Hivi ni lipi hasa kosa la Edward Lowasa? Naomba kufahamishwa!

Tafuta ile riport ya Mwakyembe imo humu ufanye rejea. Usiwe mvivu jishughulishe.

Na hata kama angekuwa hana kosa kama ambavyo unaelekea kujiulizishia kaswali ka kizushi hapa; huwezi kufika level ya kuwa Waziri Mkuu halafu ukajipima wewe mwenyewe bila shuruti ukaamua kustep down kwa tuhuma za kutokuajibika ipaswavyo na sakata la Richmond halafu uje baadaye tukuone msafi kuwa na sifa ya kugombea hata Urais - ni Tanzania tu! Na naweza kukuhakikishia kuwa haitatokea!
 
Looks like humjui Lowassa na kama unamjua, basi utakuwa unafaidi au unataka kufaidi kutoka kwake. How is this guy clean by the way!! Kama kiongozi anaweza kuchukua mashine ya kufulia nguo za wagonjwa iliyotolewa kama msaada hospitali ya Mkoa Mount Meru akshirikiana na Kinana mwaka 1993, huo u-clean unatokea wapi? He is not patriotic na mimi nitashangaa sana watanzania kumpa urais mtu ambaye hata marehemu baba wa taifa alimwona hafai. What makes him clean today while the history tells us otherwise. Wakati akiwa Waziri wa ardhi alijigawia ardhi kila kona, tena ikiwa ni sehemu ya miradi ya serikali. Sisi hatukatai rais wa nchi kuwa na utajiri ila utajiri wake awe ameupata kwa njia halali, awe na integrity, etc. Marekebisho ya katiba ya sasa lazima yawe wazi kuhusu hili. Rais akiingia madarakani, awe assessed in terms of intergrity, uhalali wa kile anachomiliki, vision yake kuhusu maendeleo ya nchi na record ya utendaji. Asiwe pia na kinga ya kushtakiwa pale atakapokuwa amekwenda kinyume na matarajio ya watanzania - ufisadi, uvunjifu wa haki za binadamu etc. Integrity ya Lowassa ni very low na ana historia ya kutumia madaraka vibaya kwa faida binafsi, etc. Let's think alound on where we want to take this country!! Si kwa kulinda maslahi ya watu wachache (Lowassa and the group). There have been good leaders in this country with very good reputation, if one wants I can mention!!
Mara ya pili nasikia uhusiano wa EL na hospitali. Niliwahi kusikia mahala kuwa alichukua matofali ya hospitali ya Monduli na kwenda kujengea nyumba yake Arusha.So sad.
 
Ni kweli Lowassa alifanya kosa lakini kosa gani lisilosameheka. Mafisadi kila kona kwa kweli tukae tutafakari makosa ya Lowassa ni wengi tu wanayafanya.

Mbona alishasamehewa na JK kama alivyowasamehe mafisadi wengine wa EPA. kwani kafungwa, au kakiri makosa? By the way si unajua wanamwita eti waziri mkuu mstaafu? This kind of person ambaye kajiuzuru kwa ufisadi lakini analipwa na kuhudumiwa kama PM mstaafu. HUU NI WIZI!Oim
 
Kuachana na siasa itakuwa haitendei vema dhamira yake. Anataka kuwa rais wa Tanzania. Katika chaguzi za Tanzania huwezi kushinda bila kutoa rushwa. Huwezi kushinda kwa hoja wala kwa uadilifu. Hivyo ni lazima uwe na fedha nyingi. Utapataje pesa nyingi kwa njia ya uadilifu? Hi ni sawa na ngamia kupita tundu la sindano. Kuiba pesa za EPA, RICHMOND nk ni strategy tu ya kufikia kiti cha urais ili baadaye itumikie vema nchi yake. Ni ufisadi wenye nia njema baadaye. TUKITAKA KUTHIBITISHA TUMPE URAIS. Mbona Sofia Simba amepewa pamoja na kushindwa kujibu maswali kwa ufasaha lakini aliweza kutoa rushwa.
 
Kwa nini huulizi mazuri yake ni yapi? Hatumtaki hatuna haja au sbabu ya kumpenda, period
 
Tuambie kwanza, utajiri alionao lowassa aliupataje?

Shida kubwa ya Watanzania wanataka kila mtu awe masikini. Ukiwa na hata kajumba kadogo watu wanasema wewe fisadi wakati umewekeza na kuwa na mipango ya maendeleo kila kuchwapo. Kwangu mimi ni bora kumchagua raisi mwenye mali lakini mchapa kazi, kuliko kutafuta mtoto wa mkulima ambaye hana mchango wowote.
 
Shida kubwa ya Watanzania wanataka kila mtu awe masikini. Ukiwa na hata kajumba kadogo watu wanasema wewe fisadi wakati umewekeza na kuwa na mipango ya maendeleo kila kuchwapo. Kwangu mimi ni bora kumchagua raisi mwenye mali lakini mchapa kazi, kuliko kutafuta mtoto wa mkulima ambaye hana mchango wowote.

Wewe utakuwa ama ni b.w.e
g.e wa kutupwa au mtu alieamua kuuza utu wake unashamedly! Who told your idiotic brain kuwa Watanzania wanapenda wenzao wawe maskini? Unajua jengo ambalo lina host wizara ya miundo mbinu ni la nani? Alishaulizwa kuhusu utajiri wake? Hata kama hujui ni lazima uuweke wazi u.b.w.e.ge wako in public?
 
whether ni jambazi or not, but I'd rather have him as Tz prez. than huyu Vasco Da Gama.

BUT.Why should you compare him with the outgoing president? Unajua hawawezi kabisa kuingia katika ulingo wa mashindano.U would rather compare him na watu wengine,Expected Candidates kama Zitto,Membe,Nchimbi,Dr Slaa and others.
 
Muhujumu uchumi wa nchi,hafai hata kuwa hata katibu kata,ingekuwa nchi kama china angeshanyongwa kitambo
 
Tatizo la Lowasa rejea hotuba za Mwalimu. Kuwa ukiona mtu anatamani kuingia Ikulu na hata kutumia pesa mwogope kama ukimwi. Na jiulize ni biashara gani anaenda kufanya huko, na pesa anazotumia kupata huo u Rais atazirudishaje?. Na kwamba Ikulu hakuna biashara ni mzigo.
Lowasa anatumia pesa nyingi sana hata kudiriki kuhonga hata makanisani ali mradi tu aingie Ikulu. Hajui kuwa nafasi yake kwa sasa ni finyu sana. Zamani iliwezekana kwa mtendaji ndani ya Serikali kutuhumiwa au kuwajibika kwa rushwa au ufisadi kama alivyowajibika Lowasa na baadaye ukasafishwa na kurudi tena kwenye uongozi. zama hizo zimepitwa na wakati sifa yako ikishachafuka mbele ya jamii ndiyo imetoka na huwezi rudi tena. Ndani ya CCM Lowasa bado ni maarufu na ataendelea kuwa maarufu kwa kuwa CCM imejengwa juu ya misingi ya rushwa na ufisadi na hakuna mtu mwenye ujasiri wa kumkemea au kumnyoshea kidole mwingine. Lakini nje ya CCM Lowasa hana sifa ktk jamii sana sana anaonekana ni jambazi tu wa raslimali za nchi yetu. Pengine nimkumbushe tu kuwa sifa kuu ya mgombea nafasi yoyote ya kuwakilisha wanannchi uwe udiwani, ubunge au U Rais mwaka 2015 itakuwa ni uadilifu wa mgombea ktk jamii. Wananchi watakuwa tayari kumchagua maskini kwa kuamini kuwa ni mwenzao na kumuacha tajiri kwa kuamini kuwa ndio waliotufikisha hapa tulipo leo. Kwa kigezo hiki tayari Lowasa anakosa sifa.
Tatizo kubwa ni kuwa Viongozi ktk nchi hii hawaoni kama matatizo lukuki ya wananchi ni mzigo kwao, bali wanachojali ni maslahi yao tu. Tunataka viongozi watakaokuwa tayari hata wakifa maskini lakini wawatumikie wananchi na wawafikishe ktk neema.
Hebu fikiria Mke wa mtoto wa Rais anapewa mkopo wa kusoma kwa asilimia 100 lakini mtoto wa maskini kijijini anakosa. Viongozi wamejaa ubinafsi hivi ni kweli mtoto wa Rais atashindwa kumlipia mke wake?. Si kweli bali viongozi ktk nchi hii wamejiundia kikundi cha watu wachache ambao wanajiona ndio wenye haki ya kufaidi raslimali za nchi hii tu na watoto wao pamoja na wapambe wao.
Lazima tukatae na Lowasa asome alama za nyakati kuwa mwaka 2015 hatutaendelea kuwa wajinga kama anavyofikiria.
 
Back
Top Bottom