Baadhi ya maeneo Karikoo mawasiliano ni kizungumkuti

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Licha ya kuwa Karikoo ni Jiji la kibiashara lakini hali ya mawasiliano imedaiwa kuwa kizungumkuti kwenye maeneo mbalimbali hali ambayo imekuwa ikipelekea malalamiko ya muda mrefu.

Katika kufuatilia kwa kina jambo hilo na imebainika uwepo changamoto hiyo, ambapo baadhi ya mitaa ili uweze kufanya mawasiliano inatakiwa utumie 'app' zinazotumia internet, mfano WhatsApp au Telegram lakini kinyume na hivyo mawasiliano ni ya kusuasua.

Baadhi ya wafanyabiashara kwenye maeneo yanayokumbwa na changamoto hiyo hususani eneo ilipo benki ya Akiba, Mtaa wa Kongo Narung'ombe wamesema changamoto hiyo ni kikwazo kwenye biashara zao ambapo wamedai kuwa swala hilo wameshalifikisha kwa viongozi wao.

Peter Endson Mbilinyi ambaye ni Katibu Mkuu wa Jumhiya ya Wafanyabiashara Karikoo, amesema wameshapokea malalamiko hayo na kuyafanyia uchunguzi, ambapo amesema kuwa walibaini yana ukweli huku akidai kuwa nayeye binafsi amekuwa muhanga wa changamoto hiyo.

"Kariakoo ukiingia sehemu nyingi huwezi kupata mawasiliano mtu huwezi kupokea au kutuma sms, inakutaka ukitaka kumtafuta mtu lazima ungie kwenye internet mfano uingie kwenye WhatsApp call " amesema Peter Endson Mbilinyi

Katibu huyo amesema kuwa wameshachukua hatua za kufikisha madai hayo kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambapo amedai kuwa walielezwa kuwa changamoto hiyo inatokana na 'Buster' zilizofungwa kwa ajili ya kuwezesha mawasiliano kwamba zina uwezo mdogo.

Amesema kuwa taarifa hiyo waliifikisha kwenye mamlaka husika kipindi mrefu zaidi ya miaka miwili iliyopita lakini bado ufumbuzi wa jambo hilo haujapatikana, ambapo amedai kuwa changamoto hiyo imekuwa endelevu.

Katika uchunguzi wa jambo hili imebainika changamoto hii inawakabili zaidi wahysika amabao wapo ndani ya majengo hasa ya gorofa ambazo kulingana na mandhari ya kariakoo zimefatana, mtaa wa Kongo Narung'ombe ambao ni maarufu kwa uuzaji wa nguo na viatu ni kati ya maeneo yenye maduka ya ndani ambayo yamekuwa na mkusanyiko wa watu wengi.

Mmoja kati ya wafanyabiashara wa nguo kwenye Mtaa huo wa Kongo Narung'ombe unaodaiwa kuwa na changamoto hiyo kwa sana amesema kuwa imekuwa ikiwalazimu wakitaka kuwasiliana na wateja lazima waende maeneo maalum ili kupata mawasiliano.

"Suala ili ni tatizo kubwa hapa simu tunakuwa nazo kama hatuna, ukifika ndani dukani simu inakuwa kama kopo, ukitaka kuwasiliana na mteja wako lazima utoke uende sehemu ambapo afadhari kuna unafuu ndio unapata mawasiliano, hii sio sawa kwa kariakoo hatuelewi tatizo nini lakini linatukwamisha sana" amesema mfanyabiashara huyo ambapo hata kauli za wengine walio ulizwa hazikotofautia sana na hiyo.

Ikumbukwe Kariakoo ni eneo la kibiashara ambalo limekuwa lango la mapato, ambapo kwa taarifa mwanzoni Mwezi July 2023 iliyotolewa na mamlaka ya kodi Tanzania iliutaja Mkoa wa kikodi wa Kariakoo kuvunja rekodi kwa kukusanya Sh bilioni 40.8 sawa na asilimia 102 kwa mwaka.
 
Back
Top Bottom