Hivi mtu akifa na hela zake ziko benki na Mpesa, tukiwa na cheti cha kifo tunaweza fuatilia?

mkuu kwanza ningependa kukipata kitabu chako kinacho husu sheria katika mfumo wa soft copy

pili ningependa kuuliza swali, kuna uwezekano wa kufungua faili la mirathi kwa mtu aliye fariki miaka kumi iliyopita licha ya kuwa msimamizi wa mirathi nae alisha kufa miaka kadhaa iliyopita ?
Inawezekana kufungua file upya mkuu, kwa sharti moja kwamba ueleze ni kwasababu gani umechelewa kufungua shauri la mirathi ndani ya muda wa miaka 3 iliyowekwa kisheria. Kimsimgi, sababu tayari umeshaitaja, na ni ya msingi kisheria, kwamba msimamizi wa mirathi alifariki kabla ya kuthibitishwa na mahakama (kama nimekuelewa vizuri).

Kitabu naweza kukupatia kwa soft copy, karibu PM.
 
FRESHMAN wewe kama mwanaume umetafuta mali na mke wako kipenzi lakini ukitangulia kuondoka hizo mali zinauzwa warithi wanagawana. Sasa kama una nyumba moja wakishagawana yeye utu uzima ushawadia, kukimbizana hawezi tena, unafikiri yeye ataenda wapi.

Nawaza nimpoteze babachanja wangu halafu nyumba yangu nilivyoisotea Mimi na yeye iuzwe ili warithi wapate chao halafu Mimi nikaanze kutafuta makazi.

Maumivu juu ya maumivu
Kwani wewe ndo uliemlea mpaka akakua na akakuoa? Hukumbuki kuna watu walitumia rasilimali zao na wana haki na wao kupata ktk alivyochuma?
 
Sasa Mwanamke kama huyo Wewe ni wa nini? Yaani why do you have such a woman ?

Kama mmeamua kuishi pamoja maana yake ni lazima kuwe na Transparency na Truth.

Kitu kama ATM au Mpesa is very Common.

Like me; simu yangu Muda mwingi ipo kwa mikono ya my wife, au Mimi nikiwa na shida ya hela ya haraka nachukua Kadi yake naenda Bank ATM kutoa hela, like wise yeye pia . those are very common details kwa wanandoa.

Sijaona Essence ya huu Uzi
Mkuu basi mshukuru mungu kwamba uko kwenye ndoa yenye uadilifu na transparency kiasi hicho.Ukweli wa mambo ni kwamba ni ndoa chache zenye kufikia viwango hivyo vya maelewano na uwazi.
 
Kwanza poleni kwa msiba mkuu.

Fateni taratibu zifuatazo: Kwanza wanafamilia wakae kikao na kuandaa muhtasari wa kikao ambao pamoja na mambo mengine; utampendekeza msimamizi wa mirathi ya marehemu (endapo marehemu hakuacha wosia).

Baada ya hatua hiyo hapo juu, msimamizi wa mirathi ya marehemu aliyependekezwa atapaswa akathibitishwe na Mahakama (endapo hakuna pingamizi), ambapo atapewa 'hati ya usimamizi wa mirathi ya marehemu'. Kama marehemu alikuwa muislamu, mtaenda Mahakama ya mwanzo, kama marehemu alikuwa mkristo basi mtaenda Mahakama ya Wilaya/Mahakama ya hakimu mkazi, lakini kwa Mahakama ya Wilaya/Mahakama ya hakimu mkazi basi kuna maombi maalumu ambayo yanapaswa kuandaliwa na wakili na ndiyo yanapelekwa mahakamani, isipokuwa mkienda Mahakama ya mwanzo ambapo mtajaza tu fomu maalumu.

Viambatanisho muhimu ambavyo msimamizi wa mirathi aliyependekezwa kwenye kikao anatakiwa kuwa navyo ni cheti cha kifo cha marehemu na orodha ya mali za marehemu.

Bilashaka umenielewa mkuu. Karibu ununue Kitabu changu chenye jina; DONDOO MUHIMU ZA NAMNA YA KUKABILIANA NA KESI ZA ARDHI, JINAI, MADAI, MIRATHI NA NDOA HASA KWA WASOMAJI WASIO WANASHERIA NA WANASHERIA WACHANGA:SOMO FUPI LA SHERIA KWA VITENDO. Bei ni TZS 10,000 tu. Nipo Dodoma ila mikoani natuma pia. Au naweza kukutumia softcopy ukipenda. Aksante.
Weka namba zako mkuu

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mmefiwa, hata siku tatu hazijaisha, mshaanza kuwaza hela za marehemu benki na M-pesa. Kweli dunia....!



JESUS IS LORD.
Ndg yangu Bora wawai mapema kufunguwa Mirathi, maana ukichelewa kuna Wajanja watafunguwa Mirathi na watapita nazo hizo pesa!!
 
Back
Top Bottom