Inawezekana vipi mtu kuweka roho yake kwenye mti?

Masharti yake yakoje, Kama hutojali?

Kwenye family yako yupo/wapo waliofanyiwa?

Nimependa kwa kweli. Heshima kwao wazee!

🙌
Masharti yake ni madogomadogo kwa kipindi cha wiki moja tangu kuzindikwa.
Kila koo ina mizimu ya kukuongoza na masharti yake

Kwenye familia yetu sijajua maana huenda kuna mtu anaenda kisirisiri, ila kwenye ukoo wetu, wapo wengi sana, Sisi Wafipa, utatuambia nini kwenye haya masuala?
Sema koo zetu zimesambaa wengine wako Kaliua Tabora, kuna walioko Milala, Sumbawanga mjini, Tanganyika huko, Kigamboni na Mpimbwe.
Japo nina wajomba zangu wako kijijini Chipu....unapajua?, uliza kwa watu.
Mie hata sasa nikitaka kuwa mchawi inawezekana, uchawi wetu uko malangoni.
Hapa kwa Wafipa nazungumzia upande wa mama
Baba ni kule Tanga...
 
Tuna Mzee wetu hapa tunamuuguza kwa muda mrefu miaka mitatu sasa tunampambania nae alipata tatizo kuparalalaizi mpaka sana yupo ICU hali yake sio nzuri miguu yake imeanza kuoza

Imenibidi kuandika thread hii humu sababu siku mbili hizi tumepigiwa simu huko kijijini kwamba Mzee wetu twende huko kijijini wanafamilia wote tukafanye mambo ya Mila twende na kondoo wawili inasemekana Mzee wetu Kuna miti miwili ndio aliweka roho yake

Kwahiyo tutaendelea kupoteza muda kumuuguza atakufa mpaka aoze mwili wote inatubidi tuende tukafanye mambo ya Mila maana tukimuacha aoze mwili mzima ndio afe hali hiyo itakuja kumkuta mwanafamilia
Huo uchawi wa kuoza polepole hadi kufa upo na mzee mwenyewe anahusika. Kuweni makini kuna mtu kati yenu anapaswa kurithi huo ushenzi. Wewe kama unanielewa usikubali kamwe kushiriki hizo mila au matambiko mizimu itakuandama. Lakini hata hivyo ukoo wenu ni wachawi sana.
 
Haya matukio yangekuwa yanatokea kweli yangekuwa yameshavuta wawekezaji. Hii dunia matajiri, viongozi, watu wenye nguvu adui yao ni kifo. Wangeungana wajue ni nini hicho.
Kwenye sayansi ya kiafrika Yapo kweli mkuu.
Nimeyashuhudia. Ila huwa nashangaa kwanini wanatafuta njia ya kuwauwa?
Kwanini wasithubutu kuangalia mwisho wake?
 
Kwenye sayansi ya kiafrika Yapo kweli mkuu.
Nimeyashuhudia. Ila huwa nashangaa kwanini wanatafuta njia ya kuwauwa?
Kwanini wasithubutu kuangalia mwisho wake?
Sayansi ya kifikra na dini zimo humo boss na serikali haikatazi dini. Kwanini hii inafichwa fichwa. Unless kuna mambo yanafanyika kinyume na ustaarabu wa mwanadamu wa sasa.
 
Sayansi ya kifikra na dini zimo humo boss na serikali haikatazi dini. Kwanini hii inafichwa fichwa. Unless kuna mambo yanafanyika kinyume na ustaarabu wa mwanadamu wa sasa.
Hapana mkuu
Kumbuka bado tunatumia elimu ya kikoloni.
Na ili ukoloniwe ndio tukaambiwa vitu vyetu vyote ni vyakishenzi na si vyakistaarabu.
Haya ni matokeo ya ukoloni
 
Hapana mkuu
Kumbuka bado tunatumia elimu ya kikoloni.
Na ili ukoloniwe ndio tukaambiwa vitu vyetu vyote ni vyakishenze na si vyakistaarau.
Haya ni matokeo ya ukoloni
Mkuu, tiba mbadala ni ruksa nchini kwetu. Hakuna mzungu anayetuzuia, hakuna wakoloni wanaotuzuia. Kuna jambo halipo sawa.
 
Hii kitu iliwahi kumtokea ata mzee mmoja uko morogoro 2022 aliitwa jumajuma, alikuwa anazaid ya miaka 100 sometimes alikuwa anakata moto adi anapoa mwili barid mara anaamka tena ad alipofanyiwa mila ndio week tu amakata moto mazima, walimsubir masaa zaid ya 8 labda ataamka kama kawaida yake ndio ikawa safari, alizikwa na mvua ilipiga kubwa kinoma.. dah aya mambo ni mazito... Walioishi enz za akina mwanamalundi waliona vingi

Wa
 
Mkuu, tiba mbadala ni ruksa nchini kwetu. Hakuna mzungu anayetuzuia, hakuna wakoloni wanaotuzuia. Kuna jambo halipo sawa.
Upo sawa.
Juzi tumeona wizara ilianzisha tahasusi za dini mbili. A level
Je kati ya hizo umeona hata moja inayohusu hao wazee wa mila?
Km sivyo ni kwanini haipo?
Yote ya mila za kiafrika ni mabaya?
 
Masharti yake ni madogomadogo kwa kipindi cha wiki moja tangu kuzindikwa.
Kila koo ina mizimu ya kukuongoza na masharti yake
Samahani tena, unaweza kuwa specific hata kutaja japo masharti mawili matatu.
Kama inawezekana?

Kwenye familia yetu sijajua maana huenda kuna mtu anaenda kisirisiri, ila kwenye ukoo wetu, wapo wengi sana, Sisi Wafipa, utatuambia nini kwenye haya masuala?
Okay wafipa.
I bet watakuwepo kwenye family maana naona ni jambo linahitaji usiri pia ukifanyiwa.

Sema koo zetu zimesambaa wengine wako Kaliua Tabora, kuna walioko Milala, Sumbawanga mjini, Tanganyika huko, Kigamboni na Mpimbwe.
Huku kote umetaja ndio wanasifika wakali wa hizo kazi.

Japo nina wajomba zangu wako kijijini Chipu....unapajua?, uliza kwa watu.
Chipu…
Ngoja niwaulize

Mie hata sasa nikitaka kuwa mchawi inawezekana, uchawi wetu uko malangoni.
Huko malangoni ndio wapi ama Una maana gani hapa?

Hapa kwa Wafipa nazungumzia upande wa mama
Umewahi kushuhudia hii science ya wazee wa Afrika live?

Unafahamu aina yoyote ya science hii na unaweza kuitenda?
Huogopi?

Baba ni kule Tanga...
Madam, uko vizuri. 🙌
 
Upo sawa.
Juzi tumeona wizara ilianzisha tahasusi za dini mbili. A level
Je kati ya hizo umeona hata moja inayohusu hao wazee wa mila?
Km sivyo ni kwanini haipo?
Yote ya mila za kiafrika ni mabaya?
Ushawahi kusikia malalamiko ya wenye hii elimu kuzuiliwa kufanya haya mambo ya tiba mbadala? Unless ni mambo ya ramli chonganishi au inahususha viungo vya binadamu au wanyama bila kibali.
 
Samahani tena, unaweza kuwa specific hata kutaja japo masharti mawili matatu.
Kama inawezekana?

Okay wafipa.
I bet watakuwepo kwenye family maana naona ni jambo linahitaji usiri pia ukifanyiwa.

Huku kote umetaja ndio wanasifika wakali wa hizo kazi.

Chipu…
Ngoja niwaulize

Huko malangoni ndio wapi ama Una maana gani hapa?

Umewahi kushuhudia hii science ya wazee wa Afrika live?

Unafahamu aina yoyote ya science hii na unaweza kuitenda?
Huogopi?

Madam, uko vizuri. 🙌
Mkuu Coach Slamah Hamad kuna mengi ambayo siwezi yaweka wazi hapa.
Ila jua tu, haya mambo yapo....kwa sisi ambao kwetu ndio hiko, nakwambia tu yapo.
Malangoni ni nyumbani, ndani ya nyumba ambayo mtu huishi.
Mengine siwezi kuyaweka hapa.
Ngoja tuone...🤔
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom