Hivi ni lipi hasa kosa la Edward Lowasa? Naomba kufahamishwa!

Msiwe mnauliza maswali ya kitoto. Kwani nani asiyejua kuwa Lowassa ni mwizi? We unadhani hayo mapesa ya kununua uchaguzi wa ccm ameyatoa wapi? Ulizeni maswali ya maana.
 
kosa lake ni kukipenda chama chake sana yaani he's soo loyal to ccm he doesnt deserve the lack of respect he's gettin from his fellow members.....
 
Anahonga CCM yote kuanzia baba zao, mama zao, na watoto wao. hela yake ya rushwa inasababisha mafuriko ya hela ktk uchumi.
 
hii ni tz bwana m2 jana kachakachua pale leo mnampeleka kule achakachue vizuri 4m impossible maybe those blinds ni bola kumpa m2 mke wangu kuliko kumpa nchi Ruasa fisadi mkubwa
 
EL ni mwanasiasa,mkulima,mfugaji,mfanyabiashara na mwanadiplomasia ktk maisha yake Mungu .amemfanya azitumie vzr fursa alizozipata kutokana na talents hizo, baadhi ya watanzania ambao nao walikuwa na fursa hizo pia walizutumia ktk anasa na kutapanya mali. mwisho sasa wamekuwa na wivu, choyo na husuda juu ya EL na kutaka kuwaaminisha watu kuwa kiongozi wa siku nyingi asiye na mali ndiye msafi nasema si kweli na hawafai kuwa viongozi wetu. tukubali viongozi wanafursa nyingi za kuwa na utajiri halali wakizitumia vzr fursa walizonazo toka mishahara na masurufu mengine na ziara wanazofanya ndani na nje ya nchi wawekezaji mbalimbali wanaokutana nao ushawishi wanao jenga[tukubaline ni rukhsa kiongozi kuwa na hisa ktk makampuni] viongozi wengine wavivu wa kufikiri juu ya familia zao na taifa kwa jumla huishia kuwaita wenzao waliosugua akili kuwa fisadi.vingozi hao hakika ni waongo na wakuogopwa kama ukoma.
 
Naomba kuelimishwa waungwana!

Hata mini nilikuwa nimekwazwa na mengi waliyokuwa wanasema watu. Lakini sasa naanza kuwa na wasiwasi naye kutokana na nguvu kubwa ya pesa inayosemekana anaitumia kuutafuta u-Rais wa Tanzania. Kama ni kweli anatumia pesa kuusaka ukubwa, hiyo pesa anaipata wapi? Ni biashara gani anafanya inayompa faida kubwa kiasi hicho baada ya kulipa kodi?

Labda kama watu wanamsingizia, lakini kama ni kweli anafanya hivyo, basi ni mtu wa kuogopwa kama UKOMA.
 
Kama unauliza Lowassa ana kosa gani tafuta daktari mapema akusaidie lakini kama wewe siyo Mtanzania kwa taarifa tu huyu ndiye aliyefanya nchi tajiri ya Tanzania ikageuka ombaomba wakishirikiana na rafiki yake mkubwa Jakaya Kikwete. Wameibia nchi kupitia Richmond na Dowans lakini pia kama hujui huyu aliibia AICC hadi mwalimu Nyerere akasema Lowassa hafai kuwa kiongozi wa hata kikundi cha Bongo Flavor. Kumbuka pia viwanja na majumba ya CCM yalivyofanywa mtaji Lowassa akihusika....Mimi nimeapa siwapi tena CCM kura yangu labda wabadilishe chama kama walivyobadili TANU na walete viongozi wapya wanaokerwa na ufisadi.
 
naona hakuna majibu ya moja kwa moja na pia n sababu gani eti baba wa taifa hakupenda aje kuwa raisi ni nini haswa
 
Huyu jamaa,ame mkosea adi Mungu.yawezekana watanzania tuka mshindwa kwa ajili ya pesa alizo waibia wavuja jasho wa tanzania ila Mungu awezi mshindwa.
 
pole , umebwia kwenye dimbwi la kutokufahamu, kosa la lowassa ni kufanya kazi kwa bidii na hivyo kumu outshine boss wake, na kama matokeo ya hilo wapambe wakiongozwa na membe na zoka wakamtaarifu rais kuwa lowassa anajiandaa kugombea 2010 kukuangusha, rais akaogopa akamtengenezea lowassa mtego kwa ahadi kemu kemu na mwisho akamtosa. MEMBE NA ZOKA WABISHE HAPA, AU MMM AMBAYE NI SWAHIBA MKUBWA WA MEMBE ABISHE HAPA, ANAJUA A TO Z NA NDO SABABU ANAMPIGIA MEMBE KAMPENI KUPITIA JF

mwizi tu huyo km wale waongezao sifuri kwenye figure za pesa za miradi ili waiibie sirikali. mwizi mwizi mwizi.
 
Back
Top Bottom