Hongera CHADEMA, Tumekubali mmeshinda! Timizeni AHADI zenu!

Mzee naamini unachekea chini, maana mpinzani wako mkubwa EL kabwagwa, any way ndo demokrasia yenyewe, ila naomba wewe na chama chako mjifunze kukubali matokeo kwa haraka na sio kusumbua vijana kulinda kura usiku kucha, kisa tu ninyi ni wagumu wa kukubali kushindwa, naomba mfikishie mwenyekiti wako haya mawazo yangu, vurugu mnasababisha wenyewe mzee.
 
hongera kwa kuukubali ushindi la kujiuliza kwa nini chama kinazidi kuporomoka????????????????

Acha kuwashtua. Waache waendelee kulala miaka 50 wameshindwa kuleta tofauti. Sasa tumeamua kuwakata jumla hakuna kubipu. Vijana la muhimu ni kuzitumia shahada zetu kama huna wakati wa kujiandikisha hakikisha unapata shahada hio ambayo ndio silaha ya kuyaondoa haya mazee kama wasira na wenzake. pipooo!!
 
Wewe dogo unapotea!!yaani ulisimama jukwaa 1 na mtuhumiwa ufisadi arumeru!!mkambeba Sioi ambae tulimkataa mapema! 2015.
 
napeeee! PEOPLESSSSSSSSSSSSS...................... JIBU BASI, NTARUDI BADAE NIKUTE UMEJIBU HY SALAMU
 
nnauye umeonesha ukomavu but you are running short of something. Japo cdm wameshinda chaguzi hizi kama wawakilishi wa wananchi nina imani watakuwa sauti ya wananchi na wataipaza sana na kwa nguvu zao zote. Kwa kuwa chaguzi hizi haziwapatii cdm authority ya kukusanya kodi na kuitumia ni dhahiri kuwa the burden of proof kuhusu ubora wa maisha ya watanzania popote walipo bila ya kujali wanawakilishwa na chama gani cha siasa yapo kwenye chama chenye dhamana ya kukusanya kodi ya wananchi na kuitumia kwa manufaa ya wananchi wote (ccm).

Ulichotakiuwa kuongezea ndugu nnauye ni kusema 'kwa kuwa chama chako cha ccm ndicho kinaunda serikali yenye dhamana ya kutoza watanzania kodi na kuitumia kwa manufaa yao kitafanya kazi kwa karibu na wawakilishi wote wa wananchi bila kujali wanatoka vyama gani kwa faida ya taifa na wananchi kwa ujumla', kukaa kimya kuna maana kuwa ccm inakubaliana na matamshi ya waziri nagu kuwa wakichagua wapinzani watahujumiwa kwa kucheleweshewa maendeleo na serikali ya ccm. Huko ni kuvunja katiba na kiapo kuwa rais ataitumikia nchi na watu wote bila kujali itikadi zao.

Ccm itakuwa salama kama ndani ya utawala wake wananchi watapata maendeleo bila ya kujali walimchagua nani kuwa mwakilishi wao. Mkihujumu majimbo yanayowakilishwa na vyama vingine mtakuwa mmeihujumu tanzania as a country na hamtakuwa na legitimacy ya kuongoza baada ya 2015.

word !
 
Wewe dogo unapotea!!yaani ulisimama jukwaa 1 na mtuhumiwa ufisadi arumeru!!mkambeba Sioi ambae tulimkataa mapema! 2015.
 
Umefunguka vizuri saana! Keep on touch kwan hizi ni siasa tu! Hongereeeni saaana Makamanda wa Chadema kwa kazi nzuri.
 
Nape hapa kwenye Jamii Forum Wiki Tatu zilizopita alikuwa anatuambia Ubunge ni wa CCM Arumeru

Kijana Wake Mchemba hata hapatinani maeneo yoyote hii ndio Siasa ya kushidwa ya CCM?
 
Chama Cha Mapinduzi, kimeyapokea matokeo ya kura zilizopigwa na kutangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa chaguzi ndogo zote, ule wa Arumeru Mashariki na zile za kata nane zilizofanyika jana nchini kwenye maeneo husika.

Kwa heshima nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati watani zetu, CHADEMA kwa ushindi walioupata Arumeru Mashariki na kwenye kata tatu(Kirumba, Kiwira na Lizabon). Lakini pia nawapongeza CUF kwa kushinda ile kata ya Tanga. Katika kata nane zilizokuwa zikifanya uchaguzi CCM tumeshinda kata nne. Tunawashukuru wananchi kule walikoendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kata hizo nne. TUNAWAAHIDI KUWATUMIKIENI KWA MOYO WOTE.

Matokeo ya kura hizi kwa ujumla yameonyesha sauti ya wapiga kura kwenye maeneo husika, ndo maana tunaheshimu maamuzi yao. Tunatoa wito kwa vyama vilivyoshinda kwenye maeneo hayo kuhakikisha vinatumia muda na dhamana waliyopewa kutekeleza yale waliyowaahidi wapiga kura wao.

CCM tutatumia matokeo haya kufanya tathimini ya kina na kuangalia wapi tuliteleza ili tufanye marekebisho kuhakikisha makosa hayarudiwi tena. Kimsingi uchaguzi huu umeisha na tufunge mjadala wa uchaguzi tujikite katika kuwaletea maendeleo wale waliotuchagua.

Nawatakieni kila lakheri wote mliochaguliwa, nawatakieni utumishi uliotukakuka!

mission ni kuizika ccm. wakitekeleza, wasipotekeleza (kwa sababu kama alizotoa yule mama 'anayeitwa' dokta mary nagu, kwamba wakichagua chadema watacheleweshewa maendeleo) sisi wengine tushajiapiza kama wapemba walivojiapiza kwa CUF. shida, raha, mimi ni chadema mpaka kifo!
 
Kaka Nape nafikiri mkikubali kwa dhati kwamba mna washindani mnaweza sasa kuamka na kufanya kazi, lakini kwa sasa CCM haina matumaini kabisa ni chama ambacho hakina mwelekeo inasikitisha hata sisi wapenzi wake tunakuwa muda mwingi tunasononeka, kujivua gamba imekuwa ngumu, mafisadi ndiyo hao wanatamba, ahadi hazitekelezeki, hivi sasa kila waziri anajifanyia anavyotaka utadhani rais hayupo, kwa kweli mtakapofanya uchaguzi ondoeni mazee yote anza na kina Wasira, sijui Sitta, na wengine hawana tena mvuto. Pia kuwe na uwajibikaji wa viongozi kwenye majukumu waliyopewa siyo maneno mengi vitendo hakuna.
 
Chama Cha Mapinduzi, kimeyapokea matokeo ya kura zilizopigwa na kutangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa chaguzi ndogo zote, ule wa Arumeru Mashariki na zile za kata nane zilizofanyika jana nchini kwenye maeneo husika.

Kwa heshima nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati watani zetu, CHADEMA kwa ushindi walioupata Arumeru Mashariki na kwenye kata tatu(Kirumba, Kiwira na Lizabon). Lakini pia nawapongeza CUF kwa kushinda ile kata ya Tanga. Katika kata nane zilizokuwa zikifanya uchaguzi CCM tumeshinda kata nne. Tunawashukuru wananchi kule walikoendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kata hizo nne. TUNAWAAHIDI KUWATUMIKIENI KWA MOYO WOTE.

Matokeo ya kura hizi kwa ujumla yameonyesha sauti ya wapiga kura kwenye maeneo husika, ndo maana tunaheshimu maamuzi yao.
Tunatoa wito kwa vyama vilivyoshinda kwenye maeneo hayo kuhakikisha vinatumia muda na dhamana waliyopewa kutekeleza yale waliyowaahidi wapiga kura wao.

CCM tutatumia matokeo haya kufanya tathimini ya kina na kuangalia wapi tuliteleza ili tufanye marekebisho kuhakikisha makosa hayarudiwi tena. Kimsingi uchaguzi huu umeisha na tufunge mjadala wa uchaguzi tujikite katika kuwaletea maendeleo wale waliotuchagua.

Nawatakieni kila lakheri wote mliochaguliwa, nawatakieni utumishi uliotukakuka!

Ushauri huu mngeutumia pia kwenye chama chenu nchi hii isingekuwa hapa ilipo kama kuku aliyekatwa kichwa (headless). Unaonyesha kama unautoa kwa masimango...the writings are on the wall for everyone even a 'fool' to see.
 
ongera Nnape kwa kuliona hilo,but nijuacho mimi ccm hamuwezi kubadilika maana mnatumia watu ambao tumewachoka hawakitangazi chama wala sera za chama, pia na ninyi viongozi wa juu ni waongo wa kutupwa hivyo hapa tumeanza kuwamega taratibu na mwisho mtabaki kama meno kitika cha kikongwe mwenye miaka 125. So tathimini haina maana anzisheni chama kipya tu kile chako cha CCJ sema wewe na CCJ wenzio mmekuwa waongo sana nacho mkikileta mtaparanganyika tuuu! PEEEEEEEEEEEEEEOOOOOOOOOOOOOPLEEEEEESSSSSSSSSSSSSSSSS P O W E R ! ! ! ! !
 
Huyu Nape analeta utani kwenye kazi??? Hivi anatakakusema wanapochakachua matokeo na kundinda ni utani ama?? Watu wako serious na nchi yeye anasema utani?? On top of it kuna watu bado wanamsifia!!!! Kama Watanzania tutaendelea na huu ujinga wa kugeuza siasa kama mpira wa Simba na Yanga then tusahau mabadiliko na maendeleo kwa kizazi hiki!!!
 
democracy at work!
CCM mnanishangaza sana na zile sera zenu za "Msipomchagua mgombea wetu, msitegemee kabisa huyo wa upinzani kupata ushirikiano kutoka Serikalini".
Hii ni kauli ya kitumwa,kibabe na kidikteta na wala sio demokrasia hata kidogo,tena inakiuka misingi ya uwepo wa vyama vingi!
Hawajafahamu jinsi wananchi wanavyoilewa vibaya hiyo kauli. Na ndiyo itawamaliza! Kuna mikoa iliachana nao ikafanyiwa roho mbaya. Walitumwa makachero kuhakikisha hata mzunguko wa fedha za miradi unasitishwa lakini wananchi hawajatikisika, wamo tuuu! Tena ndiyo wanazidi kusonga mbele maana hawaitegemei serikali tena. Badala yake wanaichukia serikali. Na huko viongozi hawaendi endi ovyo kama wanavyotembelea sehemu fulani na machine gun mfukoni. Na kwahiyo wananchi hawawaogopi "and they have taken ownership of the development projects".
Sasa naona inasambaa mikoa kibao. Mwisho wa mwanzo wa kuanguka kwa CCM umekamilika Arumeru!
Mungu ibariki Tanzania iondoke kwenye ujinga wa kuongozwa kibabe-babe, kihuni-huni, kichawi-chawi, kiuwaji-uwaji, kijinga-jinga na kifisadi-fisadi.
 
Chama Cha Mapinduzi, kimeyapokea matokeo ya kura zilizopigwa na kutangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa chaguzi ndogo zote, ule wa Arumeru Mashariki na zile za kata nane zilizofanyika jana nchini kwenye maeneo husika.

Kwa heshima nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati watani zetu, CHADEMA kwa ushindi walioupata Arumeru Mashariki na kwenye kata tatu(Kirumba, Kiwira na Lizabon). Lakini pia nawapongeza CUF kwa kushinda ile kata ya Tanga. Katika kata nane zilizokuwa zikifanya uchaguzi CCM tumeshinda kata nne. Tunawashukuru wananchi kule walikoendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kata hizo nne. TUNAWAAHIDI KUWATUMIKIENI KWA MOYO WOTE.

Matokeo ya kura hizi kwa ujumla yameonyesha sauti ya wapiga kura kwenye maeneo husika, ndo maana tunaheshimu maamuzi yao. Tunatoa wito kwa vyama vilivyoshinda kwenye maeneo hayo kuhakikisha vinatumia muda na dhamana waliyopewa kutekeleza yale waliyowaahidi wapiga kura wao.

CCM tutatumia matokeo haya kufanya tathimini ya kina na kuangalia wapi tuliteleza ili tufanye marekebisho kuhakikisha makosa hayarudiwi tena. Kimsingi uchaguzi huu umeisha na tufunge mjadala wa uchaguzi tujikite katika kuwaletea maendeleo wale waliotuchagua.

Nawatakieni kila lakheri wote mliochaguliwa, nawatakieni utumishi uliotukakuka!

Haleluiah! Praise be to God.

This is how my dream country looks like.

Asante Nape
 
Mimvi,ooh!nipo fiti kwa mapambano!apambane na nani?labda wewe Nape na 6 lakini sio NGUVU YA UMMA aka cdm.mkwewe sioi vp?
 
Back
Top Bottom