nice 2
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 747
- 520
Zitto, Mnyika watikisa Korogwe |
Monday, 20 February 2012 07:27 |
Boniface Meena, Korogwe WABUNGE wa Chadema, Zitto Kabwe wa Kigoma Kaskazini na John Mnyika wa Ubungo, wametikisa wilayani Korogwe baada ya wananchi kuwataka wawe mstari wa mbele kupigania hasa zao la mkonge, ambalo wabunge wao wanalisaliti. Pia, wananchi hao walimtaka Zitto kuhakikisha anarudisha hoja binafsi ya kutaka zao la mkonge liwe zao la mwaka 2012 kwa sababu mbunge wao, Yusuf Nassir, amewasaliti kwa kushawishi Spika wa Bunge kuzuia hoja hiyo. Wakizungumza kwa hasira mbele ya wabunge hao wa mkutano wa hadhara, wananchi hao waliwataka wawe watetezi wao kutokana na unyanyasaji wanaopata kutoka kwa wabunge wa CCM. Walimshtaki mbunge wao kwa Zitto wakitaka akamshughulikie ipasavyo kwa kuwa, anawasaliti wananchi wa Korogwe kwa kushindwa kutetea mkonge huku akijua ndiyo kazi yao kubwa. Katibu wa Wakulima Wadogo wa Shamba la Mwelya/Usambara, Ernest Mbezi, aliwaeleza Zitto na Mnyika kuwa wanashangaa mbunge wao na wengine wa Tanga kushindwa kuwatetea katika zao la mkonge. Akijibu hoja hizo, Zitto alisema atahakikisha anawasaidia wananchi hao kutetea hoja zao ili waweze kunufaika na mkonge, ambao ni zao linalowasaidia kwa maendeleo. Tunataka kila mkulima amiliki shamba lake la mkonge na aweze kufaidika na kilimo cha zao hilo, ili maendeleo na uchumi wa Tanga uweze kukua, alisema Zitto. Kabla ya mkutano huo, wabunge hawa walitembelea shamba la mkonge Mwalya/Usambara kujionea jinsi kilimo hicho kinavyofanyika na baadhi ya wakulima walisema kama wasipopigania zao hilo uchumi waoutaendelea kudidimia. Kwa upande wake, Mnyika alisema Serikali ya CCM na wabunge wake wamekuwa wakiwadanganya wananchi kuhusu mambo mbalimbali, ikiwamo suala la zao la mkonge ambalo linahitaji kusaidiwa. Mnyika alisema hali ya Serikali ya CCM sasa ni mbaya, imefanya uchumi wa nchi kuyumba kitendo ambacho kinafanya maisha ya wananchi kudidimia. Updates kutoka ukurasa wa Twitter wa Mh. Zitto 21/2/2012 - Ziara ya Tanga Jana tumemaliza Muheza.Tumekwenda kata ya Zirai-ambapo shule yao ya kata kati ya wahitimu 63 (form4),61 wamepata sifuri na wawili darajala 4. Tumehutubia Muheza mjini.Ujumbe wetu jana ni 'ukosefu wa ajira na ufisadi waweza kuangamiza Taifa iwapo hatua hazitochukuliwa. Sisi tunaelekeza nguvu kuisukuma Serikali kuweka fursa za uwekezaji kwenye Kilimo na viwanda vya Kilimo(uchumi wa vijijini) ili kukuza Ajira. Katika kupiga vita ufisadi, tutaendelea kuibua kashfa za ubadhirifu wa Mali za umma Kama njia ya kuzuia (deterrent). #ZiarayaTanga |