Huyajui maeneo haya!?Basi huifaham Dsm.

kadoda11

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
21,453
20,712
1-Kariakoo jirani na mzunguko wa magari (round about):wanapatikana wauzaji wa dvd za ngono za kila aina,muuzaji mmoja alinidokeza kuwa kijiwe hicho kinafahamika pia kwa viongozi wa serikali.Wao pia ni wateja wao wakubwa wa dvd hizo.kuna wakati wanaenda wenyewe au hutuma wap ambe wao wakawachukilie mzigo.
2-Posta mpya jirani na mgahawa wa azam take away:Hiki ni kijiwe cha matapeli waliobobea katika utengenezaji wa vyeti bandia vya kitaaluma,kuiga sahihi za viongozi,uuzaji wa fedha bandia za kigeni,uchongaji wa mihuri,usajili wa kampuni hewa za kibiashara nk.Kwa wale mnaopeda kupita njia za mkato kufikia mafanikio sio vibaya mkianzia hapa.
3-Kariakoo gerezani-hili ni eneo ambalo vijana wako busy n asana na kazi ufundi.Kila kijana yuko imara kwa kazi za mikiki mikiki na shuruba.
Ila lina sifa ya ziada.kama umeibiwa kifaa chochote kilichoundwa kwa shaba,chuma,bati nk.Sehemu ya kwanza kuanza uchunguzi wako ni eneo hili.Hapa ndipo wanapo patikana mabingwa wa kuuza vyuma chakavu,kutengenisha spare za magari ya wizi na hata kuyabadilisha rangi.Ukiibiwa gari na ukafika hapa,kuna mawili kukuta gari lako likiwa na muonekano tofauti au kulikosa na zana zake kuuzwa katika maduka ya used auto spares yaliyotapakaa kila kona jijini.
4-Kariakoo mtaa wa aggrey:mnao tumia bidhaa halisi za blackberry,nokia,iphone ,sumsumg nk.hili ni eneo muhimu kulifahamu.
Ni kipande kidogo cha mtaa wa aggrey kama unelekea kiwanda cha bia cha tbl.Hapa wanapitaikana vijana watanashati madalali wa bidhaa za simu za mkononi.Kama simu yako ya gharama imeibiwa nashauri uchunguzi wako uanzie mtaa
wa aggrey.Na kama ukakuta kijana anauza simu yako usipandishe hasira na kutoa vitisho.Elewana nae ili akuuzie upya anagalau kwa bei nafuu.Kinyume na hivyo uhakika wa kuipata ni mdogo.Hii ndio dsm akili kichwani mwako.
Wakuu kama kuna sehemu sijaitaja sio vibaya mkaitaja pia.
 
Mkuu hapo umenena maana sina sehemu ya kuongezea. Ila pale tazara pana eneo linaitwa Mapambano hapo utapata mahitaji muhimu ya vifaa vya ujenzi kwa bei nafuu kama madirisha na nondo lakini feki
 
k/koo mnadani umepasahau, hapo ukiibiwa kifaa chochote kwenye gari lako jaribu kuwahi hapo.
 
Posta ya zamani pale garden ya benki kuna wauza kahawa,madereva tax,wamekaa mda wote wanacheza draft..ulizia chochote pale utapata cheti,visa(adi ya ukimbizi),paspot,kiwanja,nyumba ya kupanga/kununua,machangu wa high class,ajira,kununua bank statement nene za kufanikishia michongo,gari ya kukodi/kununua na magumashi yote apa mjini..

Kuna chocho lingine pale Mwenge...aah nisijearibu dili za watu bure.
 
Back
Top Bottom