Hivi mtu akifa na hela zake ziko benki na Mpesa, tukiwa na cheti cha kifo tunaweza fuatilia?

Kuna mtu alifariki January mwaka jana taratibu zote zikafuatwa na msimamizi wa Marathi na pesa katika bank accounts zote zikapatikana lakini cha ajabu pamoja na kukamilisha kila kitu pesa bado hajapewa mkewe. Anaambiwa zipo hazina hajui tena afanye nini kishajichokea.
Itakua alizikopea au ziko fixed account
 
Mkuu kwa hiyo wanaekufa na kuacha pesa kwenye akaunti ni mme tu na mke ndio mwenye wajibu wa kuzifatilia vinginevyo badili kichwa cha habari.
 
Bushmamy kuna matukio mengi wamama wamelazimika kuacha mali za familia ziuzwe baada ya waume zao kufariki ili warithi wagawiwe mali. Mimi sio mwanasheria na sijui hii sheria ya mirathi imekaaje hapo?
Badae kidogo ntakufafanulia
 
Ila mimi hii hoja nimeiangalia kwa masikitiko sana na namna ya Maisha ya sasa yanavyokwenda.

Ni dhahiri kwamba mahusiano ya ndoa mengi hayana mpango chochote. Yaani watu wanaishi siku ziende.

How could that be mke hajui password ya Mpesa ya Mume wake ? How could that be mke au mume hajui ATM password ya mwenzi wake ?

Kuliko kuishi maisha ya kipumbavu kama hayo ni bora nisiwe na mwanamke.

Ninachojua mimi Mke wako au Mume wako ndio mtu wa kwanza Kwenye maisha yako kujua hizo details. It is such a shame mtu kufungua thread na kutuambia mke hajui password za ATM na MPESA. Huu ni WIZI unataka kufanyika. Na ndugu wa Marehemu watizame hili suala kwa karibu ; huenda kuna kitu bado hakipo sawa.

Ungesema utaratibu wa kufuatilia Mali za Marehemu kama vile Majumba, Viwanja, pesa zake ndani ya Bank n.k ingekuwa ni SAWA kuomba Ushauri na utaratibu.

But Akaunti ya MPESA au ATM , mke hajui, that is shame!

Yaani Mimi kama huyo aliyekufa ni kaka yangu; literally mwanamke atachukua share ndogo sana maana sioni kama ni Mtu mwenye akili ikiwa hujui hizo details za mtu unaelala nae kitanda kimoja na probably mna watoto . USELESS!

Anyway, .... tambua Mahakamani haitokuwa peke yako, bali ni familia halisi ya marehemu. Ndugu zake pamoja na watoto, wazazi kama wapo hai ambao watapewa nafasi pia.

maisha hayawezi kuwa so simple Kwenye hiyo chain.
Baada ya kuugua nikajifunza kitu ,Kisha nikajiona mi mjinga kutomshirikisha wife kwenye masuala nyeti.Saizi anajua password zangu zote za ki bank pamoja na simu card .Ni muhimu watu wajitambue,watoto wanaweza kosa stahiki zao kipumbavu sababu ya password zenye tarakimu nne tu au tatu,mgogoro pia hauepukiki kwa ndugu
 
Kuna mtu alifariki January mwaka jana taratibu zote zikafuatwa na msimamizi wa Marathi na pesa katika bank accounts zote zikapatikana lakini cha ajabu pamoja na kukamilisha kila kitu pesa bado hajapewa mkewe. Anaambiwa zipo hazina hajui tena afanye nini kishajichokea.
Ni kweli pesa za mirathi baada ya mahakama kutoa hukumu ya mirathi na msimamizi wa mirathi kujulikana, pesa zote zilizopo kwenye accounts za mabenki au kwenye makampuni ya simu uhamishwa kwenda Hazina wizara ya fedha kwenye akaunti ya Mirathi Benki Kuu ya Tanzania. Na baada ya hapo Hazina uandika hundi kwa kila mhusika kwa mujibu wa sheria na wosia wa marehemu.

Kumbuka mabenki na makampuni ya simu kisheria hawana uwezo wa kutoa pesa za marehemu kwa wafiwa moja kwa moja bali kupitia Hazina kupitia Benki Kuu ya Tanzania.
 
Ni kweli pesa za mirathi baada ya mahakama kutoa hukumu ya mirathi na msimamizi wa mirathi kujulikana, pesa zote zilizopo kwenye accounts za mabenki au kwenye makampuni ya simu uhamishwa kwenda Hazina wizara ya fedha kwenye akaunti ya Mirathi Benki Kuu ya Tanzania. Na baada ya hapo Hazina uandika hundi kwa kila mhusika kwa mujibu wa sheria na wosia wa marehemu.

Kumbuka mabenki na makampuni ya simu kisheria hawana uwezo wa kutoa pesa za marehemu kwa wafiwa moja kwa moja bali kupitia Hazina kupitia Benki Kuu ya Tanzania.
Mkuu soma hii link.

 
Kwa nini mtu anaweka Password ambayo hata mkewe haijui ?? Akifa milolongo inakuwa mingi mnooo ya kujitakia tuu. Pesa yenu halafu inaanza kuwatesa.
 
Wajuzi naomba msaada.

Ndugu kafa. Ana akaunti benk ila password hazijulikani pia ana mpesa na pesa zipo ila no password. Mkewe ana death certificate. Atapataje pesa za mmewe? Pia ana cheti cha ndoa.

Msaada
Bank inawezekana iwapo mna vielelezo husika lakini kwa hawa Mpesa duh..!
Sidhani maana wengi mnaona jinsi magumashi yalivyotawala
 
Jamani eh! Tuwapeni pin zetu watu wetu wa karibu ili tutakapodondoka basi inakuwa rahisi kuzifungua simu/bank acc/jf/fb/Twitter etc
Nalog off
 
Mm naona anayepaswa kurithi mali za marehemu kama alikuwa ni mme,basi ni watoto,mke na wazazi nao angalau kama wako na hali duni, kama marehemu ni mke thats obviously mwanaume ni kichwa cha familia. Lakn unakuta kuna hawa ndgu vizabinabina sijui makaka, madada,wajomba hawa ambao hawakushiriki hata kusimamia tu nyumba yako wakat unajenga halafu ukifa nao wanataka share. Naamini wanatakiwa wapewe endapo marehemu alishaweka tamko au ridhio la ndgu zake wengine hao wapate but vinginevyo haipaswi kugombania ili hali unajua kabisa kuna mke,kuna mtoto/watoto au wazazi.
Kwakwel sometimes kama figisu figisu zinafanyika mahakamani watu muhimu wanakosa haki zao za kurithi mali basi ndipo mtu unaona kumbe kuroga kuna faida maana wengine wanatumia mabavu kuonea na kukandamiza haki za wasio na hatia
 
Mleta mada kuwa mfano kati ya ndugu zenu kwa kutotaka hata kijiko kwenye mirathi ya marehemu
 
Was b
Msichoke hela huwa inatoka..fuateni taratibubhusika hasa kesi ilipofanyikia..maana hela huwa inaenda BOT....so ikishaenda hukwo ni jukumu la kuarrange na mahakama iliyokuwa inasikiliza kuwapa uhalali wa malipo ya hela yenu iliyopo BOT
 
Wajuzi naomba msaada.

Ndugu kafa. Ana akaunti benk ila password hazijulikani pia ana mpesa na pesa zipo ila no password. Mkewe ana death certificate. Atapataje pesa za mmewe? Pia ana cheti cha ndoa.

Msaada
Kwanza poleni kwa msiba mkuu.

Fateni taratibu zifuatazo: Kwanza wanafamilia wakae kikao na kuandaa muhtasari wa kikao ambao pamoja na mambo mengine; utampendekeza msimamizi wa mirathi ya marehemu (endapo marehemu hakuacha wosia).

Baada ya hatua hiyo hapo juu, msimamizi wa mirathi ya marehemu aliyependekezwa atapaswa akathibitishwe na Mahakama (endapo hakuna pingamizi), ambapo atapewa 'hati ya usimamizi wa mirathi ya marehemu'. Kama marehemu alikuwa muislamu, mtaenda Mahakama ya mwanzo, kama marehemu alikuwa mkristo basi mtaenda Mahakama ya Wilaya/Mahakama ya hakimu mkazi, lakini kwa Mahakama ya Wilaya/Mahakama ya hakimu mkazi basi kuna maombi maalumu ambayo yanapaswa kuandaliwa na wakili na ndiyo yanapelekwa mahakamani, isipokuwa mkienda Mahakama ya mwanzo ambapo mtajaza tu fomu maalumu.

Viambatanisho muhimu ambavyo msimamizi wa mirathi aliyependekezwa kwenye kikao anatakiwa kuwa navyo ni cheti cha kifo cha marehemu na orodha ya mali za marehemu.

Bilashaka umenielewa mkuu. Karibu ununue Kitabu changu chenye jina; DONDOO MUHIMU ZA NAMNA YA KUKABILIANA NA KESI ZA ARDHI, JINAI, MADAI, MIRATHI NA NDOA HASA KWA WASOMAJI WASIO WANASHERIA NA WANASHERIA WACHANGA:SOMO FUPI LA SHERIA KWA VITENDO. Bei ni TZS 10,000 tu. Nipo Dodoma ila mikoani natuma pia. Au naweza kukutumia softcopy ukipenda. Aksante.
 
Wajuzi naomba msaada.

Ndugu kafa. Ana akaunti benk ila password hazijulikani pia ana mpesa na pesa zipo ila no password. Mkewe ana death certificate. Atapataje pesa za mmewe? Pia ana cheti cha ndoa.

Msaada

Iko hivi
Kaeni Kikao cha Ukoo, Pitisheni Distribution na Namna Mali za Marehemu zitagawanywa kwa wategemezi, Chagueni Msimamizi wa Mirathi, halafu nendeni Kortini.
Korti ikishampitisha Msimamizi wa Mirathi ndio aende huko Vodacom na Nakala yanku thibitishwa kuwa Msimamizi wa Mirathi Pamoja na Barua ya Mahakama, viambatanisho ni Death certificate, Barua ya Form ya Msimamizi wa Mirathi, atapewa hiyo hela na Line ya Simu kufungwa
 
Back
Top Bottom