Jamani hawa ma last born watatupasua vichwa!

B' umejiuliza ile kwa ukweli kabisa nafasi yako wewe kwa yeye kua alivo sasa??
Maana kama video games ndo anapenda, kucheza mpira but responsibilities
hataki, mie naona hizo ndo zingekua weapons za kumweka katika mstari...

mi naona uko sawa but malezi ni muhimu ashaiii.
 
kitu muhimu sana hicho umeshauri,thanks for the thought.Siku zote wazazi tunatamani wanetu wakue wawe na mafanikio,tuna toil,tunaamka usiku kuwapeleka shule,tunafuatilia home work zao,kwa hiyo ina frustrate unapoona katoto wala hakaelewi yaani kanakuwa kapo kapo tu na ku take for granted.

Kila mzazi anapenda hilo mkuu na anapenda asifiwe kwa malezi na maendeleo ya mtoto
Hata wewe unajisijia faraja sana ujnapoona maendeleo ya mtoto
Ila inapokuwa tofauti na hapo inakuwa ni balaa sana
 
unakuta toto kubwa linalilia nyonyo na mama yake anampa, sasa kosa la nani hapo? mtoto au mama?
 
nina watoto wengi tu na wengine wamekwishamaliza chuo wanafanya kazi,i have never in my life picked a mjeledi na kumchapa mwanangu.
Utotoni wewe ulichapwa? unadhani ilikusaidia? maishani mwangu sijawahi kuchapwa na baba wala mama yangu(RIP wote wawili).Bakora nilikung'utwa shule,tena sa ingine zile za kupigwa vidole na mgongo wa rula na sidhani kama zilikuwa zinanisaidia lolote.I abhore violence ndo mana hata wanawake zangu huwa siwapigi,wakiniudhi nina namna yangu ya kuwaadhibu.

hapo red .. mh!!!!!!!!!!!!!

Kwa Lugha ya Malkia wanasema - "Tupa Fimbo mtoto aharibikiwe"
 
unakuta toto kubwa linalilia nyonyo na mama yake anampa, sasa kosa la nani hapo? mtoto au mama?
ahsante Zanta,angalau nimecheeeeeeeka,mama anakatuma dukani na kenyewe kanasema ..'mama nikirudi utanipa nyonyo?',na hao huwa ni ma last born ananyonya mpaka anaanza la kwanza mbuyuni.
 
Jaribu kumpiga marufuku hizo game au kumpangia muda wa kuangalia na kumpa conditions kwamba ataangalia baada ya kumaliza homework.
Pia ukae chini na mweleweshe kwamba Video games kwake sio muhimu sana kwa maisha yake na haitamsaidia huko mbeleni aendako.Mwambie atakuja kuwa na maisha yake peke yake ninyi wazazi wake hamtaishi naye maisha yake yote.
 
nina watoto wengi tu na wengine wamekwishamaliza chuo wanafanya kazi,i have never in my life picked a mjeledi na kumchapa mwanangu.
Utotoni wewe ulichapwa? unadhani ilikusaidia? maishani mwangu sijawahi kuchapwa na baba wala mama yangu(RIP wote wawili).Bakora nilikung'utwa shule,tena sa ingine zile za kupigwa vidole na mgongo wa rula na sidhani kama zilikuwa zinanisaidia lolote.I abhore violence ndo mana hata wanawake zangu huwa siwapigi,wakiniudhi nina namna yangu ya kuwaadhibu.

Nadhani kwa mtizamo wangu hapo ndipo lilipo kosa. Mimi nilichapwa na sijutii kuchapwa na wazazi wangu. Kwa sasa ingawa sijazaa wanangu lakini bado naamini katika nguvu ya kiboko kwa watoto wa umri flani (kuanzia miaka 5 hadi atakamoliza form six). Na watoto za dada na kaka zangu nawachapa inapostahili. Na kwangu mie naona inasaidia kuwanyoosha wanapokengeuka. Hata wa kwangu ntawachapa pia. Siamini kwamba viboko ni ukatili bali ni njia mojawapo ya kumkumbusha mtoto kuwa kakosea
 
mtoto umleavyo ndio akuavyo

badilika kitabia katika malezi ya huyo mtoto , unatakiwa mtoto umwelekeze nini anatakiwa kufanya kuanzia asubuhi hadi usiku akitaka kulala .. na naaamini malezi hayana tofauti kati ya first, mid na last born
 
hebu acha kutusingizia. Wewe umemlea kimayai mayai. Mie last born lakini enzi nipo shule wa kwanza kuwah, nafanya hmw on time. Naenda shule mwenyewe, chuo nimetafuta mwenyewe. Nimeenda mwenyewe. Nadhani mzazi yangu alikua ananifundisha kuwa independent. Hata kazi nilitafuta mwenyewe no ndg wa kusaidia, kujiendeleza kielimu mwenyewe. Kwa sasa naishi popote bila shida.
 
Bishanga nitamwambia sawa lakini umeshafanya home work,umefua sox na nk kama bado fanya kwanza mchezo na video game baadae.

kumnyima sio? yataka moyo,huwa unajisikiaje mwanao anapokuomba kitu tena kwa upole kabisa....mummy please naomba nicheze kidogo...don't you melt inside?
 
Baba Enock,do you believe in violence as a way of correcting a person?

Viboko sio violence kama wewe unavodai. Kwani hata hiyo approach mnayosuggest ya "kaa nae umwambie" wengine tunaweza sema unatumia psychological torture kwa kumtia hofu kuwa "ipo siku mzazi nitakufa utabaki peke yako and blah blah blah" so inategemea unavoidifine.
 
mimi ni last born,nikijilinganisha na dada zangu,mimi ndio niliokuwa msikivu na nilikuwa sio msemaji.maisha niliyokulia ni ya dhiki tupu,ila namshukuru mama yangu kwa malezi aliyonipa,sikuwa nadeka ila nimejifunza mengi tu.ila kwa kuwa anapenda hizo game,jambo la kwanza ni kumstopisha hizo game,bila ya kufanya school work,hakuna game wala tv.na umsimamie kidete.watoto wengine huwaogopa sana baba kuliko mama.
 
Wazazi wenzangu jamani hebu tujuzane,nyie ma last born wenu mna wa handle vipi.Wa kwangu yaani pasua kichwa,homework kufanya kwa mbinde,nguo ndo hivo anavaa zimejikunja,ukiingia chumbani mwake utadhani ni Kandahar,chakula ale sahani aache hapo,anachofikiria yeye ni video games,kucheza mpira,sinema,ili mradi basi tu. Toto kubwa la miaka 12 mpaka leo linalialia,yaani.
Na mamemba humu ambao na ninyi ni ma last born hebu nipeni experience ya makuzi yenu,mahusiano yenu na wazazi na kaka/dada zenu yalikuwaje wakati mnakua? pliz pliz tell me something.

heri ya wewe mkuu wako mkubwa walau mnaweza kuelewana. Wangu mie ni kadogo halafu kamejua kuwa ndo mtoto peke yake, yaani kila kitu tunaenda opposite
 
Mi kabla sijachangia nina maswali haya:
1. Huyo last born ni jinsia gani?
2. Wako watoto wangapi jumla katika familia?
3. Je kuna tofauti ya miaka mingapi kutoka kwa last but one?

Ahsante kwa ushirikiano...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom