Kwanini Watanzania wamekubali kudanganywa kwamba kuna Elimu ya bure?!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,651
5,126
Kwa kweli hata mimi🤣🤣🤣 cha ajabu zaidi walimu hao hao wa kata wnaapeleka watoto private yaani kama Nina uwezo siwezi peleka mwanangu kwenye huo upuuzi wa shule za serikali
Kuna msemo kwamba, " to every decision you make there is a price to pay or consequences"!

Kwamba katika kila uamuzi ufanyao kuna gharama utakazolipa au athari zitakazo jitokeza.

Suala la elimu kwa watoto wetu hapa Tanzania linafanyiwa mzaha sana na wazazi walio wengi na hata viongozi wanatuongoza !

Kuna mjadala(thread) uliletwa humu na MwanaJF mwenzetu LIKUD kwamba yeye hawezi kutoa mamilioni kusomesha mtoto wake shule za English Medium!

Mjadala ni mkali na hasa ukizingatia Watanzania walio wengi wanavyopenda vitu vya bure, kasumba ya kijinga tuliyojengewa na mfumo wa ujamaa tulio anza nao kama Taifa baada ya kupata Uhuru!

Haya ni mawazo yangu niliyotoa katika mjadala huo unaendelea.

Elimu siyo kupata division one au kufaulu mitihani tu ! Ni zaidi ya hapo!

Elimu inatakiwa kumpa mtu maarifa ya kupambana na mazingira yake hata kuishi popote duniani.

Shule za m
Msingi na Secondary nyingi za Serikali ni kama VITUO VYA KUZUIA WATOTO wasilete vurugu mtaani wakati wenzao wanasoma!

Jiulize ni kwa nini hata Diwani , Wakuu wa vituo vya Polisi ,Walimu Wakuu wa Shule za Serikali n.k ,watoto wao wanasoma English Medium na hawataki kuwapekeka Watoto katika hizo Shule za Serikali !?

Wabunge na Mawaziri wanasomesha Watoto wao Feza Schools tena hawataki hata mtaala huu wa NECTA! wanasomesha Watoto wao kwa mtaala wa CAMBRIDGE ambapo ada kwa mtoto inafika au ni zaidi ya milioni 20 kwa mwaka!

Elimu ni kitu ghali sana lakini wapumbavu wengi kama wanadanganywa na wao wanakubali eti elimu ni bure!

Ukitaka kuona tofauti ya hizi elimu jaribu kukaa na Watoto wa hizi shule za Kayumba na English Medium uongee nao na kupima maarifa yao katika mambo mbalimbali uone!
Kuna tofauti kubwa mno!

Serikali imeficha aibu yake kwa kuanzisha mitihani ya majibu ya kuchagua (a,b,c,d)! Eti hata hisabati majibu ni ya kuchagua!
Hoja dhaifu wanayokupa eti kurahisisha usahishaji mitihani ,eti wanafunzi ni wengi.
Ushahidi wa upuuzi huo ni kukuta Wanafunzi waliofaulu darasa la Saba kutoka Shule za Serikali wakiwa Secondary huku hawajui Kusoma na Kuandika!

Hata sisi tunaojinyima na kusomesha Watoto wetu English Medium ukilinganisha na wanaosoma mtaala wa CAMBRIDGE kuna tofauti kubwa sana!

Kusomesha Kayumba kwa asilimia kubwa ni kuchagua kuandaa Washabiki wa Simba na Yanga na wapiga kura basi! wenzenu wanaandaa Global Citizens ( raia wa Dunia)!

Kuna Wazazi juzi kati hapa habari zinarushwa eti wanapigana na Walimu kwa kuchangishwa shilingi elfu mbili (2,000) katika hizi shule za Serikali!

Watu tutafute pesa kadri tunavyoweza tuwape Watoto wetu elimu ya maana na tuache kabisa huu upuuzi wa ELIMU BURE!

Ogopa sana kuandaliwa chakula na mtu ambaye yeye hataki kabisa kutumia chakula hicho!

Nionyeshe mtoto wa Waziri au Mbunge anayesoma shule za Kayumba nikuonyeshe udhaifu wa elimu ulioko katika Shule za Serikali!

Angalia matokeo ya kidato cha pili 2023 katika Shule ya Sekondari DIPLOMASIA tena iliyoko Dar es Salaam ! ni aibu! Watoto wanapata Division 4 na Ziro basi!
Angalia shule binafsi kama Feza, Marian, Kemibos,Musabe,Waja n.k.
Hizo shule walishavuka habari za kujadili Division one, wao wanahadili wangapi wamepata Division One za point 7!
Serikali inawadanganya Wazazi masikini na wapumbavu kwamba mtoto mwenye Division Four naye amefaulu!

Shule ya Sekondari kama DIPLOMASIA ina andaa Mama Lishe , Wauza Vocha (Dadapoa), Mashabiki wa Simba na Yanga na wapiga kura basi!

Mwenye maarifa ashtuke wakati wapumbavu wanadanganywa na upuuzi wa ELIMU BURE!
 
Kuna msemo kwamba, " to every decision you make there is a price to pay or consequences"!
Hivi hali halisi ya watanzania unaijua au huijui? Serikali hailazimishi wananchi kupeleka watoto wao shule za serikali! Serikali imepanua wigo (fursa) kwa wananchi woote pamoja na masikini kupata elimu! Suala la kusoma na kufaulu linabaki kuwa jukumu la mwanafunzi na mzazi.

Wako wanafunzi waliotoka kaya masikini sana wakasoma shule za serikali chini ya kauli mbinu (elimu bure) na wamefaulu vizuri. Mleta mada kama una ukwasi wa kupelekea mwanao shule za binafsi usilete dharau kwa wasiomudu!
 
Mleta mada anaonyesha taswira ya viongozi wetu wanaoaminiwa na watanzania kushika nyazifa serikalini ili hali hawajui hali halisi ya watanzania. Ni kama kiongozi mmoja aliyeletewa habari ya wananchi wake kugoma na kuandamana kwa kupanda bei ya mkate! Kiongozi kashaangaa kuona wananchi wanalilia mkate akasema wapeni keki badala ya mkate.

Sasa kama mwananchi ameshindwa kumudu mkate ataweza keki? Serikali kutoa fursa ya elimu bure ni kuwawezesha wazazi ambao watoto wao wangeishia mitaani tena kwa umri mdogo kwa kuwapa fursa ya elimu. Tena mpaka wanamaliza kidato cha nne (kwa lazima) watakuwa na upeo na umri sahihi wa kupambana na maisha.

Walio makini wanafauli na kwenda kidato cha tano au vyuo na kupata taaluma. Sasa mleta mada sijui kama anaufahamu wa jamii pana ya kitanzania!
 
Hivi hali halisi ya watanzania unaijua au huijui? Serikali hailazimishi wananchi kupeleka watoto wao shule za serikali! Serikali imepanua wigo (fursa) kwa wananchi woote pamoja na masikini kupata elimu! Suala la kusoma na kufaulu linabaki kuwa jukumu la mwanafunzi na mzazi.

Wako wanafunzi waliotoka kaya masikini sana wakasoma shule za serikali chini ya kauli mbinu (elimu bure) na wamefaulu vizuri. Mleta mada kama una ukwasi wa kupelekea mwanao shule za binafsi usilete dharau kwa wasiomudu!
Swala si watoto wa wazazi masikini kupata furusa ya watoto wao kwenda shule. Kinachoongelewa ni mfumo mbovu wa elimu na mazingira mabovu ya kile kinachoitwa elimu bure.

Hii sera ilihasisiwa kisiasa bila kuangalia athari za huu mpango wa elimu bure. Kilichofutwa ni Karo tu ya sh. elfu 40 au 70, na kwa kiasi kikubwa ni mateso kwa walimu maana serikali haipeleki fedha ya kutosha na kwa wakati kuzipa pengo la hiyo fedha. Shule nyingi idadi ya wanafunzi ni kubwa ukilinganisha idadi ya walimu wanaotakiwa. Miundombinu mibovu nk.
 
Waliosoma hizo Feza schools na sisi tukasoma Kayumba schools tumekutana nao chuo kikuu na tunawaburuza kwelikweli.

Hao watoto wa shule za gharama hawana tofauti na kuku wa kizungu.
 
Hii kauli mkuu ya zamani. Hao wa feza wanajiamini, ni wachache sana utakutana nao vyuo vyetu hivi wao walishajiandaa tangu mwanzo kusomea mamtoni na huwezi wakuta wakitembeza bahasha maofisini.
Waliosoma hizo Feza schools na sisi tukasoma Kayumba schools tumekutana nao chuo kikuu na tunawaburuza kwelikweli.

Hao watoto wa shule za gharama hawana tofauti na kuku wa kizungu.
 
Swala si watoto wa wazazi masikini kupata furusa ya watoto wao kwenda shule. Kinachoongelewa ni mfumo mbovu wa elimu na mazingira mabovu ya kile kinachoitwa elimu bure.

Hii sera ilihasisiwa kisiasa bila kuangalia athari za huu mpango wa elimu bure. Kilichofutwa ni Karo tu ya sh. elfu 40 au 70, na kwa kiasi kikubwa ni mateso kwa walimu maana serikali haipeleki fedha ya kutosha na kwa wakati kuzipa pengo la hiyo fedha. Shule nyingi idadi ya wanafunzi ni kubwa ukilinganisha idadi ya walimu wanaotakiwa. Miundombinu mibovu nk.
Kwahiyo unatakaje?
 
Back
Top Bottom