Sangarara
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 13,100
- 5,649
- Thread starter
- #21
Ile misingi inayotumika katika kujenga hoja wakati wa kuprove theorem ndiyo msingi inayotumika pia katika kujenga hoja ya kutatua matatizo mengine ya kijamii. Usichukulia reproduction ya material bali angalia application ya methods. Mathematician mzuri siyo mkurupukaji katika mambo yake; kila jambo analiangalia kwa makini na kina sana. Huo utamadunbi wa kuangalia mambo kwa kina ndio unawafanya wawe na mtazamo mpana sana wa kila jambo na hata katika mambo ya jamii. Utashangaa kuwa mathematician aliyeiva hawezi kukubali kuwa 3+1.0=4, ingawa watu wa kawaida wanaojua hesabu za kukokotoa tu watamshangaa.
Umesema vyema sana, "Mathematician Mzuri" kama haya mambo unayoyasema yanafanywa na mathematicians kwa nini kila mtu apitishwe kwenye tanuru la hesabu? wewe mwenyewe lini katika maisha yako uliishakutana na senerio iliyokufanya utumie logarithm.
Alafu umesema vyema zaidi "watu wa kawaida", kwa nini na watu wakawaida wanyimwe nafasi za kwenda chuo kikuu kwa sababu wamefail hesabu? why?