Jamani kama Intellectuals hebu tuweke ushabiki pembeni, tujadili haya madai ya madereva wetu

Lakini pia wanapotafuta haki za kuingia katika mfumo rasmi wa ajira, wakubaliane pia na vigezo vingine vya ajira rasmi kama vile minimum & maximum age ya kuwa employed na kustaafu. Kutekelezwa kwa ajira rasmi kukiwachuja baadhi ya madereva kwa kukosa sifa hizo za umri wasianze tena kupiga makelele
 
Mimi sio intellectual however i still have an opinion to air on this.

Ukitoa hilo la bima yote yanawezekana provided wapanda mabasi wako tayari kulipia hizo gharama za nyongeza kama mleta mada alivyogusia. Sasa basi tujikumbushe tu mwaka jana nauli zilivyoongezwa ni jinsi gani abiria walivyo chachamaa na hakuna exactly hoja kutoka kwa wafanyabiashara wa mabasi ni kiasi gani inabidi abiria wafidie hili kuweza timiza madai ya madereva im thinking na makonda pia.

Lakini hilo la bima ni hadithi kwanza huo mshahara sijui unatakiwa upande kwa kiasigani ili kuongeza huu wa sasa ambao aumudu maisha na kuwe na cha juu ili kuweza kulipia pension fund. Isitoshe kuna wafanya biashara wangapi ambao wako stable kwa sababu pension fund nyingi zinamuda wa kuchangia kabla ya kufikiriwa kimalipo.

The only way ili linawezekana kama wafanyakazi wenyewe wanaweza ridhia kujikatia bima wao wenyewe na kazi ikisimama wajue ni muda gani wanatakiwa kuchangia watafute mbinu za kuendelea kulipia, kwa sababu hakuna pension fund inayolipa bila ya muda fulani wa mchango wako sasa.

Apart from that ni madai ya msingi kabisa isipokuwa mazingira sidhani kama yanaruhusu utekelezaji.

Wewe una mtazamo kama wangu hapo kwa red

Ndo maana nikasema kama watalazimisha mazingira yaruhusu inamaana mzigo utamuelemea mteja ambaye ni abiria. Tuwe wawazi mfanyabiashara mwenye gari moja sijui 2 hawezi kulipa hizo stahiki jamani, tukitaka alipe basi nauli zipande tena kwa kiwango cha kufidia hizo gharama
 
We ndio unataka kuchanganya mambo, utaratibu wa sasa ni kuwa, mtu ukiagiza basi, ukimalizana na tra, unakwenda wizara ya kazi na ajira, kujaza form ya mkataba wa ajira baina ya tajiri na dreva, yote mliokubaliana yanakuwa kwenye mkataba, mnasaini mbeleya afisa kazi, unabandika na picha ya dreva husika, wanaipitisha na kugonga mihuri, wanampa tajiri anazipeleka SUMATRA, nao wakishazikagua ndio wanatoa, kibali cha route husika. Sasa cha ajabu kinachofanyika sasa ni kuwa tajiri anakwenda wizara ya ajira na picha ya mtu anayodai kuwa ndio atakuwa ni dreva wake anagongewa mihuri na mkataba unapita kimagumashi, anaupeleka sumatra anapewa route, bila kumuona huyo dreva physically!! Sasa unaposema kuwa madai yao yataongeza nauli sio kweli, na serikali hapa sio kwamba inapanga kiwango cha mshahara wao, kila sector, ina kiwango chake cha chini cha kulipa wafanyakazi ambacho serikali ilikipanga siku nyingi, wao wanataka waajiliwe wamechoka kuwa vibarua, na sheria za kazi zipi wazi, sifa za kibarua ni zipi, sasa mtu anaefanya kazi miaka 10,bado ni kibarua!! anakuja kwa baba yake ambaye ni serikali unamkana na kumwambia mi hayo hayanihusu kakae na boss wako, mtayamaliza!! siku zote bepali yeye ni ku maximise profit tu, Can u imagine dreva analipwa mshahara wake kwa kupitia mpesa, tg pesa?? hapo serikali kodi inapata vipi? matokeo yake ni kuzidi kuwaumiza hawa wafanyakazi wengine ambao wako kwenye ajira rasmi, kwani tax Base, inakuwa ni ile ile miaka nenda rudi, Wao wanataka ajira rasmi ambapo hataweza kufukuzwa kwa njia ya simu, na wengi wao wanalipwa posho na sio mishahara. Ila ugumu unakuwa wenye kusimamia haya mambo ndio hao hao wanyonyaji, kwani ukiwaajiri kwenye mifuko ya jamii lazima upeleke, nakufukuzana ovyo hakutakuwepo, Kuhusu bima hapa wanataka bima ya maisha, na sio bina ya afya kama unavyosema wewe, wewe fanya utafiti kidogo tafuta dreva wa hata roli wa zambia, kenya au rwanda akwambie maslahi yake, wa hapa kwetu utawaonea huruma, na tajiri hamtambui tingo, wewe kama una mtaka mtafute kwa pesa yako wewe!! utakuwa una mlipa kwa mileage yako!! Tuwe wakweli mchawi wa yote haya ni SERIKALI,. Watu wakose haki zao eti huku wengine tutapata shida!! wee umekula maharage ya wapi??? Mbona wenyewe kwenye ESCROW hawakuona kama watatuletea balaa kubwa kama hili la pesa yetu kupolomoka kiasi hiki!??? mtu adai ujira wake halali unatwambia atakuletea balaa!! hiyo miradi inayojengwa kila leo chini ya viwango huzioni impacts zake, we bwana vipi?!!

Mkuu umeongea vizuri, ila hapo kwa red naomba ufafanuzi kidogo, hiyo picha ya dereva tajiri anaitoa wapi? je anakuwa ni dereva kweli? kama kweli ni dereva, inakuwaje anampa wakati anajua utaratibu ukoje?

Pia hapo kwa blue unaposema nauli haziwezi kupanda, unaweza kutoa maelezo kidogo mtu mwenye bus moja kwa mfano atawezaje kumudu kulipa stahiki hizo bila nauli kupanda kwa abiria?
 
Lakini pia wanapotafuta haki za kuingia katika mfumo rasmi wa ajira, wakubaliane pia na vigezo vingine vya ajira rasmi kama vile minimum & maximum age ya kuwa employed na kustaafu. Kutekelezwa kwa ajira rasmi kukiwachuja baadhi ya madereva kwa kukosa sifa hizo za umri wasianze tena kupiga makelele

Exactly mkuu!

Madai yao ni kweli ni ya msingi, ila utekelezaji wake ni lazima kurasmisha kwanza ajira yao ndipo vigezo na masharti vizingatiwe. Na hii ina maana kama ulivyosema wengi wao watapoteza sifa hivyo watakuwa jobless
 
white wizard

Walau umetufungua zaidi kuhusu asili ya mzozo

Lakini bado kuna maswali hususan kuhusu daladala.

Ni kiasi gani daladala moja inatengeneza kwa mwezi na majukumu ya mfanyabiashara ya madeni kila mwisho wa mwezi (ata kama kanunua cash lazima hiyo hela iangaliwe in terms returns pia); kwa sababu ukisha muweka mtu permanent ina maana akiumwa pia unatakiwa umlipe sehemu ya mshahara wake (kama siko sahihi nisahihishwe). Je daladala wakati inatumia huyo temporary driver wakati huyu anatibiwa ina uwezo wa kujiendeshwa kwa faida? What about gari ikiaribika mwajiri anaweza lipa mshahara au hela yake ya mfukoni ndio inabidi iwe contingency pia?

How much costs/profit ratio iliyopo kwa fair za sasa (kwanza ni kiasi gani fair), maana hivi vitu vyote lazima vizingatiwe na kiasi gani ni mshahara wa sasa roughly kwa dereva, wao wanadhani ni kiasi gani kiwe kima cha chini after the owner has paid for their security funds and tax deductions to the new salary.

Mantki ni kujua kama inawezekana kwa nauli za sasa.

Uko sahihi mkuu, tukipata majibu ya maswali yako, tutaweza kujua kama wamiliki wa magari wana uwezo wa kulipa hayo madai bila kuhamishia mzigo kwa abiria

Unajua hili suala la mgomo wa madereva tunalichukulia kiushabiki zaidi kuliko kiuhalisia
 
kabla basi halijapewa leseni sumatra lazima ukatie comprehensive insurance na nakala ipelekwe sumatra bima hiyo inakinga gari dereva na abiria wanapodai bima hapa kuna tatizo limefichika kama sio haya mabasi kusajiliwa kama pikipiki.

kabla haujapewa leseni na sumatra mmiliki anapeleka mkataba wa dereva sumatra pamoja na picha ya dereva, haya malalamiko yanatokea wapi hasa?

Sheria gani inayolazimisha basi kukatiwa Comprehensive insurance cover? tusiandike kwa kudhani tafadhali .....kwanza hata Insurance company zenyewe nyingi zinakimbia mabasi yanayotaka comprehensive sababu ya risk yake ........
 
Comprehensive insurance inacover gari na abiria tu dereva hayumo, usiongelee kitu kama hukifahamu. Dereva hatambuliki kwenye bima ya gari kimkataba wa bima(insurance policy), ndio maana wanahitaji kuwa na bima zao wakiwa kazini, wao wanajua hivyo.

Well said Mkuu..!!
 
Nilishawahi kwenda kusajili trucks SUMATRA,moja ya masharti ni lazima upeleke mkataba wa kazi wa dereva uliopitishwa na kusainiwa wizara ya kazi! Na nilikwenda wizara ya kazi ni kitu kinachochukua si zaidi ya saa moja kama una documents zote. Taratibu na sheria zipo ila kuna watu hawafanyi kazi yao.

Mkuu ungefafanua kidogo hapo pekundu ungetusaidia wengi tusio na uelewa wa suala hili kwa undani
 
In short ni kuwa madereva wanataka utaratibu wa mtu kuwa na daladala moja au mbili uondolewe.
Ili kukidhi mahitaji yao inabidi kuwe na kampuni zenye magari mengi na mfumo madhubuti wa kuwasimamia. In the end hata mapato yao yale ya magumashi yatakosa mwanya, watalalamika tena.

Mimi naona wanajikaanga wenyewe.

Kuhusu kufukuzwa kazi kiholela, sidhani kama mmiliki anaweza kumfukuza mtu anayeheshimu masharti ya kazi na kulitunza gari.

Halafu,next mgomo kwenye hili utakuwa wa mahouse girl. Hawa pia ajira yao haijadalimishwa na hawalipiwi nssf. Kwahiyo kama unaunga mkono madereva, jiandae kuunga mkono mahousegirl pia.

Mi nakubaliana na wewe asilimia zote mkuu, ulichosema ni sahihi kabisa
 
Mkuu ungefafanua kidogo hapo pekundu ungetusaidia wengi tusio na uelewa wa suala hili kwa undani

Wamilki wanatumia mtu mwingine kwenye kusajili gari na anaendesha mwingine asie na mkataba. Sasa Sumatra na wizara husika wakishatoa vibali hawafuatilii nani anaendesha gari gani na mkataba gani.

Deiwaka wengi ndio wanaendesha haya magari,mikataba ni ya kukatia leseni za biashara tu!
 
kabla basi halijapewa leseni sumatra lazima ukatie comprehensive insurance na nakala ipelekwe sumatra bima hiyo inakinga gari dereva na abiria wanapodai bima hapa kuna tatizo limefichika kama sio haya mabasi kusajiliwa kama pikipiki.

kabla haujapewa leseni na sumatra mmiliki anapeleka mkataba wa dereva sumatra pamoja na picha ya dereva, haya malalamiko yanatokea wapi hasa?

Mkuu hivi vyote ni viini macho hakuna linalofanyiwa kazi hata moja
 
Mi nakubaliana na wewe asilimia zote mkuu, ulichosema ni sahihi kabisa

Lakin tukubali hizo gharama zote nssf, bima atakaye zilipa ni mteja wa mwisho ambaye ni abiri
Na tutegemee mabadiliko ya nauli
 
Wamilki wanatumia mtu mwingine kwenye kusajili gari na anaendesha mwingine asie na mkataba. Sasa Sumatra na wizara husika wakishatoa vibali hawafuatilii nani anaendesha gari gani na mkataba gani.

Deiwaka wengi ndio wanaendesha haya magari,mikataba ni ya kukatia leseni za biashara tu!

Asante nimekuelewa vizuri ndg

Ila huoni kama hata hao wanaotoa picha zao kutumika kwenye mikataba na wale deiwaka wanaokubali kuendesha bila kuwa na mkataba ni sehemu ya tatizo? tena kwa mtazamo wangu wao ndo chanzo cha tatizo badala ya kuwalalamikia Sumatra na wizara ya kazi?
 
Uko sahihi mkuu, tukipata majibu ya maswali yako, tutaweza kujua kama wamiliki wa magari wana uwezo wa kulipa hayo madai bila kuhamishia mzigo kwa abiria

Unajua hili suala la mgomo wa madereva tunalichukulia kiushabiki zaidi kuliko kiuhalisia
huwezi kununua basi la m100 ushindwe kumlipa dereva hata laki 2 kwa mwezi, nssf 50,000/mon. na nhif. asiyeweza kulipa atafute biashara nyingine
 
Lakin tukubali hizo gharama zote nssf, bima atakaye zilipa ni mteja wa mwisho ambaye ni abiri
Na tutegemee mabadiliko ya nauli

Exactly mkuu, hii kwa kweli ndo msingi wa hoja yangu. Tujue kabisa mwisho wa siku ni kupanda kwa nauli, halafu watu watalalamika tena
 
Back
Top Bottom