Nadhani misahafu ndio imetufikisha hapa tulipo! Moja, kwa kuwa misahafu inasema tajiri ni ngumu kufika mbinguni. Matokeo yake ni kuleta dhana ya kupeana nafasi, ya kwamba tajiri atafaidi duniani, hana haja ya faida ya mbinguni. Maskini anahofu ya moto wa milele hivyo hayuko tayari kupigania haki yake, kuiba, kuwaadhibu majajiri ambao ni wezi wa share yake. Matarajio ya maskini ni kuwa tajiri ataadhibiwa na Mungu mwenyewe.
Hitimisho: nadhani kizazi cha maskini kilichopo sasa ni batili (hakina mtazamo wa mbali). Tumeambiwa tuitawale dunia na mambo yake. Sisi tumeshindwa, dunia ya wadhalimu inatutawala. Tumeshindwa kutekeleza maagizo ya Mungu. Kimsingi, nadhani Mungu ameamua kuteketeza kizazi hiki ili aanze upya na binadamu watakao kuwa tajiri na maskini wenye kujua haki na wajibu wao. Naamini Mungu yupo kwa kuwa napumua kwa msaada wake, nayo ni huruma tu kuona kama nitabadilika na kutambua wajibu na haki zangu, amasivyo ataniondoa siku yoyote!