Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,063
- 22,755
Mkuu The Boss, mimi nimeshangazwa sana na kushangaa kwako. Magufuli alikuwa serikalini miaka 20 akiwa Waziri lakini katika kampeni yake muda mwingi alionesha kushangaa kwa nini mambo mengi yalikuwa hayaendi. Kwa kawaida mtu wa aina yake ilitakiwa aogopwe kama ukoma lakini cha ajabu Watanzania walichukulia huko kushangaa kwake kama sifa ya kupewa Uraisi. Hebu soma hili jibu lililotolewa na anayejiita Barbarosa kama sababu ya wagonjwa ku"share" vitanda Muhimbili, nanukuu;Yaani leo nimeshangazwa mno na sisi watanzania tulivyo
eti Magufuli anarudi pale pale kutoa ahadi ile ile na inakuwa ni 'new event'
yaani hata siku 100 hazijaisha....tushasahau
Hapa tayari yupo Mtanzania, Barbarosa, anayeshangaa kama Magufuli alivyokuwa akishangaa kwenye kampeni kwa nini idadi ya watu Dar inaongezeka mwaka hadi mwaka (sijui alitegemea iweje!) Ni sawa na mtu anayeshangaa kwa nini leo tuko milioni 50 wakati tukipata Uhuru tulikuwa milioni 9 tu.Barbarosa said:...kumbuka Hospitali zote Dar zimejengwa wakati Dar ikiwa na wakazi chini ya milioni Moja leo hii tuko zaidi ya milioni 4.5...
Bila shaka Magufuli mwenyewe alishangaa kuambiwa wako wagonjwa wanalala chini siku mia baada ya serikali yake kuwahakikishia wananchi kwamba tatizo hilo limetatuliwa. Hii ndiyo sababu nakushangaa wewe kuwashangaa Watanzania wanaposhangaa ahadi za kushangaza zinazotolewa kwa mshangao mkubwa!