Inawezekana Magufuli sio tatizo?

Idadi ya watu ikiongezeka hata productivity inaongezeka,,vivyo hivyo mapato ya nchi yataongezeka.,!!hivyo wingi wa watu sio shda.tatizo ccm wakati wote mpo 'location'!!



Hiyo theory ni wapi wewe? Embu niambie inatumika wapi? Ni nchi iliendelea bila kufanya population control?
 
Mi nashindwa kuelewa eti mtanzania anasema sisi tuko wengi mpk serikali inashindwa toa huduma mana hata sehem ya vitanda akuna ndo serikali kufeli kaz yake na akuna rais aliyeshindwa basi kufanya kaz yake madaktari sio tatizo ukiona muhimbili mtu kaenda direct bac ana hela ndefu masikini unapita kwa zahanati na kwengine kisha transfer muhimbili shida vifaa akuna ndo mana transfer na ndo mana muhimbili wakishindwa unaenda india utaalamu sawa lkn vifaa kwetu akuna
 
Wangalau sasa utaanza kujibu kwa nidhamu, toka lile sakata la mkulu kukimbia mabalozi na.huu ukweli unaoendelea kuwa hadharani utawafanya muache kusifia kila kitu kwa itikadi ya kiccm. Tulisema haya mambo hayahitaji kupenda sifa bali kuchunguza hasa ni nini matatizo yetu na jinsi ya kuyatatua na sio kuita camera kuongopea umma eti sasa tumepata kiongozi muarubaini wa matatizo yetu. Tuache kupenda sifa kwa ajili ya maksi za kisiasa kwani tatizo ni kibwa kuliko kupenda sifa za kisiasa.
Ahahahaha kama nafasi akuna mbona wamepata nafasi ya kutandika mashuka na wengine kuweka magodoro chini kaka tetea ila tumia akili kidg eneo pia sio shida serikali ina jkt maengineer kibao au ndo wanataka hisani ya kujengewa nn au umeandika upate mtu wa kureply text yako nn kama una uwezo na unapatapa uduma acha masikin tupaze sauti wazungu watusaidie kwa majengo na vitanda mana ndo njia yetu hiyo nyie subirin mchango wa sherehe za bunge mnunue vitanda mbona hela ya kusitisha live bunge amja nunua vitanda
 

Tatizo la Wagonjwa kushirikiana vitanda halisababishwi na uhaba wa vitanda, bali linasababishwa na uwingi wa wagonjwa na nafasi ni ndogo hivyo hakuna kitu Muhimbili wanaweza kufanya kwa maana hakuna nafasi sasa vitanda wataviweka wapi?

Changamoto kwenye sekta ya Afya kama kulivyo sehemu nyingine bado ni kubwa sana, ni lazima kwanza Hospitali zetu za Wilaya kama Amana, Temeke, Mwananyamala zote ziboreshwe na pia kujengwa nyingine zitakazoendana na idadi ya wakazi wa Dar, kumbuka Hospitali zote Dar zimejengwa wakati Dar ikiwa na wakazi chini ya milioni Moja leo hii tuko zaidi ya milioni 4.5 na kila mama anapata wastani wa watoto 2.6 Tanzania ambayo ni kasi kubwa sana!

Wewe nawe bwana. Kama nafasi ya kuviweka vitanda hivyo haitoshi, hao wagonjwa waliorundikana chini walikuwa wamening'nizwa juu ya dari??

Wakati mwingine unapokuwa umegongwa jaribu kunyuti tu, sio kila kitu ni kutetea tuuuu mbele kwa mbele hadi watoto wa
chekechea watakuona hamnazo!!
 
Siku 100 zimeisha kwa kuanza upya yale yale aliyoyafanya siku ya kwanza
Mimi nilikuwa nimempa siku 90 toka aapishwe...nasikitika kuripoti kuwa bado nipo kwenye mshangao, inaelekea tuliuziwa mbuzi kwenye gunia. Kikwete ilidaiwa aliangushwa na wasaidizi wake, Magufuli sina hakika anaangushwa na nani, oops, Mzee Mwanakijiji ananinong'oneza kuwa Magufuli anaangushwa na wale wanaotaka serikali yake ianguke isifanikiwe. Siku watu watakapogutuka na kung'amua jipu linalohitaji kutumbuliwa ni lipi hasa, tutapona hapo hapo.
 
tatizo liko kwetu wananchi na hasa media?
tumeletewa 'sanaa tukaishangilia huku ukweli tunaujua'?
sababu muhimbili hali yake sio siri
lakini tulipoambiwa mambo sasa ni saafi tuliruka ruka na kushangilia...
huku kiukweli hali ni ile ile tu.....
Ukweli ni kuwa MEDIA zimekuwa washabiki na wapotoshaji wakuu wa jinsi mambo yanavyokwenda, si watu wa kuhoji na kutafuta ukweli!
 
Ninaposema population control namaanishwa kwamba ongezeko la watu nchini mwetu ni kubwa sana na haliendani na ukuwaji wa uchumi wetu hivyo hakuna kitu tunafanya ni kama uwe na watoto 2 una mshara wa laki tano halafu unaongeza watoto wawili tena na mshahra unaongezeka mpaka laki tano na nusu tu ni dhahiri kwamba utakuwa na mapungufu ya karibia kila kitu kwenye familia yako ukilinganisha na ulivyokuwa na watoto 2 tu!

Na ndicho kinachotokea TZ, hizo Hospitali za Rufaa za Mikoani unazoziongelea utazijenga na nini? Unahitaji kwanza ukuaji wa uchumi ili uweze kuwa na fedha ya kuzijenga, sasa maadamu kila mwanamke Tanzania anapata wastani wa 2.6 na uchumi wetu unakuwa kwa asilimia 6 - 7 tu hatuwezi kufanya hayo yote ni lazima Uchumi wetu ukuwe kuzidi ongezeko la watu ili ilete maana na hili kwa hali ya kawaida na ngumu hakuna nchi waliowahi kufanikiwa na ndiyo njia pekee ni kupunguza ongezeko la watu kwa mfano iwekwe utaratibu mwisho watoto wawili ambao Serikali inawalipia kila kitu na kila mtoto wa tatu au nne unamlipia mwenyewe na kodi unayokatwa inaongezeka hii itasaidia vinginevyo hakuna kitu tutafanya!
Kwa watu ambao wanaishi dar watakubaliana na wew uzaaji wa hovyo hovyo ndo unachangia matatizo MENGI,hasa ya kiafya katika jij la dar unakuta mtoto wa miaka kumi na sita tayari ana watoto wawili tayari,na kuna takwim zinaonyesha dar ni miogoni mwa majiji yanayo kuwa kwa kasi ,kama newyork ina miaka mia moja lakin ina watu milion 8 lakin dar ina umria wa mika kumi natano na ina watu 4.5 mil unategemea lazima kutakuwa na changamoto sio tu kwenye afya pia kwenye miundo mbinu
 
Leo ukifuatilia taarifa ya habari Magufuli katembelea tena Muhimbili kwa kustukiza
kakuta matatizo tele hasa amewakuta wamama waki share vitanda hadi watu watano
na wengine wakilala chini.....

Utakumbuka few months ago tulitangaziwa kuwa baada ya Magufuli kwenda Muhimbili
vitanda vilipelekwa hadi vikakosa wagonjwa
kuna picha zilisambazwa paka kalalia kitanda kipya Muhimbili
na kwamba sasa mambo ni tofauti kabisa...vitanda tele na kila kitu saafi

Sasa binafsi siamini kabisa Muhimbili imewahi kuwa safi na matatizo yakaisha
ambacho najiuliza why 'maigizo yale ya kuwa mambo ni saafi' yaliruhusiwa
kuendelea ?

why sisi wananchi na waandishi wa habari hatukupinga kabisa habari za kuwa
mambo ni saafi muhimbili?
why habari ya leo iwe kama habari mpya
while in reality watu wameendelea kulala chini tu kama zamani?

Inawezekana kabisa tatizo haliko kwa wanasiasa?

tatizo liko kwetu wananchi na hasa media?
tumeletewa 'sanaa tukaishangilia huku ukweli tunaujua'?
sababu muhimbili hali yake sio siri
lakini tulipoambiwa mambo sasa ni saafi tuliruka ruka na kushangilia...
huku kiukweli hali ni ile ile tu.....

Na leo tena wananchi wamemlilia tena Magufuli bila kujiuliza
ni kweli Magufuli hali iliyopo haijui?si alikwenda juzi tu hapo hapo Muhimbili?
au haya matatizo ni mapya kabisa?
Mkuu the Boss matatizo ya nchi hii ni kuwa tuna wananchi wajinga kupindukia... Ingawaje na media zetu zinatumika kisiasa hili nalo ni janga..
 
Ni nani amewaambia wananchi kwamba matatizo yametauliwa? Sijawahi kusikia mahali popote tangu Raisi magufuli aingie madarakani akisema kwamba matatizo ya Muhimbili au afya yametatuliwa hilo nalisikia kwako, nilichosikia ni kwamba hali imeboreshwa kulinganisha na ilivyokuwa hapo mwanzo kama ununuzi wa vitanda, mashine na upatikanaji wa dawa ktk MSD, lkn siyo kutatuliwa hilo sijawahi kulisikia!
Acha kuzungusha maneno kubali tu kuwa huu ni usanii..
 
Tatizo letu Watanzania ni kufikiri kwamba kuna mtu fulani sehemu fulani mwenye wajibu wa kuyashughulikia matatizo yetu kwa mapana yake!. Serikali ni mimi na wewe, ni wewe na yule, ni kila mtu. Ni dhana potofu kudhani kwamba kuna watu fulani ambao wao humaanisha uwepo wa serikali. Hizi akiliza lawama lazima zitutoke vichwani mwetu kwanza, halafu baada ya hapo ndipo tutakuwa tayari kuelewa maana ya uwajibikaji. Anatazamwa Magufuli na wasaidizi wake kama vile ni watu wametoka sayari nyingine kuja kutuondolea maelfu ya matatizo yetu.

Hakuna kitu kama hicho. Tatizo ni sisi wote kwa ujumla wetu. Kila mtu atambue kuwa yeye ni serikali. Kule Marekani anaposhinda urais mgombea mmoja, haapishwi na kupewa ofisi siku inayofuata, hupewa muda wa miezi zaidi ya miwili ili aweze kuelezwa mambo yote yanayohusiana na urais wake. Haijalishi yeye ni republican au democrats, lazima aelezwe ni mambo gani anayotakiwa kuyatanguliza kwa maslahi ya taifa la Marekani.

Siasa za vyama vingi zimekuja kwetu pasipo ujio wa miiko ya usimamiaji wake. Uvivu wetu binafsi tunataka kuutafutia sababu za kuuhalalisha. Tujitathmini kwa kina ili tuweze kuikoa nchi hii.
Nchi imeelaniwa hii mkuu, usipoteze mda kuiwaza sana.
 
Mkuu hao vijana wasikuumize kichwa...luwasa ameishatangaza kuwania urais 2020 sasa wameishaanza kampeni hao...

Usitarajie kuisema vizuri serikali ya Magufuli...ila wasichojua ni kuwa wanapambana na kivuli chao...Magufuli ni namba nyingine.

Magufuli ameishaeleweka dhamira yake na watanzania tuko nyuma yake tunamuunga mkono kwa kufanya kazi na sio kumvizia kakosea wapi ili tuanzishe thread...

Ni aibu kuona kampeni ndio zimeisha ila watu wanaendeleza siasa badala ya kazi...ukiona hivyo jua watu hao hawako sawa yaani ni punguani....
Jadili hoja acha kuingiza habari za siasa. This shows how dumb you are..!!!
Mnashindwa kutimiza wajibu mnasingizia siasa... sooo low...
 
Kuna ngazi ya maendeleo ambayo nchi hufikia ambapo sasa wananchi wenyewe wanaweza kujicontrol kama zilipofikia nchi zilizoendelea lkn hii ni hatua ya mbele kabisa!

Lkn asikudanganye mtu nchi zilizoendelea wote wanafanya population control sema mbinu tu ndiyo tofauti kwa mfano nchi tajiri zote watoto wa kike hupewa birth control pills au vidonge vya kuzuia ujazito sasa maana yake nini?
Ni kwamba mtoto wa kike wa Ulaya, Marekani, Japani au nchi tajiri yoyote hawezi kupata mimba ya bila kutarajia yaani kama atapata mimba ni kwamba ameamua kupata mimba na siyo bahati mbaya sisi kwetu hakuna hilo ina maana msichana yoyote yule anayelala na mwanaume ana hatari ya kupata mimba wakati wowote ule na ukiangalia takwimu za serikali wasichana wanaopata mimba bila ya kupanga yaani kuwa tayari kuwa na mtoto ni wengi sana jaribu kuangalia tu mtaani na hesabu wasichana waliozaa kabla ya wao kuwa tayari kuwa na familia au kijijni ukienda, sasa hii maana yake nini?
Ina maana huyu msichana kwanza hana elimu ya kumuwezesha kupata ajira yaani yeye mwenyewe bado hajaweza kujisimamia halafu tayari tena ana kiumbe ambacho anapaswa akihudumie sasa Umaskini utawezaje kuisha au kupungua hapo?!

Hivyo basi kwa kuwa sisi hatuna uwezo wa kuwapa wasichana wetu vidonge vya kuzuia mimba hatuna budi kutafuta njia mbadala, ili mtoto azaliwe tu na yule mwenye uwezo wa kumuhudumia na si vinginevyo!

Ukiangalia hiyo picha hapo chini utaona ninachoongelea, wapo wengi kama wangekuwa na vidonge vya kuzuia kupata mimba wengi wao wasingeamua kupata mimba!

images
Wewe akili yako sio nzima kabisa au unatumia Masaburi kuwaza,badala ya kuimarisha forward yako ili ifunge magoli team ipate ushindi wewe unakuja na wazo la kupanua magoli. Wewe kila tatizo kwako suluhisho ni depopulation sasa tukianza na hilo tatizo la wagonjwa kulala chini halafu tuje kwenye tatizo la maji,foleni,ajira na elimu then tupunguze population tutabaki Watanzania wangapi?. "Hapa Kazi Tuu" teh teh teh
 
Mahitaji ya muhimbili yanaongezeka kila leo hivyo hilo si jambo la kushangaza...
Sometimes uache utoto hizi habari kawaambie facebook,
The plan should be there in order to tackle the situation...
Huwezi ukaja na majibu mepesi hivi kama umeamkia kwa mchepuko...
 
Morogoro? Dah watanzania kwa uongo!!! I salute you
Uongo ni kuambiwa mashine mpya imenunuliwa badala ya kuambiwa imechukuliwa kwingine.Inatokea Dodoma,kusema Morogoro ndiyo ni makosa ya uandishi lakini nadhani ujumbe umeupata.
 
Leo ukifuatilia taarifa ya habari Magufuli katembelea tena Muhimbili kwa kustukiza
kakuta matatizo tele hasa amewakuta wamama waki share vitanda hadi watu watano
na wengine wakilala chini.....

Utakumbuka few months ago tulitangaziwa kuwa baada ya Magufuli kwenda Muhimbili
vitanda vilipelekwa hadi vikakosa wagonjwa
kuna picha zilisambazwa paka kalalia kitanda kipya Muhimbili
na kwamba sasa mambo ni tofauti kabisa...vitanda tele na kila kitu saafi

Sasa binafsi siamini kabisa Muhimbili imewahi kuwa safi na matatizo yakaisha
ambacho najiuliza why 'maigizo yale ya kuwa mambo ni saafi' yaliruhusiwa
kuendelea ?

why sisi wananchi na waandishi wa habari hatukupinga kabisa habari za kuwa
mambo ni saafi muhimbili?
why habari ya leo iwe kama habari mpya
while in reality watu wameendelea kulala chini tu kama zamani?

Inawezekana kabisa tatizo haliko kwa wanasiasa?

tatizo liko kwetu wananchi na hasa media?
tumeletewa 'sanaa tukaishangilia huku ukweli tunaujua'?
sababu muhimbili hali yake sio siri
lakini tulipoambiwa mambo sasa ni saafi tuliruka ruka na kushangilia...
huku kiukweli hali ni ile ile tu.....

Na leo tena wananchi wamemlilia tena Magufuli bila kujiuliza
ni kweli Magufuli hali iliyopo haijui?si alikwenda juzi tu hapo hapo Muhimbili?
au haya matatizo ni mapya kabisa?
Now you are talking
 
Uongo ni kuambiwa mashine mpya imenunuliwa badala ya kuambiwa imechukuliwa kwingine.Inatokea Dodoma,kusema Morogoro ndiyo ni makosa ya uandishi lakini nadhani ujumbe umeupata.

Acurasy katika kutoa taarifa ni mihimu sana, Morogoro na Dodoma wapi Na wapi?
 
Back
Top Bottom