Innocent Killer (The Revenge)

FEBIANI BABUYA

JF-Expert Member
Mar 5, 2022
1,035
1,925
Stori: Innocent Killer (The Revenge)
Msimuliaji: Bux the story teller
Umri: 18+
Sehemu ya Kwanza:

NB: Hadithi hii ni ya kubuni na kufikirika haihusiani na maisha ya mtu yeyote, wala taasisi yoyote wala mamlaka yoyote ile, lengo lake ni kuburudisha na kutoa burudani kwa wasomaji wangu.

ANZA NAYO.........................

Saa 6:59 za usiku kukiwa na kiza kinene na mvua kali sana nje kukisindikizwa na radi zisizo isha pamoja na upepo mkali wakati huo wa usiku kwenye chumba kimoja kidogo cha vitabu ambacho ndani yake anaonekana mwanaume mmoja akiwa kwenye meza ndogo ambayo alikuwa akiitumia kusomea anapokuwa ndani ya hicho chumba mbele yake palikuwa na vitabu kumi ambapo saba alikuwa ameviweka pembeni kuonyesha alikuwa amevisoma vilibakia vitatu ambavyo navyo ilikuwa ni lazima avimalize usiku huo huo kabla hakuja pambazuka. Vitabu vyote kumi vilikuwa ni vitabu vya sheria ya nchi ya Tanzania, aliangalia saa yake mkononi muda ulikuwa umeenda sana lakini hakuwa na namna ya kufanya ilikuwa ni lazima atimize kile ambacho kilikuwa mbele yake alipiga miayo na kuiweka vizuri miwani yake usoni akainama kinyonge sana kwenye kitabu huku akiwa na mawazo lukuki kwenye kichwa chake.

"Sina uhakika wa maisha yangu kuwa marefu baada ya kesho kwa maamuzi nitakayo yaamua najiona kuwa na maisha mafupi mno lakini mimi siwezi kuipindisha sheria ambayo nimeisomea kwa muda mrefu na naijua vizuri kuliko hata herufi za jina langu eeh MUNGU naomba unisaidie na kuniongoza katika hili" alitoka kwenye mawazo na kuivuta pumzi ndefu sana kisha akatulia na kuinamia chini kukipitia kitabu cha nane kati ya vile kumi ambavyo ilikuwa ni lazima amalize kuvisoma usiku huo.

Markvelous Japhary jaji mkuu wa nchi ya Tanzania ndilo lilikuwa jina la huyu mwanaume ambaye alikuwa ndani ya makataba yake ndogo nyumbani kwake akiwa anaendelea kujisomea vitabu vya sheria ambazo alizijua kiundani kuliko binadamu yeyote kwenye nchi yake. Kesho yake alikuwa na kesi kubwa sana ya kuitolea hukumu mbele ya mahakama ambayo ilikuwa inasubiriwa na taifa zima na ni tukio ambalo lilikuwa linaenda kurushwa na kushuhudiwa moja kwa moja mbele ya watu wote ndani ya nchi hii, alikuwa anaenda kuifanyia maamuzi kesi moja ya gaidi mmoja ambaye alikuwa na shutuma mbaya za kuweza kumuua mheshimiwa raisi wa nchi ya Tanzania kwa kumpiga risasi tano kwenye kichwa chake.

Alivuta kumbukumbu zake vizuri siku mbili zilizopita akiwa ndani ya ofisi yake maeneo ya posta simu yake ya mfukoni iliita aliiangalia alikuwa ni mheshimiwa makamu wa raisi aliipokea na kupokea taarifa nzito ambazo zilimfanya aache kila alichokuwa anakifanya aliambiwa kwamba raisi wa nchi ya Tanzania alikuwa amefariki dunia kwa kuuawa msako ulikuwa unafanyika kuweza kumpata mhusika na tayari kuna watu wamekamatwa kwa ajili ya mahojiano, hakuendelea na kazi tena siku hiyo alibeba kila ambacho kilikuwa ni cha kwake na kupanda gari yake ambayo aliiendesha kwa kasi sana bila kujali kama kuna tatizo zito linaweza kutokea kama angepata ajali na hilo gari lake, alikuwa amechanganyikiwa mwanaume ambaye alikuwa amekufa kwake hakuwa raisi wake tu alikuwa ni rafiki yake mkubwa ambaye walikua wote tangu wakiwa wadogo na kusoma pamoja alikuwa zaidi ya ndugu kwake aliumia mno aliitoa miwani yake na kufuta machozi yake akiwa yupo makini barabarani, alifika nyumbani kwake alimpita mkewe kama hamjui na kwenda chumbani ambako alikaa kwa dakika tano tu na kutoka akiwa amebadilika sura yake alijitahidi kujificha ila ilikuwa inatoa machozi muda wote.

"Who did this to my friend, oooh noooooo it's definitely impossible how can they let this happen?" Alikuwa amepanda kwenye gari yake alitoa simu mfukoni na kuipiga mahali.

"Nitakuwa hapo kwa dakika thelathini zijazo" aliongea kwa uchungu na kukata simu yake alitoka kwake kwa spidi mpaka mlinzi wa getini alibaki anamshangaa sana bosi wake alikuwa ni mtu mpole na alimjua vyema hakuwa mtu wa pombe kabisa kwenye maisha yake leo alikuwa kama mtu aliye lewa kama sio kupandwa na wazimu hata mkewe ambaye alikuwa amesimama juu ya nyumba hiyo ya ghorofa alibaki anamshangaa mumewe kwa hali ambayo alikuwa nayo jioni hiyo. Safari yake ilienda kuishia nje ya nyumba moja kubwa maeneo ya Makongo juu hapo palikuwa nyumbani kwa CDF mkuu wa majeshi wa nchi ya Tanzania mheshimiwa Jaiwelo mkupi makubilo, alikuwa anajulikana sana hapo ila alishangaa leo anavyotaka kuingia alizuiliwa mlangoni na kuulizwa kama alikuwa na miadi ya mtu huyo alimpiga jicho kali sana huyo mlinzi ambaye alimzuia bila shaka alikuwa ni mwanajeshi.

"We mjinga hivi unajua unaongea na nani ambaye unanizuia leo kuingia humu ndani?" Aliongea macho yake yakiwa mekundu wakati huo alikuwa amemkunja mwanajeshi huyo shingoni ilikuwa ni dharau sana kijana mdogo kama huyo kumsimamia jaji mkuu wa serikali na kumzuia kirahisi sana namna hiyo
"Najua lakini tumeambiwa tusimruhusu mtu yeyot....." Kabla hajaongea maneno yake yote simu yake ya mfukoni iliita, aliipokea na kuitikia mara moja tu.

"Nisamehe mkuu" kisha akasogea pembeni kumuacha jaji huyo apite kuonyesha kwamba aliipokea amri ya upande wa pili kumuacha mwanaume huyo aingie ndani bila kupata kizuizi chochote kile.

"We mjinga kwa hiki ulicho kifanya baada ya hapa nitakurudia uelewe namna ya kuishi na watu wakubwa kwenye nchi hii" mheshimiwa jaji mkuu alikuwa kama amechanganyikiwa usoni kwake kulikuwa na machozi mengi kama mtoto mdogo, alinyoosha moja kwa moja mpaka juu kabisa sehemu ya makutano ni wazi alikuwa mwenyeji sana kwenye nyumba hiyo alimkuta mtu ambaye alikuwa amemjia hapo.

"Unajua kilicho tokea?" Alisahau hata kusalimia alimuuliza mtu huyo huku akiwa amemkazia macho kwa hasira sana
"Ndiyo"

"Nina imani utakuwa umejua nani aliye husika na hili kupitia jeshi lako"?" Jaiwelo mkupi makubilo hakuongea chochote alitembea mpaka kwenye droo moja ndogo sana akatoa frashi ndogo na laptop akaja nayo mpaka pale alipokuwa amekaa mheshimiwa jaji mkuu, aliichomeka hiyo frash kwenye hiyo laptop na kuifungua ilionekana video moja tu humo ndani akairuhusu iweze kuanza kisha akaigeuzia kwa mheshimiwa jaji mkuu.

"Yuko wapi huyu shetani" aliuliza kwa hasira sana akifuta machozi yake baada ya kuweza kushuhudia namna mheshimiwa raisi alivyoweza kuuawa.

"Tayari yupo kwenye mikono yetu amekamatwa muda sio mrefu baada tu ya kutenda hili tukio"
"Amewekwa wapi muda huu namhitaji kwenye mkono wangu".

"Mark relax this is not easy as you may think, aliye uawa ni raisi wa nchi sio raia wa kawaida tu mtaani"
"No matter what I'm going to kill this idiot".

"Please don't do that kwa usalama wako na wa familia yako nisikilize kwa sasa tu tafadhali sana usifanye chochote" hakumjibu kitu mkuu wa majeshi zaidi ya kuibeba frash hiyo ambayo ilikuwa na ushahidi wote kisha akarudi zake nyumbani kwake akiwa amechanganyikiwa sana, kumbukumbu zake ziliishia hapo.


**********************
Raia wengi walilaani sana hicho kitendo cha mtu huyo kufanya hilo jambo walitaka auawe mpaka kunyongwa mbele ya mahakama wakiwa wanaona iwe kama fundisho kwa watu wengine, ushahidi kwa asilimia zaidi ya miamoja ulikuwa ukionyesha kwamba ni kweli mtu huyo alihusika moja kwa moja na hayo mauaji lakini mheshimiwa jaji mkuu alikuwa amepokea simu nyingi sana za kumtaka afanye namna yoyote ya kuipindisha hiyo kesi na kutengeneza ushahidi wa uongo ambao ungemuweka salama mtuhumiwa huyo ambaye mpaka muda huo hakuwa akijulikana ni nani. Akiwa ameanza kusoma kitabu chake hicho cha nane ghafla sana radi kali ilipiga umeme ukazima alihema kwa wasiwasi akianza kutokwa na jasho jingi usoni kwake mara simu yake ikaanza kuita kwenye hicho kiza kinene aliangalia namba ilikuwa ngeni kabisa hakuwahi kuiona kabla alisita kuipokea iliita mpaka ikakata. Sekunde kama kumi tu uliingia ujumbe ambao alisita sana kuufungua lakini hakuwa na namna.

"ANGALIA DIRISHANI KWAKO HAPO KWA NJE UTAONA MTU, KAMA KESHO UKIFANYA UJINGA WOWOTE ULE BASI FAMILIA YAKO ITAINGIA KWENYE KUNDI LA WANADAMU AMBAO WALIWAHI KUFA KIKATILI SANA ZINGATIA NILICHO KWAMBIA KESHO SAA NNE ASUBUHI MAAMUZI YAKO NDIYO YATAKAYO AMUA HATIMA YA MAISHA YA FAMILIA YAKO" ni ujumbe ambao ulimfanya aanze kutetemeka sana alitoa kitambaa mfukoni na kujifuta jasho lililokuwa linamtiririka usoni, aliiwasha tochi yake kubwa na kusogea dirishani kukiwa bado kuna kiza cha kutisha nje alifungua dirisha taratibu na kuchungulia nje alimulika tochi alishangaa baada ya kumuona ninja mmoja akiwa na mapanga yake mawili mgongoni amesimama pale chini, alionekana ni muda mrefu sana alikuwa ananyeshewa na mvua muda wote pale aliogopa mno.

Aligeuka nyuma baada ya kusikia kama kuna hatua za mtu lakini akahisi ni kichwa chake hakipo sawa aliyarudisha macho yake pale chini hakuona kitu chochote wala hapakuwa na alama ya uwepo wa mtu alianza kurudi nyuma taratibu kwa uoga aligeuka na kuchomoa bastola yake akainyooshea sehemu ambayo alihisi kuna mtu anakuja ghafla sana umeme ulirudi alishangaa mkewe amesimama mbele yake akimshangaa mumewe ameshika bastola tena ameelekezea kwake, aliishusha na kuiweka mfukoni haraka huku akiwa anatokwa na jasho jingi mno, mkewe alimfuata pale na kumkumbatia akiwa ana mpiga piga mgongoni.

"Punguza mawazo mume wangu najua siku ya kesho inakuumiza sana akili muachie MUNGU ila hakikisha unaamua kile kilicho bora mimi siku zote nipo nyuma yako kwa kila jambo" sauti moja ya kinanda mrembo sana ilimfanya atabasamu kwa mara ya kwanza tangu kuingia kwenye hicho chumba, huyu ndiye binadamu pekee ambaye alikuwa anamjua kuanzia unyayo wake mpaka nukta ya mwisho ya unywele wake kichwani, akiwa mbele ya huyu mwanamke alikuwa anapata amani sana ya moyo aliinama na kumbusu mkewe tumboni ambapo palikuwa pametuna kuonyesha ilikuwa ni mimba kubwa tu.

"Is my son wonderful?" Aliuliza akichekelea kuonyesha wazi aliifurahia mimba hiyo kuwa ya mtoto wa kiume japo moyoni hakuwa na furaha yoyote ile.

"Hahahaha ananipiga mateke tu nafikiri dada yake atafurahia sana akizaliwa maana alikuwa anatamani sana kuwa na kaka yake pale anapokuwa anaonewa" mkewe alijibu huku akijitoa mwilini na kusogea pale mumewe alipokuwa anasomea.

"Jitahidi basi mume wangu uwe unapata muda wa kupumzika na leo usichelewe sana kulala kesho ni siku mhimu sana" alitabasamu baada ya kuisikia sauti ya mwanamke aliye mpenda sana, alimfuata na kumbusu kwenye paji lake la uso.

"Nakuja baada ya nusu saa tu mke wangu" alijibu kiunyenyekevu hakuhitaji kumuudhi mama kijacho wake alitabasamu na kuanza kuelekea mlangoni lakini aligeuka kabla hajatoka.

"Jason umempigia simu kumueleza hichi kinacho endelea?" Swali la mkewe lilimshtua kidogo mwanaume ambaye alikuwa anauliziwa hapo alikuwa ni mdogo wake wa damu kabisa ambaye alikuwa nje kimasomo jina lake alifahamika kama Jason Japhary na walizaliwa wawili tu.

"Anapenda mno kulala yule nitampigia simu baada ya kumaliza kesi kesho usijali" aliongea kikakamavu ila mwili wake ulikuwa unamsaliti alikuwa akitetemeka sana mkewe alimuonea huruma sana mume wake alikuwa kwenye wakati mgumu sana hakuwa na namna aliondoka na kwenda kulala. Jaji mkuu alibaki kwenye hicho chumba lakini hakuwa na mood ya kusoma tena alibaki akiiwazia ile meseji aliyotumiwa pamoja na alicho kishuhudia nje alijikuta akiogopa mno.

Ndo kwanza tunaifungua sehemu ya kwanza kabisa ya hadithi yetu mpya ya INNOCENT KILLER (THE REVENGE), the magic finger mwenyewe nipo na kalamu yangu....Bux the story teller.

TWENDE PAMOJA MPAKA MWISHO
FB_IMG_1666177524791.jpg


Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
TELLER: Bux the story teller
WhatsApp: 0621567672
Email: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA PILI
SONGA NAYO................

Kulikucha asubuhi na mapema sana baada ya kunyanyuka kwenye kitanda chake aligeukia pembeni yake hakuweza kabisa kumuona mumewe kipenzi alishtuka sana mama kijacho wa jaji mkuu, aliamka haraka na kujisogeza kwenye chumba cha kujisomea ambako ndiko alijua mumewe mara nyingi sana mtu huyo alikuwa anapenda kuwa. Alimkuta kama alivyo muacha jana yake usiku hakupata hata tone la usingizi alikuwa amejiinamia mkononi ameishika kalamu yake ya wino akiwa anaiangalia kwa umakini sana mkewe alimsikitikia mno mumewe alikuwa anateseka sana.

“Umelala hata kidogo?” alimuuliza kwa upole japo alielewa kwamba mtu huyo tangu jana yake hakuweza kabisa kulala wala kuigiza kuupata usingizi.

“Najihisi kama nimelala mwaka mzima sina hata tone la kuigiza tu la usingizi mwili wangu umegoma kabisa kuleta hisia za kitu kinacho itwa usingizi tangu jana ulivyo niacha hapa”

“Unahisi utajitesa hivyo mpaka lini? Kwa sababu kuna muda kwa nafasi yako utakuwa ukikutana na kesi za ajabu za kutisha sana kama unajiona kwamba hauko sawa una nafasi ya kumteua jaji mwingine yeyote asimame kwa niaba yako leo mahakamani”

“Hakuna kesi ambayo itakuja kuwa mbaya na ya kutisha kuizidi kesi hii huyu aliye uawa ni mheshimiwa raisi wa nchi lakini ukiacha hilo aliyekufa ni rafiki yangu halafu unakuja kuniambia nimuachie mtu mwingine kesi hii unahisi kuna mtu gani ataweza kuzikataa pesa kwa majaji waliopo? Kuna muda uwe unawaza kama mtu mzima” aliongea kwa hasira sana akiwa anatokwa na machozi haikuwa kawaida kwake yeye kuongea kwa ukali sana namna hiyo mbele ya mkewe, mkewe alijua amemkosea mumewe alihitaji kumuomba msamaha lakini ni kama alichelewa mtu huyo alitoka humo ndani muda huo huo alienda kujifungia chumbani ambako baada ya dakika kumi tu alitoka akiwa amevaa zake suti na begi mkononi hakuweza hata kumuaga mkewe siku yake ilikuwa imeharibika asubuhi na mapema kabisa.

Alifika nje na kutoa maagizo kwa walinzi wake haikuwa taabu kwa sababu alikuwa mtu mkubwa hivyo hata ulinzi wake ulikuwa ni wa namna yake, aliondoka na gari yake pamoja na walinzi kadhaa na dereva wake kuelekea mahakamani. Akiwa njiani mawazo yalimpeleka mbali sana.

“Unajua kwanini sipendi siasa?”
“Haujawahi kabisa kunipa sababu”

“Siasa ina mambo ya kutisha sana ndani yake ndiyo maana naiogopa sana nilishawahi kusikia kesi kadhaa nikajikuta nawaogopa mno hawa wana siasa rafiki angu nakuona kabisa umenogewa sana huko jiangalie sana maisha yako ndugu yangu tunaishi mara moja tu”

“Mark shida yako wewe ni muoga sana unajua hii nchi inahitaji viongozi wenye maono makubwa ambao bado ni vijana na hao viongozi wenyewe ndio sisi, ebu acha kuogopa kiasi hicho rafikio angu kama kila mtu angekuwa muoga sana namna hiyo basi mpaka leo nchi hii isingekuwa imepata uhuru tungekuwa tupo bado chini ya watu”

“Huwa naipenda sana nukuu ya methali moja inasema KINGA NI BORA KULIKO TIBA ina maana kubwa sana ndani yake ukiielewa vizruri. Ni kweli nchi inahitaji viongozi wenye maono na vijana lakini hao wenzetu ambao unawaona wanafanya hivyo tayari wana watu, wana mifumo na wana njia mbalimbali za kukimbilia hasa pale yanapotokea matatizo, wanajua tunaingilia hapa na tunatokea hapa sasa wewe hapo likitokea tatizo utakimbilia wapi na anakulinda nani? kumbuka hapa nakushauri kama marafiki ambao tumetoka mbali sana pamoja mimi sihitaji kukupoteza kabisa kwenye maisha yangu” zilikuwa ni kumbukumbu za Markvelous Japhary akiwa ndani ya gari lake, alikumbuka siku moja akiwa anamshawishi rafiki yake ambaye alikuwa anaipenda na kuihusudu siasa kuliko kitu chochote kile kwenye maisha yake lakini mwenzake huyo hakuweza kabisa kukubaliana na hilo jambo aliamua kuziishi ndoto zake ambazo kweli zilimpeleka mpaka Ikulu akasimama kama raisi wa nchi na ndiye ambaye aliweza kumteua Markvelous Japhary kuwa jaji mkuu kutokana na uwezo wake mkubwa lakini pia kama rafiki ambaye wametoka naye mbali sana.

Huyu ndiye aliyeweza kuyabadilisha maisha ya jaji mkuu wa Tanzania

“Kwa yeyote aliyehusika na hili hakika sitaweza kumuacha akiwa hai haitajalisha nitajiingiza kwenye matatizo gani ila lazima nihakikishe amekufa mbele kabisa ya mahakama kama malipo kwa walicho kifanya kwa rafiki yangu, najua watakuwa wameandaa watu wengi kwa ajili ya kumtetea mtu wao ili aachiwe huru ila mwamuzi wa mwisho ni mimi hapa lakini kuna maswali najiuliza huyo muuaji aliweza vipi kupatikana kirahisi sana namna ile? Mkuu wa majeshi hajanipa undani wa mambo ebu ngoja kwanza niweze kumalizana na hili kisha nikae nae vyema aweze kunisimulia kwa undani” alishtuka kutoka kwenye kuongea mwenyewe baada ya mlinzi wake kumfungulia mlango alijiweka saw ana kushuka tayari alikuwa kwenye eneo la mahakama.

“Afe huyo, afe huyo”
“Hakikisha unamuua hawezi kutuondolea kiongozi wetu”
“Afe afe ikiwezekana aletwe kwetu tuondoke naye afe huyo afe” zilikuwa ni kelele ambazo alizisikia kwa wananchi wenye hasira kali walichukizwa mno na raisi wao ambaye walimpenda sana kuuawa walihitaji mtuhumiwa aweze kuuawa. Hilo jambo lilimpa nguvu sana jaji baada ya kuona wananchi wote walikuwa wapo upande wake, akiwa anajiandaa kuanza kuelekea lilipo lango kuu la mahakama aliivua miwani yake baada ya kuona gari la magereza linaingia likiwa na ulinzi mkali mno dakika mbili zilipita alishushwa mwanaume mmoja mwenye upara na ndevu nyingi sana ambazo ni muda mrefu hazikuwahi kunyolewa, alikuwa kwenye minyororo mizito alivyo inua uso wake moja kwa moja alikuwa anaangaliana na jaji mkuu mwanaume huyo alimkonyeza jaji mkuu huku akitema mate chini, ni moja ya dharau kubwa sana ambayo aliifanya hapo. Markvelous aliitoa miwani yake na kumuangalia vizuri huyo mwanaume kwa hasira ambazo wazi wazi macho yalizungumza kwamba kama leo ukipona wewe shetani basi mimi naacha kazi ya kuwa jaji narudi kijijini kulima vitunguu na kuchambua dagaa.

Alianza kutoka pale na kuelekea kwenye ofisi yake humo mahakamani akavae nguo za kazi wakati huo maaskari wakiwa wanatangulia na mtuhumiwa kumpeleka kizimbani, akiwa anaingia kwenye lango kuu la mahakama alipokea meseji mbili kwenye simu yake ambazo zilipishana kwa dakika moja na nusu tu moja ilikuwa imetoka kwa CDF Jaiwelo Mkupi Makubilo na nyingine ilitoka kwenye namba ambayo bila shaka alikumbumbuka kwamba ilimtafuta jana yake usiku wa manane.

‘’USIFANYE MAAMUZI YA HASIRA MARK HILI NI JAMBO ZITO SANA LA NCHI NZIMA, HII NI KWA USALAMA WAKO NA FAMILIA YAKO LAKINI PIA KWA TAIFA ZIMA LINATEGEMEA MAAMUZI YAKO SAHIHI LEO” aliisoma meseji ya CDF ila hakujihangaisha hata kuijibu aliifungua hiyo ya pili.

“UNA DAKIKA CHACHE SANA ZA KUFANYA MAAMUZI YA BUSARA KWA AJILI YA KUIKOMBOA FAMILIA YAKO KISHA BAADA YA HAPO UTAINGIZIWA SHILINGI ZA KITANZANIA BILIONI KUMI KWENYE AKAUNTI YAKO YA BENKI UTAKAPO TOA TO MAAMUZI YA BUSARA NA YA KIUME ILA ZINGATIA SANA KAMA UKIENDA KINYUME KITABU CHAKO NA FAMILIA YAKO KINAENDA KUFUTWA KWENYE HUU ULIMWENGU” hii ni meseji ambayo ilimfanya atoe kitambaa kwenye mfuko wake na kujifuta jasho ambalo lilikuwa limeanza kumtoka kwenye uso wake alihisi joto kali mno, alihema kwa nguvu na kuizima simu hiyo hakuhitaji kujisumbua nayo tena.

Tukio la kesi ya mtuhumiwa wa mauaji ya mheshimiwa raisi lilikuwa linaonyeshwa moja kwa moja mubashara kabisa kwenye kituo kikubwa cha televisheni cha nchi kilicho julikana kama Tanzamax, kilikuwa ni kituo ambacho siku zote kilitoa habari za kuaminika na zenye uhakika zaidi na kilipendwa sana na wananchi hususani wale ambao huwa wanapenda sana kupata habari moto moto ambazo huwa zinajiri ndani ya nchi yao kutoka kwa watangazaji wao mahiri ambao walipendwa sana ndani ya nchi ya Tanzania.

“Tanzania oyeeeeeee”
“Nchi yetu oyeeeee”
“Idumu nchi yetu ya amani”
“ALale mahali pema peponi kipenzi chetu raisi wetu ambaye tutampenda siku zote za maisha yetu”
“Tanzania ya amani inawezekana”
“Uishi miaka mingi mheshimiwa jaji mkuu”
“Tanzania oyeee”
“Sisi ni watanzania”
“Tunaipenda Tanzania yetu” zilikuwa ni sauti kubwa za shangwe na vigelele vingi japo vilitoka kwenye vinywa vya watu kwa majonzi sana baada ya kusikia kauli ambayo iliwafariji sana na kuyafuta machozi yao kwa kumpoteza mpendwa wao ambaye ni wazi walimpenda sana

“WITH THE CLEAR EVIDENCE FOUND I SENTENCE YOU TO PUBLIC DEATH BEFORE THE COURT MR ABIR MUSHKANI (KWA USHAHIDI WA WAZI ULIO PATIKANA NAKUHUKUMU KIFO CHA HADHARANI MBELE YA MAHAKAMA MHESHIMIWA ABIR MUSHKANI)” Hii ndiyo kauli kutoka kwa jaji mkuu ambayo iliwapa matumaini wananchi ambao walikuwa nje ya mahakama na hata wale ambao walikuwa wanaona hilo tukio moja kwa moja kwenye runinga, hukumu hiyo ilifuata baada ya takribani masaa manne kupita wakiwa wanaiendesha kesi hiyo ambapo wanasheria wengi wakubwa na wabobevu walikuwa wakimtetea sana mtuhumiwa ila wote walikuja kunyong’onyea baada ya jaji mkuu mwenyewe kuonyesha ushahidi wa video moja kwa moja wa mtu huyo akiwa anafanya hilo tukio, ni jambo ambalo lilikuwa wazi hakukuwa na namna ya kulikataa tena.

Mtuhumiwa aliyejulikana kama Abir Mushkani alinyongwa hadharani mahakamani akiwa na minyororo yake mwilini kwa sababu alionekana kuwa mtu hatari sana kama angefunguliwa hapo, hilo tukio lilionyeshwa moja kwa moja ili kama kuna wengine wenye tabia kama zake waweze kukoma mara moja, ni tukio ambalo lilimpa heshima kubwa sana Markvelous Japhary ambaye aliona kama ametua mzigo mzito kwa kulipa kisasi kwa kifo cha rafiki yake japo kwa kutenda haki. Alitoka mahakamani na kuingia kwenye chumba chake aliichukua simu yake kwenye begi lake akaiwasha, alijaribu kumpigia mkewe kwa sababu asubuhi waligombana alihitaji kumuomba msamaha kwa kumkosea na kumtamkia maneno makali sana simu iliita kidogo na kukata akahisi huenda mkewe bado alimkasirikia, alijaribu kupiga kwa mara ya pili haikupatikana akajaribu tena na tena lakini haikupatikana kabisa.

Akiwa amekata tamaa alipokea ujumbe kwenye simu yake meseji zilikuwa mbili ilionekana zilitumwa muda kidogo sema kwa sababu aliizima simu ndiyo maana ziliingia kwa kuchelewa watumaji walikuwa ni wale wale.

“UMEFANYA MAKOSA MAKUBWA SANA MARK ILE VIDEO HAIKUTAKIWA KUONYESHWA HADHARANI NAMNA ILE UNAYAJUA MADHARA YAKE?” Ilitoka kwa CDF haikumshtua sana yapili ilitoka kwenye ile ile namba ambayo tangu jana ilimpa sana onyo.

“UNA DAKIKA KUMI NA TANO TU ZA KUWAHI NYUMBANI KWAKO KAMA UTAFIKA NDANI YA HUO MUDA UNAWEZA UKABAHATIKA KUIKUTA FAMILIA YAKO SALAMA ILA ZAIDI YA HAPO UTAUJUTIA SANA ULIMWENGU HUU NA NILIKWAMBIA MAPEMA” meseji iliishia hapo hakukumbuka hata kulivua vazi lake linalo mtambulisha kama jaji mkuu alitoka nje akiwa anakimbia sana.

Mchezo ndo kwanza unaanza chukua juisi safi na popcorn tuweze kusonga pamoja.

Bux the story teller.
 
Hii ni simulizi ya kijasusi.....ambayo inamhusu kijana mmoja aliyepatwa kuitwa Jason.

Kijana huyu alikuwa ni mdogo wa jaji mkuu wa nchi ya Tanzania. Ambaye alikuwa akisoma ndani ya nchi ya Marekani.

Alikuwa kijana wa kawaida sana kwenye macho ya watu ambaye alikuwa na mpenzi wake waliyekuwa wakisoma wote.

Mpenzi wake huyo alikuwa ni Agenti wa CIA bila kijana huyo kujua.

Kisa kinaanzia wapi?

Raisi wa nchi ya Tanzania anapigwa risasi tano za kichwa akiwa kwenye gari safarini baada ya kufika Manzese Tiptop darajani. Kesi hiyo inaangukia kwenye mkono wa jaji mkuu, ambaye alikuwa ni rafiki wa karibu wa raisi, anaapa kumuua aliye husika na tukio hilo mbele ya mahakama.

Lakini je nini sababu ya mheshimiwa raisi kupigwa risasi na mhusika ni nani?

Jaji huyo usiku mmoja kabla ya hukumu anapewa onyo kwenye simu kwamba aupindishe ukweli siku ya hukumu....

Siku ya HUKUMU.
Anamsomea hukumu ya kunyongwa mhusika ambaye ananyongwa mbele ya mahakama. Baada ya kutekeleza hilo anapokea simu ya kumpa dakika 15 tu za kuiokoa familia yake.

Anakimbia na kufika nyumbani anakuta mkewe amechomwa kisu cha tumboni akiwa mjamzito, hali yake ikiwa na matumaini mengi ya kukatika muda mchache ujao, huku mwanae wa kike akiwa ameuliwa.

Anapiga simu kwa mdogo wake kumpa taarifa lakini naye anatokewa na mtu, kisha anauliwa huku akiwa amefanikiwa kumtamkia mdogo wake kwamb..... "THEY HAVE KILLED YOUR BROTHER"(Wamemuua kaka yako).

Mauaji anayofanyiwa yanafanana na namna raisi alivyo uliwa. Sasa kama mtuhumiwa alinyongwa vipi mauaji yawe yale yale kama ya raisi? INAZALIWA SITOFAHAMU.

Kijana huyo kwa uchungu anarudi kumzika kaka yake na mheshimiwa raisi wa nchi yake ambaye walijuana vyema kwa mengi yaliyokuwa yamejificha nyuma.

Siku kadhaa baada ya msiba, watu wanakutana na tangazo ambalo linawataka wahusika wa mauaji ya jaji mkuu na raisi wajitokeze hadharani, mtu huyo anawapa miezi sita, wakisha jitokeza, waombe msamaha kwa jamii atawaacha hai..kama muda huo utaisha bila wao kufanya hivyo basi huyo mtu atafanya anavyotaka yeye..

Hapo ndo tunaenda kumfunua huyo Jason na kumjua yeye ni nani baada ya kuanza kufanya mauaji ya kutisha sana.
FB_IMG_1680324048558.jpg
 
Wasalaam,

Kwema?

Ni natumaini yangu mpo safi kabisa.

Hii ni simulizi yangu ya 5 kuiandika na ndiyo ambayo tunaenda kuanza nayo kwa sasa, ukiachana na hii nimeandika simulizi zifuatazo;

1. ULIMWENGU WA WATU WABAYA
2. I WANT TO DIE JUDGE
3. GEREZA LA HAZWA
4. HATIMA YA UJINGA WAKE
5. INNOCENT KILLER ambayo ndiyo hii.

Simulizi hii mpaka hivi ninavyo ongea ipo ukurasa wa 70 na bado inaendelea kuandikwa.

Mpaka nilipo fikia ukiitaka yote ni 5000.

Hii ndiyo ambayo tutakuwa tunaisoma kwa sasa na kwa sababu sijaimaliza, tutakuwa tunaisoma mara mbili kwa wiki, jumatano na jumamosi.

Jumatano ambayo ni leo, kwa sababu tunaanza nitaweka kurasa zake mbili, halafu tutaendelea tena jumamosi.

Ni hayo tu ila nawakaribisha wote,

Wasomaji,wenzangu ambao huwa wanatutia moyo kwa kutokuwa na uchoyo wa kukomenti na kuchangia chochote kitu pia, wale wapita kimya, na hata wale ambao huwa wanatutolea uvivu waandishi, kasoro tu wanao tukana (hakuna anaye kukataza ila ni ustaarabu tu) NAWAKARIBISHENI MNO.

Pia naombeni kwa wote ambao nitakuwa nimewakwanza kwa namna moja ama nyingine mnisamehe sana. Huenda nimeteleza na najua nitaendelea kuteleza pia.



0621567672 (whatsapp)
FB_IMG_1680324048558.jpg
 
Gereza la Hazwa imeondolewa leo JF au vp? Maana nilikuwa pg ya 250.Leo hata ukisearch haipatikani
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
TELLER: Bux the story teller
WhatsApp: 0621567672
Email: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA TATU
SONGA NAYO................

Teri meri, meri teri prem kahani hai mushkil
Do lafzon mein yeh bayaan na ho paaye
Ik ladka ik ladki ki yeh kahani hai nayi
Do lafzon mein yeh bayan na ho paaye

Yours and mine, mine and yours, love story is difficult,
can't tell it in two words,
This story of a girl and a boy is new,
can't express it in two words..

Teri meri, meri teri prem kahani hai mushkil
Do lafzon mein yeh bayaan na ho paaye
Ik dooje se hue juda Jab ik dooje ke liye bane

Yours and mine, mine and yours, love story is difficult,
can't tell it in two words,
Separated from each other when made for each other..

Tumse dil jo lagaya toh jahaan maine paaya
Kabhi socha na tha yoon meelon door hoga saaya
Kyun khuda tune mujhe aisa khwaab dikhaya
Jab haqeeqat mein use todna tha
When I loved you, I got the world,
but never thought (even) your shadow will be miles away,
O god why you gave me such a dream,
when you had to break it in reality..

Ik dooje se hue judaa, jab ik dooje ke liye bane
Teri meri, meri teri prem kahani hai mushkil
Do lafzon mein yeh Bayaan na ho paaye

Teri meri baaton ka har lamha sabse anjaana,
do lafzon mein yeh bayaan na ho paaye
Every moment of your amd my talks is unknown to all else
can't express it in two words..

Har ehsaas mein tu hai har ik yaad mein tera afsaana
Do lafzon mein yeh bayaan na ho paaye

You're in every feeling, and your story in every memory
can't express it in words..

Sara din beet jaaye, Saari raat jagaye
Bas khayal tumhara lamha lamha tadpaye
Yeh tadap keh rahi hai mit jaaye faasle
Tere mere darmayaan hai Jo saare

The entire day passes, all the night I am awake,
Your thought troubles me day and night,
this longing is saying that the distances should go
which exist between you and me..

Ik dooje se hue juda Jab ik dooje ke liye bane
Teri meri baaton ka har lamha sab se anjaana
Do lafzon mein yeh Bayaan na ho paaye

Har ehsaas mein tu hai har ik yaad mein tera afsaana
Do lafzon mein yeh bayaan na ho paaye

Teri meri, meri teri prem kahani hai mushkil
Do lafzon mein yeh bayaan na ho paaye

Ni moja ya wimbo bora sana kwenye historia ya mapenzi duniani, ni muziki ambao unapatikana kutoka kwa moja ya waigizaji bora sana kutoka bara la Asia ndani ya taifa la India, anaitwa SALMAN KHAN (THE BIG BOSS) pamoja na Himesh Reshammiya japo waimbaji wa wimbo huo ni Rahat Fateh Ali Khan, Shreya Ghoshal. Jina la wimbo unaitwa TERI MERI unapatikana kwenye movie ya BODYGUARD yakwake SALAMAN KHAN wakati akiwa anamwimbia mtoto wa bosi wake ambaye alimpenda Kwa siri muda mrefu sana bila SALMAN KHAN mwenyewe kujua kwa sababu yeye alikuwa ni mlinzi wa mtoto huyo wa kitajiri.

Huo wimbo haukuja tu bali zilikuwa ni kumbukumbu nzito ambazo zilikuwa zinakisumbua kichwa cha mwanaume mmoja akiwa ndani ha gari yake akiwa anamuwahi yule nyonga mkalia ini wake, Markvelous Japhary ndiye mwanaume ambaye alikuwa anayakumbuka maneno matamu sana ya kwenye huo wimbo yalimpeleka mbali sana na kumfanya afute machozi yake usoni.

Miaka kadhaa iliyopita nyuma alikuwa akiyasikia hayo maneno kutoka kwenye kinywa cha mtu ambaye alikuja kukiri mbele ya dunia kwamba alimpenda sana mwanamke huyo, alijitahidi sana kuweza kuficha lakini bahati mbaya sana ulimwengu ulitaka kumuumbua na maradhi yake hakuweza tena.

LOVERS DREAM LOUNGE
Ilikuwa ni lounge moja ya kisasa Kwa aina yake ambayo haikuwa mbali sana na barabara kubwa ambayo ndipo magari mengi sana yalikuwa yanapita, siku moja kijana mmoja baada ya kumaliza elimu yake ya kidato cha sita alikuwa na kazi nzito sana ya kumpambania mdogo wake wa damu ambaye naye alikuwa akimsomesha mwenyewe, licha ya kusubiri majibu yake ya kuweza kwenda kuendelea na elimu yake ya chuo kikuu alikuwa anapambana na mtaa ili kuweza kumuandalia mazingira mazuri mdogo wake ambaye alimpenda sana kwenye maisha yake, hakuna kitu kingewekwa mfano wa kulinganisha na namna alivyokuwa akimpenda na kumjali ndugu yake wa pekee. Usiku mmoja akiwa.anatoka kwenye moja na mbili za kutafuta chochote kitu ili mdogo wake aamke na furaha ya aina yake ndipo alipo bahatika kupita kwenye lounge hiyo ambayo ilikuwa ni maarufu sana kwa sababu ilikuwa ndiyo njia ya yeye kupita kila siku.

Leo ilikuwa ni tofauti kidogo alivuka Ile sehemu lakini nafsi yake iligoma kabisa akaamua kurudi hatua mbili ili aamini kama masikio yake yalikuwa yanamdanganya au yalikuwa yapo sahihi kama.alivyohisi, baada ya kurudi zaidi hatua kama kumi nyuma ndipo alipopata bahati ya kukithibitisha kile ambacho alikisikia. Ni moja ya sauti nzuri sana ambazo hakuwa na uhakika kama aliwahi kuisikia mahali popote pale tangu ujio wake kwenye huu ulimwengu, ilikuwa ni sauti ambayo ilimfanya ayafumbe macho yake kwa hisia nzito sana ilimpenya vilivyo alijikuta mpaka machozi yanamtoka, lakini mpaka muda huo alikuwa hata hajajihangaisha kugeuka na kumuangalia ambaye alikuwa anaimba huo wimbo.

TERI MERI ndio wimbo ambao alikuwa anausikia kutoka kwenye sauti moja nzuri sana na ndio wimbo ambao ulimfanya atoe machozi Kwa namna ulivyoweza kuziteka hisia zake za ndani kabisa, aliyafumbua macho yake na kugeuka ile sehemu ambayo alikuwepo mtumbuizaji japo alikuwa nje ila ndani palikuwa panaonekana vizuri sana, bahati mbaya ilikuwa kwake alishuhudia tu gauni moja la kisasa sana kutoka kwenye mwili ambao bila shaka MUNGU alitenga muda wa kutosha kuutengeneza kwa hicho kiumbe, gauni lilikuwa linaishia kwenye chumba ambacho ni wazi kilikuwa ni cha kubadilishia nguo, alijikuta anatabasamu na kutamani sana kuweza kumjua mwanamke huyo ila alijua hicho kitu hakiwezekani Kwa sababu alikuwa ameshachelewa tayari.

"Princes prisca atakuwepo hapa kwa wiki nzima hapa kwa ajili ya kuwapatia burudani hivyo kesho muda kama huu atakuwa yupo live tena mwambie na mwenzako hakikisha haukosi" ni sauti kutoka kwa mwanaume mmoja ambaye bila shaka hakuhitaji maelezo mengi kutambulika kama ni MC wa ile lounge. Hayo ni maneno ambayo yalimuingia vizuri sana kijana huyo akijiapia kesho yake lazima awahi hilo eneo ili aweze kufaidi kwa umakini sauti hiyo pamoja na kuitazama sura ya mwanamke huyo ambaye hakufanikiwa hata kumuona.

Markvelous alijifuta tena machozi akimhitaji dereva wake aongeze zaidi kasi ya gari ili aweze kuwahi nyumbani kwake alikuwa na wasiwasi mno.

Huenda umesha unganisha doti kinacho fanyika, unahisi hizi nyimbo zimeingiaje kwa huyu mwanaume?

Najua huenda imekugusa sana ila nadhani muda utaamua kukupatia kisa hiki cha kusikitisha sana chenye mapigano ya hali ya juu mno.

Wasalaam

Bux the story teller
 
Stori: Innocent Killer (The Revenge)
Msimuliaji: Bux the story teller
Umri: 18+
Sehemu ya NNE:

Songa nayo.............

Mheshimiwa jaji mkuu hakuwa na amani kabisa mpaka wakati huo hivyo alimsisitiza sana dereva wake kuweza kuongeza sana mwendo wa gari, alikuwa na imani kwamba familia yake haikuwa kwenye eneo salama sana hivyo ni yeye pekee ndiye ambaye alikuwa anatakiwa Kwenda kuikomboa familia hiyo huku machozi yakiwa yanauzonga zonga uso wake mpaka makamasi kwenye pua yake ilikuwa sehemu ya kumfanya kuwa na wasi wasi zaidi.
“Nisamehe sana mke wangu nisamehe sana mama” alikuwa anaongea mwenyewe akiwa ndani ya gari hiyo, alikuwa akimhusudu sana mwanamke huyo kwenye maisha yake na alizoea kumuita mama ni kwa sababu mwanamke huyo aliichukua nafasi ya mama yake mzazi, alimdekeza mwanaume huyo, alimpa mapenzi mazito ambayo alikuwa ana imani kabisa kwamba kwa kizazi hiki kulikuwa na watu wachache sana ambao walikuwa wana uwezo wa kuyapata mapenzi ya kweli kama hayo. Huyo mwanamke kwake alikuwa zaidi ya mke alifikia kiwango cha kumfanya kuwa kama mama yake alimjali yeye pamoja na mdogo wake Jason ambaye mpaka kwa wakati huo hakuwepo ndani ya nchi ya Tanzania na ukizingatia asubuhi yake walikuwa wamekwaruzana na mkewe hivyo alitamani sana awahi akamuokoe kwenye hilo janga ambalo aliambiwa lazima litamkuta mkewe pamoja na Kwenda kumuomba msamaha.

DREAM LOVERS LOUNGE
Mwanaume kumbu kumbu zake zilirudi ndani ya hilo eneo, siku ile baada ya kufanikiwa kuisikia moja ya sauti ambayo alimsifia sana MUNGU kuiumba duniani na yeye akapata bahati ya kuweza kuisikia ilikuwa ni siku ya furaha sana kwenye maisha yake, alikuwa mwenye furaha sana siku ile hata aliporudi nyumbani kwenye sehemu ambayo alikuwa akiishi na mdogo wake, bwana mdogo alimshangaa sana kaka yake kwani siku zote huwa ni mtu ambaye anakuwa na mawazo sana lakini siku hiyo alikuwa mwenye furaha kupita kiasi alifanya kazi zake zote akiwa anacheka cheka mwenyewe ilimlazimu mdogo wake amuulize siri ya mafanikio hayo lakini hakujibiwa zaidi ya kuishia kuchekeana tu.

Alitamani sana kesho yake ifike haraka ili awahi lile eneo majira ya jioni aweze kubahatika kuiona sura ya mwanamke huyo ambaye aliishia kuisikia sauti yake tu, muda huwa ni daktari mzuri sana siku hiyo alikuwa amewahi kwenye mizunguko yake ambayo aliimaliza mapema sana na Kwenda kukaa eneo la nje kabisa na ile lounge sehemu ambapo kulikuwa na tax nyingi alijipenyeza hapo mapema sana akiwa anasubiria mwanamke huyo aweze kupanda jukwaani kama alivyokuwa amesikia tangu jana yake kwamba princess Prisca angekuwa hapo kwa muda wa wiki nzima akiwa anatoa burudani kwa wateja wa eneo hilo hali iliyo pelekea eneo hilo kufurika sana. Majira ya saa nne za usiku ndio muda ambao malkia huyo alikuwa anapanda jukwaani, hali hiyo ilimfanya kijana huyo ambaye kwa wakati huo damu yake ilikuwa ikimchemka sana kuongeza umakini ili aweze kumuona mwanamke huyo, bahati mbaya sana kwake ambayo ilimpelekea kusonya kwa nguvu eneo la jukwaa kulikuwa na taa za pink na blue zilizo mfanya ashindwe kuing’amua sura nzuri ambayo aliitarajia yeye kwenye nafsi yake. Zilipita dakika kama tano bendi ikiwa inasikika kwa mbali ndipo ile sauti ya kumtoa nyoka pangoni, sauti safi ambayo ilipangiliwa kama zile nyaya za gitaa ambavyo huwa zinatengenezwa kwa ufasaha ili pale mtaalamu wa gitaa anapo lishika liweze kuziteka hisia za wasikilizaji ilisikika kwenye maiki ya mkononi ambayo ilishikwa na mwanamke huyo, ukumbu mzima ulitulia kila mtu alitamani sana kuweza kuisikia sauti hiyo kwa usahihi zaidi hata na wale ambao walikuwa wanakula walisimamisha zoezi lao kwa muda kwanza malkia aifanye kazi yake.
Hicho ndicho kilichompa umakini mkubwa kijana Mark kuweza kuisikiliza sauti hiyo akiwa amekodoa macho pima kwenye jukwaa ambalo alikuwa amesimama mlimbwende huyo, ghafla sana uliwaka mwanga mweupe na hapo ndipo ambapo aliona sura ambayo ilimfanya mdomo ubakie wazi, alijikagua kwanza yeye juu mpaka chini alitingisha kichwa chake kujikataa yeye mwenyewe.

When your day is long
And the night, the night is yours alone
When you’re sure you’ve had enough
Of this life, well hang on

Don’t let yourself go
‘Cause everybody cries
Everybody hurts sometimes

Sometimes everything is wrong
Now it’s time to sing alone

When your day is night alone (hold on, hold on)
If you feel like letting, go (hold on)
If you think you’ve had too much
Of this life, well hang on

‘Cause everybody hurts
Take comfort in your friends
Everybody hurts

Kwa yeye suala la kujisikitikia lilikuwa ni kujipimanisha au kujilinganisha kama anaweza kuendana kwa namna yoyote na yule mwanamke lakini jibu lilikuwa ni Hapana, ile shingo ndefu kiasi ambayo ilikuwa ni laini sana kwa sababu ya mafuta safi na maisha safi ambayo yaliizunguka, ule mwonekano wa kutamanisha wa Rihanna kwenye umbo la kifuani, sura ya malkia wa mziki duniani Beyonce, bila kusahau ule mgawanyiko wa kile kiuno na umbo la nyuma mithili ya Kim Kardashian yule wa Kanye West na ile miguu iliyo elekeana na Zarina Hassan mama yake na Princess Tiffa bila kusahau gauni la pink lililo ishia magotini na vile viatu mchuchumio vya bei ndefu ndicho kilicho mfanya ajikatae kabisa kwamba kwa yeye hakuwa mwanaume wa kukatiza mbele ya mwanamke huyo na akaweza kumuelewa kwa chochote kile. Tafsiri halisi ya mapenzi imeuliwa na neno pesa na yeye hakuwa kijana ambaye maisha yake yalikuwa safi ndio kwanza kula kwenyewe ilikuwa milo miwili wala sio mitatu kama wengi waishivyo angeanzia wapi kuyavaa kwa mwanamke mwenye ngozi nyororo na uzuri wa kumfanya ndege wa mwituni kumsifu kwa sauti nzuri kila apitapo kama huyo? Maisha yake yalikuwa ni ya maumivu makali sana asingeweza kufanya kitu chochote kile mbele ya mwanamke huyo au ambacho kingemsaidia yeye kuweza kumpata huyo mwanamke.

Akiwa kwenye hayo mawazo mazito ya kujikatia tamaa ya maisha yake ndipo ilipo sikika sauti nzuuri sana tena zaidi ya sana na hiyo ndiyo ambayo ilimfanya yeye kuja hapo majira ya usiku huo, nyimbo moja safi sana ambayo ilitoka mnamo mwaka wa 1992 kutoka kwa R.E.M.’S ijulikanao kama EVERYBODY HURTS ni wimbo ambao uliyarudisha matumaini makubwa sana kwenye moyo wake na kuna mstari ambao aliupenda sana kwenye wimbo huo ambao unasema

Usijiache wewe mwenyewe uende
Kwa sababu kila mtu hulia
Kila mtu huumia muda mwingine

Kuna muda kila kitu hakiwi sawa
Sasa ni muda wa kuimba mwenyewe

Kutoka kukata tamaa mwili wake ulipata sana nguvu kwa sababu yeye alijihisi kwamba ndiye mtu mwenye matatizo sana kwenye maisha yake ila aligundua kwamba kila mtu kuna muda huwa anapitia wakati mgumu sana kwenye maisha ila kikubwa ni kuendelea kuwa mstahimilivu pale unapo kutana na nyakati ngumu sana kwenye maisha yako, alivutiwa sana na kila kitu kutoka kwa huyo mwanamke alitabasamu na kuanza kucheka mwenyewe alicheka sana huku akiwa anaufuatisha wimbo huo ambao hata hakujua anaimba nini, moyo wake ni kama ulikuwa umepata ahueni kubwa sana tangu aweze kuujua na kuutambua uwepo wa mwanamke huyo kwenye maisha yake, kuna madereva tax ambao walikuwa wapo pembeni wakiwa wanasubiria wateja ambao wangetoka humo ndani walibaki wanamshangaa kijana huyo na kuhisi huenda hakuwa na akili timamu huenda alikuwa na matatizo ya akili.

Muda ulivyo zidi kwenye ndivyo watu wengi walikuwa wakinogewa na mwanamke huyo ambapo huo wimbo ulirudiwa kwa mara tano huku watu wakiwa wanatikisa vichwa na wengine wakiwa wanatoa vitambaa vyao na kuyafuta machozi ambayo yalikuwa yanashuka kwenye mashavu yao, ni wimbo ambao ulikuwa unahuzunisha mno tena sana ndiyo sababu watu walikuwa wakilia kimya kimya huku wakiwa wanaufuatisha wimbo huo ambao ulitendewa haki bara bara na mrembo ambaye alikuwa ameishika maiki yake yeye mwenyewe machozi yakiendelea kumshuka taratibu huku akiuimba wimbo huo kwa hisia kali sana.

Kijana Mark alijikuta anashawishika taratibu na kuanza kusogea eneo ambalo alikuwepo mwanamke huyo aliyekuwa akiuimba wimbo huo maeneo hayo, aliingia mpaka mlangoni ambapo hapakuwa na mlango bali ni mbao tu za kisasa ambazo zilizungushiwa kote na kumfanya hata mtu wa nje kuona vizuri ndani, kutokana na watu hao kutekwa na utamu wa mziki hata walinzi hawakuwa na muda na mlango tena macho yao yalikuwa jukwaani na hiyo ndiyo nafasi ambayo Mark aliitumia kuingia humo ndani, alivyokuwa akisogea ndivyo alivyokuwa akizidi kunogewa na sauti ya mwanamke huyo na kujikuta anashawishika kutamani kumgusa hata ngozi yake mrembo Prisca, wakati anakaribia kupanda kwenye hilo jukwaa kuna mlinzi mmoja alimrukia baada ya kumuona anaelekea sehemu ya jukwaa bila ruhusa alimbeba kwa nguvu na kumbamiza kwenye meza iliyokuwa pembeni kwa kasi akihisi huenda alihitaji kumvamia mwanamke huyo, kichwa chake kilianza kutoa damu alipiga sana kelele kwa maumivu makali ambayo aliyapata usiku ule.

“Bosi bosi bosi”
“Eeeh mama uko salama?” alishtuka kwenye hayo mawazo mazito baada ya kuitwa, alihisi ni mkewe anamuita ndipo aliposhtuka kwamba alikuwa ni dereva wake, aliogopa sana mwili wake ukiwa na jasho sana hata suti ilikuwa imeloa japokuwa ndani ya gari hiyo kulikuwa na kiyoyozi cha kutosha.

“Bosi tumefika nyumbani ila nimesimamisha mbali kidogo maana nimeona kama kuna mwili wa mtu getini pale umelala na geti lipo wazi” dereva wake alimpa maelekezo bosi wake huku akiwa ana msikitikia sana, alijua wazi mheshimiwa alikuwa anapitia kipindi kigumu sana.

“A a a a saaante sana nitakupigia simu nikikuhitaji hiyo gari nenda nayo” Aliongea kwa kitete midomo yake ikiwa mizito sana inatetemeka huku akiwa anashuka ndani ya gari hiyo, hakusubiri hata jibu la mtu huyo tena alikuwa tayari ameshafika mlangoni, aliogopa sana baada ya kuona miili ya watu watatu ipo chini ikiwa inamwaga damu. Damu ilionekana kuwa bado mbichi sana na wote walipigwa risasi za kichwa alikimbia mpaka kwenye mlango wa nyumba kubwa hapo alisita kidogo baada ya kukuta walinzi wake wengine wote watano wamepigwa risasi za kichwa, mwili ulimsaliti kabisa alianza kuogopa kuingia kwenye nyumba yake yeye mwenyewe hakutamani kile ambacho alikifikira akutane nacho humo ndani.

Alianza kusogea taratibu kwa uoga ni michirizi ya damu tu ndiyo ambayo ilikuwa inaonekana mpaka kwenye kochi hapo alicho kiona alipiga magoti machozi yakiwa yanashuka yenyewe hakuelewa alie kwa sauti au aendelee kuangalia alichokuwa anakiona mbele, binti yake wa pekee ambaye aliikamilisha furaha ya maisha yake kwa kuwa baba kwa mara ya kwanza hapa duniani, walimwengu walikuwa wameondoka na nafsi yake hakuwa hai wala kuwa na matumaini ya kuwa hai tena kwenye ulimwengu wa wanadamu hawa wanao jivunia pumzi kama walijipa wao.

Sijui ilikuwaje na nini kinaenda kufanyika ila niseme tu kufikia hapa sehemu ya 4 sina la ziada.


Wasalaam

Bux the storyteller.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom