Hivi mtu akifa na hela zake ziko benki na Mpesa, tukiwa na cheti cha kifo tunaweza fuatilia?

Mambo yote mahakamani.
Wala asiogope .atafute wakili wa kumuongoza atazipata bila wasiwasi.
"Haki ya mtu haipotei"
 
Hazina Tena kwa kujichotea.
Ndo maana huu UTAWALA hauna baraka.
Pesa za marehemu utazichukua vipi?
Kuna mtu alifariki January mwaka jana taratibu zote zikafuatwa na msimamizi wa Marathi na pesa katika bank accounts zote zikapatikana lakini cha ajabu pamoja na kukamilisha kila kitu pesa bado hajapewa mkewe. Anaambiwa zipo hazina hajui tena afanye nini kishajichokea.
 
Umeamkaje na jazba lote hilo sasa Hahahaa.... ukiendelea hivyo utakujaga kufia usingizini haki🤣🤣🤣🤣 Wewe rudi uendelee kusoma Uzi utakutana na mijadala ya huo ubovu. Hata sijashupaa na kubana pua kama unavyodai, tuko kwenye mjadala kawaida tuu. Punguza chuki na jazba, Usikurupuke tena hivyo eeeh! Sawa!?
Wewe unavyodai eti mali ulitafuta na marehem mumeo zitauzwa na warithi kugawana.

Na sheria inasema warithi halali ni mke na watoto. Na wewe mke ndio msimamizi wa mirathi.

Sasa ulikua unatakaje? Kwamba ziuzwe zote upewe peke yako, watoto mliozaa (ambao ni watoto wako pia) wasipate, upate peke yako tu?

Una akili timamu?
 
Baada ya hatua hiyo hapo juu, msimamizi wa mirathi ya marehemu aliyependekezwa atapaswa akathibitishwe na Mahakama (endapo hakuna pingamizi), ambapo atapewa 'hati ya usimamizi wa mirathi ya marehemu'. Kama marehemu alikuwa muislamu, mtaenda Mahakama ya mwanzo, kama marehemu alikuwa mkristo basi mtaenda Mahakama ya Wilaya/Mahakama ya hakimu mkazi, lakini kwa Mahakama ya Wilaya/Mahakama ya hakimu mkazi basi kuna maombi maalumu ambayo yanapaswa kuandaliwa na wakili na ndiyo yanapelekwa mahakamani, isipokuwa mkienda Mahakama ya mwanzo ambapo mtajaza tu fomu maalumu.
Mfiwa pole sana, pata moyo mkuu.

Mwanasheria habari za wakati huu, pole na shughuli.

Kwa nini taratibu - kwa mujibu wa maelezo yako - zinawalazimu Wakristo kupitia kwa Hakimu Mkazi, na kwa mwanasheria, na kupeleka maombi maalum, hatua ambazo ni ndefu, ngumu na za gharama ilhali Muislamu "anajaza fomu tu" mahakama ya mwanzo ?
 
Wewe unavyodai eti mali ulitafuta na marehem mumeo zitauzwa na warithi kugawana.

Na sheria inasema warithi halali ni mke na watoto. Na wewe mke ndio msimamizi wa mirathi.

Sasa ulikua unatakaje? Kwamba ziuzwe zote upewe peke yako, watoto mliozaa (ambao ni watoto wako pia) wasipate, upate peke yako tu?

Una akili timamu?

Achana na hizo ETI zako buana.

Huu ni mjadala uko jukwaani kujadiliwa, kila mmoja anajifunza na kutoa kile anachojua. Sasa shida yako hapo ni nini? Au shida ni comment ya mama D😎

Mimi akili timamu ninazo kabisa ndio maana napost ninachokijua na kusoma majibu kufahamu yale nisiyoyajua... ila naona kwa jazba hili kama zako haziko timamu halafu hata hujioni😂😂😂

Heri ya mwaka mpya 2021
 
Unajishebedua tu baada ya kugundua kuwa ulitia boko.
We kubali kuwa uliandika pumba. Uwe unauliza kwanza kama kitu hujui.
 
Mfiwa pole sana, pata moyo mkuu.

Mwanasheria habari za wakati huu, pole na shughuli.

Kwa nini taratibu - kwa mujibu wa maelezo yako - zinawalazimu Wakristo kupitia kwa Hakimu Mkazi, na kwa mwanasheria, na kupeleka maombi maalum, hatua ambazo ni ndefu, ngumu na za gharama ilhali Muislamu "anajaza fomu tu" mahakama ya mwanzo ?
Swali zuri. Habari za wakati huu ni njema, na asante sana kwa kunipa pole ya majukumu, pole na kwako pia mkuu.

Kimsingi, huo ni utaratibu tu uliowekwa kisheria bila kujali misingi ya udini; kwamba kwasababu ni waislamu basi wawe na taratibu nyepesi, na wakristo wawe na mlolongo mrefu, ingeweza hata kuwa vice-versa. Hata hivyo, mawakili hawaruhusiwi kutoa uwakilishi katika Mahakama za Mwanzo, na ndiyo maana ukiwa na kesi Mahakama ya mwanzo ukataka kuweka wakili basi ni sharti uombe kuhamisha kesi hiyo iende Mahakama ya Wilaya/Mahakama ya hakimu mkazi.

Nilisahau kumalizia kwenye comment yangu ya msingi, kwamba akishapata ile hati ya usimamizi wa mirathi kutoka Mahakamani basi ataandika barua na kuipeleka kwenye mtandao husika wa simu huku akiiambatanisha hati yenyewe. Fedha zitatolewa na atapatiwa msimamizi wa mirathi kwa minajili ya kuzigawa kwa warithi wa marehemu. Asante.
 
Hivi wanakulipa fees hawa?

Mbona unajitutumua sana?
 
Hivi wanakulipa fees hawa?

Mbona unajitutumua sana?
Mkuu, Biblia Takatifu kwenye 1 Petro 4:8 na Warumi 12 inatufundisha kwamba "Kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, aitumie kwa kumuhudumia mwingine, kama wakili mwema wa neema mbalimbali za Mungu".

Naamini mimi kuwa Mwanasheria wala siyo kwa akili zangu mwenyewe bali ni kwa uweza wa Mungu, hivyo sinabudi kuwahudumia wengine.

Pesa zipo tu mkuu. Na Biblia hiyohiyo kwenye Kitabu cha Yoshua Bin Sirra inatufundisha kwamba, "yoyote autafutaye utajiri kwa nguvu hataupata".

Uwe na j2 njema mkuu.
 
Unajishebedua tu baada ya kugundua kuwa ulitia boko.
We kubali kuwa uliandika pumba. Uwe unauliza kwanza kama kitu hujui.
Watu huwa wanaulizie chumbani?
Nenda taratibu mwaka ndio kwanza umeanza huu
 
Mimi nilishaufanya mchakato huo nikiwa msimamiz wa mirathi. Death Certificate ni ka document kamoja tu, unapoenda huko M pesa au Bank kufatilia pesa unapaswa uwe na Document ya Kikao cha Familia kilichokuteua kuwa msimamiz wa mirathi, Uwe na nakala Za hukumu ya Mahakaman nk.

Hapo kama kaacha Mke inabidi ndio afatilie. Wewe kama aliyefariki ni kaka yako tambua kuwa huna sifa ya kuwa mrithi kabisa kisheria.Warithi halali hapo ni Mke na Watoto na Wazazi wa Marehem.
Hivi mfano nikifanya Huyo mchakato kumne MPesa ameacha 500 si hasara Hiyo!?

au inajulikana kwanza kiasi ndo hatua zinafuata?
 
Swali zuri. Habari za wakati huu ni njema, na asante sana kwa kunipa pole ya majukumu, pole na kwako pia mkuu.

Kimsingi, huo ni utaratibu tu uliowekwa kisheria bila kujali misingi ya udini; kwamba kwasababu ni waislamu basi wawe na taratibu nyepesi, na wakristo wawe na mlolongo mrefu, ingeweza hata kuwa vice-versa.
Sheria umesema inaangalia dini yako kujua ufuate utaratibu gani. Halafu hapo hapo unasema utaratibu huu haujali misingi ya kidini. Huoni kwamba unaji contradict ?

Na unasema sheria imewekwa hivyo mlolongo wa Wakristo uwe mrefu...

Hukumuuliza professa wako chuoni KWA NINI MLOLONGO WA WAKRISTO UMEWEKWA UWE MREFU ???

Nimekuvumilia nimeshindwa ustaarabu. Umesoma wapi shule wewe schmucko ???
 
Fuateni taratibu zote za kuteua msimamizi wa mirathi. Ikiwemo pia kwenda mahakamani.

Mahakama ikishatoa nyaraka za kumteua msimamizi wa mirathi, huyo ndiye atakayefuatilia kwa bank na kampuni ya simu ili kupata pesa.

Kumbuka kuwa jukumu la msimamizi wa mirathi ni kutambua na kukusanya mali na madeni yote ya marehemu. Jukumu la pili ni kugawa mali kwa warithi halali kisheria.

Hivyo, Msimamizi wa mirathi atakayeteuliwa ndiye atakayefuatilia na kupewa hizo pesa. Naye atazigawa kwa warithi halali kwa mujibu wa sheria.

Kwa suala lako, ingependeza huyo mke ndio apewe usimamizi wa mirathi.

mkuu mimi baba yangu alikufa hivyo baba mkubwa ndie aliye kuwa msimamizi wa mirathi na mpaka sasa hakuna kina kinacho endelea licha ya mam kusem kuwa baba alituekea watoto wake fedha benk ambazo zingetusaidia pindi tutapo anza elimu ya juu ila mpaka sasa nipo mwaka wa mwisho chuo na sijajua ni jinsi gani ningeweza kufatilia hizo fedha benk licha ya kwamba ninacho cheti cha kifo cha baba
 
Hivi ni kwamba tunakosa watu sahihi wa kuoa/kuolewa nao mpaka tunashindwa kushare vitu muhimu kama hivyo vya kipesa?
 
mkuu mimi baba yangu alikufa hivyo baba mkubwa ndie aliye kuwa msimamizi wa mirathi na mpaka sasa hakuna kina kinacho endelea licha ya mam kusem kuwa baba alituekea watoto wake fedha benk ambazo zingetusaidia pindi tutapo anza elimu ya juu ila mpaka sasa nipo mwaka wa mwisho chuo na sijajua ni jinsi gani ningeweza kufatilia hizo fedha benk licha ya kwamba ninacho cheti cha kifo cha baba
Sio kwamba mmeshatapeliwa?
 
Back
Top Bottom