Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 222
- 529
Karibu kila mwaka takwimu za wanaofaulu kutoka elimu ya sekondari kwenda vyuo vikuu na vya kati inazidi kuongezeka hii inaenda sambasamba na idadi ya wanaohitimu vyuo vikuu na vya kati kila mwaka wanaongezeka mtaani
Kuongozeka kwa ufaulu darasa la saba na kidato cha nne kila mwaka ni vema wadau waelewe kabisa kuwa sio kwamba kizazi hiki kina akili sana! La hasha!
Kwanza walimu wanapewa maelekezo maalumu ya usahihishaji. Fanya uchunguzi binafsi kwa walimu wanaosahihisha mitihani ngazi ya NECTA
Pili mitihani ya siku hizi ni rojo rojo sana! Ukilinganisha na mitihani ya miaka kadhaa nyuma utacheka mwenyewe
Hali hii imepelekea kushuka kwa taaluma za vyuo vikuu. Kulibaini hili angalia wahitimu wetu lakini pia chunguza wahadhili wa vyuo vikuu
Matokeo ya haya yote ni nini?
Taifa linazalisha vijana wasioweza kuhoji chochote. Leo NHIF inazozana na vituo binafsi vya kutolea huduma za afya kwa ubadhilifu walioufanya wenyewe wa kujikopesha zaidi ya Bil.41 za michango ya wanachama halafu mzigo wanatafuta wa kuwatwisha badala ya kulipa.
Wachangiaji wa NHIF ni wasomi lakini hawana uwezo wa kuhoji haki yao. Waziri wa afya anajiongelesha tu kwasababu anajua hakuna raia wa kumuhoji chochote na kushinikiza aachie ngazi
Leo wasitaafu wanaandaliwa kikokotoo ambacho kitawaacha na fedha kiduchu ya pensheni. Hapa wanafidia pengo lililosababishwa na kujikopesha pesa za NSSF kujenga UDOM. Wanafanya haya kwasababu wanajua hakuna wenye nguvu za kuhoji
Taifa limeua elimu na sasa shule, vyuo vikuu na vyuo vya kati vinazalisha machawa wa wanasiasa na viongozi ambao kila kitu ni ndioo na kusifia ujinga.
Dharau ya serikali kwa wananchi inazidi kuwa kubwa kwasababu wanafahamu walishaua ubongo tayari.
Hata hivyo, hatima ya yote haya ni Taifa kuanguka kwa wasiowaaminifu na kutawaliwa kama familia ya mtu