi kikubwa zitahuishwa na kuimarishwa. Kila shule ni lazima ikaguliwe angalau mara moja kwa muhula.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Mishahara na Makazi ya walimu; [/FONT][/FONT]
Serikali ya CUF itaongeza mishahara ya walimu kama ilivyo kwa watumishi wote wa umma ili kukidhi mahitaji muhimu ya mwalimu wa shule ya msingi. Suala la makazi bora ya mwalimu litakuwa ni jukumu la msingi kabisa kwa serikali ya CUF ambalo litaanzisha mradi mkubwa wa ujenzi wa nyumba za walimu utakaosimamiwa na Serikali kwa haraka ndani ya miaka mitano ya kwanza ya uongozi wa nchi.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]ELIMU YA SEKONDARI [/FONT][/FONT]
Tanzania ni nchi iliyoachwa nyuma sana duniani katika maendeleo ya elimu ya sekondari, Chimbuko la Taifa letu kuwa nyuma mno katika elimu ya sekondari linaanzia katikati ya miaka ya sitini pale serikali ilipotangaza kuwa elimu ya darasani (formal education) haina maana sana, ati kwa kuwa ilikuwa inachukuwa miaka 20 hadi 30 mpaka matunda yake yaanze kuonekana na taifa lisingeweza kusubiri na hivyo mkazo ungeelekezwa kwenye elimu ya msingi na ya watu wazima, kutokana na msimamo huo athari zifuatazo zilijitokeza:
- Elimu haikuonekana tena kuwa ni haki kwa kila mtoto kujiendeleza hadi mwisho wa upeo wake.
- Dhana ya kufaulu kwa ajili ya kujiunga na masomo ya sekondari iliuawa na sehemu yake ikapandikizwa dhana ya kuchaguliwa.
- Watu na taasisi binafsi, hata waliokuwa na uwezo, walikatazwa kuwekeza kwenye elimu ya sekondari.
- Serikali haikujihangaisha kuwekeza katika mashule mapya ya sekondari ukiondoa mawili matatu ya mchepuo wa kilimo.
- Serikali ya awamu ya nne imejenga sekondari za kata bila maandalizi ya walimu wa kutosha na vifaa muhimu vya kufundishia kama vile mahabara na maktaba

- Hivi leo elimu ya sekondari imekuwa ghali mno kulingana na uwezo mdogo wa wananchi wengi walio masikini, japokuwa CCM inajisifia kuwa imeondoa ada na michango katika shule za sekondari ukweli unabakia palepale kuwa maelfu ya watoto wanashindwa kujiunga na sekondari kutokana na mzigo wa michango. Mathalani, ili mtoto ajiunge kidato cha kwanza anahitaji aende shule na vifaa au mchango wa dawati, mwalimu, mlinzi, jembe, panga, fyekeo, godoro, tahadhari na ada nakadharika hivi vyote vinaleta gharama kubwa, wazazi wangapi wanamudu elimu hii ambayo serikali ya CCM wanasema ni bure?
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Dira ya Mabadiliko ya CUF; [/FONT][/FONT]
Kama ilivyo kwa elimu ya msingi, elimu ya sekondari nayo inahitaji kupanuliwa na kuboreshwa. Ongezeko la bajeti ya elimu kwa ujumla litatupa uwezo wa kufanya marekebisho yanayohitajika. Serikali ya CUF inakusudia kutumia si chini ya asilimia 25 ya bajeti ya elimu kuimarisha na kuboresha elimu ya sekondari. Pamoja na kusudio hili Serikali itachukua hatua zifuatazo ili kuyafikia malengo haya:
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Elimu ya sekondari bure; [/FONT][/FONT]
Katika kuongeza nafasi za elimu ya sekondari Serikali ya CUF itahakikisha kuwa ada na michango yote katika ngazi hiyo ya elimu vinafutwa; na nafasi za kutosha katika elimu ya sekondari zinapatikana ili kila kijana aliyepata alama za kufaulu katika mtihani wa darasa la saba aweze kuendelea na masomo ya elimu ya sekondari, bila kikwazo chochote.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Kuhamasisha ujenzi wa shule binafsi; [/FONT][/FONT]
Serikali itafanya juhudi kubwa kuwahamasisha watu binafsi, mashirika ya dini na mengine yasiyokuwa ya kiserikali, na makampuni ya biashara kujenga mashule zaidi ya sekondari. Aidha Serikali itatoa kila aina ya msaada unaohitajika ili kufanikisha lengo hili ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo visivyo na sababu katika usajili wa shule binafsi. Ili wananchi walio wengi waweze kumudu gharama za kuwasomeshea watoto wao kwenye mashule haya, Serikali haitayatoza kodi yeyote.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Marekebisho ya mitaala; [/FONT][/FONT]
Serikali ya CUF itafanya marekebisho kwenye mitaala inayotumiwa na shule za sekondari ili pamoja na mambo mengine:
- Kupunguza idadi kubwa ya masomo ya lazima ambayo kwa kiasi fulani yanachangia mwelekeo uliopo hivi sasa wa wanafunzi kusoma kwa ajili ya kufaulu mitihani badala ya kuwajengea uwezo wa kukuza uelewa.
- Kuingiza elimu zaidi ya vitendo kuliko nadharia.
- Kuingiza somo la kompyuta na matumizi ya mtandao wa internet.
- Kuhamasisha wanafunzi kujifunza masomo ya hisabati na sayansi.
- Somo la uraia liboreshwe ili kuwajenga vijana katika utamaduni wa kuthamini haki za binadamu na kwa hivyo kuwa mstari wa mbele katika kutetea haki hizo.
- Ufundishwaji wa katiba ya nchi katika mashule ya sekondari itakuwa ni moja kati marekebisho ya mtaala yatakayopaswa kuingizwa mashuleni.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Huduma za ukaguzi; [/FONT][/FONT]
Kama ilivyo kwa shule za msingi, itakuwa ni lazima kwa shule za sekondari kukaguliwa angalau mara moja kwa muhula.

• Maslahi ya walimu na makazi bora;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Mishahara ya walimu na mazingira bora ya walimu wa shule za sekondari vitaboreshwa. Serikali ya CUF itahakikisha kuwa kila mwalimu wa shule ya sekondari ya umma anaishi katika nyumba bora itakayojengwa na serikali na iliyo eneo lake la kazi isipokuwa atakavyopenda mwenyewe kuishi eneo jingine bila kuathiri utendaji wa kazi yake. [/FONT]
[/FONT]ELIMU YA JUU
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Elimu ya juu kwa Taifa lolote ni muhimu kwa sababu inalenga katika kuwaandaa wataalamu mbali mbali kuja kukabidhiwa majukumu mbalimbali kwenye jamii. Kutokana na ukosefu wa mipango makini tangu awali katika kuboresha elimu kwa ujumla, Tanzania tumekuwa na udhaifu mkubwa katika suala zima la kuwaandaa wataalamu wetu. Siyo tu kwamba idadi ya wataalamu wanaoandaliwa ni wachache ikilinganishwa na mahitaji halisi, lakini pia ubora wa maandalizi yao hauridhishi. Waajiri wengi nchini, na hasa wale wa sekta binafsi wamekuwa na upendeleo wa wazi wa wahitimu walioandaliwa kwenye vyuo vya nje kuliko wale walioandaliwa nchini. Ni dhahiri kabisa kuwa kwa hali tuliyonayo nchi yetu itakwama katika juhudi za kuboresha uchumi na kujiletea maendeleo iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa mapema siyo kuongeza tu idadi ya wataalamu tunaowaandaa, lakini pia kuboresha utoaji wa taaluma katika taasisi zetu za elimu ya juu. [/FONT]
[/FONT]Hali halisi ilivyo sasa katika sekta ya elimu ya juu nchini;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Tanzania pamoja na kwamba ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu kuliko nchi zote za Afrika Mashariki, ndiyo ya mwisho kwa idadi ya wananchi wake wenye walau shahada moja. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Kumekuwa na wimbi kubwa la wahadhiri katika taasisi zetu za elimu ya juu kuondoka na kwenda vyuo vya nchi zingine za kiafrika kutokana na maslahi duni wanayopata hapa nchini. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Katika taasisi zetu nyingi za elimu ya juu huduma za kitafiti zinalegalega kwa kiasi kikubwa kutokana na serikali kushindwa kutenga fedha kwa shughuli hiyo. Huduma hizi pale ambapo zipo kwa kiasi kikubwa zinafadhiliwa na wahisani wa nje ambao mara nyingi wao ndiyo wanaoamua ni aina gani ya utafiti wanataka ufanywe. Hali hii imesababisha taifa kutonufaika kikamilifu na matokeo ya tafiti mbalimbali zinazofanyika kwenye taasisi hizi. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Bila kujali kwamba kimsingi Tanzania haijafikia wakati wa kuhitaji wanafunzi wetu wanaosoma katika taasisi za juu za elimu kuchangia gharama, Serikali ya CCM imeulazimisha utaratibu huo kutumika bila kuzingatia mizania ya faida na hasara zake kwa jamii yetu. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Kumekuwa na kulazimisha kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma katika taasisi za juu kusikoendana sanjari na uboreshaji wa huduma za msingi zinazohitajika. Matokeo yake ni kwamba mazingira ya wanafunzi wanaosoma miaka hii ni magumu kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Elimu ya juu imefanywa kama ni anasa na mzigo mkubwa kwa serikali, wanafunzi wa elimu ya juu wananyanyasika vya kutosha kutokana na utaratibu wa utoaji mikopo, wanafunzi wengi wanakopeshwa kwa madai ili waweze kuja kuitumikia nchi yao hali hii inaondoa uzalendo kwa Taifa tunalolilea kwani iwapo vijana hawathaminiwi na serikali hawatakuwa na mchango wowote kwa taifa baadaye. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Utoaji wa udhamini wa mikopo kwa madaraja; vigezo vya utoaji wa mikopo kwa wanafunzi hauzingatii hali halisi ya maisha na uwezo wa kifedha za wazazi wa wanafunzi, mathalani wale [/FONT]

[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]watoto waliosoma shule zisizo na walimu na wakapata daraja la tatu na la pili kwa wavulana na la tatu kwa wasichana ndio wanaonyimwa mikopo.Wale watoto wa vigogo wanaosoma shule nzuri na zenye walimu wa kutosha ambako ni rahisi kufaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza ndio CCM imewatengea mikopo. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Sehemu kubwa ya gharama za posho wakati wa mafunzo kwa vitendo yanayoenda kufanywa na mwanafunzi wa chuo kikuu yanagharamiwa na mzazi na mwanafunzi peke yake. Serikali haioni umuhimu wa mafunzo haya na ina mchango kidogo sana katika kuwezesha mafunzo bora ya vitendo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Wanafunzi wa vyuo vikuu leo wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa makazi ya kuishi, Serikali imeliacha suala hili kuwa mikononi mwa wanafunzi na wazazi. Kinachotokea ni kuwa wanafunzi wengi wanaishi kwenye baadhi ya nyumba duni za kupanga zilizoko katika maeneo ya mbali na vyuo vyao. Kwa mfano; kwa Dar es Salaam mwanafunzi kuishi Mbagala Chalambe na kusoma Chuo kikuu cha Dar es Salaam humchukua masaa 4 kwa siku kwenda na kurudi chuoni lakini pia hayo mazingira ya makazi ya Mbagala na kujisomea elimu ya juu ni mashaka makubwa. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Kiwango cha mkopo wanachopewa wanafunzi kwa ajili ya kujikimu ni shilingi 5,000/- kwa siku. Kiasi hiki ni kidogo na hakitoshelezi kumfanya mwanafunzi kuweza kulipia gharama za chakula, malazi, anunue madaftari, sabuni, nauli, mawasiliano, matibabu, nakadharika. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Kushindwa kuviunganisha vyuo vikuu ndani ya nchi na huduma ya intaneti ya uhakika pamoja na kuvipatia kompyuta za kutosha ni tatizo linaloathiri uharaka wa kujifunza na kuendana na karne ya sayansi na teknolojia. Utafiti uliofanywa na serikali ya wanafunzi ya chuo kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) mwaka 2007 ulibainisha kuwa katika chuo kikuu hicho sehemu ya mlimani kompyuta moja inatumiwa na wastani wa wanafuzi 400. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Dira ya Mabadiliko ya CUF; [/FONT][/FONT]
Pamoja na kwamba Serikali ya CUF imedhamiria kutumia si chini ya asilimia 25 ya bajeti yote yote ya elimu kuboresha elimu nchini, Serikali pia itachukua hatua zifuatazo kuhakikisha kuwa malengo haya yanatimizwa;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Ugharimiaji (uchangiaji) wa elimu ya juu; [/FONT][/FONT]
CUF inaamini kuwa Tanzania haijafikia wakati wa kuhitaji wanafunzi wa elimu ya juu kuchangia gharama. Serikali ya CUF itaweka utaratibu utakaowawezesha vijana wote wenye sifa na waliochaguliwa kujiunga katika chuo kikuu chochote ndani ya nchi kupata elimu ya juu bila vikwazo. Serikali ya CUF itagharamia mahitaji yote ya msingi ya mwanafunzi wa elimu ya juu bila MKOPO, ikiwa ni pamoja na kugharamia bima ya afya ya kila mwanafunzi. Uboreshaji wa eneo hili la elimu ya juu utafanyika hatua kwa hatua kwa kuzingatia hali halisi ya ukuaji wa uchumi na mahitajio mengine ya Taifa.
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Posho za kujikimu vyuoni na wakati wa mafunzo kwa vitendo; [/FONT][/FONT]
Serikali itakayoongozwa na CUF itatoa mchango wa kutosha na kuhakikisha kuwa wanafunzi wa elimu ya juu wanapatiwa posho zinazokidhi mahitaji wanapokuwa vyuoni na wanapokuwa katika mafunzo kwa vitendo, Serikali ya CUF itaongeza posho za kujikimu vyuoni kutoka shilingi 5,000/- ya sasa na kuwa kuanzia shilingi 10,000/- wawapo vyuoni na shilingi 15,000/- wawapo katika mafunzo kwa vitendo ili wawe na uwezo wa kusoma kwa utulivu na kujifunza mambo yote muhimu kwa ufasaha kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu.

• Matumizi ya intaneti;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Serikali ya CUF itatengeneza mtandao mzuri wa matumizi ya intaneti katika vyuo vikuu vyote vya Serikali na kuhakikisha kuwa panakuwa na kompyuta za kutosha kwa uwiano wa kompyuta moja wanafunzi wawili au kila mwanafunzi na laptop yake. Hali hii itawafanya wanafunzi wetu kujielimisha vizuri zaidi ili waendane na ushindani wa soko la taaluma na ajira kutoka nchi nyingine zilizoendelea duniani. [/FONT]
[/FONT]• Makazi ya wanafunzi wa elimu ya juu;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Serikali ya CUF itahakikisha kuwa kila chuo kikuu cha umma kinakuwa na makazi thabiti yatakayotosheleza wanafunzi wote. Makampuni makubwa ya ujenzi yatapewa tenda za kujenga mabweni ya kisasa ya wanafunzi yaliyounganishwa na mtandao wa intaneti katika kila chuo. Lengo la Serikali litakuwa kuwezesha kila mwanafunzi apate makazi rafiki kwa usomaji, isipokuwa kwa yule ambaye kwa sababu binafsi atataka kukaa mahali pengine. Aidha uanzishwaji wa miji mipya ya vyuo vikuu pembezoni mwa miji mikuu litazingatiwa ili kuandaa mazingira bora zaidi ya kujifunza na kuondokana na msongamano wa vyuo kuwa katikati ya miji. [/FONT]
[/FONT]• Mazingira ya kazi ya wahadhiri;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Serikali ya CUF itaandaa mpango maalum wa makazi na mishahara ya wahadhiri wa vyuo vikuu vyote vya umma nchini ambapo kila mhadhiri atapewa nyumba maalum na kulipwa mshahara unakidhi hali halisi ya maisha ya wakati husika. [/FONT]
[/FONT]• Uboreshaji wa mitaala;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Serikali kwa kushirikiana na wataalamu mbali mbali toka kwenye vyuo vinavyohusika itaanzisha programu ya kuifanyia mitaala inayotumika marekebisho ili ilenge zaidi kwenye kuandaa wahitimu walio tayari kwa kazi. [/FONT]
[/FONT]• Kuongeza nafasi zaidi za masomo ya Sayansi na Teknolojia;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Pamoja na kwamba Serikali ya CUF inakusudia kuipanua elimu ya juu nchini kwa ujumla, ongezeko la nafasi kwa fani za sayansi na teknolojia litapewa kipaumbele. Chini ya mkakati huu madaktari, mainjinia, wanasayansi na wataalamu wa kompyuta wengi zaidi wataandaliwa kila mwaka. Serikali pia itaendelea kuziunga mkono juhudi za watu binafsi, mashirika ya dini, na taasisi nyingine zenye malengo ya kuanzisha vyuo vikuu kwa ajili ya taaluma mbali mbali. [/FONT]
[/FONT]• Kuimarisha huduma za kitafiti;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Ukiondoa maslahi madogo, udhaifu mkubwa katika huduma za kitafiti ni sababu nyingine kubwa inayowafanya wataalamu mbali mbali kuzikimbia taasisi zetu za elimu ya juu. Serikali ya CUF itajitahidi kuziimarisha huduma hizi kwa kutoa fedha zaidi kwa ajili ya vifaa na masurufu. Aidha, itaanzisha kitengo maalumu cha uratibu wa kuzifanyia kazi tafiti/vumbuzi mbalimbali zinazopatika kutokana na jitihada zilizofanywa katika vyuo vyetu. [/FONT]
[/FONT]• Ujenzi wa miundombinu katika vyuo vikuu vyote;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Serikali ya CUF itatengeneza miundombinu ambayo itawezesha mazingira ya vyuo kuvutia wanafunzi wa ndani na nje ya nchi. Vifaa vya kitaalam na kiteknolojia, vitabu vya kutosha, kuboresha vyumba vya masomo, barabara, korido zenye mapaa juu yake kwenye kila njia zinazounganisha darasa na darasa, ofisi za wahadhiri, sehemu za chakula, mabweni na maeneo mengine. Mtandao huu utasaidia kurahisisha mawasiliano na kuendana na muda na vipindi madarasani kutosimama hasa nyakati za mvua ambapo wanafunzi na wahadhiri wengi hushindwa kufika madarasani. [/FONT]

[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Maktaba zenye uwezo mkubwa; [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Miaka 49 sasa tangu tujitawale hali ya maktaba zetu imekuwa duni, Serikali ya CUF itahakikisha kuwa maktaba zetu zinakuwa na uwezo mkubwa sawa na maktaba za nje, na kwa kutumia mawasiliano ya intaneti wanafunzi wa vyuo vyetu wataweza muda wote kutumia TEKNOHAMA itakayowaruhusu kusoma vitabu mbalimbali vilivyoko katika maktaba za vyuo vikubwa duniani kwa njia za ki-elektroniki. [/FONT]
[/FONT]ELIMU MAALUM KWA WALEMAVU
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Kwa bahati mbaya baadhi ya ndugu zetu wetu nchini ni walemavu na wana mahitaji ya elimu maalum yanayohitajika kuweza kujiendeleza. Kwa kawaida watoto au watu wenye ulemavu kwa ujumla wake huwa wana mahitaji maalumu ikiwemo ya uangalizi wa muda wote, hili upelekea kuwepo kwa gharama za kuwahudumia waangalizi. CUF tunaamini kuwa kuzisaidia familia zenye watoto wenye ulemavu kutasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na vikwazo vya kielimu wanavyopata watoto wenye ulemavu. [/FONT]
[/FONT]Hali ilivyo sasa;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Kukosekana kwa sera ya elimu inayojumuisha mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu kumesababisha idadi kubwa ya vijana wenye ulemavu kukosa fursa ya kupata elimu. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Huduma zilizoko katika taasisi mbalimbali za elimu kuanzia ngazi ya msingi, sekondari, na vyuo hazijazingatia mahitaji maalum ya walemavu. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Hali duni ya maisha ya wazazi ni kikwazo kwa watoto wenye ulemavu kupata elimu bora. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Ukosefu mkubwa wa vifaa vya kujifunzia ni kikwazo kwa watoto wenye ulemavu kupata elimu bora. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Ukosefu wa kupewa kipaumbele na kutozingatia kutenga bajeti ya kutosha ya taifa kusaidia watoto wenye ulemavu ni kikwazo. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Ulaghai wa kisiasa unaofanyika kwa baadhi ya walemavu na kusahau kusimamia haki za msingi za watu wenye ulemavu. [/FONT]
[/FONT][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Mazingira hatarishi ya maisha ya watu wenye ulemavu. [/FONT]
[/FONT]Dira ya Mabadiliko ya CUF;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Kwa kutambua umuhimu mkubwa wa kuwaendeleza watoto wenye ulemavu na kuwapunguzia wazazi mzigo wa ziada katika kuwahudumia, Serikali ya CUF itachukua hatua zifuatazo: [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Itazindua sera mpya ya elimu ambayo itakuwa imeyajumuisha kwa ukamilifu mahitaji maalum ya wanafunzi wenye ulemavu. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Itafanya marekebisho mbalimbali ya kiufundi kwenye taasisi mbalimbali za elimu ili kuondoa vikwazo mbalimbali vinavyowakwaza wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma katika taasisi hizo. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Mahitaji maalum ya kielimu kwa watoto wenye ulemavu yatajumuishwa katika mitaala ya vyuo vya waalimu ili kuongeza idadi ya waalimu wenye uwezo wa kutoa elimu kwa watoto wenye ulemavu. [/FONT]
[/FONT][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Serikali itagharamia kwa asilimia mia moja gharama zote zinazohusiana na masomo ya wanafunzi wenye ulemavu katika ngazi zote za elimu.[/FONT]

[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]ELIMU YA WATU WAZIMA [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Hivi sasa inakadiriwa kuwa asilimia 27.4 ya Watanzania wenye umri wa zaidi ya miaka 15 sawa na wananchi milioni 6.4 kati ya nguvukazi ya watu milioni 21 hawajui kusoma na kuandika. Sehemu kubwa ya watu wanaohesabiwa wanajua kusoma na kuandika, uelewa wao ni mdogo sana. Idadi hii ni kubwa mno katika nguvu kazi ya watu wasiozidi milioni 16. [/FONT]
[/FONT]Hali ilivyo sasa;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Kuupuza kwa muda mrefu umuhimu wa kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule wameandikishwa shule kumechangia sana katika kuongeza idadi ya vijana wanaoingia katika utu uzima ilhali hawajui kusoma na kuandika. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Kuanguka kwa ubora wa taaluma inayotolewa katika shule za msingi kumesababisha kundi kubwa la watoto kumaliza darasa la saba wakiwa na uwezo kidogo sana wa kusoma na kuandika. Wengi wa hawa hupoteza ujuzi huu baada ya miaka michache huko mitaani kwa sababu ya kutoweka kwa kiasi kikubwa kwa utamaduni wa kujisomea miongoni mwa wananchi. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Hivi sasa maktaba mbalimbali za Serikali zinatoza ada kwa wanaotaka huduma ya kujisomea. Hali hii inazidi kufifisha hamu ya wananchi kujifunza na kujiendeleza kielimu. [/FONT]
[/FONT][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Mkazo uliokuwepo katika miaka ya 70 kuhusu elimu ya watu wazima uliachiwa taratibu kufifia hadi hatimaye ukatoweka kabisa. Kwa hivi sasa fedha za bajeti ya elimu ya watu wazima zinatolewa lakini haziwanufaishi walengwa. [/FONT]
[/FONT]Dira ya Mabadiliko ya CUF;
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Serikali ya CUF itahuisha upya madarasa ya elimu ya watu wazima. Serikali itaandaa utaratibu utakaowezesha kila shule ya msingi iliyoko nchini kuendesha madarasa ya elimu ya watu wazima kila siku jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa. Kwa hali hii fedha za bajeti ya elimu ya watu wazima zitatumika ipasavyo na hivyo kuwanufaisha walengwa. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Serikali ya CUF itafuta ada zote zinazotozwa na maktaba za Serikali hivi sasa na kuhakikisha kuwa huduma katika maktaba hizi zinaboreshwa kwa kiwango cha juu ili kukidhi haja ya wananchi kujiendeleza kielimu. [/FONT]
[/FONT][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Maktaba zitaunganishwa na mtandao wa internet. [/FONT]
[/FONT]ELIMU YA UFUNDI
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Kati ya mambo ambayo Serikali ya CCM haijafanikiwa ni kuimarisha vyuo vya elimu ya ufundi. Nchi yoyote iliyowekeza katika elimu hii inajiweka katika mazingira mazuri ya kuleta maendeleo haraka kwani vijana wengi wanapata ujuzi na kujiajiri katika sekta binafsi au zisizo rasmi. [/FONT]
[/FONT]Dira ya Mabadiliko ya CUF
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book][FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]Elimu ya Ufundi kuwa nyenzo muhimu ya maisha ya vijana; [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Shule za ufundi zitaongezwa katika kila wilaya kwa kadri ambavyo uchumi wa nchi unavyokua na serikali itazisimamia ipasavyo. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Kila mtoto asiyejiunga shule ya sekondari lazima apate nafasi ya kusoma masomo ya ufundi ili ajijengee mazingira ya kupata ajira au kuwa na uwezo wa kujiajiri katika sekta binafsi. [/FONT]
[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]• Serikali itawapeleka walimu wengi zaidi katika mafunzo ya juu ya ufundi ili vyuo vya ufundi [/FONT]

[FONT=ITC Officina Sans Book,ITC Officina Sans Book]viwe na wataalam wa kutosha watakaokuwa wakiwafundisha wanafunzi kwa kuzingatia msisitizo wa mafunzo kwa vitendo kuliko nadharia. [/FONT]
[/FONT][/FONT]
[/FONT][/FONT]
[/FONT]
[/FONT]
[/FONT]
[/FONT]
[/FONT][/FONT][/FONT]
 
Nimeipenda hiyo ilani ya chadema. Hiyo ndio itamuondoa mtanzania katika maisha duni kielimu.
 
Back
Top Bottom