Nayaandika haya huku moyo wangu unavuja damu. Uchungu mwingi sana

Mpauko

R.I.P
Jan 19, 2019
2,323
3,353
Nakumbuka ilikuwa mwaka 1994, Kihanga, huko Iringa Vijijini, kwa mipango yako nilizaliwa, mtoto mdogo mwenye afya njema.

Miaka sita mbele hakika nilibadilika hasa, kijana mchangamfu, mchapakazi, mwenye akili nyingi na fuarha tele, wazazi wangu walikuwa ni wenye kujivunia kijana huyu,

Ndugu na jamaa walipenda kunibeba huku wakitafuta chochote nilichofanana nao waseme kauli kama ana kichwa kama changu, oooh uso kama wangu, oooh kisogo kama mimi. Ilifurahisha sana.

Mwaka 1999, tulihamia Dar es Salaam, nikipata marafiki wengi mno, hakika nilifurahia sana maisha ya pale Ubungo, Msewe, tabasamu halikuniisha usoni mwangu kamwe.

Nakumbuka nilianza chekechea mwaka wa 2001, nilikua genius kamwe alama ya kosa sikuwa na urafiki nayo kabisa na hii ilinifanya kuwa na urafiki wa kudumu na zawadi za viatu, nguo na vikolokolo vingi mno vya michezo.

Mwaka 2003 nilianza darasa la kwanza Msewe primary uwezo wangu mkubwa uinifanya kupendwa na kila mtu ni mara moja tu nilionja adha ya viboko vya makalioni kwa kosa lililotokana na ubishi wangu.

Nakumbuka nilipewa zawadi ya buti maarufu kwa wakati huo, zile za rangi ya khaki "Timberland" kwa wasiozijua tazameni wimbo wa ferouz "starehe" alivalia kiatu hiki pendwa.

Rangi yake ya khaki haikuruhusiwa shuleni kama mnavyokumbuka kilitakiwa kiatu cheusi.

Kwa mapenzi yangu kwa kiatu kile nilikuwa nakivaa hadi nilipopigwa marufuku kuonekna shuleni na kiatu kile.

Nilichofanya ni kuiba Kiwi ya baba na kukipaka, nilichoambulia ni bakora za kutosha tu na kiatu changu mwalimu alikichukua.

Nakiri kuwa hizi ndizo nyakati pekee nzuri, nyakati za furaha ya kweli, amani ya kweli na niliufaidi vilivyo utamu wa dunia hii pamoja na viumbe wa dunia hii sikuwaza kama kila kitu kitabadilika na kubaki kuwa historia. Naumia sana. Ee Mola kwanini uliacha iwe hivi?

Mwaka 2004, tulihamia mkoani Mtwara na tuliwasili kwa meli jumatano asubuhi ya mwezi ule wa tano.

Mwaka huu 2004 kila kitu kikabadilika katika usiku ule wa Jumapili ya mwezi wa tano. Nasikitika sana na kutamani iwe ndoto lakini haikuwa hivyo.

Nilipoteza uwezo wa kusikia. Ndio nilipoteza usikivu wangu. Nilihisi hivyo. Nilisikia kwa shida sana lakini hakuna aliyeweza kulijua hilo nami sikuwa na ufahamu wa kilichotokea zaidi ya kuhisi utofauti masikioni mwangu.

Vipigo vilianzia palepale nyumbani. Ilikuwa ngumu kupitisha siku bila kuchezea fimbo. Nina kiburi!

Tayari nilikuwa darasa la pili, vipigo kwa upande wa shuleni na nyumbani vilinifanya taratibu kuwa muoga mno, nikiitwa tu nilijua ni fimbo hizi

Hatimaye mwalimu mmoja akalin'gamua hili, mzazi akaja akasem hata hakuwa anajua, Hospitali zote mkoani Mtwara hazikuzaa matunda, hatimaye Muhimbili na Aga Khan pia hakukuwa na matumaini nasikitika sana.

Sasa nikawa kituko darasani taratibu vipigo na kupokonywa Tsh20 yangu vilipamba moto, ile haiba yangu ya miaka 7 nyuma ikaishia hapa, nikawa mkimya, mpweke mwenye mawazo mengi na muoga hasa.

Ulikuwa ni wakati wa kuyasahau yote yaliyopita, sikuwa na sauti tena ilieleweka kwamba nilikuwa mwanafunzi wa ziada tu, wakati ulifika ambao sitozisikia tena nyimbo nilizozipenda sana, sitomsikia juma nature akiimba "ugali", sitowasikia tena Mabaga Fresh, GK, Saida Karoli wala kidali poo! Hakika niliumizwa sana na hili.

Maisha sasa yalikwishakubadilika hadi ninahitimu darasa la saba 2009, tayari nilikwishajitenga na maisha ya kawaida na kuihi katika ulimwengu wa pekee kabisa.

Upweke, ukimya na kukosa marafiki viliadhiri maisha yangu kwa ujumla, sasa sikuwa na rafiki yeyote wa kweli kila nilipojaribu kutengneza urafiki na walio wengi bado dharau na dhihaka havikufichika. Hivi anaskia kweli huyu? Mtukane kwanza! Hey hey! Oooowa kaskiaaa! Hivyo ili kujiepusha na maumivu ya moyo kukaa peke yangu ilikuwa ni bora zaidi.

*************

Screenshot_2019-07-17-23-56-27.jpeg

mwaka 2009 ulimalizika kuhitimisha miaka 7 ya kudharaulika, kubaguliwa, uonevu wa wazi wa walimu wanafunzi kebehi na lugha mbaya iliyoniumiza moyo...niliyaacha yapite.

Mahangaiko hayo yote yalinifanya nijenge nadhiri ya kutotaka niajiriwe na yeyote, nilitaka niwe bosi, niliamini sitodharaulika katika wadhifa huu, nilota usiku na mchana nikiwa tajiri mkubwa naniliamini its the matter of time...

Saafri ya elimu ya sekondari ilikuwa ngumu zaidi kuliko nilivyotarajia, vipigo vilizidi, usomaji ukawa mgumu zaidi lugha ilikuwa changamoto mno..

Hapakuwa na namna zaidi ya kukubaliana na hali halisi, sasa ilinilazimu kutumia nguvu nyingi kuweza kuendana na masomo haya ya kiingereza.

Kushindwa kufanya vizuri katika midahalo na morning speech kulinivunja moyo kwani niliishia kuwa kituko zaidi kwa kutokujua jinsi maneno yalivyopswa kutamkwa katika kiingereza, ningelisikia vipi wayatamkapo walimu na wenzangu?... Nilikuwa kituko kwelikweli. Eti nationi! Kumbe nesheni bwana!

Sasa nikawa na shughuli mbili, kutumbua macho hadi vipindi viishe kisha ndio nianze kujielekeza notes zile. Sikuwa na rafiki wa kweli kutembea nami katika wakati huu mgumu.

Ni mengi sana machungu, kutimuliwa darasani, kuadhibiwa kwa makosa nisiyostahili, kuwa wa ziada katika kila kitu, kejeli za wazi wazi za walimu na wanafunzi yanaumiza sana.

Nakumbuka mwaka 2012 nikiwa kidato cha tatu, nilikatishwa tamaa sana na matukio ya kunihuzunisha kila siku, uamuzi niliofikia ni kununua vidonge 8 vya malagin, hizi ni pakti nne, kila pakti ikiwa na vidonge viwili.

Nilibugia zote, lakini bado shida hizi zilinihitaji zaidi kuliko kuniacha nipumzike, nilipona.

Baada ya kufeli kwa jaribio hili, nilinunua sumu ya panya, niliishia kuharisha ajabu.

Haukuwa mwisho, nilikusanya viwembe vitatu nkiavikatakata na kuvitia katika kikaratasi, nikanywa na kusubiri vnimwage utumbo.

Lakini unafahamu kilichotokea? Ni kwamba hakukuwa na athari zozote hata leo hii hujiuliza ni wapi vilikwenda?

Hatimaye sasa mwaka 2013 ukafika salama salimini, nikashukuru kwa kufika hapa Mungu alikuwa nami nilifaulu vizuri.

Bado niliishi na ndoto yangu, kusomea biashara, nijiajiri, niwe bosi ili niaidharaulike tena!, hivyo nilikataa kwenda kidato cha tano, i believed i was destinied to be a bos not otherwise and thats what i wished tangu nikiwa shule ya msingi.

Hatimaye nilikuwa Stella Maris College (St Augustino) nikavalia suruali yangu ya kitambaa na shati langu bora kabisa, ilikuwa ni siku yangu ya kwanza chuoni.

Niliamini sasa nitapumzika na kuheshimika nikiwa mahali hapa.

Baada ya kuingia eneo la chuo kila mtu alikuwa busy, sikuelewa darasa ni lipi na kipi ni kipi, nilichanganyikiwa!

======

SOMA MWENDELEZO HAPA

Nikaamua kuingia tu katika ukumbi uliokuwa pembeni yangu, tukasoma eti scheme of work!... Nikaelewa basi? Hatimaye kipindi kikaisha.

Nikabaki palepale, wakaingia wengine tukasoma eti computer virus..... Nikibaki😳😳😳 nikasema hii ndo university bwanawe!

Babahti nzuri nikakutana na bwana mmoja tuliishi mtaa mmoja, akaniuliza nasomea nini nikamjibu CBA... Akaniambia nenda paee notice board kuna ratiba na venue.. Akili ikanikaa sawa sasa..

Ni notisi pekee nizitumiazo... Kazi ikaja hapa leicturer haandiki yupo tu kama anahubiri jukwaani.. Sielewi!

Wiki ikaisha hakuna nilichoandika.. Hakuna kitu kichwani... Wenzangu wameandika samary.. Haisomeki ikaeleweka..

Siku moja tukiwa tunasoma leicturer aliniona namkodolea macho sana akajua namwelewa sana, si akaniuliza swali, nikabaki namtumbulia macho tu..

Mwisho wa kipindi nikatoka nje kinyonge, sielewi niache chuo au nifanyaje, notisi hamna..!

Yule leicturer alipotoka akaniona nimesimama nikiwaza, akaja akanipa ujanja kuitumia internet.. Asante sana mr. Kumbe kila kitu kipo mubashara katika internet...

Wiki ya pili nakumbuka tulikuwa darasani, leicturer alikuwa padri mnoja mwenye nafasi za juu pale chuoni, mwisho wa kipindi akatamka swali, wala sikulisikia nashangaa wenzangu wanaandika katika karatasi na kukusanya, nindike nini sasa?

Akaniona siandiki akaja, weweeee mbona huandiki,nikamjibu sikuwa nimelisikia swali.

"wewe ni kiziwi"aliuliza kwa sauti kubwa.

"ndiyo" nilimjibu.

"sasa hapa umekuja kuolewa au? " akauliza

Watu waliangua vicheko, kisha akanitaka nimfuate ofisini, mja kwa moja akanipeleka kwa pincipal...... Alitaka nifukuzwe nilimtazama tu.

Principal akaniambia niende tu niendelee na masomo,padiri yule alichukia sana.

Maisha yachuoni yakawa machungu kuliko katika ngazi zote nilizopitia.

Leicture ilibeba zaidi ya wanachuo 500, halafu leicturel anasema "mtazame huyu kiziwi anasomea usimamizi wa biashara, atamwajiri nan? " nilitamani ardhi ifunguke nipotee.

Maneno kama haya yakawa yanazungumzwa mno kiasi kwamba kila tuwapo leicture nilikuwa na hofu nikiwaza leo nitatupiwa dongo gani!.. Leicturer hawakuniheshimu.
Unaweza tafakari ni kiasi gani niliishi maisha yasiyoridhisha... Chuo kinajumuisha watu wengi sana, watu wazima.. Kutendewa kama mtoto iliniumiza sana.

Nilikonda mno mwaka ule wa kwanza, nilipomaliza certificate tuuuu... Nikawafata wazazi wangu..

"mama na baba kwa kweli mim maisha ya kusoma naishia hapa..." niliongea kwa uchungu sana na machozi yalinitoka.

Kmbukumbu za kutendewa isivyo chuoni zilinitia uchungu sana, nilitamani mno ningelibaki na masikio yangu, lakini haikuwezeka.

Hakuna aliyekuwa tayari kunielewa, hawakujua uchungu niliokuwa nao moyoni mwangu.

Nilichoamua ni kununua pakti ya sumu ya panya, nilimeza pakti ile, nilihitaji kupumzika, nilihitaji kujaribu kuishi kwingine.

Nilipoteza fahamu na kukaa miezi miwili hospitali, niligoma kunywa dawa, nilihitaji kupumzika.

Nyakati fulani wagonjwa walifariki pale wodini, nilitamani ningekua mimi.

Dunia hii ilinihitaji zaidi, nilipona, nilijitahidi kujiweka mbali na wanadamu ili kuitafuta furaha, binadamu hakuwa na upendo nami tena,

Nilijaribu kunywa panadol 12 bado nilipona, kwanini nipone Mungu hujaona maisha dhalili ninayoishi?

Kila kitu kilikuwa kimeharibika kwa sasa, ilikuwa ni lazima nianze upya, hatimaye nikasema yess, nitarudi chuo.

Mwaka 2016 nikatuma maombi katika mfumo wa udahili wa serikali kwa kada ya elimu, nikachaguliwa chuo binafsi St. Benard TTC Singida.

Maisha ya hapa hayakuwa na tofauti sana na maisha yaliyopita lakini ilinipasa kuwa mvumilivu.

Maneno ya "huyu mwalimu atafundishaje? " "huyu nae kaacha kusome ufundi cherehani kaja huku" hata hivyo hawakuwa na jipya, nilikwishakuyazoea hayo.

Mwishoni mwa mwaka wangu wa kwanza pale chuoni, familia yngu ilinifahamisha kuwa nyumbani kuna matatizo, baba kafukuzwa kazi....

Kwa maana hiyo rudi nyumbani tu.,,, hili sikukubaliana nalo, nilipenda kuwa mwalimu.

Kwa babati nzuri ada ya mwaka wa kwanza nilikwishakuilipa, nitafanya nini mwaka wa pili??

*****************

Nilikuwa na laptop ambayo niliiegemea kwa ajili ya kutafuta na kuhifadhi notes, ilinilaziku kuiuza, pia niliuza baadhi ya mali za nyumbani hatimaye nilipata laki sita.

Nililipa ada tshs laki 5 salio la deni lilikuwa 1. 1 milioni hii nitaipata wapi,siufanikiwa kuipata na mambo yalipozidi kuwa mabaya sikuwa na jinsi zaidi ya kuzungumza na uongozi wa chuo. Hatimaye nikafanikiwa kumaliza chuo.

Wakati wa kuingia mtaani kufanya vibarua ili nipate ada iliyosalia nikomboe vyeti vyangu.

Niliwasili mtwara sasa, hali niliyokuta nyumbani haikuwa nzuri, haikuwa nyumba kubwa nzuri tena bali lilikuwa pagala, mapazia ndio pekee yaliyokuwa dirishani, haikuwa na milango hii ililazimu kuezeka tu bati.

Maisha yalikuwa mapya, kula mlo mmoja ama kukaa hata siku mbili bila kula, ilichosha lakini ndiyo yalikuwa maisha etu... Nilisikitika sana.

Mda wa kuingia mtaani kupambana ulikuwa ni huu sasa.

Lakini mambo yalikuwa na matarajio tofauti, kwani vibarua vilihitaji kuwa na mtu wa kati, kwa kuzingatia ugeni wa eneo hili ugumu ukajitokeza wazi wazi.

Shida nyingine ikaibuka, mtazamo wa jamii, kwani nilipohitaji kazi kutokana na umbile dogo. Nilionewa huruma!, lakini mbona wapo wenye miili midogo zaidi yangu? Jbu ni kwamba sikuwa nasikia vizuri.

baada ya kwenda huku na ule bila mafanikio ya kupata vibarua, niliigeukia taaluma yangu.

Nikaandaa barua za maombi ya nafasi ya kujitolea katika shule binafsi.

Hawakuwa na imani nilijikuta nikimaliza shule zote binafsi, lakini hakukuwa na manufaa kwaninilikayaliwa na nafasi kupewa wengine.

Hali hij haikunikatisha tamaa, nilikuwa imara, niliaza kutafuta kazi katika hoteli na hospitali binafsi, kazi za usafi na utunzaji mazingira.

Nilizunguka kwa miezi kadhaa bila ya mafanikio, ilinipasa kuwa mchaguzi wa ajira niombazo, linipasa kuomba ile tu iliyo ndani ya uwezi wangu.

Hivyo sikuwa na wigo mpana katika kutafuta fursa hizi za ajira.

Kuna wakati niliandika barua katika shule moja ya kanisa katoliki, nikaitwa kwenda lakini walipobaini changamoto ya masikio walinikatalia, nilichoka!

Nikatafakari na kujisemea kumbe kupambana kwenyewe ndo huku!

Nakumbuka ilikuwa ni mwezi hivi tangu nijiunge JamiiForums, nikaandaa mradi wa kuchoma vitafunwa na mtaji ukawa 100,000.

Sina mtaji na ajira bado ni kizungumkuti, nitajaribu jamiiforum.

Matokeo yake hayakuwa mazuri kwaninlishambuliwa kwa maneno mengi, niliumia sana na nilijutia sana uamuzi wangu wa kuomba mtaji katika JamiiForums.

Nakumbuka siku moja nilipokea ujumbe katia jamiiforum, wakati huu nilikuwa njitolea katika shule ya serikali.

Akaniambia, yupo tayari kunipa msaada wa mtaji hadi shilingi laki tano, kwa sharti moja kwamba nimfuate kituo kikuu cha polisi mtwara na niulizie Afande Tall!

Siku iliyofuata nikiwa na furaha, baada ya kipindi changu cha asubuhi nkatoka kwenda kituo kikuu cha polisi baada ya kuulizia walishindwa kumtambua.

Nikamtumia ujumbe kuwa nipo kituoni(jamiiforum) akaniambia yeye yupo tayari kunitumia mtaji ama kuniajiri katika biashara zake endapo tu, nitaikopy thread niliyoandika jamiiforum, kama ilivyo kisha niipost katika ukuras wangu wa facebook na akiuona tu atanpatia ofa y mtaji au kazi.

Lilikuwa ni sharti gumu sana, facebook ni mahali ambapo hata wadogo zetu, jirani zetu, walimu wetu na wengine wengi, je itakuwa vipi wakiona post hii....

Haiyumkin hali mbaya ya famlia yangu, kukosa ajira na kipato chochote, nilihitaji mno mtaji au ajira ile kuliko kitu chochote.

Maamuzi niliyogikia yalikuwa ni kupost ujumbe wa thread ile, kwa kuukopy kama ulivyo na kuuweka katika facebook.

Unaweza kufikiria nilikuwa katika wakati mgumu kiasi gani? Na unajua ni nini kilichotokea?

Ujumbe ule ulisomwa na kila aliyenifahamu lakini ulikuwa na likes 13 pekee na coment sita za pole.

Idadi hiyo likuwa baada ya siku tatu, ilishangaza sana kwani picha yangu au post yoyote ilichukua masaa matatu hivi kufikisha mamia ya likes na coment.

Bwana yule baada ya hapo akaniblock katika whatsap, niliumia sana na kutazama nilivyojivua nguo, nilufuta ujumbe ule na sijajua lengo la bwana yule, hakunitendea uungwana.

Basi sikuwa na la kufanya zaidi ya kuendelea kujitolea shuleni pale, sikuwa na furaha, ilinilazimu kutembea masaa mawili kwenda shuleni, sikumudu nauli shilngi 400.

Kadhaika niliendelea kutafuta ajira hapa na pale bila mafanikio.

Ndugu zangu hawakunipenda tena, kwani waliniita mzigo, niliumizwa na hili kwani ilinikumbusha upendo wao mwingi sana kwangu kipindi kile ningali na usikivu, vipi leo waniite mzigo?

Familia yangu nayo ilianza kunichoka kwani sikuwa na msaada wowote licha ya hali ngumu ya nyumbani hapa.

Sikuwa na cha kujitetea, ni kijana mkubwa wa kiume, umri wangu pia ulinipasa kuwa na mchango, nilijaribu lakini bado sikufanikiwa.

Ilinipasa kujaribu kila nilichoweza kukifanya, wakati huu niliamua kwenda kijiwe cha bajaji na bodaboda, nilitengeneza urafiki kwa miez kadhaa.

Kisha nikamwomba mmojawapo anifundishe bajaji, waliposikia walicheka na kebehi, bado niliendelea kujaribu lakini sikupata ushirikiano.

Baada ya kushindikana, sasa niliwaza nawezaje pata cheti changu ili nikitumie kuomba ajira hususani ajir za serikali.

Nikamfuata afisa elimu ambae ananifahamu kwani alikuwa anakujakuja pale shuleni na anajua changamoto ya usafiri.

Nikamweleza hali ya kwetu, changamoto ya usafiri, hali ya cheti changu kushikiliwa na chuo,hivyo nikamuomba aangalie anavyoweza kunisaidia kwanafas yake. Akasema sawa nisubiri.

Nikarudi kuendelea na majukumu kule shuleni, wiki hatimaye mwezi nikaenda kwa afisa kuuliza suala langu, hakunikaribisha vizuri kwan nilimkuta mapokezi na watu wakiwa wengi tu ikabidi tuongee hapohapo

akaniambia ana kazi nyingi mmi nikasubirie tu na akanikataza kwenda ofisini kwake.

Ukapita mwezi nikamsms afisa hakujibu, nikamtumia dadaangu kumpigia hpokei simu basi nikaachana nae.

Mamaangu akaanza kuumwa umwa ikabidi niache kujitolea na kulima mihogo wa ajili ya chakula baba hana kazi uzunguka hapa na pale akirud ma miatano sawa, buku sawa,

Baada ya hali ya mama kutengamaa, nikakumbuka katika thread flani kna mtu alinishauli kwenda kwa Dc au Rc, nikaenda kwa dc

nikajieleza akasema nisubiri kisha niende tena, nikaenda akasema ataniandikia barua ya kuchangisha hela, but mwezi ushaisha hajaniandikia na amehamishwa

Now nikienda kule ofisini hawanipi ushirkiano mzuri, mara hayupo wakat gar yake ipo nje, seem DC mpya anafahamu shida yangu ila kapuuzia ndio maana hata wao hawatoi ushirikiano.

But nilirudi tena nkaambiwa ataniandikia barua ya kuchangisha hadi leo ni kimya nikaachana nao.

Nikanza kuwalisha vizuri kuku watatu mitetea waliokuwepo nymban kwa kuwapa chakula cha ziada na hatimaye wakaanza kutaga

Walitaga mayai 10+ kila mmoja nikawawekea mayai 10 kila mmja wakatotoa nikapata vfaranga 25, nikawajengea mahali kwa mabox chumban kwangu, nikawapa dawa za asili.

Wiki tatu tu nikaishiwa akiba ya chakula na sina hata elfu 2 ya pumba na mkaa kwan niliwawekea chombo cha joto, japo ni chumban but hakina madirisha zaidi ya mapazia tu, pia mlango huegesha bati na hakna dari hivyo sikyoa hatari kuchoma mkaa chumba cha kulala

Vifaranga wakaanza kufa wakafa 4 nikaaaume njaa kwan niliwapa makombo machicha ya nazi na uchafuuchafu, nikaamua kuwarudishia wale kuku vifarangavyao, bahati mbaya hakuna aliyesurvive wakafa na wengine wakaliwa na paka.

******************

Lakini sasa hapa ndipo nilipo sasa, miaka 20 ya kuishi katika kivuli cha huzuni na masumbuko ya moyo.

Miaka 20 ya kujaribu kupigania furaha, miaka 20 isiyo na matumaini. Naumia sana.

Chanzo cha yote ni usikivu hafifu, haikuwa bahati mbaya, kwa waamini tutasema mapenzi ya Mungu.

Siku zote inasemwa ya kwamba Mungu hawezi kumpa binadamu jaribu asiloweza kulishinda.

Lakini jaribu gani hili? Kwa sababu ya jaribu hili nimepoteza kila kitu maisani mwangu. Kila kitu kimfaacho binadamu kuishi maisha ya kawaida.

Kwa sababu ya hili nimepoteza marafiki, nimepoteza kujamiiana (socialization)

Kwa sababu hili nimekosa afya njema kwa kusumbuliwa na msongo wa mawazo na nykati zote nilizojaribu kuondo uhai wangu, nimepata maumivu makali ya mwill nikiwa katika jitihada za kupumzika upande wa pili.

Kwa sababu ya hili naishi katika maisha ya upweke uliokithiri.

Kwasababu ya hili msamiati wangu ni mbaya ikumbukwe masikio na mdomo vina uhusiano

Kwa sababu hii hupata kizunguzungu hususani wakati wa usiku.

Kwa sababu hii sina uwezo wa kusikiliza neno la mungu, hali inayodhoofisha imani.

Kwa sababu ya hili siwezi kuburudika kwa muziki, kupata habari.

Kwa sababu ya hili siwezi kufanya kazi nilizotmani kuzifanya kabla.

Kwa sababu ya hili naishi maisha dhalili sana maisha ya dharau za kiwango cha juu.

Karibu kila kitu umeondoka nacho wewe, umeniachia uchungu na maumivu mengi sana.

Moyo wangu unauma sana na nakulaumu wewe Mungu wangu nakulaumu sana kwa kweli.

Mzigo mzito uliomtwisha mja wako ni mzito sana. Mzito sana bwana moyo wangu unaumia.

Machozi yangu yana maana kubwa sana bwana, yamebeba maumivu mengi sana, mpaka lini bwana?

Ee Mungu kama ulivyonigusa nikapoteza kila kitu, niguse tena bwana, Roho yangu inahangaika.

*******************

MWISHO
Pia soma: TANZIA: Mwana JamiiForums Miguu ya Kuku/ Mpauko afariki dunia
 
Kama nitafanikiwa kupata mtoto kabla ya kuondoka hapa duniani basi sitathubutu mwanangu apitie maisha mabaya na mateso nliyoyapitia enzi za utoto kutoka kwa wazazi wangu na ndugu, yaliyoua kwa asilimia 100% future yangu na uwezo wa kujikubali + kujiamini.

pole mkuu. Wazazi hizi nyuzi mzisome kwa umakini sana, haya mateso tunayoyapitia sasa yalitengenezwa toka utotoni, kama utamlea mwanao kwa nidhamu ya uoga na hofu basi akija kuishi maisha haya tunayoishi usishangae sababu ulishachokonoa saikolojia yake kitambo kwenye umri wa makuzi yake.
 
Nikaamua kuingia tu katika ukumbi uliokuwa pembeni yangu, tukasoma eti scheme of work!... Nikaelewa basi? Hatimaye kipindi kikaisha.

Nikabaki palepale, wakaingia wengine tukasoma eti computer virus..... Nikibaki😳😳😳 nikasema hii ndo university bwanawe!

Babahti nzuri nikakutana na bwana mmoja tuliishi mtaa mmoja, akaniuliza nasomea nini nikamjibu CBA... Akaniambia nenda paee notice board kuna ratiba na venue.. Akili ikanikaa sawa sasa..

Ni notisi pekee nizitumiazo... Kazi ikaja hapa leicturer haandiki yupo tu kama anahubiri jukwaani.. Sielewi!

Wiki ikaisha hakuna nilichoandika.. Hakuna kitu kichwani... Wenzangu wameandika samary.. Haisomeki ikaeleweka..

Siku moja tukiwa tunasoma leicturer aliniona namkodolea macho sana akajua namwelewa sana, si akaniuliza swali, nikabaki namtumbulia macho tu..

Mwisho wa kipindi nikatoka nje kinyonge, sielewi niache chuo au nifanyaje, notisi hamna..!

Yule leicturer alipotoka akaniona nimesimama nikiwaza, akaja akanipa ujanja kuitumia internet.. Asante sana mr. Kumbe kila kitu kipo mubashara katika internet...

Wiki ya pili nakumbuka tulikuwa darasani, leicturer alikuwa padri mnoja mwenye nafasi za juu pale chuoni, mwisho wa kipindi akatamka swali, wala sikulisikia nashangaa wenzangu wanaandika katika karatasi na kukusanya, nindike nini sasa?

Akaniona siandiki akaja, weweeee mbona huandiki,nikamjibu sikuwa nimelisikia swali.

"wewe ni kiziwi"aliuliza kwa sauti kubwa.

"ndiyo" nilimjibu.

"sasa hapa umekuja kuolewa au? " akauliza

Watu waliangua vicheko, kisha akanitaka nimfuate ofisini, mja kwa moja akanipeleka kwa pincipal...... Alitaka nifukuzwe nilimtazama tu.

Principal akaniambia niende tu niendelee na masomo, padiri yule alichukia sana.

Maisha ya chuoni yakawa machungu kuliko katika ngazi zote nilizopitia.

Leicture ilibeba zaidi ya wanachuo 500, halafu leicturel anasema "mtazame huyu kiziwi anasomea usimamizi wa biashara, atamwajiri nan? " nilitamani ardhi ifunguke nipotee.

Maneno kama haya yakawa yanazungumzwa mno kiasi kwamba kila tuwapo leicture nilikuwa na hofu nikiwaza leo nitatupiwa dongo gani!.. Leicturer hawakuniheshimu.
Unaweza tafakari ni kiasi gani niliishi maisha yasiyoridhisha... Chuo kinajumuisha watu wengi sana, watu wazima.. Kutendewa kama mtoto iliniumiza sana.

Nilikonda mno mwaka ule wa kwanza, nilipomaliza certificate tuuuu... Nikawafata wazazi wangu..

"mama na baba kwa kweli mim maisha ya kusoma naishia hapa..." niliongea kwa uchungu sana na machozi yalinitoka.

Kmbukumbu za kutendewa isivyo chuoni zilinitia uchungu sana, nilitamani mno ningelibaki na masikio yangu, lakini haikuwezeka.

Hakuna aliyekuwa tayari kunielewa, hawakujua uchungu niliokuwa nao moyoni mwangu.

Nilichoamua ni kununua pakti ya sumu ya panya, nilimeza pakti ile, nilihitaji kupumzika, nilihitaji kujaribu kuishi kwingine.

Nilipoteza fahamu na kukaa miezi miwili hospitali, niligoma kunywa dawa, nilihitaji kupumzika.

Nyakati fulani wagonjwa walifariki pale wodini, nilitamani ningekua mimi.

Dunia hii ilinihitaji zaidi, nilipona, nilijitahidi kujiweka mbali na wanadamu ili kuitafuta furaha, binadamu hakuwa na upendo nami tena,

Nilijaribu kunywa panadol 12 bado nilipona, kwanini nipone Mungu hujaona maisha dhalili ninayoishi?

Kila kitu kilikuwa kimeharibika kwa sasa, ilikuwa ni lazima nianze upya, hatimaye nikasema yess, nitarudi chuo.

Mwaka 2016 nikatuma maombi katika mfumo wa udahili wa serikali kwa kada ya elimu, nikachaguliwa chuo binafsi St. Benard TTC Singida.

Maisha ya hapa hayakuwa na tofauti sana na maisha yaliyopita lakini ilinipasa kuwa mvumilivu.

Maneno ya "huyu mwalimu atafundishaje? " "huyu nae kaacha kusome ufundi cherehani kaja huku" hata hivyo hawakuwa na jipya, nilikwishakuyazoea hayo.

Mwishoni mwa mwaka wangu wa kwanza pale chuoni, familia yngu ilinifahamisha kuwa nyumbani kuna matatizo, baba kafukuzwa kazi....

Kwa maana hiyo rudi nyumbani tu.,,, hili sikukubaliana nalo, nilipenda kuwa mwalimu.

Kwa babati nzuri ada ya mwaka wa kwanza nilikwishakuilipa, nitafanya nini mwaka wa pili??

*****************

Nilikuwa na laptop ambayo niliiegemea kwa ajili ya kutafuta na kuhifadhi notes, ilinilaziku kuiuza, pia niliuza baadhi ya mali za nyumbani hatimaye nilipata laki sita.

Nililipa ada tshs laki 5 salio la deni lilikuwa 1. 1 milioni hii nitaipata wapi,siufanikiwa kuipata na mambo yalipozidi kuwa mabaya sikuwa na jinsi zaidi ya kuzungumza na uongozi wa chuo. Hatimaye nikafanikiwa kumaliza chuo.

Wakati wa kuingia mtaani kufanya vibarua ili nipate ada iliyosalia nikomboe vyeti vyangu.

Niliwasili mtwara sasa, hali niliyokuta nyumbani haikuwa nzuri, haikuwa nyumba kubwa nzuri tena bali lilikuwa pagala, mapazia ndio pekee yaliyokuwa dirishani, haikuwa na milango hii ililazimu kuezeka tu bati.

Maisha yalikuwa mapya, kula mlo mmoja ama kukaa hata siku mbili bila kula, ilichosha lakini ndiyo yalikuwa maisha etu... Nilisikitika sana.

Mda wa kuingia mtaani kupambana ulikuwa ni huu sasa.

Lakini mambo yalikuwa na matarajio tofauti, kwani vibarua vilihitaji kuwa na mtu wa kati, kwa kuzingatia ugeni wa eneo hili ugumu ukajitokeza wazi wazi.

Shida nyingine ikaibuka, mtazamo wa jamii, kwani nilipohitaji kazi kutokana na umbile dogo. Nilionewa huruma!, lakini mbona wapo wenye miili midogo zaidi yangu? Jbu ni kwamba sikuwa nasikia vizuri.

baada ya kwenda huku na ule bila mafanikio ya kupata vibarua, niliigeukia taaluma yangu.

Nikaandaa barua za maombi ya nafasi ya kujitolea katika shule binafsi.

Hawakuwa na imani nilijikuta nikimaliza shule zote binafsi, lakini hakukuwa na manufaa kwaninilikayaliwa na nafasi kupewa wengine.

Hali hij haikunikatisha tamaa, nilikuwa imara, niliaza kutafuta kazi katika hoteli na hospitali binafsi, kazi za usafi na utunzaji mazingira.

Nilizunguka kwa miezi kadhaa bila ya mafanikio, ilinipasa kuwa mchaguzi wa ajira niombazo, linipasa kuomba ile tu iliyo ndani ya uwezi wangu.

Hivyo sikuwa na wigo mpana katika kutafuta fursa hizi za ajira.

Kuna wakati niliandika barua katika shule moja ya kanisa katoliki, nikaitwa kwenda lakini walipobaini changamoto ya masikio walinikatalia, nilichoka!

Nikatafakari na kujisemea kumbe kupambana kwenyewe ndo huku!

Nakumbuka ilikuwa ni mwezi hivi tangu nijiunge JamiiForums, nikaandaa mradi wa kuchoma vitafunwa na mtaji ukawa 100,000.

Sina mtaji na ajira bado ni kizungumkuti, nitajaribu jamiiforum.

Matokeo yake hayakuwa mazuri kwaninlishambuliwa kwa maneno mengi, niliumia sana na nilijutia sana uamuzi wangu wa kuomba mtaji katika JamiiForums.

Nakumbuka siku moja nilipokea ujumbe katia jamiiforum, wakati huu nilikuwa njitolea katika shule ya serikali.

Akaniambia, yupo tayari kunipa msaada wa mtaji hadi shilingi laki tano, kwa sharti moja kwamba nimfuate kituo kikuu cha polisi mtwara na niulizie Afande Tall!

Siku iliyofuata nikiwa na furaha, baada ya kipindi changu cha asubuhi nkatoka kwenda kituo kikuu cha polisi baada ya kuulizia walishindwa kumtambua.

Nikamtumia ujumbe kuwa nipo kituoni(jamiiforum) akaniambia yeye yupo tayari kunitumia mtaji ama kuniajiri katika biashara zake endapo tu, nitaikopy thread niliyoandika jamiiforum, kama ilivyo kisha niipost katika ukuras wangu wa facebook na akiuona tu atanpatia ofa y mtaji au kazi.

Lilikuwa ni sharti gumu sana, facebook ni mahali ambapo hata wadogo zetu, jirani zetu, walimu wetu na wengine wengi, je itakuwa vipi wakiona post hii....

Haiyumkin hali mbaya ya famlia yangu, kukosa ajira na kipato chochote, nilihitaji mno mtaji au ajira ile kuliko kitu chochote.

Maamuzi niliyogikia yalikuwa ni kupost ujumbe wa thread ile, kwa kuukopy kama ulivyo na kuuweka katika facebook.

Unaweza kufikiria nilikuwa katika wakati mgumu kiasi gani? Na unajua ni nini kilichotokea?

Ujumbe ule ulisomwa na kila aliyenifahamu lakini ulikuwa na likes 13 pekee na coment sita za pole.

Idadi hiyo likuwa baada ya siku tatu, ilishangaza sana kwani picha yangu au post yoyote ilichukua masaa matatu hivi kufikisha mamia ya likes na coment.

Bwana yule baada ya hapo akaniblock katika whatsap, niliumia sana na kutazama nilivyojivua nguo, nilufuta ujumbe ule na sijajua lengo la bwana yule, hakunitendea uungwana.

Basi sikuwa na la kufanya zaidi ya kuendelea kujitolea shuleni pale, sikuwa na furaha, ilinilazimu kutembea masaa mawili kwenda shuleni, sikumudu nauli shilngi 400.

Kadhaika niliendelea kutafuta ajira hapa na pale bila mafanikio.

Ndugu zangu hawakunipenda tena, kwani waliniita mzigo, niliumizwa na hili kwani ilinikumbusha upendo wao mwingi sana kwangu kipindi kile ningali na usikivu, vipi leo waniite mzigo?

Familia yangu nayo ilianza kunichoka kwani sikuwa na msaada wowote licha ya hali ngumu ya nyumbani hapa.

Sikuwa na cha kujitetea, ni kijana mkubwa wa kiume, umri wangu pia ulinipasa kuwa na mchango, nilijaribu lakini bado sikufanikiwa.

Ilinipasa kujaribu kila nilichoweza kukifanya, wakati huu niliamua kwenda kijiwe cha bajaji na bodaboda, nilitengeneza urafiki kwa miez kadhaa.

Kisha nikamwomba mmojawapo anifundishe bajaji, waliposikia walicheka na kebehi, bado niliendelea kujaribu lakini sikupata ushirikiano.

Baada ya kushindikana, sasa niliwaza nawezaje pata cheti changu ili nikitumie kuomba ajira hususani ajir za serikali.

Nikamfuata afisa elimu ambae ananifahamu kwani alikuwa anakujakuja pale shuleni na anajua changamoto ya usafiri.

Nikamweleza hali ya kwetu, changamoto ya usafiri, hali ya cheti changu kushikiliwa na chuo,hivyo nikamuomba aangalie anavyoweza kunisaidia kwanafas yake. Akasema sawa nisubiri.

Nikarudi kuendelea na majukumu kule shuleni, wiki hatimaye mwezi nikaenda kwa afisa kuuliza suala langu, hakunikaribisha vizuri kwan nilimkuta mapokezi na watu wakiwa wengi tu ikabidi tuongee hapohapo

akaniambia ana kazi nyingi mmi nikasubirie tu na akanikataza kwenda ofisini kwake.

Ukapita mwezi nikamsms afisa hakujibu, nikamtumia dadaangu kumpigia hpokei simu basi nikaachana nae.

Mamaangu akaanza kuumwa umwa ikabidi niache kujitolea na kulima mihogo wa ajili ya chakula baba hana kazi uzunguka hapa na pale akirud ma miatano sawa, buku sawa,

Baada ya hali ya mama kutengamaa, nikakumbuka katika thread flani kna mtu alinishauli kwenda kwa Dc au Rc, nikaenda kwa dc

nikajieleza akasema nisubiri kisha niende tena, nikaenda akasema ataniandikia barua ya kuchangisha hela, but mwezi ushaisha hajaniandikia na amehamishwa

Now nikienda kule ofisini hawanipi ushirkiano mzuri, mara hayupo wakat gar yake ipo nje, seem DC mpya anafahamu shida yangu ila kapuuzia ndio maana hata wao hawatoi ushirikiano.

But nilirudi tena nkaambiwa ataniandikia barua ya kuchangisha hadi leo ni kimya nikaachana nao.

Nikanza kuwalisha vizuri kuku watatu mitetea waliokuwepo nymban kwa kuwapa chakula cha ziada na hatimaye wakaanza kutaga

Walitaga mayai 10+ kila mmoja nikawawekea mayai 10 kila mmja wakatotoa nikapata vfaranga 25, nikawajengea mahali kwa mabox chumban kwangu, nikawapa dawa za asili.

Wiki tatu tu nikaishiwa akiba ya chakula na sina hata elfu 2 ya pumba na mkaa kwan niliwawekea chombo cha joto, japo ni chumban but hakina madirisha zaidi ya mapazia tu, pia mlango huegesha bati na hakna dari hivyo sikyoa hatari kuchoma mkaa chumba cha kulala

Vifaranga wakaanza kufa wakafa 4 nikaaaume njaa kwan niliwapa makombo machicha ya nazi na uchafuuchafu, nikaamua kuwarudishia wale kuku vifarangavyao, bahati mbaya hakuna aliyesurvive wakafa na wengine wakaliwa na paka.

******************

Lakini sasa hapa ndipo nilipo sasa, miaka 20 ya kuishi katika kivuli cha huzuni na masumbuko ya moyo.

Miaka 20 ya kujaribu kupigania furaha, miaka 20 isiyo na matumaini. Naumia sana.

Chanzo cha yote ni usikivu hafifu, haikuwa bahati mbaya, kwa waamini tutasema mapenzi ya Mungu.

Siku zote inasemwa ya kwamba Mungu hawezi kumpa binadamu jaribu asiloweza kulishinda.

Lakini jaribu gani hili? Kwa sababu ya jaribu hili nimepoteza kila kitu maisani mwangu. Kila kitu kimfaacho binadamu kuishi maisha ya kawaida.

Kwa sababu ya hili nimepoteza marafiki, nimepoteza kujamiiana (socialization)

Kwa sababu hili nimekosa afya njema kwa kusumbuliwa na msongo wa mawazo na nykati zote nilizojaribu kuondo uhai wangu, nimepata maumivu makali ya mwill nikiwa katika jitihada za kupumzika upande wa pili.

Kwa sababu ya hili naishi katika maisha ya upweke uliokithiri.

Kwasababu ya hili msamiati wangu ni mbaya ikumbukwe masikio na mdomo vina uhusiano

Kwa sababu hii hupata kizunguzungu hususani wakati wa usiku.

Kwa sababu hii sina uwezo wa kusikiliza neno la mungu, hali inayodhoofisha imani.

Kwa sababu ya hili siwezi kuburudika kwa muziki, kupata habari.

Kwa sababu ya hili siwezi kufanya kazi nilizotmani kuzifanya kabla.

Kwa sababu ya hili naishi maisha dhalili sana maisha ya dharau za kiwango cha juu.

Karibu kila kitu umeondoka nacho wewe, umeniachia uchungu na maumivu mengi sana.

Moyo wangu unauma sana na nakulaumu wewe Mungu wangu nakulaumu sana kwa kweli.

Mzigo mzito uliomtwisha mja wako ni mzito sana. Mzito sana bwana moyo wangu unaumia.

Machozi yangu yana maana kubwa sana bwana, yamebeba maumivu mengi sana, mpaka lini bwana?

Ee Mungu kama ulivyonigusa nikapoteza kila kitu, niguse tena bwana, Roho yangu inahangaika.

*******************

MWISHO
 
Ooohhhhhhpss pole sana mkuu daah!

Wale wote walio kuwa wamekudhihaki na kuku kashifu humu baada ya kuanzisha uzi wa kuomba msaada

Sijui watajisikiaje baada ya kuusoma huu uzi ''Bila Shaka watafurahi maana mijitu katili huwa haina hata chembe chembe za huruma. Huyo aliye kuambia u-post thread yako. Nature imlaani tena alaanike haswaa period.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom