don-oba
JF-Expert Member
- Dec 8, 2011
- 1,387
- 677
Tangu jana nilielezea kwamba nimepata taarifa kuvuja kwa hukumu ya mh Lema. Mods aliunganisha link yangu na nyingine zilizokuwa zinashabihana na hilo. Kitaaluma mimi ni mwanasheria na hakika kila mwenye taaluma hii na aliyekuwa akifuatilia kesi atabaki mdomo wazi juu ya hukumu iliyotolewa. Huyu jaji alichofanya ni kucheza na akili za watu, na nina uhakika alikua na hukumu mbili mkononi.
Hata mwanafunzi wa sheria mwaka wa kwanza anajua kwamba katika 'tort' ili kosa lionekane limetendwa ni lazima aliyetuhumiwa athibitishe ameathirikaje na hizo tuhuma. Inakuwaje 3rd party ndo athibitishe hilo?
Batlida hajawahi kuja mahakamani. Kesi hii inaandika historia katika mhimili wa mahakama juu ya uhuru wake. Kuna haja ya majaji katika mahakama kuu kufanyiwa enterview kama kule kenya wanavyofanya. Hii hukumu imenikumbusha mengi katika tasnia ya sheria, daima itabaki kuwa kumbukumbu mbovu kwenye mhimili wa mahakama.