Jakaya M. Kikwete ZINDUKA CHADEMA wanakuondoa!

Ninaomba niwe mkweli katika hili. Nilikuwa ninampenda sana Jakaya Kikwete na bado nitaendelea kumpenda, japo mimi ni mtoto wa mkulima tena wa jembe la mkono niliyebahatika kusoma vizuri enzi hizo kwa sababu ya sera za Hayati Mwl. Nyerere - Baba wa Taifa.

Jakaya Mrisho Kikwete ni mtu mstaarabu na muungwana sana. Hapendi kukosana sana na watu, hususani anaowafahamu. Hilo ndilo nilomtafuna kwa kasi yeye binafsi na chama chake!

Wito wangu kwa Mh. J.K, chondechonde zinduka CHADEMA wameishaingia sebureni bado tu kuingia chumbani! Walianza pole pole na tukadhani ni kikundi cha msimu, lakini ishara na viashilia vyote vinaonyesha, CHADEMA siyo tena Chama cha Msimu. Ninaandika haya nikijua kuwa hapa jamvini wengi ni CDM, lakini sina namna yoyote ya kukutumia ujumbe wa kukushauri sababu ya itifaki yako kama Rais. Baadhi ya watu wako waliokuzunguka aidha hawakushauri vizuri au bado wana underestimate CHADEMA.

Dr. Slaa kama kamanda mkuu wa CDM ni mtu makini, jasiri, mvumilivu na mpiganaji wa kweli. Ninampenda sana na kumuombea kwa Mungu afya njema japo sipo CDM. Ninapoandika haya ninajua ninachokisema na sina ushabeki wowote ni CDM wala CCM.

J.K tafadhari, zinduka CHADEMA wameingia sebureni sasa wanajipanga kuingia master bedroom!

Please man. Kikwete ni Fisadi number moja na wizi wake wakura, uzembe, kuficha siri za wizi wa mali za watanzania na kushiriki kuwamaliza wananchi ndivyo vimechangia jk kuwa incompetent. Tafadhari sijawahi kuona kiongozi anasifa unazozisema, maybe unataka kuwadanganya tena kwa mbinu mpya kama za dairy news na tbs. Not this time ....
 
It is too late kuzinduka. Aombe afike 2015 salama maana kufika ni majaliwa - umma ukiongozwa na chadema unaweza kumtoa kabla ya muda kutokana na maisha magumu.
 
Kaka MIKAEL P AWEDA,

Hilo la Serikali kuondolewa kwa nguvu ya Umma sahau! Ni ndoto ya mchana. Kwa tathmini yangu, si watanzania wengi kiasi hicho wanaopenda nguvu ya umma itumike katika kuleta mabadiliko.

Pia ujue, kimya kingi kina mshindo. Sidhani kama Mh. J.K na Serikali yake hawaoni, hawasikii na wala hawaguswi na kinachoendelea.......Sisi watu wa kawaida inatugusa tena sana sembuse wao?

Wewe na mimi tutakuwa mashahidi.........tumuombe Mungu tuendelee kuwa hai na JF iendelee kuwepo.....2015, utaniambia....

Otherwise, shukrani!
 
tshsssssss mwache arare asharara sana hata akiamka atakuwa na wenge tz is veryy big for ccm waachie ngazi kiukweli hata kikwete mwenyewe ni shabiki wa cdm basi tu anaona aibu kusema.

Rekebisha kiswahili chako...eti "kurara" "arare" na mwenzako amesema "sebureni" kwenye kiswahili fasaha na sanifu tuna "kulala", "alale", "sebuleni"
 
Unaanza kwa kujidai kuwa "niliyebahatika kusoma vizuri" halafu tazama hayo niliyoyaweka nyekundu. Huo ndio usomi mzuri? labda ulibahatika kujuwa kusoma Ngurumo na Mzalendo ukajiona tayari umeshasoma sana. Nakusahihisha hapa chini ili siku ingine usirudie kutuchafulia lugha hii tamu:

sebureni = sebuleni

viashilia = viashiria

ushabeki = ushabiki

Tatizo ni kufikiria kuwa wote waliosoma enzi za Nyerere walisoma walisoma au kukijuwa kiswahili vizuri kama wewe!!! Kama wewe ni Maimuna wa Kiingereza wenzako ni akina Maimuna wa Kiswahili!!!!!
 
JK hana la kufanya, anajua kwamba hiyo ni laana ya Mwl. J.K. Nyerere. Walisubiri alivyofariki tu wakajivinjari na yaleyale aliyokataza - JK & EL. No way back, huo ndio mzimu wa Mwalimu.

Laana ya nyerere kama nani hata impate mtu? labda hiyo laana kaipata yeye, aliyeuwa hii nchi. Unayajuwa ya nyerere au unasikia tu uongo wakumsifu? Nashanga!
 
Ninaomba niwe mkweli katika hili. Nilikuwa ninampenda sana Jakaya Kikwete na bado nitaendelea kumpenda, japo mimi ni mtoto wa mkulima tena wa jembe la mkono niliyebahatika kusoma vizuri enzi hizo kwa sababu ya sera za Hayati Mwl. Nyerere - Baba wa Taifa.

Jakaya Mrisho Kikwete ni mtu mstaarabu na muungwana sana. Hapendi kukosana sana na watu, hususani anaowafahamu. Hilo ndilo nilomtafuna kwa kasi yeye binafsi na chama chake!

Wito wangu kwa Mh. J.K, chondechonde zinduka CHADEMA wameishaingia sebureni bado tu kuingia chumbani! Walianza pole pole na tukadhani ni kikundi cha msimu, lakini ishara na viashilia vyote vinaonyesha, CHADEMA siyo tena Chama cha Msimu. Ninaandika haya nikijua kuwa hapa jamvini wengi ni CDM, lakini sina namna yoyote ya kukutumia ujumbe wa kukushauri sababu ya itifaki yako kama Rais. Baadhi ya watu wako waliokuzunguka aidha hawakushauri vizuri au bado wana underestimate CHADEMA.

Dr. Slaa kama kamanda mkuu wa CDM ni mtu makini, jasiri, mvumilivu na mpiganaji wa kweli. Ninampenda sana na kumuombea kwa Mungu afya njema japo sipo CDM. Ninapoandika haya ninajua ninachokisema na sina ushabeki wowote ni CDM wala CCM.

J.K tafadhari, zinduka CHADEMA wameingia sebureni sasa wanajipanga kuingia master bedroom!
Kipindi hicho Dr Slaa ni katibu Mkuu....Zitto naibu katibu bara.

CDM ilikuwa inatisha....na wafuasi wake tulikuwa critical and objective.
 
JK ni mwanaume. Amefanya kile ambacho hata nyerere alikuwa hawezi kukiruhusu wala kukivumilia. Enzi za Nyerere leo hii watu kama Slaa wangekuwa ukimbizini. Kikwete anasoma alama za nyakati. anataka kujenga Tanzania ya watu majasiri wanaoamua nani awe kiongozi wao na nani asiwe.

Wengi sana na hasa ndani ya ccm hili linawauma sana. Wanapigwa mawe. Wanazomewa. wanafanywa chochote na wananchi, lakini Jk hana habari. Katulia tuli na Salma. Kikwete ni mwanamapinduzi kwa maana ya kuruhusu wananchi wajiamulie aina ya watu wanaotaka kuongozwa nao.

JK nakuomba sana. Popote pale ulipo, ruhusu maandamano, ruhusu watu kuzungumza na kukusanyika, agiza vyombo vya usalama kulinda raia bila ubaguzi wa kiitikadi, waache watanzania wajikomboe wanavyotaka wao.

CCM imejaa mizee yenye misimamo ya kinyonyaji. JK mwenyewe anajua, lakini anakosa la kufanya. Anachoona ni busara ni kunyamaza. Safi!

Long live JK.
Kwa sasa demokrasia i shakani
 
Back
Top Bottom