JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
Pasco hakuna sababu ya kukwepa ukweli.. Mfumo wa ELIMU nchini ni mboivu na Uvunjwe...Aliyasema haya Malima na wakamzushia mambo makubwa zaidi lakini nimechunguza kwa undani sana na kukuta kwamba kweli upo mfumo mbaya sana ktk ELIMU a AFYA nchini jambo ambalo sikuwahi kulikubali hata kidogo. Tuliyakataa haya haya wakati wa Nyerere kuhusu wanawake na hii inajionyesha zaidi leo wapo watu wanaamini wanawake hawawezi kuwa viongozi.
Kwa nini watu wanapenda kuulinda mfumo uliopo, mimi sielewi hasa sababu ya watu kushabikia kitu hali hawajui chochote au wanajua fika kwamba wana wakandamiza.. Kusema kweli binafsi siwaoni tofauti na wabunge wanaolilia posho zaidi japokuwa wanajua fika kwamba wanawaumiza wananchi. Tukitaka haki tuyachunguze malalamiko ya hawa watu kisha tujue ukweli ni UPI hapo ndipo tunaweza kuja na hoja ya kumpinga..Lakini kabla hatujawa na ukweli mkononi ni Ujinga mwingine kukumbatia kitu usokijua undani wake.
Mkandara,
..Prof.Malima alidai kuna hujuma ktk mfumo mzima wa usahihishaji mitihani.
..akaenda mbali na kudai kwamba wanafunzi hawatumii namba za mitihani wakati anajua fika kwamba namba za mitihani zilikuwepo tangu hajateuliwa kuongoza wizara hiyo.
..mimi nadhani tatizo letu ni kwamba linapokuja suala la elimu tunajali zaidi QUANTITY kuliko QUALITY. hata Prof.Malima alikuwa anajadili "idadi" na siyo "viwango."
..wakati wa zoezi la UPE serikali iliweka umuhimu mkubwa ktk kuandikisha watoto wengi shule ya msingi bila kuhakikisha kwamba watoto hao wanapatiwa elimu inayokidhi viwango.
..shule za sekondari za kata nazo zimeanzishwa kwa mtindo uleule, na mentality ya enzi za zoezi la upe. tumejikita ktk idadi na siyo viwango.
..kwanini wananchi wajenge shule 10 zisizo na waalimu wa kutosha, maabara, na maktaba? kwanini wasianze na shule 3 zilizojitosheleza?