Happy Birthday to me, kwaheri ujana. Sasa ni muda wa busara za kiutu uzima

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
HAPPY BIRTHDAY TO ME. KWA KHERI UJANA. SASA NI MUDA WA BUSARA ZA KIUTU UZIMA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Namshukuru Mungu. Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwangu. Nikiwa nimetimiza Rasmi miongo mitatu kamili(miaka 30). Nimejifunza mengi. Nimefanya mengi kwa muda huo.

Namshukuru Mungu hata ningekufa leo hii sina deni. Na wala nisingehitaji muda wa nyongeza. Najivunia ujana wangu. Umekuwa ujana wenye changamoto zenye furaha. Sina ninachojutia hata kimoja. Maisha yalikuwa rahisi sana.

Wakati nipo mtoto kabisa moja ya mambo niliyomwomba Mungu ni anipe changamoto zenye Furaha, anipe matatizo yenye utamu, anipe huzuni yenye tabasamu. Na hili Mungu amekuwa mwaminifu kwangu. Nilimwomba Mungu yule aliyeniumba na yule anijuaye vilivyo aniongoze katika maisha yangu. Na kamwe asiniache. Hata kama gharama ya jambo hilo ingekuwa ni Umaskini au kutokuwa tajiri basi nilikuwa nipo tayari.

Nilimuahidi Mungu nisiyemuona kupitia shahidi ambaye ni nafsi yangu mwenyewe kuwa, kama nitaishi dunia hii walau miaka 30 tuu basi nitakuwa mwaminifu katika kusaidia Watu maarifa na elimu atakayonipa Muumba wangu kwa gharama sawa bure kabisa. Na hiyo kwangu ingekuwa ni moja ya mafanikio makubwa katika maisha yangu ambayo yangenifanya nijihisi furaha.

Nakiri, nimefanikiwa. Kila muda nilipopata nafasi na yeyote aliyewahi kukutana na mimi tangu nikiwa mdogo anaweza kuwa shahidi kuwa nilikuwa mwema katika kutoa mawazo mema bila wivu, husda, na bila kuchangisha chochote. Na wale ambao hawakuwahi kuonana na mimi walipata maarifa na ujuzi kupita maandishi yangu.

Sihitaji miaka mingi kufanya sehemu yangu katika huu ulimwengu
Sihitaji umri mrefu kufurahia maisha yangu. Nilimwomba Mungu na kuahidi nafsi yangu kuwa NITAKUFA BILA YA DENI. NItaishi kwa furaha. Kila dakika kwangu itakuwa ni dakika ya furaha. Kwa sababu nitaipenda Haki, kweli, akili na Upendo.
Kwenye maisha, matarajio yangu makubwa ni muda nilionao sasa. Kufanya Wema ndio kitu pekee ambacho ninahitaji akili yangu isikisahau.

Sasa nimefikisha miaka 30. Mungu akiwa ameulinda ujana wangu. Ninaingia hatua ya pili muhimu kabisa. Hatua ya utu uzima. Hatua ambayo nitakuwa na BUSARA na Hekima itazidi sana.

Ni wakati ambao hata kama ninajua kitu sitakuwa mzungumzaji sana. Ni wakati ambao majibu yanaweza kuwa elfu moja lakini nikatoa jibu moja.
Ni hatua ambayo nitakuwa mratibu na mtazamaji lakini sitakuwa front.

Ninamshukuru Mungu kwa ujana wangu nime-inspire vijana wengi. Wapo waliodhani mimi ni mtu mzima. Lakini kumbe utu uzima sio Umri.
Na wapo Watu wazima wengi ambao wanamshukuru Mungu kwa kuniumba. Kile ambacho Mungu alitaka wajifunze kupitia mimi walikipata.
Nimebadili mitazamo ya wengi kwa namna ya ajabu. Namna bora zaidi.

Nilifanikiwa kuongea mambo ambayo kwenye jamii kwa wengi ni magumu kuzungumza. Niliweza kuonyesha kuwa uhuru wenye mipaka ndio Akili na maisha yenye furaha. Nilipinga utumwa wa kile kiitwacho mila na desturi na mapokeo ambayo ni potofu na ulaghai ili kuwatesa Watu.
Niliwasha taa kwenye vichwa vya Watu waliogizani wapate kuona.
Nilikuwa pilipili na shubiri kwa wale wasiotaka kweli na wanaopenda dhulma na wenye ubinafsi.

Nafahamu niliwakosea Watu wengi hasa wenye kupenda kudhulumu Haki za wengine. Nafahamu nilikuwa mbaya kwa wale Watu wasiotaka Ukweli usemwe.
Najua, wale wasiopenda maarifa na hekima walinichukulia kwa namna ipi.
Naelewa wenye mioyo ya chuki hawakupenda niutangaze UPENDO wa kweli kwa sababu kwao ubinafsi na dhulma ndio upendo. Vilio vya wengine kwao ndio sherehe. Kuwanyanyasa wengine kwao huchukulia kama heshima.

Kwangu mtu ni mtu tuu ingawaje wenye dhulma huondoa utu wa wengine kwa vigezo vya kijinsia, hadhi, elimu, dini na ukabila n.k.

Sijutii kuzaliwa. Pia sijutii kuishi. Kama vile ambavyo sitajuta nitakapokabiliwa na Hatma yangu. Sitaomba hata dakika moja ya nyongeza kuongeza maisha yangu. Kwa sababu kwangu maisha ni zawadi. Muda niliopewa nitautumia vizuri kwa uwezo wa Mungu.

Kitu pekee ambacho katika umri wa ujana ninachoweza kuwaasa vijana, kwani sasa nimeingia utu uzima ni mambo haya machache kwa ufupi;
1. Hakikisha unajitambua na kutambua watu wengine.
2. Jifunze kujidhibiti kihisia, kimwili, kiakili na kiroho.
Usikubali mwili au hisia au akili ikuendeshe.
3. Tafuta ujuzi na kazi. Ujitegemee.
4. Anzisha familia bora lakini ili Familia iwe bora lazima nawe uwe bora.
5. Heshimu Watu wengine bila kuwabagua.
Chukia maovu lakini usichukie muovu. Elewa Watu hubadilika. Aliyemuovu huweza kubadilika na kuwa mwema. Na aliyemwema huweza kubadilika kuwa mbaya.

6. Maisha yako lazima yawe na mchango katika jamii. Usikubali kuishi bila tija. Hakikisha jamii inapata mambo mema kutoka kwako, iwe ya kifikra, huduma, pesa au msaada wowote.
7. Usipende kufanyiwa vitu. Jitahidi ujitegemee.
8. Usilaumu wengine na usiwe malalamishi.
9. Usiwe kikwazo katika mafanikio ya wengine bali kuwa daraja. Usiwe mchoyo.

10. Usiendeshwe na maoni ya wengine hasa wenye mitazamo Hasi.
11. Penda Haki kwani ndipo amani yako ilipo.
12. Penda Ukweli kwani ndiko uhuru wako unapopatikana
13. Penda Maarifa na elimu kwani huko ndiko utakufanya uishi maisha mazuri yenye thamani
14. kuwa na UPENDO, kwani utaishi maisha ya furaha.

Sasa mimi nimeshaingia utu uzima. Miaka thelathini hii mingine nipo tayari kukabiliana na changamoto zenye furaha katika ngwe ya pili. Ombi langu ni lilelile ambalo natamani liwe lako pia. Yule aliyekuumba akuongoze na yeye ndiye ajuaye kilichobora kwako.

HAPPY birth day to Me, Taikon Master. Mtibeli halisi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Heri yakuzaliwa mkuu , wewe ulikua na busara za uzee katika ujana , kwa umri wako ni nadra sana kukuta kijana wenye maarifa makubwa hvyo kuhusu maisha, ukitoa mambo ya imani za ki Mungu nimejifunza mengi sana kutoka kwako,hongera sana mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom