Hivi mtu akifa na hela zake ziko benki na Mpesa, tukiwa na cheti cha kifo tunaweza fuatilia?

Wajuzi naomba msaada.

Ndugu kafa. Ana akaunti benk ila password hazijulikani pia ana mpesa na pesa zipo ila no password. Mkewe ana death certificate. Atapataje pesa za mmewe? Pia ana cheti cha ndoa.

Msaada
Kama hivyo vipo atapewa ila kabla hajenda huko ajaribu kutafuta njia ya kujua kiasi gani maana kuna mikamouni mingine ikishajua hivyo inapunguza au kutaifisha mkienda mnaambiwa hamna salio
 
Hio dealth certificate huwa hawaipokei bank wala mpesa, wanapokea death certificate tu. Sijui hata kwanini!

Warudishie RITA hio dealth certificate, halafu waambie wakupe death certificate. Halafu nenda mahakama ya mwanzo fungua shauri la kuomba kufungua mirathi ya huyo marehemu, mahakama watawapa barua ya usimamizi wa mirathi ndio mwende bank au huko mpesa mkazitoe hela, kama kuna nyumba au kiwanja kaacha mtauza. NA KAMA MAREHEMU AMEACHA MADENI, MTALIPA!

Usipo fanya hivo, jiandae na kesi ya uhujumu uchumi kwa kujipatia pesa kutumia njia ya udanganyifu (Hata kama hela ni Sh 2,000/=, uhujumu uchumi haina dhamana).
Aseee ha ha ha ha ha
 
Msimamizi wa mirathi akafungue kesi mahakamani kwanza, kisha mahakama ndio itatoa oda kama benki watoe hela za kwenye account zake na kumpa huyo mke wake.
Hapana chetu cha kifo hakitoshi ndugu. Inatakiwa kufungua kesi ye Mirathi na msimamizi anayeidhinishwa na Mahakama ndiye atakayefuatilia kwa kutumia nyaraka za Mahakama. Ukweli ni kuwa Kuna hela nyingi sana kwenye Mpesa au simu za marehemu ambazo zinaotea kwa kutokufuatiliwa.
 
Sheria ya mirathi kwa upande wa wajane kina mama inatakiwa kuangaliwa upya
Huwa najiuliza hivi inawezekanaje mkeo asiijue password ya kadi zenu za Bank?? Hapa huwa naona kama kuna shida kwa baadhi ya wanaume, aisee mimi card zetu tuna share password yake naijua na yangu anaijua hivyo yeyote anaweza kwenda kutoa pesa mda wowote zinapo hitajika.

Aisee hata nikifa ghafla mwenzangu anaweza kwenda chukua fedha zote
 
Ndugu mbona inawezekana sana hiyo mkeo kujua password za tigo pesa anaweza asijue kutokana na maelewano yenu ndani mkoje hata mwanamke anaweza kuwa na kazi pia akafariki vipi hilo swala na mwanamke ndo huwa hataki kabisa ukafahamu hela zake shida Sana kwahiyo inawezekana kutokujua password za bank au M pesa hilo mbona ndo Sana 75%
Hizo ni ndoa za machekibobu.
 
FRESHMAN wewe kama mwanaume umetafuta mali na mke wako kipenzi lakini ukitangulia kuondoka hizo mali zinauzwa warithi wanagawana. Sasa kama una nyumba moja wakishagawana yeye utu uzima ushawadia, kukimbizana hawezi tena, unafikiri yeye ataenda wapi.

Nawaza nimpoteze babachanja wangu halafu nyumba yangu nilivyoisotea Mimi na yeye iuzwe ili warithi wapate chao halafu Mimi nikaanze kutafuta makazi.

Maumivu juu ya maumivu
Ipo sawa maana sheria ya ndoa imewabeba sana
 
Kwa mujibu wa sheria,kama marehemu aliacha pesa hamuwezi kugewa moja kwa moja.ni lazima ufungue shauri la mirathi mahakama ya mwanzo.baada ya hapo atapewa barua msimamizi wa mirathi aipeleke benk au kampuni ya simu.Akishapeleka pesa zote zitapelekwa bank kuu.Kutoka kule ndio zitarudishwa mahakamani kama cheki na mahakama ndio itagawa cheki zile kwa warithi kama mlivyokubaliana katika kikao cha familia kumteua msimamizi wa mirathi.Ni process ndefu sana na inaweza kuchukua si chini ya mwaka mmoja toka marehemu afariki.kuwa na subira tu.Lakini kama angekua na password anatoa tu hela na habari inaishia pale
 
Kuna mtu alifariki January mwaka jana taratibu zote zikafuatwa na msimamizi wa Marathi na pesa katika bank accounts zote zikapatikana lakini cha ajabu pamoja na kukamilisha kila kitu pesa bado hajapewa mkewe. Anaambiwa zipo hazina hajui tena afanye nini kishajichokea.
Mzee baba huko hazina ndipo kwenye shida.mara nyingi Bank hutoa check mapema na kuzipeleka hazina.Sasa kasheshe ni cheki kutoka hazina kurudi mahakamani.Haloo ni mwendo wa nenda rudi kesho.mara hazijasainiwa.mara hazionekani.zikionekana utaambiwa njoo wiki ijayo tena kwa maneno matamu wale watu hazina Mungu anawaona.kila siku ni story.mimi nilikua nikiambiwa njoo wiki ijayo narudi kesho asubuhi.nilifanya hivyo miezi sita chek zikatoka ila jasho la meno lilinitoka
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Sina hakika hapo issue ni nini.

Ila ninadhani hii inatokana na kuwa siku hizi wakati mwingine unakuta kuna yale masuala ya pesa kutumwa bank kuu au akaunti ya mahakama.

Sasa kama baada ya uteuzi wa msimamizi wa mirathi, barua ya mahakama inasema pesa ziwekwe bank kuu au akaunti ya mahakama, basi taasisi husika inalazimika kulipa pesa huko. Sasa si unajua taratibu za serikali zinavyokuwa?

Ni jukumu la msimamizi wa mirathi kufuatilia. Ndio kazi yake hiyo.

Ila nina uhakika kuna baadhi ya kamoubi za simu zinalipa moja kwa moja kwa wasimamizi wa mirathi. Hili nimelishuhudia binafsi kwa ndugu zangu
Hakuna kampuni inayolipa moja kwa moja kwa mtu.Ila nilipoenda NMB kutoa taarifa kwamba mteja wao amefariki nilipewa pole milion moja.Ndio yote tulitumia kujisogeza wakati Tunasubiri mirathi itoka nayo tulikamilisha kila kitu ila ikachukua mwaka mzima kutoka
 
Fuateni taratibu zote za kuteua msimamizi wa mirathi. Ikiwemo pia kwenda mahakamani.

Mahakama ikishatoa nyaraka za kumteua msimamizi wa mirathi, huyo ndiye atakayefuatilia kwa bank na kampuni ya simu ili kupata pesa.

Kumbuka kuwa jukumu la msimamizi wa mirathi ni kutambua na kukusanya mali na madeni yote ya marehemu. Jukumu la pili ni kugawa mali kwa warithi halali kisheria.

Hivyo, Msimamizi wa mirathi atakayeteuliwa ndiye atakayefuatilia na kupewa hizo pesa. Naye atazigawa kwa warithi halali kwa mujibu wa sheria.

Kwa suala lako, ingependeza huyo mke ndio apewe usimamizi wa mirathi.
Inategemea kama huyo mke ana akili timamu na uelewa wa kusimamia hilo. Wengine ni shida.... Akishika mzigo huo ni kutumbua tu....
 
Hio dealth certificate huwa hawaipokei bank wala mpesa, wanapokea death certificate tu. Sijui hata kwanini!

Warudishie RITA hio dealth certificate, halafu waambie wakupe death certificate. Halafu nenda mahakama ya mwanzo fungua shauri la kuomba kufungua mirathi ya huyo marehemu, mahakama watawapa barua ya usimamizi wa mirathi ndio mwende bank au huko mpesa mkazitoe hela, kama kuna nyumba au kiwanja kaacha mtauza. NA KAMA MAREHEMU AMEACHA MADENI, MTALIPA!

Usipo fanya hivo, jiandae na kesi ya uhujumu uchumi kwa kujipatia pesa kutumia njia ya udanganyifu (Hata kama hela ni Sh 2,000/=, uhujumu uchumi haina dhamana).
 
Fuateni taratibu zote za kuteua msimamizi wa mirathi. Ikiwemo pia kwenda mahakamani.

Mahakama ikishatoa nyaraka za kumteua msimamizi wa mirathi, huyo ndiye atakayefuatilia kwa bank na kampuni ya simu ili kupata pesa.

Kumbuka kuwa jukumu la msimamizi wa mirathi ni kutambua na kukusanya mali na madeni yote ya marehemu. Jukumu la pili ni kugawa mali kwa warithi halali kisheria.

Hivyo, Msimamizi wa mirathi atakayeteuliwa ndiye atakayefuatilia na kupewa hizo pesa. Naye atazigawa kwa warithi halali kwa mujibu wa sheria.

Kwa suala lako, ingependeza huyo mke ndio apewe usimamizi wa mirathi.

Habari yako mkuu, naomba kuuliza swali. Kwa mfano marehemu kipindi cha uhai wake alimpa eneo ndugu yako wakiume kiwanja kama zawaidi. Japo haikuwa wazi , yaani marehemu Hakumtaarifu ndugu yeyote. Ikiwa na maana hata ndugu na familia ya marehemu inajua kuwa hiyo property ilikuwa ni ya marehemu. Japo mzawadiwa anaumiliki halali wa eneo kisheria yani alifuatikia hati ya kiwanja na kuipata.

Swali langu ni endapo property hiyo ikiorodheshwa na msimizi wa mirathi kama mali inayositahili kurithiwa, Je Mmiliki halali wa kisheria anawezaje kuichoma property hiyo kwenye orodha?
 
Hv ni kwann wanaume tu ndo tunandikaga wosia na utaribu wa mali tutapoanza kufa? Hv sisi wanaume ndo ishakua 22/7 kutangulia kufa? Au sisi tu ndo wenye mali?
 
Sasa Mwanamke kama huyo Wewe ni wa nini? Yaani why do you have such a woman ?

Kama mmeamua kuishi pamoja maana yake ni lazima kuwe na Transparency na Truth.

Kitu kama ATM au Mpesa is very Common.

Like me; simu yangu Muda mwingi ipo kwa mikono ya my wife, au Mimi nikiwa na shida ya hela ya haraka nachukua Kadi yake naenda Bank ATM kutoa hela, like wise yeye pia . those are very common details kwa wanandoa.

Sijaona Essence ya huu Uzi
Hongera sana mkuu
 
We nae umekalia kushobokea eti sheria mbovu. Ubovu wake huelezei, watu wanakuelewesha hapa bado umeshupalia (huku umebana pua) "sheria mbovu"
Umeamkaje na jazba lote hilo sasa Hahahaa.... ukiendelea hivyo utakujaga kufia usingizini haki🤣🤣🤣🤣 Wewe rudi uendelee kusoma Uzi utakutana na mijadala ya huo ubovu. Hata sijashupaa na kubana pua kama unavyodai, tuko kwenye mjadala kawaida tuu. Punguza chuki na jazba, Usikurupuke tena hivyo eeeh! Sawa!?

Sheria ya mirathi kwa upande wa wajane kina mama inatakiwa kuangaliwa upya
Upya kwa sababu gani? Ina mapungufu gani?
FRESHMAN wewe kama mwanaume umetafuta mali na mke wako kipenzi lakini ukitangulia kuondoka hizo mali zinauzwa warithi wanagawana. Sasa kama una nyumba moja wakishagawana yeye utu uzima ushawadia, kukimbizana hawezi tena, unafikiri yeye ataenda wapi.

Nawaza nimpoteze babachanja wangu halafu nyumba yangu nilivyoisotea Mimi na yeye iuzwe ili warithi wapate chao halafu Mimi nikaanze kutafuta makazi.

Maumivu juu ya maumivu
Huwa inakuwa kubwa Sana kama kuna watoto wa pande mbili tofauti na walikuwa hawapendani kingine kwamba na suala la elimu nalo tatizo kubwa Sana aisee ukikosa elimu sometimes huwa tatizo tena
Sasa inauzwaje kama mama ndo kabaki kichwa cha familia atakaeuza ni nani? mana tayari mama yupo muuze ili iweje tatizo ndo linakujaga hapo kukosa busara kwa baadhi ya Wana ndugu shida Sana
Busara v/s Sheria
Kumbuka pesa haina undugu
 
Back
Top Bottom