Riwaya: Muuaji mwenye kofia nyekundu

Attelan

JF-Expert Member
Oct 12, 2023
433
695
images.jpeg

(image via itl.cat)

MUUAJI MWENYE KOFIA NYEKUNDU
SEHEMU 001

Yalikuwa ni majira ya usiku wa saa sita kamili, John Otieno alikuwa akikatiza kwenye mtaa uliotulia maeneo ya Iwambi jijini Mbeya. Mtaa huu ulijaa nyumba za kifahari tupu, hakukuwa na kelele za muziki wala kelele za watu waliokuwa wakiongea. Nyumba nyingi zilifungwa kamera za ulinzi ili kurekodi matukio yote ambayo yangetokea katika maeneo hayo. John Otieno aliyevalia nguo nyeusi tii na kichwani akivalia kofia nyekundu alikuwa akisonga kwa haraka sana na hatimaye alifika kwenye nyumba aliyokuwa akiikusukudia, mbele ya macho yake kulikuwa na nyumba kubwa ya kisasa iliyokuwa na ukuta mrefu tena uliowekwa nyaya za umeme. Hii ilikuwa nyumba ya Bwana Abdul Jumbe, huyu alikuwa mfanyabiashara mkubwa na alikuwa akimiliki maduka makubwa ya vifaa vya kielektroniki yaliyokuwa katika mikoa zaidi ya kumi nchini Tanzania.

“Oops!” John Otieno aliguna na kuamua kuizunguka nyumba ile kubwa lakini kabla hajafika mbali alikoswakoswa kumulikwa na gari kubwa aina ya tipa ambalo lilikuwa likisonga kuelekea kwenye nyumba ya Bwana Abdul Jumbe. Kwa haraka sana John alijitupa kwenye nyasi zilizokuwa karibu na baada ya hapo alijilaza chini kwa haraka akisubiri gari lile lifike getini kwakuwa alijua mpango wake ungeanzia pale. Baada ya tipa lile kufika kwenye geti dereva alipiga honi na hapo mlango mdogo ulifunguliwa na mlinzi aliyeshikilia bunduki aina ya SMG alitoka na nyuma yake alitoka mlinzi mwingine aliyemulika kwenye upande wa dereva akiwa na tochi kubwa ambayo ilikuwa na mwanga mkali.

“Wamefika, sawa bosi!” aliongea yule mlinzi wa pili na baada ya hapo gari liliruhusiwa kuingia ndani. Muda wote huu John Otieno alikuwa chini ya gari akining’inia kama kinyonga kwenye tawi la mti. Gari lilisogezwa mpaka sehemu ya kupakia magari na baada ya hapo lilizimwa na dereva alishuka garini. Muda huu John akiwa chini alisikia hatua nzito nzito za mabuti zikisonga kuufuata upande aliokuwa chini ya gari.

“Bosi yupo ndani unaweza ingia kumuona” iliongea sauti ambayo John aliitambua kwamba ilikuwa ni ya yule mlinzi aliyekuwa akiongea na simu nje ya nyumba pale getini. Kila hatua ambayo yule mlinzi alikuwa akiipiga ilikuwa ikimpa mashaka mno kwani utembeaji wake ulionesha alikuwa mbobevu wa mapambano na inawezekana aliwahi hata kuwa mwanajeshi. Mawazo haya yalimtoka ghafla baada ya kusikia mlango wa gari lile ukifunguliwa na hapa ndipo alipojua alitakiwa kuchoropoka kutoka chini ya gari kwa haraka. Kama isingekuwa uchapu wake basi alikuwa anaupoteza mguu ambao ulibaki kidogo kugongwa na tairi ya nyuma ya gari ile ambayo ilipelekwa kwenye gereji ambayo ilikuwa kwenye nyumba hiyo. Muda huu John Otieno alikuwa amejivika ile ile kofia yake nyekundu na alikuwa amejibanza kwenye ukuta na alifanikiwa kuchungulia kwa haraka kwenye dirisha na alimuona Bwana Abdul Jumbe ambaye kwa muda huu alikuwa akinywa maji, baada ya Bwana Abdul kugeuka kwa haraka alimkosa kumuona John kwa haraka sana.

“mmh!” Bwana Abdul aliguna na akaamua kuiweka glasi ya maji kwenye meza na kwa haraka alifungua mlango na kuangaza huku na huko lakini wala hakufanikiwa kuona kitu chochote zaidi ya walinzi ambao nao muda huu walikuwa wakiendelea na doria wakizunguka huku na huko ili kuhakikisha Bwana Abdul anakuwa salama, baada ya hapo alirejea mlangoni na kuamua kurudi kwenye sofa na kukaa kwa utulivu na akasogeza mkono wake kwenye glasi yake ya maji na kuyanywa. Ndani ya dakika kadhaa Bwana Abdul alianza kugalagala na alikuwa akiishika shingo yake na alikuwa akionekana kama mtu aliyekuwa kwenye maumivu makali mno, hatimaye povu zito lilimtoka mdomoni na baada ya kufurukuta kwa kitambo hatimaye alijinyoosha na hapo roho yake ikawa imeuacha mwili wake. John Otieno alikuwa kwenye moja ya kona za jumba hilo na baada ya kuona alikuwa amethibitisha kuwa mtu aliyekuwa akimlenga amepoteza maisha aliifuata ngazi iliyokuwa karibu na sebule na kwa haraka alipanda ngazi na kwa juu alikutana na vyumba vingi ambavyo vilikuwa giza isipokuwa chumba kimoja na aliposogea alisikia sauti ya mwanamke aliyekuwa akiongea kwenye simu, John Otieno alitoa kifaa kidogo ambacho ni kama simu ya batani na kubonyeza kibonyezeo kimoja na baada ya hapo taa ndogo nyekundu iliwaka. Baada ya hapo alisogea karibu kwenye mlango na kuusukuma kwa ghafla.

“Mume wangu!” aliita yule mwanamke ambaye hapo awali alikuwa akiongea na simu na muda huu aliishusha simu chini na kuusogelea mlango na kuufungua. Ndani ya sekunde hizi chache tayari John Otieno alikuwa ndani ya chumba cha yule mwanamke ambacho kilikuwa kikinukia harufu nzuri. John alitafuta sehemu ya kujifichia na akajichimbia huko kwa muda.

“Bosi! Nilijua ni Abdul kumbe si yeye!”
“Nimeshangaa umeacha kuongea na mimi na kuendelea kumkimbilia Abdul”
“Samahani bosi”
“Kazi yako moja, muue na uondoke. Haujaenda hapo kuleta mapenzi”
“Sawa” aliongea yule mwanamke na baada ya hapo alisonga kwenye kitanda na kukifunua na hapo alitoa bastola yake ndogo na kuamua kuiweka kwenye mkoba wake mdogo. Muda huu hata John Otieno alishangaa na hakujua kwamba kwenye kazi hiyo aliyotumwa kuifanya kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa akitarajiwa kuifanya. Mapigo ya moyo ya John yalikuwa yakimuenda mbio kwani alipomsikia aliyekuwa akiongea kwenye simu alikuwa akiikumbukaa sauti ya kamanda Albert Nyoni (Simulizi yake iko kwenye simulizi nyingine).

“Hawezi kuwa yeye!” alijisemea moyoni na akaamua kubana kwenye kona na kutulia, baada ya dakika kadhaa yule mwanamke ambaye awali alivalia mavazi ya kujitanda sana alibadili mavazi na kuvalia suruali ya jinsi na mabuti meusi alitoka chumbani humo na alianza kushuka ngazi kwa taratibu akiwa anaangalia sehemu ya sebule ambayo ilikuwa kimya. Kwa mbali alimuona Abdul ambaye alikuwa amejilaza kwenye sofa kama mtu aliyepitiwa na usingizi.

“Nimalize kazi na kuondoka!” alijisemea yule mwanamke, upande wa pili John Otieno alitoka kwenye kona aliyojibanza na kuamua kupitisha macho yake haraka kwenye dressing table na hapo alifanikiwa kuziona passport tatu moja ya Ethiopia, passport ya Madagascar na passport ya Sudan kusini. Akili ya John ilicheza kwa haraka na aliamua kutoka kwenye kile chumba kwa haraka na kupanda kwenye vyumba vya juu zaidi.

“He ‘s already dead, there ‘s somebody in the house” (Tayari amekwishafariki, kuna mtu ndani ya nyumba) aliongea yule mwanamke na muda huu aligeuka na kunyoosha bastola yake kuelekea upande wa juu wa nyumba na hapo hakuona kitu chochote.

“You have to get out. Whoever this intruder is, he ‘s more skilled than you can ever imagine” (Unatakiwa utoke nje. Mvamizi huyo ana ujuzi mkubwa kuliko unavyodhani) iliongea sauti ya kiume na sauti hii ilimfikia vyema yule mwanamke ambaye alivalia kitu kama ki-bluetooth kidogo kwenye sikio. Muda wote huu John Otieno alikuwa kule juu kwenye vyumba vingine na alimuaa kukaa kimya bila kufanya chochote alikuwa anajua akiwahi kufanya jambo lolote angefariki kwani hakujua kama yule mwanamke alikuwa peke yake ama la.

“What about the footage?” (Vipi kuhusu zile video zilizorekodiwa?) aliuliza yule mwanamke na muda huu alikuwa akisonga na kuufuata mlango wa siri wa jumba lile na kutokomea nje ambako huko alitoka na kusonga kuelekea kwenye dirisha la nyumba moja ya jirani na kugonga mara tatu baada ya hapo dirisha lilifunguliwa na yeye alinyanyuliwa na kuingia ndani.

“We ‘ ll get rid of all the foota...” (tutafuta video zo...) kabla hata yule aliyempokea yule mwanamke kuongea alishangaa kumuona mtu aliyevalia kofia nyekundu akichomoa hard disks za kompyuta zote zilizounganishwa na kamera za CCTV. Mwanaume huyu alikuwa akifahamika kwa jina la David Webb, huyu alikuwa mmoja wa maafisa wa upelelezi kutoka nchini Uingereza waliotumwa kusaidia kazi ya kumuua mfanyabiashara Abdul Jumbe kwa maslahi mapana yaa nchi ya Uingereza. Wote wawili, David pamoja na yule mwanamke walishangaa baada ya kumuona yule mwanaume aliyevalia kofia nyekundu kupitia skrini kubwa ya kompyuta iliyounganishwa na kamera ndogo zilizowekwa kwenye nyumba ya Abdul, David alijilaumu kwa kushindwa kuweka kamera sehemu ya sebule kwani wangemuona mapema na alikuwa anajiuliza ni kivipi mtu yule mwenye kofia alifanikiwa kupita mbele ya baadhi ya kamera bila kuonekana.

“He ‘s so fucking fast!” (Yupo chapu sana!) aliongea David Webb akiwa anatazama kwenye skrini lakini jambo la ajabu ni kwamba mwanaume aliyevalia kofia nyekundu aliwasalimu kwa kuwapungia mikono.

“He knows we can see him” (Anajua tunamuona) aliongea yule mwanamke na baada ya hapo mlipuko mkubwa ulisikika na kamera zote zilizima. Muda huu John Otieno alikuwa nje ya nyumba kwa mbali akiwa amejilaza kwenye manyasi marefu akishuhudia nyumba ambayo ilikuwa ikiungua.

“Kwaheri Bwana Abdul Jumbe” aliongea John Otieno na hapo safari yake ya kuondoka mahali hapo ikaanza.

Kionjo cha Sehemu ya Pili 😋😋

SEHEMU YA 002
DAR ES SALAAM

Nje ya nyumba moja maeneo ya Mikocheni kulikuwa na gari mbili aina ya Klugger V nyeusi ambazo zilikuwa nje ya geti la nyumba hiyo. Hazikupita hata dakika mbili geti la nyumba hiyo lilifunguliwa na hapo walinzi waliovalia sare na kushikilia bunduki aina ya SMG walitoka na kulisukuma geti ili lifunguke. Msafara ule wa magari mawili ulifika kwenye sehemu ya parking na baada ya dakika kama tano hivi kupita walishuka watu wanne kutoka kwenye kila gari.

“Bosi anawasubiri” aliongea mlinzi mmoja aliyesogelea gari zile mbili, halikutoka hata jibu moja kutoka kwa wale watu nane bali waliendelea na safari ya kuelekea kwenye mlango wa nyumba hiyo ya kisasa. Kwa majira hayo ya asubuhi hali ya hewa ilikuwa na kijiubaridi na upepo ulikuwa ukivuma. Baada ya wale watu nane kuingia ndani walikutana na Daktari Elishama aliyekuwa akiwasubiri kwenye sofa lake moja la gharama. Baada ya salamu hatimaye wote walinyanyuka na kupanda kwenye ghorofa ya juu ambako huko waliingia kwenye chumba ambacho kilikuwa na viti vingi vilivyopangwa kwa kuzunguka meza kubwa na ndefu iliyokuwa na umbo la silinda (cylinder). Daktari Elishama alisonga na kukaa kwenye kiti cha mbele na hapo kwenye chumba kulikuwa na watu tisa pamoja na yeye.

“kho kho kho” alijikooza Daktari Elishama kwa taratibu akiwa analegeza tai yake aliyokuwa ameivaa. Kila mtu alikuwa kimya kusikiliza wito huo wa ghafla. Mbele ya chumba hicho kulikuwa na skrini kubwa ambayo ilikuwa imeunganishwa na Laptop iliyokuwa kwenye meza karibu na kiti alichokalia daktari Elishama.

Mnachihanguuu | Kacheda mjasiliamali | Kelsea | Numbisa | Bujibuji Simba Nyamaume |
 
Itaishia sehemu ya ngapi?
 
View attachment 2914704

Ok
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom