Jakaya M. Kikwete ZINDUKA CHADEMA wanakuondoa!

JK ni mwanaume. Amefanya kile ambacho hata nyerere alikuwa hawezi kukiruhusu wala kukivumilia. Enzi za Nyerere leo hii watu kama Slaa wangekuwa ukimbizini. Kikwete anasoma alama za nyakati. anataka kujenga Tanzania ya watu majasiri wanaoamua nani awe kiongozi wao na nani asiwe.

Wengi sana na hasa ndani ya ccm hili linawauma sana. Wanapigwa mawe. Wanazomewa. wanafanywa chochote na wananchi, lakini Jk hana habari. Katulia tuli na Salma. Kikwete ni mwanamapinduzi kwa maana ya kuruhusu wananchi wajiamulie aina ya watu wanaotaka kuongozwa nao.

JK nakuomba sana. Popote pale ulipo, ruhusu maandamano, ruhusu watu kuzungumza na kukusanyika, agiza vyombo vya usalama kulinda raia bila ubaguzi wa kiitikadi, waache watanzania wajikomboe wanavyotaka wao.

CCM imejaa mizee yenye misimamo ya kinyonyaji. JK mwenyewe anajua, lakini anakosa la kufanya. Anachoona ni busara ni kunyamaza. Safi!


Long live JK.

Mkuu umezungumza ukweli kabisa,
 
Nina uhakika Mh. J.K mara moja moja huingia mwenyewe humu jamvini, japo kwa sababu ya ratiba yake mambo mengi humpita.

Watu wengi wanajua kuwa JF ni ya wana-CCM kifikra japo kimaandishi ni CDM. JF kwa siku za hivi ni sehemu ya kupata habari juu ya mambo muhimu kwa taifa letu, hivyo ni jukwaa la watu wote, wanafunzi, wanasiasa, wanazuoni, wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi ktk nyanja zote. Wengi hawachangii, ila wanasoma sana thread zote!

Mh. J.K anao watu wanaopaswa kum-update ktk kila jambo, hususani juu ya CDM (tokea uchaguzi mkuu wa 2010) lakini hawampi yote......wanachambua na kumpatia anayotaka kuyasikia na asiyoyataka kuyasikia hawampatii hivyo kujikuta hapati picha kamili na kuendelea kukaa kimya huko bedroom wakati CDM wanavinjali sebuleni kwake!

Nimewahi kusikia mmoja wa wasaidizi wake akisema "Lazima ujue radha anayopendelea boss wako, ili uendelee kuvinjali na kulisha familia yako" :dance::dance::dance:
 
Unaanza kwa kujidai kuwa "niliyebahatika kusoma vizuri" halafu tazama hayo niliyoyaweka nyekundu. Huo ndio usomi mzuri? labda ulibahatika kujuwa kusoma Ngurumo na Mzalendo ukajiona tayari umeshasoma sana. Nakusahihisha hapa chini ili siku ingine usirudie kutuchafulia lugha hii tamu:

sebureni
= sebuleni

viashilia = viashiria

ushabeki = ushabiki


Kwani mtu akikosea spelling ndio anakuwa si msomi?. Labda alisoma nje ya nchi?. Wewe unafikiri kiswahili kinazungumzwa dunia nzima. Hii ni akili za Mmasai wa kudhani ngo'mbe wote duniani ni wa wamasai.
 
mjomba anawasikiliza wanaompigia makofi akizani wanamshangilia.mbona bado kidogo tu,wapiganaji haoooo chumbani.
 
Kumbe tupo wengi tuloliona hilo!!
Mwanzano nlihisi ninaota!!
sikuamini nlichokitathmini. nkaona ngoja nikae kimyaaaaaaaaaaaaaaa!
kumbe nawe umeliona!! LoL.
 
Tunashukuru kwa kutujulisha kwamba kuna chama kinaandaa kufanya uhaini dhidi ya serikali iliyoingia madarakani kidemokrasia na kwa mujibu wa katiba. Halafu wanajiita "Chama cha Demokrasia" lakini hawaamini katika demokrasia! Shame on them. Hata hivyo kuiondoa serikali itabaki kuwa pipe dream. Wacha wamalize soli za viatu na kubadilisha magwanda ya kaki lakini uongozi utabadilishwa kwa sanduku la kura 2015.
 
Bahati waliyonayo cdm ni kwamba hatujatunga Sheri a ya kuwazuia watu kiuota mchana. Chadema kusema wanaweza kumwondoa Rais Kikwete kabla ya 2015 ni ndoto ya mchana.
 
Tena ni ndoto ya mti alikunywa mnazi! Wanachoudhi hawataki hata kujua kwamba mazingira ya Arab world ni tofauti sana na ya hapa kwetu. Matokeo yake watabaki kama fisi na mkono wa binadamu!
 
Unaanza kwa kujidai kuwa "niliyebahatika kusoma vizuri" halafu tazama hayo niliyoyaweka nyekundu. Huo ndio usomi mzuri? labda ulibahatika kujuwa kusoma Ngurumo na Mzalendo ukajiona tayari umeshasoma sana. Nakusahihisha hapa chini ili siku ingine usirudie kutuchafulia lugha hii tamu:

sebureni
= sebuleni

viashilia = viashiria

ushabeki = ushabiki

Nenda jukwaa la lugha kule ukaoneshe umahiri wako wa lugha, hapa cha msingi message sent. PERIOD.
 
Ndugu zangu wana-CCM na Wana-CDM, mtu anapotoa hoja ambayo ata kama huipendi bora ukanyamaza kuliko kuipondaponda tena kwa chuki.....du! Kwa lugha nyingine, tusiwe na dhana ya kutaka kusikia yale tu tunayotaka kuyasikia. Tuwe tayari kusikia ata yale ambayo ni mwiba kwetu ili yatuchome kwanza kisha tutafute namna ya kuyadhibiti yasije yakatutoa roho....

Basi ili nisiendelee kuwaumiza wengine humu Jamvini, Mh. Rais endelea na mambo mengine ya kulijenga taifa CDM si lolote si chochote.....CCM ipo juu kwa kasi zaidi, nguvu na hari zaidi!
 
Bahati waliyonayo cdm ni kwamba hatujatunga Sheri a ya kuwazuia watu kiuota mchana. Chadema kusema wanaweza kumwondoa Rais Kikwete kabla ya 2015 ni ndoto ya mchana.

sio kwamba hawawezi... ni kwamba hawataki kuiingiza nchi kwenye hasara ya uchaguzi mwingine! unajua gharama ya uchaguzi?

halafu katiba bado ile ile na tume bado ni ile ile ya makame, jk na kiravu...
 
Ninaomba niwe mkweli katika hili. Nilikuwa ninampenda sana Jakaya Kikwete na bado nitaendelea kumpenda, japo mimi ni mtoto wa mkulima tena wa jembe la mkono niliyebahatika kusoma vizuri enzi hizo kwa sababu ya sera za Hayati Mwl. Nyerere - Baba wa Taifa.

Jakaya Mrisho Kikwete ni mtu mstaarabu na muungwana sana. Hapendi kukosana sana na watu, hususani anaowafahamu. Hilo ndilo nilomtafuna kwa kasi yeye binafsi na chama chake!

Wito wangu kwa Mh. J.K, chondechonde zinduka CHADEMA wameishaingia sebureni bado tu kuingia chumbani! Walianza pole pole na tukadhani ni kikundi cha msimu, lakini ishara na viashilia vyote vinaonyesha, CHADEMA siyo tena Chama cha Msimu. Ninaandika haya nikijua kuwa hapa jamvini wengi ni CDM, lakini sina namna yoyote ya kukutumia ujumbe wa kukushauri sababu ya itifaki yako kama Rais. Baadhi ya watu wako waliokuzunguka aidha hawakushauri vizuri au bado wana underestimate CHADEMA.

Dr. Slaa kama kamanda mkuu wa CDM ni mtu makini, jasiri, mvumilivu na mpiganaji wa kweli. Ninampenda sana na kumuombea kwa Mungu afya njema japo sipo CDM. Ninapoandika haya ninajua ninachokisema na sina ushabeki wowote ni CDM wala CCM.

J.K tafadhari, zinduka CHADEMA wameingia sebureni sasa wanajipanga kuingia master bedroom!


""Mkuu usimwamshe aliyelala ukimwamsha utalala wewe;""
Mkweree jilalie mweyego wakikusumbua utasingizia udini...teh teh teeeh:dance:
 
acha aendelee kulala hana ubavu wa kuwashughulikia EL na RA na ndo ndo wanatawala nchi.
 
Njia ya kutoa JK na chama chake,ni katiba tu,lakini sizani kama watakubali chama hicho cha ccm kitoke madarakani,kwanza tanzania ili uwe rais lazima ukubalike na vyombo vya dola,na huwezi kukubalika kwa vyovyo vya dola,kwanza tukubali kuwa vyombo vyetu vimeingia katika siasa,haviko huru.

Pili rais anakuwa yeye ndio Amir jeshi mkuu,ana control dola yote vipi utamtoa madarakani ? Atapiga risasi wote,wangapi wameshanyongwa ? Dr omar alokuwa makamo wa rais yuko wapi ? Na wengine walopita ? Walikufa vifo vya kutatanisha kabisa,serikali yetu ya kidicteta ever hamutaitoa madarakani kwa uchaguzi,kama hamujaingia barabarani kama Tunisia na EGYPT basi ni ndoto.

Sasa katiba mpya imeanda liwa mswada na chama cha ccm,halafu wanaitwa mawaziri wapitishe ili wapewe posho zao,ikisha unapelekwa bungeni upitishwe,na wabunge wanabembelezwa waupitishe,jee kutakuwa na haki katika mswada huo kama umeundwa kichama ?

Hizi nchi zetu zanzibar na tanganyika zinaendeswa kichama sio kikatiba,ilani ya ccm ndio inayoongoza nchi,hata serikali uwafanyie nini basi watasifia kuwa ilani ya ccm ndio juhudi zao na ndio iliyotekeleza,yaani sio kama serikali ndio wajibu wake kuwafanyia wananchi,hizi ndio mbinu za ccm,kujipigia compain katika kuwapatia wananchi huduma.

Na kwa wale wajinga hawajui nini wajibu wa serikali kuwafanyia wananchi basi ndio hurubunika mara moja,UMEME,MAJI,HUDUMA ZA AFYA,ELIMU,miundo mbinu,haya yote ni lazima serikali iwapatie wananchi,na sio juhudi za chama bali ni wajibu na lazima kwa serikali.
 
Back
Top Bottom