Inawezekana vipi mtu kuweka roho yake kwenye mti?

Haya ni mazindiko ya kiafrika, roho haikai kwenye mti ila anafanya zindiko anaungana na ule mti ukitaka kumuua ni mpaka ule mti ufe kwanza. Hizi zilitumika kama kinga enzi zile watu wanatekwa maporini safari za miguu hamna magari. Zipo nyingi ambazo nimewahi kuziona in action ni kama;
1. Dawa ya mbio- hii kulikuwa na jambazi sugu wanamtafuta kila wakija akitoka mbio hata mbwa hawafati hiyo speed ya jamaa.

2. Kukosekana kwenye hatari- hii mtu akija akudhuru anakuwa hakuoni, walihangaika na huyo mtu mpaka wakaamua kuua mwanae kwa hasira baada ya kumkosa muhusika kila wakati.

3. Dawa ya kurusha ngumi- hii ukimpiga mtu ngumi anazikwa, inafanya kazi pale tu unapokuwa unaonewa lakini ukianzisha ukorofi utapigwa kama ngoma.

4. Dawa ya kurusha jiwe au fimbo - hii kama mtu kakukimbia na huwezi mpata basi ukichukua kitu chochote ukarushia uelekeo wake humkosi, hata awe mbali wa viwanja 3 vya mpira.

Na zingine kibao kwa nyie watoto wa miaka ya 90 na 2000 hamuwezi elewa.
Kuna siku Mada Maugo alipigwa na Fransis Cheka, katika mahojiano baada ya pambano, Mada Maugo alisema Cheka katumia dawa. Alisema zile ngumi zilikuwa nzito na zinauma, ni aheri angepigwa mawe kuliko hizo ngumi.
 
Vipi kama alikula Mti wa Uzima ambao Adam na hawa walifukuzwa bustanini wasiule?je tanzania Ndio Eden ?je kuna wazee wanautambua Mti wa uzima??nilishawahi Kuambiwa kuwa Upo na ukiukata unatoa kitu kama maziwa
 
Interested, mkuu tutaamini vipi hii taarifa, tupe source ya taarifa tujifunze

kuna jamaa angu mmoja alitoka kumzika babu yake vijiji vya mkoa wa mara huko. Aliniambia kitu kama hicho aisee.

Kwamba babu yao amekufa kifo cha mateso sana maana ilifikia hatua mwili unaoza lakini bado ni mzima sababu alijifunganisha roho yake na vitu gani gani sijui vya mila zao hadi walivyofanya hizo tamaduni kutimiza masharti ndipo alifariki. Japo nilimsikiliza tu bila kuamini wala kukataa lakini ndio hivyo ilitokea.
Mti aliozindika huyu mgonjwa wetu nimepata taarifa kumbe unaogopeka sana ata ukichuma tawi la mtu unaanza kuumwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom