Hongera CHADEMA, Tumekubali mmeshinda! Timizeni AHADI zenu!

Mi nipo ifakara kibaoni mbuge aonekani barabara kilometa 60 kutoka kidatu hadi kibaoni ni mbovu zimekuwa ahadi za kila chaguzi leo ndio unakuja kuanza kuwapelekesha wenzako! Shame on u nape
 
Wewe Nape sisi Chadema sio watani zako, Chadema hatuna utani na mtu yeyote, kumbuka Mkapa alimwambia Vicent kwamba alikua anamtania yeye Vicent akachulia serious, Vicent akamjibu sisi Chadema hatuna utani na mtu yeyote, tupo kwa ajiri ya maslahi ya nchi.
 
Mtalia sana mwaka huu, tunawasubili uchaguzi mdogo wa jimbo la Segerea ndio mtajuwa hasira tulizo nazo kwa Makongoro Mahanga kuiba kura zetu.
 
Mnataka cdm watimize ahadi kwani ccm wametimiza ngapi?
Ahadi ya cdm kwa watz ni kuakikisha magamba yanatoka madarakani...
 
kama siyo unafiki wako wa kila siku basi asante, japo najua furaha yako ni kushindwa kwa lowasa
 
Ndugu Yangu Nape!! Kushinda na Kushindwa ni Wajibu Kwenye kila Chaguzi!! Ila cha Muhimu ni Fair PLay!! Asante kwa kupongeza!!
 
Huu ushindi wa CDM huko Arumeru na kwenye Kata tatu ni dalili mbaya kwa CCM.Pamoja na CCM kutumia majembe yake yote lakini imeshindwa. Mategemeo ya CCM kwa siku za karibuni imekuwa ni maeneo ya vijijini kwa kuwa sehemu za mijini imekuwa ngome ya CDM. Lakini sasa inaonekana kwamba moto wa CDM umeanza kuenea hadi vijijini na vitongojini. Sijui 2015 CCM itakuwa katika hali gani. Na kama chaguzi ndogo zitaendelea naona CCM itaendelea kumong'onyoka na kufikia 2015 itakuwa inaanguka.

Makundi yanaimung'unya CCM na bil kushughulikiwa hakika 2015 itakuwa ni kilio na kusaga meno.

Kushindwa huku iwe ndio chachu ya CCM kujiangaloa mara mbili yasije kuyakuta ya UNIP ama KANU.

Kutumia Vibaka kukata Watu Mapanga!! What a shame is This!! Akili za Lusinde!!
 
Mwache nassary afanye kile anachokijua, na cyo umshaur ww, kwn mpk leo hii huyo mwnykit wenu hana alichofanya zaid ya kusafir. nakushaur nape huo ushaur wako mpelekee mwenyekit wako kwnz.
 
Nape napenda the way umeonesha maturity. Vipi kuhusu mbunge wenu Lusinde aliyetukana hadharani?? Naamini kwa uungwana huu utatumia jukwa hili au vyombo vya habari kumkemea aache utoto wake.
 
ila bado tuna kazi hawa ELFU 26+ ni wagonjwa au nini sasa? Elimu ya uraia inaitajika wamenisikitisha sana.
 
Nape naona umeanza kukomaa kisiasa.
Ila kosa moja ambalo umelifanya ni kuonyesha wazi kuwa umefurahia kuanguka kwa mwana CCM mwenzako kwa sababu ya makundi.

Hapa ni dhahiri kuwa Nape unashabikia kuanguka kwa Lowasa ila amini usiamini wananchi hawajui hilo wenyewe wanajua ni anguko la CCM.Kama mlifanya mjungu kumwadhibu mwenzenu (Lowasa) imekula kwenu kwani hili ndio kaburi leo na hamtakaa msimame kamwe kwani kifauatacho ni kunyosheana vidole na fitina za chini kwa chini.

Mungu ibariki Tanzania na wote wapiganaji wa kweli katika ukombozi huu wa wananchi dhidi ya utawala mbovu wa CCM.
 
Kama kweli wewe ni nape basi nimependa sana huu moyo wako wa kizalendo wa kuwapongeza wenzako...huu ni ukomavu mkubwa sana .
 
Nape;huku Kyela JK alituhaidi ahadi kubwa 2 ambazo hatuoni hata dalili kama atazitekeleza!

Meli kubwa na ya kisasa ziwa Nyasa

Barabara ya Nkuyu-Ipinda-Matema

Ni vyema mngetekeleza kwanza nyie ahadi hizi ili muwabane CHADEMA wasipotekeleza walizohaidi Arumeru
 
Sawa nape lakini una kazi kubwa ya kuwashughulikia Lusinde na Bwana Mwigulu,..itabidi uwacoach kama katibu wa chama..,kwa hali hiyo wataendelea kuangusha chama hasa lusinde
 
Nawatakieni kila lakheri wote mliochaguliwa, nawatakieni utumishi uliotukakuka!

Kwa hiyo unataka kusema hamtafungua kesi ya kupinga ushindi au ndiyo yale yale .... Maana kila jimbo analoshisha CDM mnapinga ushindi isipokuwa la mtu mmoja tu.. Anaitwa Zito kabwe?????
 
...tunakijua kilichokufurahisha Nape. Umefurahi kuwa mkwe wa Lowasa ameshindwa. Tunajua kinachokufanya ni hilo anguko la E.Lowasa. Hama Nape,njoo upande huu wa pili uungane na vijana wenzio kulikomboa taifa. Unatia huruma huko. Siku hizi nawe washona na kuzivaa kombati - japo za kijani. Utawaiga Chadema mpaka lini? Njoo uungane na vijana wenzio kina Nyerere,achana na hao vijana - midebwedo kina Lusinde.
 
Hongera sana Nape,

Kupongezana katika ushindi hasa aliyeshindwa kumpongeza aliyeshinda ni kitendo cha ustaarabu wa Hali ya juu na si kionyesha udhaifu.

Mimi ni gamba pyua na ningefurahi vile vile Mkapa, Lowassa hata JK wakatoa salaam za pongezi.

Naimagine, salaam za Nape zimepunguza sana Tension huko Arumeru na mjini Arusha.

Kukubali kushindwa ni uungwana.
 

Kwa heshima nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati
watani zetu, CHADEMA kwa ushindi walioupata Arumeru Mashariki na kwenye kata tatu(Kirumba, Kiwira na Lizabon). Lakini pia nawapongeza CUF kwa kushinda ile kata ya Tanga. Katika kata nane zilizokuwa zikifanya uchaguzi CCM tumeshinda kata nne. Tunawashukuru wananchi kule walikoendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kata hizo nne. TUNAWAAHIDI KUWATUMIKIENI KWA MOYO WOTE.

Kweli walikupa kazi bila lukwambia hali halisi ya mambo yaliyoko mbele yako. Nani alikwambia CHADEMA wanafanya utani? Ulizoziona Arumeru ni harakati mahsusi za kuhakikisha ufisadi unatafuta jengo jipya, sasa na wewe unadhania ni utani wa jadi.

Na kama CHADEMA ni watani zenu, ningefurahi kusikia CUF mnawaitaje.

Wasalaaam,
Bumpkin Billionaire!
 
Chama Cha Mapinduzi, kimeyapokea matokeo ya kura zilizopigwa na kutangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa chaguzi ndogo zote, ule wa Arumeru Mashariki na zile za kata nane zilizofanyika jana nchini kwenye maeneo husika.

Kwa heshima nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati watani zetu, CHADEMA kwa ushindi walioupata Arumeru Mashariki na kwenye kata tatu(Kirumba, Kiwira na Lizabon). Lakini pia nawapongeza CUF kwa kushinda ile kata ya Tanga. Katika kata nane zilizokuwa zikifanya uchaguzi CCM tumeshinda kata nne. Tunawashukuru wananchi kule walikoendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kata hizo nne. TUNAWAAHIDI KUWATUMIKIENI KWA MOYO WOTE.

Matokeo ya kura hizi kwa ujumla yameonyesha sauti ya wapiga kura kwenye maeneo husika, ndo maana tunaheshimu maamuzi yao. Tunatoa wito kwa vyama vilivyoshinda kwenye maeneo hayo kuhakikisha vinatumia muda na dhamana waliyopewa kutekeleza yale waliyowaahidi wapiga kura wao.

CCM tutatumia matokeo haya kufanya tathimini ya kina na kuangalia wapi tuliteleza ili tufanye marekebisho kuhakikisha makosa hayarudiwi tena. Kimsingi uchaguzi huu umeisha na tufunge mjadala wa uchaguzi tujikite katika kuwaletea maendeleo wale waliotuchagua.

Nawatakieni kila lakheri wote mliochaguliwa, nawatakieni utumishi uliotukakuka!

Hongera kwako pia Nape kwa kuwa ni ushindi kwako kwa magamba ambayo yanaisumbua CCM. Huu ni ushindi dhidi ya fisadi Papa Edward Ngoyai Lowasa.
 
Back
Top Bottom