Sisemi hesabu is nothing, nacholalamika ni kwa nini kila mtu alazimishwe kuisoma na ifanywe kizingiti kwenye michakato ya kielimu wakati application yake sio ya muhimu kiivyo, Ni ya muhimu sana tena sana lakini does every one need to master it? kwani kila mtu anatengeneza ndege au meli? au kila mtu ni medical technician?
hata kama, madaktari na mafamasia kwenye mahospitali yetu wanatumia hisabati gani wakati wanatuhudimia, watakupima uzito na ulefu labda basi, why calculus? hata numerical presentation ya vipimo vyao haitusaidii wagonjwa chochote kile ni vague technical and medical industry centered jargons, hata leo wakina newton wakija ukawaambia wanamalaria 3 watabaki kushangaa,
naendelea kuuliza, kwa nini? watoto wetu wanafeli darasa la saba sababu wameshindwa kutafuta kigawe kidogo cha shirika, au eneo la nusu mlinganyo, hata wale waliofaulu, ufahamu wa kubadirisha desimali kuwa sehemu unawasaidia nini immedietly baada ya masomo yao au lately wakati wa uzee wao?
shilingi milioni 700,000,000 zilizofichwa na Mary Mramba katika kabati nyumbani kwake
Nadhani hapo ndipo kwenye mzizi wa tatizo hili. Walimu wengi hawafundishi kwa kuelezea nadharia zenyewe na namna unavyoweza kuzitumia katika maisha ya kila siku, badala yake wanafundisha namna ya kujibu maswali ya kwenye mtihani.
Hata mifano inayotumiwa kuelezea nadharia hizo wakati mwengine inakosa uhalisia wa mazingira yaliyomzunguka mwanafunzi. Walimu wanakosa ubunifu wakati wa kutumia vitabu vya kufundishia na kukosa kuvijenga kuendana na mazingira yaliyomzunguka mwanafunzi.
Naamini tatizo lipo kwenye aina ya walimu wanaopelekwa huko mashuleni. Mwalimu wa shule ya msingi ni yule aliyefeli (almost) Form four. Anafundishwa kidogo, anakabidhiwa darasa. Hatuwezi kutarajia maajabu kutoka kwa walimu hawa hususan wanapotakiwa kufundisha wanafunzi 80 kwenye darasa moja.
Mimi nilikuwa home-schooled (almost kwa primary school) na nadharia zote za hisabati zilikuwa customized wakati wa kuzieleza kuendana na interests zangu na vitu ninavyovijua vyema, hivyo ilikuwa rahisi sana ku-relate na maisha ya kila siku. Na kuweza ku-relate na maisha ya kila siku, kulinifanya niwe na interest na hisabati.
Ninachotaka kusema ni kuwa, interest na uelewa wa mtoto kwa somo la hisabati unachangiwa na mambo mengi, ikiwemo walimu, vitabu na mazingira ambayo kimsingi kwa Tanzania katika yote hayo tumepwaya sana.
mkuu zakumi,
ni kweli nimepata mafanikio mazuri kutokana na hayo mambo, na imenisaidia si tu kujenga hoja vizuri, bali imenipa busara, hekima, heshima, na kuwa na mipango mizuri katika maisha yangu ya kila siku, si hayo tu imenijenga kuwa mdadisi mfuatiliaji na mtekelezaji mzuri na wa umakini wa mipango yangu. imenijenga kuwasoma watu kuwaelewa watu na kuishi na watu kwa namna ya busara. and never to take things for granted.
si lazima watanzania wapitie njia kama yangu ila ni muhimu kama inawezekana,( na inawezekana) mafanikio sio jambo nilitakalo mimi tu ni kitu watu wote wanatamani kukipata.
nafikiri zaidi ya yote tuliyoyaonge masomo mengi yanavyofundishwa hapa kwetu ni kukopi na komeza na kutapika kwa ajili ya mitihani. hili ni kosa kubwa sana. ndio maana waajiri wanalalamika kuwa watu wanatoka chuoni hawana kitu si kweli hawana ila wameshasahau kutokana na usomaji wa kukariri akimaliza pepa usiku muulize chochote hana kashatema katika mtihani na kamalizana nalo. hapa mtu huyu hawezi kuwa mbinifu wala mtu wa kutafakari na kutumia ujuzi na uelewa wake katika maisha yake ya kila siku.
sasa tukibadili mfumo huu na kuwa na mfumo wa kuelewa na sio kuangalia A's basi taifa litabadilika.
Ndo maana kuna post yako moja umesema waajiri watahitaji angalau mtu aliyepata D kwenye hesabu katika mtihani wake wa O-level, katika hali halisi mtu aliyepata D O-level hawezi kuwa anajua Calculus na mahesabu mengine magumu magumu kama vector space, na majometri ya ajabu ajabu sana sana atakuwa anajua tu hesabu basic na milinganyo rahisi rahisi yenye single variable pamoja na hesabu zingine za Magazijuto na vijometri ya kutafuta maeneo pamoja na mizingo kitu ambacho utaweza kukitumia kujua hata ukitaka kujenga tank lako la maji lenye ujazo wa lita elfu ishirini basi liwe na vipimo gani, sasa mkuu wangu unataka tuwe na kizazi ambacho hata ukimwambia akufanyie tathmini ya tofali utakazotumia kujenga kibanda cha bati 30 anaanza kushangaa hata hajui aanzie wapi.
Tafadhali mkuu tunataka angalau basi watu waliopata D sio lazima wenye kujua mahesabu magumu ambayo mengi yanatumika kwenye engineering design.
Gaijin:
Now we converge. Nyumbani ulikuwa unafundishwa kwa kutumia mifano ya dunia yako ya ufahamu, so your home instructor was cultivating your ability to think critically naturally.
We, on the other hand, who attended public schools didn't have that luxury and we are punished for that. I am punished because I failed to answer a simultaneous equation. However, in book keeping, counting money, construction of simple building etc and in our daily lives we don't use simultaneous equations or her cousin quadratic. So why is that a big deal?
Please refer the dialog below between the great philosopher Socrates and a slave boy.
Halving a square
Naomba kusahihishwa kama nakosea, nimejaribu kuupitia tena huu uzi na nachokiona katika hoja za wengi ni majadiliano katika "mfumo mbovu" wa elimu katika Taifa letu, mfumo usiomsaidia au kumjenga mwanafunzi katika kufikiri, mfumo usioshabihiana na mazingira yetu na labla jingine ambalo halijajadiliwa sana ni nafasi ya lugha katika kutoa hiyo elimu.
Kama hayo ni sahihi then ndio sababu ya hesabu kuwa "nightmare" kwa watanzania wengi.
Ndo maana kuna post yako moja umesema waajiri watahitaji angalau mtu aliyepata D kwenye hesabu katika mtihani wake wa O-level, katika hali halisi mtu aliyepata D O-level hawezi kuwa anajua Calculus na mahesabu mengine magumu magumu kama vector space, na majometri ya ajabu ajabu sana sana atakuwa anajua tu hesabu basic na milinganyo rahisi rahisi yenye single variable pamoja na hesabu zingine za Magazijuto na vijometri ya kutafuta maeneo pamoja na mizingo kitu ambacho utaweza kukitumia kujua hata ukitaka kujenga tank lako la maji lenye ujazo wa lita elfu ishirini basi liwe na vipimo gani, sasa mkuu wangu unataka tuwe na kizazi ambacho hata ukimwambia akufanyie tathmini ya tofali utakazotumia kujenga kibanda cha bati 30 anaanza kushangaa hata hajui aanzie wapi.
Tafadhali mkuu tunataka angalau basi watu waliopata D sio lazima wenye kujua mahesabu magumu ambayo mengi yanatumika kwenye engineering design.
Nchi zote za ulaya zilikuwa zinajifunza kwa kutumia kilatini. Na kama wangeendelea kutumia lugha sijuhi kama wangeweza kufika walipo sasa.
Tatizo hatujahamua kuwa tunaweza kuwa na maarifa katika lugha zetu.
bado nasisitiza ni kutokujua ndio kunasababisha hatuipi kipaumbele falsafa katika maisha yetu ya kila siku. angalia mfn ufuatao,
matatizo ya kijamii - yanapelekea critical thinking - inapelekea application of different solns mojawapo ni hesabu halafu suluhu ya matatizo.
hapa unafikiri kipi ni muhimu kusisitizwa kufundishwa, critical thinking ndyo inayoleta hesabu kutumika if necessary.
haya ni mawazo yangu.
Zakumi
Hizi mambo za kufikiria kwamba tunaweza tukafanya any break through kwa kutumia lugha yetu huwa sielewi misingi yake ni nini? kwamba tufundishe Physics au Biliogia au chemistry kwa Kiswahili? Haiwezekani, kama tunataka kufanya hivyo basi tuhakikishe kwamba tumejiandaa na tuwe na dhamira ya dhati ya kufanya utafiti, ama sivyo hauwezi kufundisha kwa lugha yako mambo ambayo haujayagundua wewe.
Nani kasema haiwezekani? Mbona wengine wanaweza? Wachina,wajapan, wajeruman, waspain na wengine wengi tu, infact haya tunayofundishwa kwa kiingereza who told u that they were invented by britons? Hesabu, sayansi, philosophy, literature, n.k yalianzia kwa ancient Egyptians na yakapata mwendelezo mzuri na wagiriki, mbona lugha za ancient egyptian au hellenic hatuzioni zikitumika kufundishia vitu walivyogundua wao?
Your argument is fallacious Mkuu!
what stages are those? for a man to develop into his full potential he has to go through proper guidance throughout his life.Si lazima uwe na mwalimu mzuri katika kila stage. Kwa nchi kama Tanzania or for that matter, any other African country, itabidi uchukuwe wajanja wote wakafundishe.
Katika makuzi ya mtoto kuna critical period ambacho mtoto au mwanafunzi anatakiwa awe na watu makini wa kumfundisha. Katika kipindi hicho, wanafunzi wengi wa Tanzania wanakuwa wanasahauliwa.
Sielewi focus yetu ni nini? sababu kama unakubali kwamba wajerumani, waegypt,wagiriki nk wamefanya inventions na lugha zao hazitumiki kufundishia ntakuuliza why would you want to use your own language then?
why exactly do we want to use swahili in teaching? what do we want to achieve? want to do it for fun?, then, were the egyptian invention made in briton or american? au wagiriki did they use english?
Ndio maana nasema vitu ambavyo haujavindua wewe unalazimika kutumia lugha za wagunduzi kufundishia, unaweza ukasema kama ni hivyo kwa nini hatutumii lugha za kigiriki kufundishia mambo yaliyogunduliwa na wagiriki, the answer is simple. who has put our education system in place? ama sivyo pia zipo evidence nyingi tu kwamba kwa yaliyogunduliwa na wagiriki hata waingereza wanafundisha kwa kigiriki.
au tujadiri why english is a world language?