Hongera CHADEMA, Tumekubali mmeshinda! Timizeni AHADI zenu!

Actually he's trying to paint a scenario that doesn't Exist ! CCM kweli hizi bakora chache hivi zimewarudisha kwenye line? na bado watakiona cha mtema kuni.............!

Sasa twendeni kwenye zile kata zetu Arusha!
 
Mkuu Nape,
Kama wapiga kampeni wenyewe ndo kina Lusinde, nachelea kukwambia kuwa hata mgombea wa ccm akiwekwa na kivuli watu watakipigia kivuli!! Ila leo nimeikubali post yako keep it up.
 
Nakupongeza na mimi kwa kukubali matokeo lakini umekubali kwa dhati au kwa maneno tu?kama ni kutoka moyono hongera sana,ushauri wangu kwako hama chama hiki CCM hakikufai wewe kama kijana!chama kimezeeka na fikra zake ni za mika 50 iliyopita.
 
Tumepokea shukurani zako iwapo unatanguliza kutimiza ahadi jua kabisa kwamba kati ya watu wanaotimiza ahadi ni CHADEMA ninyi mlishakuwa waongo jamii inajua hivo
 
Nifuraha ya watanzania kwamba sasa haki na Nguvu ya umma inajidhirisha hata kwenye mipango mikubwa ya dhuluma, ccm ni watu waliolewa madaraka na wanafikiri walizaliwa kuitawala hii nchi milele, nasema huu ni mwanzo tu; subiri pale tume itakapo fanyia marekebisho daftari la wapiga kura, yaani pale wafu watakapotolewa kwenye daftari hilo na wale wenye umri wa kupiga kura hasa vijana watakapo ingizwa, hiyo ndiyo itakuwa kifo kwa ccm, Mungu atupe uhai 2015 sio mbali na uhuru kamili wa nchi hii tutaushuhudia.

(Igunga Pia Chadema Ilishinda)
 
Mie bado sijaelewa anaposema nyie ni watani wao. Huu utani umeanza lini? Maana huko nyuma alikuwa wanawaita Chandimu mara ghafla bin vuu sasa mmekuwa watani. Kawapandisha daraja kutoka Chandimu mpaka watani kwa uchaguzi mmoja tuu?

Na hao mnaowaita magamba mlianza lini?
 
Ndg.Nape,

Hongera pia kwa kata mlizoshinda.Tunaomba ustaarabu huu wa kukubali kushindwa muendelee nao hadi 2015.Uchaguzi umekwisha tujenge nchi yetu.Ningependa kuwashauri msije mkaingia mtegoni kwa kutafuatana wachawi.Jitahidini kuishinikiza pia serikali yachama chenu kutekeleza ahadi za uchaguzi uliopita wa mwaka 2010.Katika utekelezaji wa ahadi za uchaguzi,CCM ni mfano mbaya kwa vyama vingine na mmekosa moral authority ya kuhimiza vyama vingine katika utekelezaji wa ahadi

Ben,

Umeiweka vizuri sana hii, lakini langu moja tu la kuongezea.

Hapo kwenye red, Mifano hai ipo mingi kuthibitisha kwamba magamba huwa hawakubali katu kushindwa. Hata hii ya Arumeru si kwamba wamekubali kushindwa bali mara nyingi maeneo mbalimbali wamekuwa wakishindwa lakini hawakubali kwamba wameshindwa.

Kilichotokea kwa Arumeru ni kwamba njia zao zote za kuchakachua ushindi wetu ziligonga ukuta. Wamehamishia benki kuu pale arumeru, watu wamekula fedha lakini kura wamempigia mgombea makini. Wamejaribu kuitumia NEC na vyombo vya dola kuwaumiza watu wetu, watu wametekwa, wameteswa, wameporwa mali zao lakini bado chama chetu hakikuwatupa mkono, kikasimama nao bega kwa bega hadi leo hii tumepata ushindi mnene.

Aanachofanya hapa Nape ni kukubali kwamba safari hii Arumeru palikuwa pagumu wao kujipatia pointi za mezani, wamebanwa kona zote hadi wameingia uwanjani, game limepigwa na baada ya dakika tisini kukamilika, Trasias Kagenzi anapuliza kipenga score board inasomeka 3-0!!
 
Na bado, lazima muanze kutafuta pa kutokea, ua msiombee kuwe na uchaguzi mwingine
 
Its nape again behind the scene,...............NAPE BHANA...CHEZEA CHADEMA WEYE.
 
Chama Cha Mapinduzi, kimeyapokea matokeo ya kura zilizopigwa na kutangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa chaguzi ndogo zote, ule wa Arumeru Mashariki na zile za kata nane zilizofanyika jana nchini kwenye maeneo husika.

Kwa heshima nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati watani zetu, CHADEMA kwa ushindi walioupata Arumeru Mashariki na kwenye kata tatu(Kirumba, Kiwira na Lizabon). Lakini pia nawapongeza CUF kwa kushinda ile kata ya Tanga. Katika kata nane zilizokuwa zikifanya uchaguzi CCM tumeshinda kata nne. Tunawashukuru wananchi kule walikoendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kata hizo nne. TUNAWAAHIDI KUWATUMIKIENI KWA MOYO WOTE.

Nakupongeza kwa kukubali kushindwa, lakini hiyo peke yake haitoshi nakushauri sasa ukae chini na wenzako mtafute mchawi wenu, nawashaurini muachane na propaganda za hatari kama vile Chadema ni cha kidini, Chadema ni cha kikabila, hizi propaganda haziwasaidii sana sana zinalitumbukiza taifa kwenye migogoro ambayo inaweza kuchukua karne kuisuruhisha.

Napenda kutoa wito wangu wewe kama msemaji wa chama muanze kusahihisha propaganda zote za uongo kwa kuwaambia watanzania kuwa mliposema Chadema ni chama cha kidini mlitaka tu mpate kura za waislamu na hamkumaanisha mliyoyasema na mjikite kushughulikia matatizo ndani ya chama chenu, hata kama hii itawapotezea wapenzi lakini ni bora ukweli mchungu kuliko uongo unaofurahisha.
 
ng'wilage unyanda ng'wana nnauye alekeituja!

Yeeeeeeeh hambo hambo agichene kale na afadhali ya ng'wa Nauye,neyo eyeccm ya minu getena soni,koleka mafisadi, bagho esoma meli mjizungu mmo ighetanwa ship ale ng'ondi ikabiza khee mjizungu!!!!
 
hapo kwenye red sijui kama ni mimi nimekosea kusoma au ilikuwa typing error!! (siamini kama ni frustration...lol)

Ahsante Kaka Nnape, tunashukuru kwa salamu zako. tafakarini, jipimeni, mchukue hatua........ Kila la heri
Kuna mtu mmoja alikuwa akishukuru kwa kuteuliwa akayatumia hayo maneno, "Nitakupeni utumishi uliotukuka" lakini baadaye ikaonekana kana kwamba hatoi utumishi uliotukuka akalazimishwa kujiuzulu. Nnape bwana kaazi kwelikweli!
 
Chama Cha Mapinduzi, kimeyapokea matokeo ya kura zilizopigwa na kutangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa chaguzi ndogo zote, ule wa Arumeru Mashariki na zile za kata nane zilizofanyika jana nchini kwenye maeneo husika.
Shukran sana kwa maelezo yako yalokwenda shule.... japokuwa moja tu, hiyo Tathimini ya nini wakati unazijua sababu na ziko wazi..Labda nikwambie kubwa kuliko yote ni kushindwa kutekeleza yale mlo waahidi wananchi - Mmeshindwa kujivua magamba!
 
Nakushukuru kwa kukubali kushindwa hata kama moyo unauma na kwamba harakati za kuchakachua ziligonga ukuta. Ukweli ni kwamba nchi hii chini ya utawala wa CCM imeendelea kuwa shamba la bibi. Angalia mikataba ya madini, uuzaji wa nyumba za serikali, kashfa zisizo na idadi (EPA, Meremeta, Tangold, Uwindaji, Uuzaji wa NBC, ardhi Arumeru, uuzaji wa mashirika mabalimbali ya umma-UDA, Tanganyika Packers, mashamba ya mkonge, mashamba ya mpunga ya Mbarali n.k), rushwa sehemu mbalimbali za utoaji wa huduma n.k. Kiufupi kila Mtanzania mwenye ufahamu amechoshwa na haya mambo.

Hakuna utani katika harakati za kuleta maendeleo ya nchi hii yenye maziwa na asali za kuwafanya Watanzania waweze kuonja utamu wa kuwa Watanzania kama kutakuwa na utawala bora na madhubuti. Hii ni changamoto ambayo haiitaji utani hata kidogo kwani tunaishi kwenye dunia yenye ushindani ambao hauna huruma kwa yule aliye legelege.
 
Huu ushindi wa CDM huko Arumeru na kwenye Kata tatu ni dalili mbaya kwa CCM.

Pamoja na CCM kutumia majembe yake yote lakini imeshindwa. Mategemeo ya CCM kwa siku za karibuni imekuwa ni maeneo ya vijijini kwa kuwa sehemu za mijini imekuwa ngome ya CDM. Lakini sasa inaonekana kwamba moto wa CDM umeanza kuenea hadi vijijini na vitongojini. Sijui 2015 CCM itakuwa katika hali gani. Na kama chaguzi ndogo zitaendelea naona CCM itaendelea kumong'onyoka na kufikia 2015 itakuwa inaanguka.

Makundi yanaimung'unya CCM na bil kushughulikiwa hakika 2015 itakuwa ni kilio na kusaga meno.

Kushindwa huku iwe ndio chachu ya CCM kujiangaloa mara mbili yasije kuyakuta ya UNIP ama KANU.
 
62 Reactions
Reply
Back
Top Bottom