Mwenda tezi na omo, marejeo ni ngamani

LionsGate

Senior Member
Jun 30, 2019
112
151
Khabarini wanajamvi.

Natumai mpo shuari.

Ifuatayo ni sehemu ndogo ya safari yangu ya maisha. Huwa nafikiria sana nijaaribu kuchangia walau kidogo katika kuelimishana na kupeana uzoefu kwenye mambo kadha wa kadha ya uhai wa kila siku.

Nonetheless, it is very hard to open up and disclose some really commpelling stuff about one's life.

Pamoja na nia njema mtu aweza kuwa nayo, lakini ni vigumu mno kufunguka pasina kuziamsha hisia na mara nyingi unayaamsha yaliyo lala na pia, unayazindua mengi uliyo dhani yalitoeka.

Kama nilivo tanguliza, hili jambo si jepesi. Lakini nishukuru mno wadau kadhaa waliyo nitia nguvu kwa kuyatoa yaliyo deep down their souls kwa kutuelimisha hata kama yaliwaachia majeraha daima. Uzito mungine ni namna ya kuyafikisha; niutumie mfumo upi? Mchakato mzima nauanzaje?

Kuna nukta kadhaa zinazo nihusu sintoweka kwenye huu uzi. Imani yangu ni kwamba baadhi zipo tiyari humu JF kwenye ID hii hii ya LionsGate na siyo mengi zaidi na utakapo taka kuwa na taswira yangu, nitakupa nukta kadhaa ili ujazie uelewa wako: ukiupitia uandishi wangu waweza jifunza jambo I hope.

My part of the story takes place in a segment of the late 80's to date.

Kwa wewe msomaji; utakapo liona jambo lisilo jikita katika huo muda, basi elewa nimelifanya kusudi. Mfano technology ya huo wakati, yaani between late 80's and 2000, music and lively habits of the era, comparing to what we know today.

Dhamira kubwa: Jielewe katika kila hatua ya uhai wako. Unalo lifanya leo, tambua kuwa hiyo ni akiba yako ya yatakayo kuathiri kesho kwa namna moja au nyingine; mbuzi hula sawa na urefu wa kamba yake.

Majina ya watu au ya miji, ni ubunifu wala hayana uhusiano na hii story.

Iliyopo hapo juu, ni simulizi iliyomo tukio linalo shabihiana mno na hili nitakalo zungumzia. Huyo ni mwanamke anae ongea. Mimi ambae ni character katika huo mkasa, nitarudi baadae kuwaletea ufafanuzi zaidi ili kila kitu kieleweke kadri tunavo endelea...

Endapo itakutokea ukawa na swali lolote, tafahdali uliza, nitakujibu. Na nisipo taka kujibu nitakujuza, na ikiwa jibu lipo katika sehemu zingine za simulizi basi hapo pia nitakuomba uifanye subira.

After Thanking the Almighty God...

This is in memory of my late beloved young sister who's been with us through the whole nine yards. Thank You!!

Many thanks to my dear Brother-In-Law, Monsieur le "Capitaine de Monte Negro," You are a Real French Black Knight and you deserve to have a Queen as a wife, my Sister!

I Can't be thankful enough to my Elder Sister Queen Cleopatra, the Icon of the family. I wonder why nobody thought about calling you 'Uhuru' the very same day you were born!! The name matches best with your character, girl!!

Many thanks to My Dear Rare Ex, and Up until Now My... and My... and so many My's of You for me, you are a Gem!

Last but not least, wholehearted thanks to my offsprings...

SEHEMU YA KWANZA




Niliolewa na mwanaume mpole sana miaka mitano iliyopita, yani nikisema mpole ni mpole mno, hakunifuatilia hata sikumoja, hakuniuliza nini wala nini, alinipa uhuru wa kutosha, nikiaga naenda mahali anasema nenda, hata kama narudi saa nane usiku, atanifuata tu maana hakuwa akipenda niendeshe gari usiku hata sikumoja, nikirudi na taxi, ananikemea sana...

Gari, mafuta niliwekewa kila safari, mahitaji yangu yote niliwekewa na k... Alinikuta sawa toka college na hata kazi sikuwa nayo, akanitafutia kazi tuu baada ya ndoa, nikapata, na nikaanza.

Kuna kipindi akawa ananiambia niache gari kwani hujiskia fakhari mno kutembea na mimi kwenye gari, kifupi alinijali sana, sana sana. Sasa kule kujali yake ndio ninayo ikumbuka hadi leo hii najutiya! Kina mama, dada zangu, wanandoa, kama una mume anae kujali, mshikilie vizuri sana.


Si kwamba alikuwa hajui kuikuna nazi! Fundi haswa na kila mara mbunifu! Sijawahi kumfumania hata mara moja, na kadhalika, alikuwa muwazi sana kwangu! Kazini kwao walinijua, alipenda kunitambulisha kwa kila mtu. Kuna kipindi alienda East Scotland kikazi, ikawa kila mwezi au zaidi, huniruhusu nauli kwenye bank account naenda, siku zingine anakuja yeye hadi aliporudishwa mahala tulipo kuwa.

Huo ni upendo usiyo na kifani. Kwa wengi mno, wangeipata walau robo ya utulivu niliyo kuwa nao, wangeinyanyuwa milima kwa mkono mmoja, kwani angeweza kubadili na kuzikidhi haja zake huko huko tena kwa kujinafasi.

Nilichofaidi kwake tuu, ni kwamba nilikwenda nae kwetu tukiwa likizo Africa, akapaona palivyo, akasema atanisaidia kupaboresha; aliivunja nyumba yetu na kumjengea mama yangu kijumba kidogo cha kumtosha mwenyewe, akamuwekea na bajeti ya kila mwaka kwa kuboresha mashamba na kilimo, hadi leo namkumbuka! Kwao yeye kazaliwa mwana wa pekee, mama yake alifariki wakati amemzaa tuu. Na akasema kuwa anamlea mama yangu kama mama yake, hana dada wala kaka wa kuzaliwa tumbo moja, wako wa ndugu wengine kwa kuwa wazazi wake walikuwa na familia kubwa tuu...

NATHIBITISHA KWA KINYWA CHANGU, KIRAFIKI ULICHO NACHO CHAWEZA KUKUBADILI MSIMAMO NA KUSHUSHA AU KUZIDISHA HESHIMA YAKO! KUWA MAKINI NA LINDA UTU WAKO.

Nikiwa na rafiki zangu tuliandaa mtoko kwenda Braxtown kutembea lakini tukapanga tusiwaambie waume zetu ukweli, tudanganye maana wengi wasingekubali. Tukapanga safari, tukaongopa kwamba ni safari za kikazi.

Mume wangu hakuwa akinifuatilia kazini kabisa. Kajiajiri, kwa hiyo anaweza kuondoka muda wowote bila swali, basi akasema nitakufuata, sintowasumbua nitakaa hotelini tuu, wewe ukimaliza kikao chenu utanikuta chumbani.

Nakumbuka siku hiyo nilichukia mno yaani sana! Pale nilimuonesha nilichukia nikamwambia hapana tunalala wawili wawili, akasema basi sawa nenda...

Alinipa hela ya kutosha nikaenda na rafiki zangu tulikuwa kundi ya watu wanne tuu, watatu tumeolewa ila mmoja bado, basi kufika Braxtown, tulijipa burudani sana takriban siku tatu.

Nikiwa kule, nikakutana na kijana mmoja ambae alinitamani sana. Basi alikuwa kaja na marafiki zake wengine nafikiri nao waliijiya hiyo burudani. Sasa kila jioni, tukiingia ukumbi wa chakula, tunakutana nae, akaanza kunitongoza nikagoma! Hapo akamfuata mmoja miongoni mwa hao mafiki zangu akaomba namba akapewa. Nashangaa usiku napigiwa simu, nikakataa.

Rafiki zangu walinisisitiza sana nimkubali, kijana mzuri, katimiza vigezo kweli! Nikasema hapana, ninae mume wangu, simtaki huyu! Siku naondoka akaja na electronic diary moja nzuri sana kwenye gari yetu, akaniambia:

"Unaondoka?"
Nikasema: "ndio."
"Unataka nini?"

Kwa sauti ya uthubutu nikamuuliza.

"Mrembo, tafadhali usiwi mkakamavu namna hii!" Kwa tabasamu na sauti tulivu mno! Akanipa diary yake niichukue kama kumbukumbu, nikaikataa!

Nilipofika mjini, mume wangu alinifuata, akanipokea akaniambia: "Mke wangu, toka uende huko, nimekuwa mpweke sana!"

Wakati wote huo, sikujua kama alipiga simu kazini kudadisi zaidi... kumbe alilipata jibu kinyume na nilicho mwambia hapo awali kama sababu na madhumuni ya safari hiyo; Kazini kwangu, nimeumwa!

Japo ukweli aliujua, hajanipigia hata sim nikiwa Braxtown, nashangaa mwanaume huyu hakuniuliza chochote yu mkimya tuu, ila niliona amebadilika kwa kuwa tulipokuwa kwenye gari, alikuwa ananiangalia sana! Kila nikifanya kama kumtazama na mimi, anageuka na kuangalia pembeni...


Nikamuuliza: "Vipi?"
Akasema: "Nimekukumbuka sana tuu mke wangu."

Tukafika nyumbani, nikaoga, nilikuwa nimechoka. Usiku ulipo wadia, mume akaniomba mambo, nikawa nimechoka, nikamkatalia sikuikidhi haja yake. Hajajibu wala kusema chochote cha kuhoji, akasema:

"Pole mama", akageuka na kulala na mimi nikalala. Asubuhi akaniambia tena: "Naomba mke wangu! Sina hali!" Nikamwambia nachelewa kazini, nitampa jioni, akasema sawa. Tukaondoka, kila mtu na gari yake.

Nilipofika kazini, HR hajaniambia chochote kama aliwasiliana na mume wangu, aliniuliza tu, "umepona?" Nikasema ndio akasema karibu tena, basi kazi ikaendelea...

Baada ya siku nne tu akaja yule kaka wa Braxtown, hadi kwangu na alielekezwa na mmoja wa hao ma best zangu! Alipofika nilishangaa nikamuuliza nini kimemleta pale, akasema tuongee kwenye gari. Basi nikaingia, ili nikazie na nikatishe misuguano kabisa!

Jamani ni kama nilirogwa naweza sema kweli tena, kama hamtaamini basi, ila naamini ALINIROGA HUYU KAKA, maana alivyokuwa akiongea na alivo jiweka njema, kwa suruwali nyepesi yenye kudhihirisha uume wake ulivo fura kwa hasira, hisia zikanijaa na nikaanza kulowa! Na alizidi kunipandishia mzuka kupita kiasi, maneno yakiniingia bila ukingo wowote kama awali, sasa nikaanza kuona uzuri wake, nikaanza kumshabihisha na mume wangu, naona huyu kijana kweli amemzidi kila kitu:

Mwanaume wangu; anayo madini na nondo zake ambazo kila muda huwa naipata tabu kwa wazo la kuibiwa mume, pale tuu mwanamke akimsogelea. Kama nilivo sema mwanzo, sijawahi kumfumania kila nikimpeleleza kutokana na wasiwasi ya namna anavo wavutia wanawake.

Nilikuwa na mazoea mara kwa mara ya kumuangalia, anapokuwa amelala. Ninapo kata na siyo kwamba nimechoka, lazima nimshukuru Bwana kwa kunipa daraja ya kuwa na kiumbe wa thamani pamoja na mapungufu niliyo kuwa nayo.

Kijana: Pale alipo nitongoza nikagoma, na hata pale alipo kuja kuniaga nikamuonesha msimamo wa kujiamini kwa majibu mkato ili niweke uzio upande wangu, sababu ni vile alikuwa na mvuto, yaani mwonekano wa kushawishi usiyo wa kawaida: mrefu. Umbo lililo tukuka.

Huwa najiuliza: Wanawake tunataka nini?

Mimi nilipumbazika pale niliiondowa picha ya mwanaume wangu akilini, nikaweka ya huyu kijana; Hilo tuu, busara haijazingatiwa na yafuatayo yakanivaa:

Hamu japo imenikaba, ilibidi nikajishauwa kidogo, akasema tuagane. Gari yake ilikuwa ya viyoo vya giza kweli. Hata mtu achungulie kwa nje, atajiona yeye ila ndani hatoona kitu. Akanivuta na kunipa busu ndefuuu! Aisee, nilihisi kama nimepigwa na umeme, nikatetemeka, moyo ukaenda mbio sana, kijasho kikanitoka!

Hapo tena sikuweza tena kuzuia lolote! Nimedata kwa ufupi! Akapitisha mikono yake kwenye mapaja yangu, kapandisha hadi kwenye tuta la shari... kisha nae akaanza kulifinya finya! Niliendelea kulowa, isingekuwa maeneo ya kazi, mkate angeun'gata siku ile ile bila usumbufu na wala nisingeweza kukataa!

Nae akawa yu tayari sana akaniomba nimsikilizie homa yake ... ni kweli nilipomshika shika tuu kitaalamu, homa ikashuka, nikamfuta akaondoka! Tokea pale nilipo ukomalia mtandao wake, nilianza kupagawa kupita maelezo! Taswira hiyo ikajichora pasina kufutika kwenye ubongo wangu.

KUMBUKENI CHA KWANZA MUME WANGU KUGUNDUA, NI PALE TUU NILIPO MKATALIA KWENDA NAE BRAXTOWN PILI, KUWA SINIPO MWAMINIFU: ILIKUWA NI KUSEMA NAENDA HUKO KIKAZI, WAKATI KAZINI HAWAJUI NA NILIAGA NAUMWA... HAJASEMA KITU JAPO TIYARI KAISHA ELEWA JAMBO.

Niliporudi nyumbani nikitoka huko, mume akanianzia mitihani: akasema anaomba tutumie gari moja tu, nyingine ibaki nyumbani. Na kadhalika, atakuwa ananipeleka kisha ananirudisha. Nilihamaki sana na nikamwambia sitaki, maana ya kuwa namagari mawili nini? Kwa nini kalinunuwa wakati alijua anaweza kunipitia?

Akasema, " Nimeamua tuu mke wangu, nini shida kwani, wewe nakupeleka nakurudisha kama una mishe mishe zako nitakupeleka nakuacha ufanye mimi naondoka badae nakufuata? Nikakataa, akasema sawa...

MTAKA NYINGI NASABA, HUMFIKA MWINGI MSIBA.

Maelezo kidogo: Nimezaliwa na vipini vya ajabu. Nimeolewa hadi najifungua mtoto wa kwanza, sijajielewa kwenye hayo maumbile. Iliwahi nitokea sikuona lolote ndani ya miezi mitatu nimejifunguwa, nikajihesabu mja mzito. Nikamjulisha mume lakini sote tukawa kama wenye kuchanganyikiwa; inakuaje na mtoto ndo bado ana miezi miwili na siku chache? Haijatosha hata itifaki zinazo husu kutohimili mimba zilizingatiwa ili tusifuatishi haraka...

Tukajielekeza hospitali ili tuijuwe hali halisi na tujuwe tunaendaje. Matokeo hamna mimba wala tatizo lolote la ki afya, tukaambiwa ni jambo linatokea, tujiskie huru, tusiwi na wasiwasi wowote, kwani hata mfumo wa kuzuia uzazi wa haraka bado una muda labda tuamue kuuondoa kabla ya miaka mitatu.

Nasaha:

NGUVU ULIYO ZAWADIWA NA MUUMBA, TAFADHALI ITUMIE KWENYE MAADILI YENYE MALENGO KWA JAMII, NA KAMWE USIITUMII KI U BINAFSI, AU KWA KUMUANGAMIZA YEYOTE YULE, HASA YULE ALIE FAULU KUIZINDUWA NA KUILINDA KWAKO.

Unatakiwa ujipe majibu chanya kwenye masuali yafuatayo:

  • Hizi nguvu, kwa nini mimi na siyo yule?
  • Mvumbuzi sijawa mi mwenyewe. Kwanini yule?

Ukibugi nilivo bugi mimi, inakula kwako.

Tafadhali endelea:

Mungu hakika ni mbora katika uumbaji wake. Kila mmoja wetu kapewa kitu au vitu vya kipekee kwenye maumbile yake. Kuna mtu alie jifunza kuvitumiya, na kuna asie weza juwa hata ni vya maana kwake japo anaviona, hadi pale atakapo kutana na mvumbuzi wa hiyo nguvu aliyo nayo, halafu nyote mkaijulia hapo hapo na ikawafaidi.

Hivi ndivo NGUVU zangu zilivo ibuka:

Kwenye uso wa mbele wa hekalu yangu kuna vitone vitatu vyeupe. Vipo kimoja chini ya karanga, na viwili pande zote mbili kwa ndani upande wa kati wa kizingiti. Kwa ufupi nyoka akiingia pangoni, lazima vitamkwaruza kichwa hadi ubavuni.

Kutokana na vile muonekano wa vitone unavyo jibadili, mara niviite vitone, mara vidoti nak... hapo vilikuwa vidogo sana na si rahisi uvione, ila mmiliki najuwa vilipo. Lakini huyu bwana aliweza kuviona na kunijulisha kaviona, nashangaa, halafu namjibu nikicheka:

"Yaani sijaona mpekuzi kama wewe! Ulitakiwa ukate nyasi tuu, siyo kufunuwa funuwa na kupekuwa vya uvunguni! Angalia uso wake unavo mcheza! Haya! Vibunie mpango sasa!"

"Mama, kosa langu nini? Huoni nimeupindisha na mgogo kabisa? sharti nimeeneza! Nyie mna tabia za kuficha vitamu huko!"

Mume wangu ni mpenda bustani fupi;

"Kandanda hainogi kwenye uwanja bila nyasi, sasa kukiwa na vijinundu-nundu vya nyembe ni miyeyusho mtupu!" (yeye huyo).

Inakuwa mfano wa nywele zake za baada ya siku kadhaa akiwa alisheviwa. Hapendi nifanye mimi nisimuharibie. Hata akisafiri muda mrefu, siwezi thubutu kupalilia, na yeye hivo hivo ananiletea kazi.

Vile muda unavo enda, vitone vikaendelea kutanua, yeye sasa mkaguzi, na ilikuwa pindi alipo rejea baada ya mwezi:

"Asali wangu, nikwambie kitu? Kama siyo hatari ki afya, naomba unibakishie hivi hivi! Hizi mavitu zimekaa poa, aiseeeee!" Anacheka...

Nikadhani anamaanisha sasa anautaka msitu! Kabla sijasema lolote, akaendelea:

"Vidoti vyako mbona vimeongezekaaa... Lakini navipenda kweliii... hasa namna vilivyo jipanga... na vimebadili raaangiii... Amen!"

Hapo kama anaigiza sauti ya padre wa kanisa katoliki. Teh!

Kwako msomaji, jaribu na wewe kwa sauti ya juu...

Tukiwa popote pale akijiskia, huwa anaurudi huo wimbo wake kwa mlunzi, au anaifanya ishara ya kupuliza filimbi ya bomba na kunikonyeza!

Kweli nilipo angalia, nikaona vimetanua, na rangi imekuwa kahawiya. Vikageuka sasa "vidoti" tunapo viongelea...

Kuna muda vilianza sasa kuwasha, hadi nakosa raha. Nikiwa ndani nipo nae tukiongea, najikuta nimeanza kujikuna kunako! Kama kawaida yake, kila kitu huzaa matani:

"Mwanaumeee! Jembeee! Hivyo siyo vidoti tena! Ni Burudaaaniiii! Kile kifurushi kutoka kwa mama bila shaka kulikuwemo zawadi yako: gimbi mbili na muhogo! Anasema hayo akichekelea "kiek kiek kiek" ndani ya mashavu yake hadi napatwa na hasira.

"Wewe! Wacha dhihaka huenda hii ni saratani! Mi mwanaume mwenzio? Sawa. Magimbi na muhogo chukuwa wewe uiwinde na uifaidi hiyo burudani mara mbili! Shwain zako! Kero imekuwa burudani lini?"

"Wanaume si ndo huwa hatunaga aibu kujikuna kunako hata hadharani? Yamekupataje? Kiek kiek kiekkhkhkh

Bila matani:

" Lakini kama ulikuwa hujui: katika magonjwa yanayo tokana na uzinzi, yanayo julikana mjini kama Burudani ni maradhi ya ngozi yanayo kuja kama vipere kwenye fimbo; Muathirika huskiya raha sana sana anapo vikuna hadi anarembuwa. Anajichubua bila kutambua."

"Weee! Sijatambua hata hivi vidude nilivyo navyo ni upuuzi gani, na wala sirembuwi sasa thubutu uzoe huko halafu unitee hapa, ndo utajuwa hujui!"

"Haki ya nani?! Ikiwa wewe je? Viwili vikikutana, ni salam na ujumbe, na zawadi kupeana! Usintishi! Burudaniiiii! Kiek kiek kiek!

"Tujipange ratiba ili tumuone daktari wa ngozi, sawa mama?"

Ikawa hivo muda mrefu tunakwenda hospitali kwa muendelezo wa vipimo na tujuwe vile hali inavo endelea. Ila pamoja na vipimo vyote tulivyo fanya, haikuwa saratani japo tu mishipa twingi tumo, wala siyo hata vijipere viitwavyo Syringomas, ambavyo havina mishipa yoyote, ni kama vipere tuu, vinavyo patikana kwenye ngozi kupitia tundu za jasho, wala havina tatizo. Lakini havileti muwasho kama nilivyo kuwa navyo.

Nikapewa dawa ya mafuta ili niwe napakaa usiku, kwa kusitisha miwasho. Ilifana na hata ilipo isha baada ya siku kumi, sijairudilia hiyo tiba hadi tukavisahau. Na vikasita kutanuka vilipo fikia kiwango cha punje ya mtama na vikawa vyeusi tiiii na mn'gao wa shanga nyeusi na karundu kaduchu mno, utadhani ni vya kubandika, yaani kama pambo tuu.

Mara ya mwisho, tulipo kwenda kukagulisha tena, daktari katupatia kartasi za matokeo ya utafiti. Lakini vyote wala tusingeelewa chochote kutokana na lugha ya kitaalam iliyomo, na tena siyo fani yangu. Lakini akatuelezea kwa uchache tuu ili tuelewe:

Inaonekana kuwa hizo punje zimejijengea ganda kwa nje mfano wa ganda la kunde, ila gumu kulikoni. Na ndiyo maana ya huo mn'gao. Kwa ndani, kunaonekana uhai: tumishipa kapilari na neva, hata uzi wa buibui ni mkubwa, tumo ndani ya ganda hilo. Utaalamu unasema kuwa hadi sasa hizo punje hazina dalili yoyote hatarishi, kwa sababu toka vipimo vya mwanzo na vya sasa, mwili haujaonesha ishara ya usambazaji sumu au vimelea vigeni popote pale. Vipo salama.

Uwezekano wa kuviondoa kwa lazer upo na ni salama pia... tukiwa tayari, tunaweza kujiorodhesha ili turatibiwe operesheni hiyo.

Daktari alipo tua, mwanaume alifanya kama anayafunga masikiyo na kufumba macho, kwa kushuka hadi akachutama na kuufanya mguno mreefu, na mshipa wa paji la uso ukamvimba. Nikashangaa!

Nikavutwa mkono tuu pale alipo nyanyuka, ili tutoke nje! Hatujaaga Wala!

"Daktari kaongea! Hizo LULU ni zangu, na ZIPO SALAMA! Huezi elewa ninavo zijali! Kwa taarifa yako, hata na mzuka wangu umehamia hapo!"

"Lulu? Zako? Kama ni za kunitia ulema nampaje fimbo bibi? Anajikongojaje? Kesho zikiufunga mlango, unaingiaje sasa? Embu niambie?"

"Nasema hivi..." Hapo kaweka kituo kireefu, halafu akaongea tataribu, ili nielewe neno moja moja:

SHUHULIKA NA BABU. BIBI NIACHIE MIMI!

"Nipo tayari kwenda popote muda wowote na hizi ripoti, tuupate mtazamo wa wengine madaktari. Siyo hii ripoti moja, na tiyari inasema hamna dalili hatarishi za chochote! Operesheni hiyo, haipo kwanza! Haipo! Nimemaliza na tuondoke."

Toka hiyo siku nikaelewa kuwa hizi "lulu zake," ndipo palipo madhaifu yake katika anavyo vipenda kwenye mwili wangu, baaada chungu cha bibi, matuta kifuani na kichuguu kilicho komazwa na Judo. Niliona ni hivo tangu aanze kuzipa umuhim kila mara, utadhani ni mfugo lazima ajuwe unaendeleaje!

Ilifikia kipindi hata mimi wasiwasi nikaondoa kwa sababu nilipenda mno vile mume wangu anavyo zifurahia LULU zake, hadi zikawa na kipaumbele kwenye uhai wetu humo chumbani kwetu.

Nirudi sasa kwenye maelezo pindi nilipo rudi nyumbani baada ya mtoko:

Usiku yake, nikamsabilia tunda. Kusema kweli, alipo anza kulipekua, mimi namuwaza kijana yule tuu! Alifanya ada yake kama ninavo ijuwa, ila niliona kabisa hayuko kawaida; alipo anza utumiaji kisu, nahisi analitia mamivu tunda ilimradi homa yake itokomee!

Nikamuuliza: "kuna shida gani?" Akasema: "hakuna shida yoyote!" Hajajiongeza kama kawaida yake, huwa anayo tabia ya kuungia kamba kwenye nyingine humo humo, na la sivo, tutaendelea na mengine halafu niupandishe tena mnara!

Namuona anauchomoa baada ya jibu lake, hajasubiri nimfute na nianze sehem ya kufuatia, huyoooo kainuka kwenda kuoga! Nayaskiya maji yanavo mwagika lakini pia na yeye akiliya kwa sauti kubwa mno!

Alikuwa na vimautundu vingi sana kwangu, nikaona siku zinavyozidi kwenda, hamna anacho nizidishia zaidi ya kunitwanga tuu, tena kwa karaha, bila utulivu! Yaani nahisi kama niko natiyana na mnyama vile, na baadae atanitafuna!

Na kila nikiwa kitandani, anapo taka kufanya yake, hunivua nguo kindakindaki almanusura inichane, hapo inanibidi nifuate upepo ili nisiji umizwa na niliyo ivaa mwenyewe! Haijalishi nimeelekea wapi, hataki ushirikiano, ilimradi nimuelekezee kunako achomeke!

Tukaenda hivo kiasi kwamba mimi sijawa tena na wepesi wa kuomba mualiko kitandani, na hata akikubali, jambo lililo kuwa nadra, yeye habadili mfumo wake aliyo uanzisha wa kunisulubu, pasina huruma mpaka nafura na kuwaka moto. Ikafikia hatua kwangu ya kughairi tendo mwenyewe.

Hilo likanijengea hoja ya kuyaanza mahusiano na kijana yule, baada ya kushawishiwa tena, na ma best wangu!!

Wazo lililo tokea kwenye maongezi na shoga zangu ni kuwa, kwa mume kimenuka, huenda kumebuma kabisa, kumbe nianze kujali pa kuangukia.

Hata mimi nikaona ni hivo tuu, japo nahisi khofu kwenye khatma yangu mdhambi nilivo mimi pamoja na huruma kwa mume wangu ambae tabia hii nimeanza imemponza na imembadili kila kitu!

Hapa suali la watoto sintoliongelea kwa kina japo tunavo chuana wazazi, athari zinawakumba pia.

Hayo mahusiano yangu mabest zangu waliyajua vizuri sana, kwa kuwa ni wao baadhi waliyaanzisha toka tunaipanga safari ya Braxtown!

Ilipo fikia siku ya kuzaliwa kwangu, nilipo toka nikamkuta Kijana yule ananisubiri nje, akanichukuwa kunipeleka hotel moja hivi iko Jane Avenue, nzuri sana nikakaa kama nusu saa wakaja mabest zangu na keki...

Nilibaki nashagaa, nikiwa hapo mume wangu alinipigia simu kuuliza niko wapi... nikakimbilia chooni kupokea simu, akauliza uko wapi mama, nikasema Nipo St Sixto Hospital, nimekuja kumuona mama yake rafiki yangu anaumwa, akasema mbona sauti ina mwangwi, na kumetulia hivyo, nikasema niko chooni nakojoa, akasema mbona hukuaga, nikasema samahani, imetokea hivo na nikaghafilika… alichosema ni kimoja tuu:

"KUWA MAKINI NA MAAMUZI UNAYOTAKA KUYAFANYA." Akakata simu...

"KUWA MAKINI NA MAAMUZI UNAYOTAKA KUYAFANYA." Akakata simu...

Nilikaa hapo bila hofu kabisa mbaya Zaidi nikisema nawahi nyumbani, wananiuliza mmoja baada ya mungine:

"Unamnyonyesha nani? Mume au watoto? Kwani we mtumwa au mke?" Dada Chief kaniuliza.

Kabla sijajibu, tiyari dada Zungu kadakia mpira juu kwa juu: " Unayo haki ya kuwa na jamaa zako, kama alivo kuwa nayo yeye! Wacha kujitia wasiwasi bure! Hawatabiriki hao! Wingu laweza kutanda ukajutia ujana wako, ukiwa tiyari chini ya mvua ya mawe!

Mwana umleavo, ndivo akuavo. Muunde unavo mtaka kuliko kumuabudu. Akivimba bichwa utajuta kuzaliwa! Mzoeze! Kwani si tuna waume kama wewe, labda huyu tausi huru kabisa!?"

"Yaani huwa natamani nisingeingia kwenye hii ndoa ndoano isiyo na kikomo hadi kifo! Mipombe na mwanaume wangu... Mwanaume?"

"Naanza tena: Mipombe ya mvulana pooza wangu inanikosesha raha mujuwe! Nilimkubali sana! Mtu poa, mambo yake yote sikuwa na la kughairi hata moja!

Pambe muhandisi alivo huyu aisee? Nilipenda nikapendeka nikapendeza nikapindukia hadi nikaifanya kufuru kwa paradiso niliyo tunukiwa, hasa pale nilipo mzaliya hili dume langu!

Hapo Zungu alikuwa anaiangalia picha kwenye simu yake, taswira ya familia ikiwa inaonekana. Hakika walipendeza sana kwenye hiyo picha wakiwa na mtoto wao.

"Vile alivo ingia kwenye ulevi usio na... "

Zungu hapo kakata kwa kupatwa na uchungu na hasira, uso na mikono yake hadi vinageuka kutokana na damu inavo mtembea, maskiyo mekundu mno!

Kukawa ukimya kwani hata sisi tumeguswa na simanzi za shost wetu... kwenye kiyoo cha simu hapo alikuwa tiyari katelezesha ndipo kukaja sasa sura ya chapombe kabisa hadi anatisha!

Mara anabadili upepo: " Lakini mwache anywe mwana kuzinywa, akafilie mbali huko huko wala sijali tena! Gauni jeusi nipo tayari kulivaa hata kesho! Hapa tumekuja kufurahi na wala siyo msibani! Sikubali mpumbavu atuharibie siku kwa kumtaja na bado hajafa tumuomboleze!"

"Dogo umenikosea lakini eti unawahi nyumbani? We acha tuu!"

"Lakini..." hapo akiwa ameelekeza kidole cha shahada juu, kichwa kapindisha.
" Kwenye uzito, kuna na wepesi pia. Subiri kwanza nimuagizie na zingine kwani tulipo fikia mimi na yeye, akithubutu kutafuta usaidizi wa kuiacha pombe namuua!"

Kweli alipiga sim kwenye duka la pombe na kumuagizia teja wake mseto kama anavo ujuwa Zungu, mimi hiyo lugha ya majina ya vichupa hivyo wala sijui...

Akacheka na sote tukaambukia kicheko hapo kwani tunakipata vema anacho maanisha:

Huyu dada Zungu, damu mbili; baba ni ndugu yetu tena mchungaji na hata mama mzungu mchungaji. Jamii ya dada ina mshikamano na kanisa lakini Zungu ni zungu mno! Kwao mtonyo ni kama wote, istoshi kaolewa na mrithi wa ghorofa hiloo... limefurika maofisi.

Kwake tunafarijika kwa mambo mengi hata baadhi ya mitoko muasisi yeye. Halafu msemaji mno; utadhani yeye mwalimu wa wanao toa vibonzo vya kuchekesha lakini fikirishi! Hana mishe ninayo iona hata moja. Ya nini? Burudani kwenda mbele!

Aliendelea;

"Au unayakumbuka mapigo ya mbwa koko? Kaa ule raha hapa bibie, maisha ndo haya haya."

"Halafu sikuficheni, mimi ndoa za kiislamu nazielewa sana: Hamna mambo ya kugandana endapo mambo hayaendi! Kitambo nshaa mtoka ..."Ahmada umelewaaaaa, Ahmada umelewaaa"...

Aliibuka kwa wimbo na uno la kufa chapombe! Akaendelea Zungu kutoa burudani:

"Wasemaje Tausi wangu?... mwenye mwendo wa maringo, hatua za hisabu... Ah mistari ya kibao cha wahenga imenitoka! Toshekeni na hayo... mwenye shingo la upangaaa! Hahhaaa! Kumbe na shingo nimelikumbuka asee!"

Akaendelea kwa umakini baada ya kukata uimbaji, na kupiga funda kadhaa za kinywaji chake:

"Naomba niumbie gauni jeusi nzuuri pamoja na kofia ya shungi la uso bomba! Usinifanyii ma bui bui yenu huko tafadhali, sijasema nataka kuwa muisilamu, bali naandaa siku ya uhuru wa taifa langu! Bendera na wimbo wa taifa nafanya mwenyewe!

Nataka niwe na taswira yangu mapema nisiji kukurupuka hiyo siku isiyo juwa mtu. Siyo masiala wee anza kazi, na tunamaliza kabisa nikiridhia na naiweka kabatini. Hata yeye nitamuonesha atowe maoni yake, si siku yake pia!? Hahaha!

Dada anae julikana kuwa ni Tausi mwenye nyodo za ajabu, ninazo taarifa zake nitakazo zieleza huko mbele na vile tunahusiana. Kwa ufupi ni mdada mzuri sana na hata aliwahi shindia taji la miondoko, pia aliingia kwenye tasnia ya tamthilia kwa kipindi kifupi tuu, akaiacha alipo jifunguwa dike mbili na kaka yao kwa mkupuo mmoja.

Na vile vile, kwa sasa ni fundi charahani mzuri na anajituma ipasavo kwenye warsha yake na ni duka la nguo, iliyo sheheni vijana chapa kazi na maonyesho ya nguo aina mbali mbali za tamaduni nyingi tuu. Asicho kijuwa, wewe mpe lisaa, ataufanya utafiti na kukuletea michoro ukose cha kuchagua. Lakini sasa ni msiri mno, hakuna anae mjuwa mpenzi wake au anatoka na yupi pindi tupo kwenye raha zetu. A Very Private Lady...

Nilikaa kweli hadi saaa mbili, nikiwa hoi, kijana akawa ameanza kunipa pombe ninywe, nilishindwa kwa kweli nikaanza kunywa divai tuu ambazo nazo sikuwa nikitumia zamani, siku yangu hiyo alinikazania sana anipe zawadi ya mkon'goto; sijaona rangi ya pesa yake. Nampa.

Dada Chief rafiki yangu akawa anaaga na kusema: "Hebu dogo tunaenda zetu! Mwenzako naona ataka umuazime kino, kwani anazo mbegu za kutwanga! Usimuachi na njaa!"

Wakaanguwa kicheko, wakainuka na kuondoka. Punde tuu, tulichukuwa chumba akanichemsha haraka, wala sijahisi uchungu japo hata yeye katika hilo sakata la chap chap kanikumbusha ninacho eshi na mume wangu huu muda wote. Cha ajabu nilipata raha sana ya penzi lake kuliko la mume wangu. Tulipo maliza, tukajitayarisha kila mtu arudi kwenye maisha yake.

Nilipofika nyumbani, namuona jamaa yake, jamaa wa karibu yetu sote, akiwa mwenye kuondoka hapo mbele ya nyumba. Tukasalimiana, ila kama namuona mwenye haraka hataki kukawia hapo, lakini nikamzuia. Alikubali, ila kama anayo wasiwasi ya kuondoka tuu.

Akatoka kwenye gari yake, akinisogelea. Nilitaka nifunguwe mlango wa gari tukutane. Akaufunga na kuushikilia, kashusha kichwa: "Mume wako ana hasira na wewe sana! Umebadilika! Kulikoni? Lakini sijataka unijibu kwani nina haraka ya kurudi nyumbani, tusiharibikiwe sote! Yule pale juu kwenye dirisha anakusubiri! Umeona anavyokuangalia yule kule juu?"

Hakika, nilipo ingia katika huo mzunguuko batili, roho yangu ilijawa na ugumu hata sioni wala sijali ninavyo bomoa ngome muhim za udugu, ngome za jamii; kama nilifanikiwa kueshi ugenini, sababu ni huyu kaka; Nilipo toka kwetu, nilifikia kwake akanipokea kama ndugu na wala hatujawahi fahamiana, yeye alinipokea kwa niaba ya mjomba wangu alie owa shangazi yake.

Pamoja na mkewe, waliniwea ndugu na wakanifariji kwa hali zote hadi nakutana na jamaa yake, mume wangu, na wakanioza wao kwa upendo nisiyo weza kusahau. Alipo ondoka kweli nilihisi aibu na huzuni, ila hapo hapo nikafuta akilini na kujiambia maneno ya ujasiri kumbe mpumbavu nimekuwa!!

Halafu niwaambie jambo: inafikia muda mtu kuwa katika kipindi cha utata na usijitambui. Ndivo ilivo kuwa hali yangu. Muda huo, ilitokea nikaurudilia wimbo wa Whitney Houston, Try it On My Own ; mashairi ya wimbo huu hayajawa mashairi tena kwangu, bali ni maandiko matakatifu hadi nahisi sasa huyu mdada bila shaka alikuwa nabii na si kitu kingine, na ujumbe huu ni wa mtu kama mimi, kutoka kwa Baba alie mbinguni! Jina lake lihimidiwe, Amen!! Na mikono naweka juu.

Hii ya "Mwanamke Huru" nitaichanganua zaidi, turudi kwenye tukio...

Nikaangalia sasa dirisha, ndipo nikamuona mume wangu. Alipoona nimemuona, akarudi nyuma na kuachia pazia.

Naingia sebuleni tuu, nae yu ashuka ngazi, akanifuata akanikumbatia kwa mashamsham na kunibusu, akisema: "Nikupokee mkoba? Kisha twende husuni ya chakula, kuna zawadi yako!" Nikazuga mapenzi ili nifuate upepo, nikampokeza mkoba halafu nikamfuata...

Nilipo fika sehem hiyo, nikakuta kuna keki! Na papo hapo akaanza kuniimbia wimbo wa B-Day, huku akitoa kwanza kitambaa kilicho funikia ndoo ya Champagne na bilauri mbili, halafu kachukuwa sahani, uma na kisu ili nikisha puliza mshumaa wa ishara ya umri wangu, tupasue keki! "Watoto mbona siwaoni?" Nikauliza. Akanijulisha aliko wapeleka kwa dhamira ya kuwa tuwe peke yetu hiyo siku.

Hii ndiyo mara ya kwanza siku yangu hiyo tupo mimi na yeye! Basi nikajikausha kama sio mie nikafurahi ili awe na Amani, nikashangaa! Mbona hasira nilizoambiwa anazo sizioni tena? Nikaikosa raha ila nikijiambia moyoni, niendelee na tamthilia ya siku hiyo, katika mazingira kwa upande wangu, tiyari ni hatarishi!

Tukakata keki tukala! Inanikaba! Hajachukuwa hata sekunde kumi, kaelekea kwenye ngazi haraka na kupanda hadi kwenye husuni ndogo ya kuelekea chumbani, mahala palipo sofa, maktaba na meza ndogo tuu, mahala pa kahawa yake asubuhi, ndipo anapo weka vitu anavyotoa mifukoni pamoja na funguo za gari, nikamfuata... Ile nafika juu tuu, akaniambia: " Nina zawadi yako ingine! Sasa njoo tukae hapa tuongee kidogo, nikupatie zawadi!" Nikamwambia: "Nisubiri basi nakuja!"

Mlango wa chumba ulikutwa tuu wazi, nikaingia na kuelekea moja kwa moja hadi chooni. Nikachukua simu nikamuandikia ujumbe kijana asinipigie maana nimefika nyumbani. Hajajibu chochote kile, basi nikaweka usafi na manukato, nikabadili nguo na kuvalia za kulalia na nikatoka kumfuata mume wangu.

"Mbona hujaniaga ulipoenda na sio kawaida yako??? Mbona hujaniambia wakati huwa unaaga japo kwa ujumbe wa simu?" Akaniuliza...

Moyo ukaenda mbio ila nikauchuna, nikamwambia kuwa mgonjwa alizidiwa, rafiki yangu akachanganyikiwa na kuniomba nimuwahishe hospitali, kwani usafiri jumuia ungesumbua kidogo...

"KUWA MAKINI NA HAYO UNAYOTAKA KUYAFANYA!"

Maneno yake tena, yakanigonga kwenye bongo kama nyundo vile! Hapo nilikutwa tiyari nimejawa na uoga, wasiwasi na kufikiria tuu jambo baya huyu mume wangu kanihifadhia!

Akanifuata: "Nakupenda sana! Jitahidi uniheshimu, usiniumize! Na endapo kuna mapungufu yoyote, naomba niweke wazi ili nirekebishe!"

Wala sioni uso wa hatari, kama tabasamu ipo, kama upole wa matamshi, vile vile ninavo mzoea. Hakika ukiwa mkosa, huezi kuwa na amani! Ndani mwangu nachemka kwa uoga na fikira zikipishana; yeye kamili yupo, ila amsha popo yake haipo: 1. Utani...

"Mungu niokowe!" Naomba moyoni, huku nikijitahidi kuwa sawa halafu nikasema:

"Sawa mpenzi! Mbona nakujali tuu sana? Hujakosa lolote na hakuna kama wewe kwangu mpenzi!" Nikajibu...

Akaniambia: "Chukuwa zawadi yako pale kwenye maktaba!" Nikajielekeza hapo, nikaikuta simu nzuri ya HTC ONE rangi ya dhahabu, na vikomo viwili vya dhahabu. Simu hiyo ni moja niliyo ifukuzia miezi kadhaa iliyo pita! Niliruka sana sana nikamkumbatia, akafanya kama kafurahi, halafu akaanza kuipandisha nguo yangu(mtindo ule ule wa purukushani nak...) pale kwenye hall!

Sikujivunga, nikasalim amri! Nikiwa napopolewa kisawasawa, akili yangu tiyari imesha hamia kwenye vile vikomo; Hili ni jambo ambalo sijawahi muambia, sijamuomba wala kumuonesha lakini tiyari hajakosea na hizi hapa bangili mkononi, nimezivaa tena mbili!! Hayo yote yalikuwa kwenye simu: maongezi yangu na mashosti wangu, humo kukiwemo na picha ya bangili hilo!!

Nilihisi aibu na kukiona kifo changu tuu, baada ya kuyapata hayo mapigo takatifu, huku nikishindwa hata ku igiza ushirikiano kwenye tendo: mkono mmoja umevalia bangili kila zikigongana kama zinaongea, zinanijuza nimeshikwa, nimeumbuka, mwizi, msaliti, muongo, mzinzi na mwizi wa fadhila!! Afadhali utukanwe na mungine, isiwe ni roho yako mwenyewe ikitoa ushuhuda wa maovu yako yasiyo na sababu ispokuwa ubinafsi!!

Mimi nikiwa katika hiyo hali na maumivu ya mfano misumari ndani ya bongo yangu, mara nasikia akipunguza kasi ya mapigo yake; kuna kitu alihisi:
2 Makombo...

Akaniangalia usoni! Nalihisi puto kama linapungua pungua na kuzimia ndani mwangu, yaani kaishia njiapanda! Akanitazama usoni akaniuliza, kwa tabasamu vile vile: " Unaburudika?" Nikajibu "Ndiyo" kwa sauti ya kuigiza kunogewa, na kusisitiza "Mpenzi twanga havijanoga!!"

"Hata maneno niliyo yaambiwa na Chief wangu yameniathiri kwa kiasi hiki?" Kule kwa kijana nilitabasamu kwa kulisikiya neno "Kino", lakini baada ya maneno kunitoka pasina utashi, nilitaharaki mno!

Hapo mwanzoni, kila anapo shindilia, vile nilikuwa sina hamu ya lolote, nilihisi maumivu kana mwamba mwichi unazifikiya figo sasa! Licha ya maumivu ya aina zote, akili haiachi kufanya kazi yake ya kunisulubu pia; Najisemeza mwenyewe na roho yangu, huku nikihisi aibu ya kufikiri labda mume wangu ananiona akilini sasa! Tena hapo pote, sijaskiya taaarifa yoyote ya vidoti, vitone nak...! Hali hii inanizidishia simanzi, yaani kuna nguvu nahisi zimetoweka: * 3 LULU hazitoi ushirikiano...*

Akasema: "Mimi naburudika zaidi, asante mpenzi!" Ila akili yangu inaniambia: "Umeyataka mwenyewe, sasa uyakubali yatakayo kutokea muda si mrefu!"

Baada ya maneno yangu ya mkosa, na siyafu zangu zikinin'gata huko kwa bibi, jamaa akamchomoa nyoka wake alie kufa kabisa! Yaani niliumia, kuliko kushukuru nimepumzishwa, nikashindwa kujikaza nikaanza kumwaga machozi...

Nikamuuliza: "Nini mbaya mpenzi?" Akajibu kuwa hamna lolote. Lakini hilo jibu lilikuja na ubaridi mwingi mno! Hapo hata yeye uhalisia ukamjaa, tamthilia ikakata! Nikataka nianze danadana na joka, hata tuende duru kumi za mieleka ilimradi achoke asinifanyii nisicho kijua na tiyari kimenisibu. Huku machozi yakiendelea kunitoka kutokana na yanayo pita kichwani mwangu na yaliyo mubashara papo hapo kwenye husuni, nikajiskia tuu natamka "Itasimama tuu mpenzi!"

Natamka lakini maneno yanakuja na kigugumizi, hata kamasi limeanza kunishuka vile vile! Lakini hamna lolote! Wapi kabisa!! Dalili sifuri! Samaki kafa wala hana mapigo ya moyo tena!!

Baada ya jitihada hizo, nilistuka akiniinuwa kichwa na kuniambia:

"Utanichubua swahiba, usifanye hivyo! Hapo basi tena! Siku yako ya kuzaliwa na iwe ya heri kabisa! Furaha na iwe kwako mzishi mwangu! Hii siku tuiandike kwenye matukio ya furaha kuu katika uhai wetu kama waanandoa!"

Akanyanyuka kwa kicheko na kushuka ukumbini vile vile alivo umbwa! Nikawa sasa na khofu, sijui nimfuate, mara akili inanionesha kifo, sijui niruke dirishani, vyote hivyo, kifo ndiyo mwisho! Halafu wanangu? Kijana wangu? Nikaona isiwi kesi, acha niingie nijifungie chumbani tuu, hamna namna au suluhu nyingine! Kama sijauliwa, kesho naondoka! Siwezi!

Sikupata usingizi, akili yangu inatembea kama umeme ikiyapitia maisha yangu ya muda huo mfupi na mahala nimefikia! Nilistuka , na kuingalia simu yangu hapo kitandani! Nikashangaa saa tisa ya usiku hiyo! Nasimama niende bafuni, huku nikiendelea kuskilizia na kufikiri nini mume wangu atanitenda! Tukio gani linalo nisubiri mie? Nitaliona kweli juwa la leo?

Nilipo kuwa bafuni, akili ikaniambia kuwa sina njia nyingine ya kutokea ispokuwa kushuka ngazi ili nitoke nje, kumbe mlango nitaufunguwa tuu! Kama mbwai, iwe mbwai! Na kadhalika, mlango huu siyo wa chuma au wa vault ya benki, angetaka, angeusukuma na usingemzuia. Mbona misuli anayo? Sina shaka, kama hajafanya lolote ni vile ananipenda, huenda asinidhuru.

Basi nikakaza roho, nikaufungua mlango. Vile alivo shuka ukumbini, hajarudi kwenye husuni ya tukio kwa sababu hata kaptura hajaichukuwa tuache nguo nyingine ile! Nikaja kumchungulia namuona ukumbini chini amekaa anaangalia movie, vile vile mtupu!

Nikashuka hadi chini, nikamuuliza: " Unashida gani usiku huu? Unatakiwa ulale mpenzi, ili kesho usishindi vibaya kazini! Tafadhali iache hiyo TV, uje tulale!" Hapo nimerudi ku igiza mke mwenye huruma, lakini roho yangu inanisuta na kuniambia niache upuuzi kwa mtu alie jawa na simanzi, na huenda akaniraruwa!

Akasema kwa sauti makini tena nzito: " Tafadhali niache, sina usingizi!"

Nilipo angalia pembeni yake, yuko na simu yangu! Moyo ukafanya paaaaaaaaaaaaaaa!! Yaani nilipo ingia bafuni, yeye alipanda na kuchuwa funguo yake ambayo hata sijakumbuka nikaingia nayo chumbani, kaufungua mlango wa chumba, kaichukuwa simu na akaufunga tena na kurudi ukumbini!

Nikamwambia: "Mbona umekaa na simu yangu?" Akasema: "SINA MIPAKA JUU YA SIMU YAKO MKE WANGU" Hapo alikuwa na sura ya kazi! Nikataka kuichukuwa kwa haraka, kaniwahi na kuishikilia. Halafu akasema: "Usipendi kutumia nguvu, sana utaumia! Chukuwa simu hii hapa nenda kalale!" Nikakuta anakunywa mvinyo, alikuwa anaangalia CD moja ambayo nilitamani kila mtu angekuwa nayo inaitwa FIND A SECRET, nzuri sana sana sana! Hii niliinunuwa mimi wakati alipokuwa East Scotland kikazi, niitumie kama kifaa cha kujifunza kumpeleleza pale atakapo kuwa ni mwenye kulisaliti penzi letu, nimgunduwe mapema.

Ila kwa muda huo, kwangu ni upanga shingoni ambao niliuleta kwa mkono wangu mwenyewe, kisa wivu! "Kapataje hii CD, ambayo ni siri yangu, na haijawa hapa nyumbani bali kwenye kabati ya kazini kwangu, oficini mwangu? Au hata yeye kainunuwa?" Naongea na roho yangu mwenyewe, nikijiuliza masuali pasina kuyapata majibu rasmi, bali ya kukisia kisia tuu...

Nikasema: "Sawa. Uliichukuwa yanini, kwani si tiyari unajuwa yaliyomo?" Akasema: "Nilipize basi nenda na yakwangu!" Sikumjibu nikarudi juu chumbani, yaani nilishindwa kuendelea udwanzi; nijitoe fahamu nilete bukta nimuambie basi avae... roho inaniambia "unataka makuu wewe kicheche! Wacha kuyashika masharubu ya simba alie jeruhiwa!" Nikaendelea hadi kitandani, nikaanza kupekua jumbe ! Kumbe kijana karejesha majibu analinisifia umbo langu na Sana tulipo fanya mapenzi, kuwa nimemtiya kiu sasa anasubiri nirudi kummalizia hamu yake roho itulie!

Hatimae hata ile electronic diary kijana alinipa pindi nilipo kuwa naenda kwenye rusha roho zetu. Na yenyewe ilikuwemo vitu vya ajabu na mimi wala sijaipitia ili nione ni vitu gani. Lakini kuna picha inayo nisuta kwenye machine hiyo, kutokana na maneno yaliyo andikwa chini siku nimeipewa.

Hii ilikuwa miongoni mwa ushahidi aliyo kuwa nao! Siku ananiacha kanisani aliionyesha na akasema anazo jumbe, picha na video vyote maana alienda kuvinakili na kuvichapisha kwa yule jamaa yetu, yeye hufanya kazi kituo cha Police!

Sijarudi kuufunga mlango wa chumba. Nilipitiwa na usingizi nikalala. Ilipo fika asubuhi, nikaamka na kufanya ratiba zangu kamili ili nielekee kazini! Lakini mandhari ya bafuni ikanionesha kuwa tiyari jamaa alipitia kwa usafi na hayupo, watoto kawaandaa basi la shuleni lishaa wapitia na sikujua ilikuwa muda gani yeye kaondoka! Hata miliyo ya gari sijaiskiya!

Nilipo fika kazini kwanza nimechelewa, haraka nimesha wahi kabatini kuviangalia vitu vyangu... mume wangu alivipitia lakini sijui kwa mtindo gani. Nikauchuna. Maji yashaa mwagika hakuna janja janja hapa! Hali ilianza kubadilika hapo, simuelewi kabisa mwenzangu, anauchuna tuu, haniulizi chochote.

"Muunde umtakavo"... na maongezi yote niliyo yaskiya kwa mashosti nayakariri akilini, na toka hiyo siku yangu ya kuzaliwa nilianza kuyafanyia kazi japo nilinaswa vikali. Vile mume alivo nichomolea nyaya chumbani, na kila akitaka kusema namshushua au nampa majibu makali, anatulia. Hapo najaaribu kuweka ngome asiongelei "LULU ZAKE", kwani hata mimi zinanifikirisha na bado sijapata mwanga wa kwa nini iwe hivo.

Nikaendelea na kijana yule, huku nyumbani basi tuu, hata ile adhabu ya kuraruliwa ilikata kabisa. Nikaizindua tena lakini kwa tabu sana, kwa sera kutoka kwa ze dadaz, kwa sababu sijawa tayari kuachana nae; hapo inatakiwa niuvunje ukuta mzito...

"Huyu mwanaume si mchepukaji, basi ugwadu umemfinya. Kijana nae, amekunata mno, kwa kuwa anakutaka hata sasa hivi. Tatizo ni pale utakuwa haupo nae kutokana na kibaruwa kwa mume. Nenda kacheze nao wote kwa viwango na umahiri hadi siku utachukuwa maamuzi sahihi"... naiskiya sauti hiyo akilini mwangu.

Walielekea wote vizuri hatimae. Ila usioni hivo, mume wangu alinisumbuwa sana kupita kiasi; kila nitakapo panga ramani ya kuingia ndani ya himaya yake ili nimshawishi afunguke, ananikwamisha halafu narudi kujipanga upya.

Siku nilifaulu, nilikumbuka kitu ambacho hakijahitaji sera au michakato niliyo kuwa nikiitoa kwa dada zangu huo muda wote. Jambo moja pekee... nguvu zangu: LULU.

Nilivizia muda wake wa kwenda bafuni, nikaingia nae na kuchukuwa bomba la maji, nikaanza kujiosha, yeye amesha anza kukojoa. Alipo niona najiosha, sijui alifikiria nini; alipatwa na hasira mno! Yaani alinguruma akiwa anayasaga meno, utadhani kuna mtu amemtumbua kwa kisu!!

Nilipo maliza kujiosha, nikatamka tuu: "Lulu zako zimerudi kuniwasha. Narudi kwa daktari leo!"
 
Kuna mahali nilishaisoma mpaka mwisho mwaka juzi
Wewe ni mfuatiliaji mzuri. Kwenye hii segment, vingi ni vya hiyo story. lakini unapo fika kwenye paragraphs za mwisho, utaanza kuuona utofauti wa story.

Nimesema katika utangulizi kuwa ni story iliyo pita humu yatu mungine tiyari. Nilicho kifanya, nimepita nayo ili niweke kilicho changu kwani kuna namna story ile inafanana na ya kwangu.

Vumilieni tuu, nina imani mtalipata jambo tofauti mno wa vitu tunavyo vizoea ila tunavipa maana nyingine.

Kama wewe ni Womanizer/Player/Kasanova. Gold Digger. Mzazi alie na wasichana kwa wavulana. Kilicho nikuta kinaweza kukufungua usiko tegemea.

I hope I'll do you justice. Stay the course.
 
Madam hii story nilishawahi soma miaka kadhaa humu humu jamii forum,,,


Inaelekea bado inatesa roho Yako,,,,pole sana.
 
Ndefu Ila nzuri umenifanya mshipa umesimama Ila sijui kwanini mwanamke akianza kuchepuka ni rahisi sana kumkamata Ila nilichojifunza kwenye mapenzi wanawake wengi wanapenda wanaume player wababe
 
Madam hii story nilishawahi soma miaka kadhaa humu humu jamii forum,,,


Inaelekea bado inatesa roho Yako,,,,pole sana.
Huenda mimi ni babu, au baba kwako au kaka mukuu. Na hiyo story ni ya bimkubwa alie jukuu sasa.

Ukiwa ulinisoma vema, kuna mahala nimeandika kuwa anae ongea ni mwanamke. Kuna codes humo, mimi nitakapo zifungua sasa utaelewa ni kitu gani...

Alitutesa roho zetu. wengi mno. Huenda pia hii story ikaisaidia roho yako kesho isiteseki.
 
Ndefu Ila nzuri umenifanya mshipa umesimama Ila sijui kwanini mwanamke akianza kuchepuka ni rahisi sana kumkamata Ila nilichojifunza kwenye mapenzi wanawake wengi wanapenda wanaume player wababe
Ni kwa sababu ma Kasanova wanao jielewa wanazijua mbinu usivo tegemea, na hata wao sometimes baadhi hawaelewi 100% wanarusha cheche gani upande wa the Ladies. Huu mwili tulio nao ni hatari sana. Omba Mungu wako usikutani na "She-Kasanova"😃.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom