Hujaeleweka unachomaanisha.Lowassa ana kosa lolote.
Tuambie kwanza, utajiri alionao lowassa aliupataje?
Naomba kuelimishwa waungwana!
Na wewe tuambie kwanza umaskini tulio nao tumeupataje?
.pole , umebwia kwenye dimbwi la kutokufahamu, kosa la lowassa ni kufanya kazi kwa bidii na hivyo kumu outshine boss wake, na kama matokeo ya hilo wapambe wakiongozwa na membe na zoka wakamtaarifu rais kuwa lowassa anajiandaa kugombea 2010 kukuangusha, rais akaogopa akamtengenezea lowassa mtego kwa ahadi kemu kemu na mwisho akamtosa. MEMBE NA ZOKA WABISHE HAPA, AU MMM AMBAYE NI SWAHIBA MKUBWA WA MEMBE ABISHE HAPA, ANAJUA A TO Z NA NDO SABABU ANAMPIGIA MEMBE KAMPENI KUPITIA JF
Mkuu heshima yako.
Mimi naona waswasi wangu unaongezeka juu ya hili kundi linalotaka kumsafisha Edward Lowasa piga ua, ni kundi ambalo linajaribu kila kukicha kuweka hoja ambayo angalau inaweka nuru juu ya jina la Edo.
Mimi ni mmoja wa watanzania ambao tuliweka angalu matumaini kwamba EL atakuwa Sokoine wa pili hasa kuwa kuzingatia kwamba yeye na huyu Sumaye walionekana ni wachapa kazi hodari.
Lakini ilikuwa ni ndoto tu kwani marehemu Edward Moringe Sokoine ambae tuliona kazi yake miaka ya mwanzo ya themanini, alikuwa ni mtu wakee na sidhani kama atatokea mtanzania mwingine wa aina ya Edward Sokoine.
Ni kazi ya kujituma kuitumikia nchi yako, kutoa maamuzi magumu (kuwashughulikia wahujumu uchumi wa nchi ambao walianza kuitafuna nchi zamani tu) kuwa tayari kusimamia haki na kuwa tayari kushiriki mwenyewe shughuli za maendeleo ya taifa, na kuwa tayari kuinua uchumi wa nchi ambao kwa wakti ule ule ulikuwa ni mbaya sana.
Hayati mwalimu Nyerere alipokuwa akitoa sababu za kuondoa jina la EL kwenye orodha ya wagombea wa uraisi mwaka 1995, alisema kwamba EL si mtu anaefaa kuwa raisi wa nchi kwa sababu alikuwa tayari ana utajiri amao ulikuwa ni zaidi ya mshahara wake akiwa ofisa wa ngazi za juu serikalini na kwamba majina ya wagombea hayakuwa yakihitaji sura fulanifulani.
BM alipochaguliwa kuwa raisi akamkumbuka EL na kumpa uwaziri na EL akatumia nafasi vizuri kufanya aliyoyafanya hasa pale ARDHI na kuna mwenzetu mmoja amekwishasema hapo juu, si unakumbuka sakata ya viwanja vya mnazi mmoja?
Mwaka 2005 Mheshimiwa Kiwete akamteua mara moja kuwa Waziri Mkuu na huo ndio ukawa wigo moana wa EL kufanyizia kila kitu. Lakini ukweli kuhusu EL halisi ulijitokeza kupitia RICHMOND na hio ilikuwa ni ndani ya miaka mitatu tu.
By the time anajiuzulu na kulihutubia bunge mwaka 2008 nilipomtazama na kumsikiliza EL alikuwa akionekana ni mtu mwenye kutojiamini na rahisi kushawishika na hio ilikuwa ni hotuba ya kutaka kusema kwamba bado nina nia ya kuongoza na kuhakikisha anatimiza malengo yake ya kujitosheleza yeye binafsi na kusahahu watanzania wenzake.
Unapojiuzulu hupaswi kujaribu kutoa hotuba bali unakaa pembeni ili utafakari kile kibaya ulichofanya hasa UFISADI na pia hupaswi kuhojihoji wachunguzi hasa ile tume iliyoundwa kuchunguza suala la RICHMOND. Kitendo cha kujaribu kufuatilia uchunguzi wa tume kulithibitisha nia na malengo ya EL na ambayo yanajulikana kwamba ni ubinafsi na tamaa ya madaraka.
Kizuri zaidi ni kwamba mkuu wa kaya amemuacha EL akihangaikahangaika kujaribu PR nyingi tu kujisafisha na yeye JK asiseme kitu hiyo niishara kwamba hata JK haoni sababu ya EL kugombea uraisi mwaka 2015 akiwa ana umri wa miaka 62.
EL aliposhughulikia suala la RICMOND alikuwa akifahamu kwamba alikuwa akilitumbiza taifa katika matatizo makubwa kiuchumi na alikuwa hajali jambo hilo. Hapa tunazungumzia mamilioni ya kodi za wananchi ambazo zingekenda kufanya shughuli za maendeleo hata kununua vitanda vya hospitali amabzo baadhi bado zina wagonjwa wanalala chini.
EL hafai kuwa raisi wa Tanzania na kama akichaguliwa basi watanzania tunaendeleza ujinga.
.
siku zote mwembe wenye matunda ndio unaopigwa mawe...... lowassa atabaki kuwa lowassa hata mumpige fitina vipi ukweli uko wazi hamumuwezi hata kidogo na wanachi sasa wanajua kumbe alipigwa zengwe tu baada ya kuona ni mchapakazi na mtu asiyeteteleka na mwenye maamuzi sahihi.
hao kila zito,slaa,sita etc waliosema fisadi hao hao ndo leo mitambo ile ile wamekuja kuomba inunuliwe na sasa inazalisha umeme kwa jina jipya la symbion .... acheni majungu ... lowassa ndio mkombozi aliyebaki jembe la ukweliiii mtapayuka sasa na ukweli tayari sasa amewashika pabaya na mtaongea sana....
Huwezi kutuaminisha huo upuuzi wako. Nani asiyejua ni fisad? Hata watoto aw chekechea wanalijua Hilo.pole , umebwia kwenye dimbwi la kutokufahamu, kosa la lowassa ni kufanya kazi kwa bidii na hivyo kumu outshine boss wake, na kama matokeo ya hilo wapambe wakiongozwa na membe na zoka wakamtaarifu rais kuwa lowassa anajiandaa kugombea 2010 kukuangusha, rais akaogopa akamtengenezea lowassa mtego kwa ahadi kemu kemu na mwisho akamtosa. MEMBE NA ZOKA WABISHE HAPA, AU MMM AMBAYE NI SWAHIBA MKUBWA WA MEMBE ABISHE HAPA, ANAJUA A TO Z NA NDO SABABU ANAMPIGIA MEMBE KAMPENI KUPITIA JF
naona umepiga porojoo tu za m4c maneno herufi nyingi ..hakuna ushahidi wa kumjibu mtoa hoja...
Heri ya hao wezi kuliko Vasco da Gama
Kujiuzulu ni kukiri kosa,hilo la kuwajibika kwa makosa ya mkubwa wake ni kosa pia kwasababu hakuna ushahidi ya kwamba alifuata maelekezo ya mkubwa wake.Kama ni kujiuzulu,angefanya hivyo kwasababu anapingana na maelekezo yenye kulihujumu Taifa.Yeye kama alikuwa mshauri,halafu ushauri wake ukakataliwa,na endapo ana mapenzi na Taifa letu,basi angejiuzulu na si kusubiri hadi kisanuke.Hilo limeonyesha upungufu mkubwa sana wa kiungozi na uzalendo kwa Taifa.Simple!Hakuwa na kosa lolote. Alijiuzulu kuwajibika kwa makosa ya mkubwa wake. Si alishasema hadharani kuwa hakuna kitu alichofanya bila maelekezo ya bosi wake? Je bosi wake ameshakanusha? EL ni mchapakazi hodari.
Umejiunga May 2012 na umeshapata like 10,hongera.Hii inaonyesah ni mchangiaji mzuri. Kwanza nakushauri utafute uzi unaohusiana na aliyekuwa katibu binafsi wa Nyerere amabye ameandika vizuri matukio ambayo yanaweza yakakupa picha ya EL. Jambo la pili tafuta kumbukumbu zozote zinazohusiana na Kasbfa ya Richmond na baada ya hapo tafuta watu walioshi na kufanya kazi la EL either Monduli na AICC: Kuna mengi yanahusiana na Richmond na kuna fununu ya kuwa aliwajibika ili kumlinda swahiba yake na hili lilijionyesha tena katika mkutanoa CCM Dodoma ambapo alisema yasiyostahili kusemwa kuhusu JK. Kwa ufundi EL ni mchapa kazi,haogopi kufanya maamuzi lakini ana tamaa mno ya mali.Naomba kuelimishwa waungwana!