Hisabati/mathematics nightmare

Penye nia, pana njia.

Wewe hutakiwi ukate tamaa mara moja hivyo. Hata hapa tulipo wengi wetu hatuielewi vyema lugha yetu. Kwa nini basi usitumie ukumbi huu kutushushia darsa kama ulivyotaka kufanya kwenye hiyo website yenu?

Naamini, kazi yako ikionekana, washirika wenye nia ya dhati watajitokeza

Nilichotaka kufanya ni kile waChina, Wajapan walichofanya. Kutafsiri vitabu muhimu katika lugha zao hili kila mtu apitie. Kwa sasa hivi uzee umeingia na sina muda wa kutosha. Hivyo ninawaachia kizazi kipya cha bongo flava kuendeleza.
 
Gaijin
Hizi takwim zinapatikana wapi? au umezitengeneza hapa kwa ajili ya kujenga hoja? msingi wa kelele zangu ni kwamba hata wale wanaotakiwa kutengeneza takwimu za namna hii for public consumption hawatengenezi so what bother us with mathematics?

Sangarara,

Hoja zako ni muhimu sana. Mfumo wa elimu Tanzania ni mfumo wa kikoloni. Kila binadamu ana haki ya kuelimisha na ujanja wa hisabati haufanyi mtu kuwa critical thinker.

Na watu wengi waliosoma math, science, engineering wako one dimensional. Maisha sio kuwa one dimensional/
 
Somebody needs to be a critical thinker to know that we don't think critically. I believe, correct me if I am wrong, there are things that you can't teach in school, one of them critical thinking.

Watanzania au for that matter waafrika, tumejenga mashule kwa kuiga lakini mashule haya hayana mazingira ya kutoa elimu ambayo ina manufaa kwa yule anayekwenda shule.

mkuu zakumi,
si kweli kuwa kutafakari kwa kina hakufundishiki. kusingekuwapo na masomo haya ya critical thinking, au logic katika falsafa. kuna namna mtu anajengwa kujihoji, kuhoji na kutafakari kauli, matendo, mambo, vitu kwa kina na umakini.
kutafakari kwa kina kunafundishwa na wapo wataalam katika fani hizo. na critical thinking kama masomo mengine yanaweza yakarahisishwa katika level ya primary na kuendelea kuboreshwa kwa kadri madarasa yanavyopanda juu.

kuhusu suala la pili la wafrika kujenga shule lakini haitupi manufaa si kwamba shule tulizonazo hazitusadii kabisa ila haziboreshwi kukidhi mahitaji yetu, na bado zinatujenga kuwa tegemezi kwa maaana ya kuajiriwa na sio kuelimika kwa asilimia 100. mf engineering ya kibongo ni kufanya maintainance sio kutengeneza vitu vipya, sasa kama tunajengwa kufanya maintanance je sio bado tunatayarishwa kupokea vya kutoka majuu ili sisi tuje kuvitengeneza vinapoharibika.

hawa wanaotengeneza mitaala wakitengenezewa mitaala bila kuingalalia mara mbilimbili ndio tunaishia hapa tulipo, wazungu hawapendi kabisa sisi tufunguke kiakili wanajua tukifanya hivyo habari kwao itakuwa imekwisha maana ujinge wetu kwao ni utajiri. ni jukumu letu kuetengeneza mitaala inayotufaa na kutusaidia kuwa na maendeleo.
 
Nilichotaka kufanya ni kile waChina, Wajapan walichofanya. Kutafsiri vitabu muhimu katika lugha zao hili kila mtu apitie. Kwa sasa hivi uzee umeingia na sina muda wa kutosha. Hivyo ninawaachia kizazi kipya cha bongo flava kuendeleza.

Hii idea ni nzuri sana, tafuta mtu umkabidhi, isipotee bure.

I'm very curious kuona vitabu gani vinaingia kwenye list ya vitabu hivyo muhimu.

Tutajie vilivyokuwa kwenye list yako
 
IL,

shule inakufanya uwe organized and systematic, but the ability to think critically is yours naturally. Visit a remote area in Tanzania where formal education is in short supply and ask people there questions about their world. They might surprise you with their answers and how they draw their conclusions. However, the same people wouldn't be well versed to answer world events such as the election in America because they have no knowledge or use of it.

Nilisoma nje ya Tanzania katika nchi ambayo CHESS ni mchezo wa taifa. They believe that playing chess improves ones ability to think critically. In my classes, many examples were revolving around the game of chess. Being a person who didn't play chess, I had tough life and they probably thought I was the dumbest person in my class. I wasn't.

Wanafunzi watanzania hawana waalimu mashuleni na masomo hayafundishwi ipasavyo. Hivyo sioni sababu ya kuzua issue ya critical thinking wakati knowledge hawana.
 
Kimsingi Zakumi yuko sahihi, hayo mambo ya critical thinking, falfasa hata maths ni kama vilabu vya pombe, wanaoyang'ang'ania na kuyatukuza ni wale ambao wanaelewa vocabrary zake ama sivyo hayamake sense hata kwao wenyewe.

Kwa mfano falfasa, nashindwa kuitofautisha na clabu ya watu waliofundishwa misingi fulani ya kubishana, ndio maana utamsikia mtu anauliza umesoma somo la argumentation basics sijui nini na nini, ndio maana hata sheria, somo la msingi kabisa katika maisha yetu lakini na lenyewe limekuwa compricated kwa kuwekewa legal language ili tu liwe for the few.
 
Katika mfumo wa uingereza, vitabu vya hesabu vina mifano michache na kumwachia mwanafunzi sehemu kubwa kujibu maswali mwenyewe. Lengo lao ni kumfanya mwanafunzi atumie muda kufikiri. Mfumo huu umeigwa na nchi zilizo tawaliwa. Kwa waliosoma Tanzania, wanaelewa kuwa ni kawaida kwa mwalimu kufundisha kwa kutumia kitabu fulani na kutoa maswali kutoka kitabu kingine.

Kwa watu waliosoma nchi za mashariki, asia na Marekani, wanaelewa kuwa kuna vitabu vya mazoezi ambavyo vina maswali na majibu. Mwanafunzi hafichwi kitu. Kama anazo juhudi za kuelewa, kila kitu anapewa. Kwa kufanya hivi nchi hizi ziliweza kufunga pengo (gap) la elimu kwa kipindi kifupi sana.

Vitabu ambavyo tuli-plan vilikuwa ni kuondoa hiyo complication ya mwingereza.
 
sasa nafikiri unaanza kukubaliana na mimi kuwa cha msingi katika hesabu ni kule kufikiri anakojengwa mtu fikra nzito iliyozama katika kutafuta ufumbuzi. ndio cha msingi zaidi.
 
Kimsingi Zakumi yuko sahihi, hayo mambo ya critical thinking, falfasa hata maths ni kama vilabu vya pombe, wanaoyang'ang'ania na kuyatukuza ni wale ambao wanaelewa vocabrary zake ama sivyo hayamake sense hata kwao wenyewe.

Kwa mfano falfasa, nashindwa kuitofautisha na clabu ya watu waliofundishwa misingi fulani ya kubishana, ndio maana utamsikia mtu anauliza umesoma somo la argumentation basics sijui nini na nini, ndio maana hata sheria, somo la msingi kabisa katika maisha yetu lakini na lenyewe limekuwa compricated kwa kuwekewa legal language ili tu liwe for the few.

mkuu,
kwanza umekubali kuwa kumbe mtu anaweza akafundishwa misingi ya kubishana, basi watu wanaweza wakafundishwa misingi ya kutafakari kwa kina cha hali ya juu vilevile.
falsafa ina mengi zaidi ya huko munakokuita kibishana, falsafa haijawekwa ili watu wawe wabishi, bali wasikubali vitu ovyoovyo pasipo kujiridhisha kuwa na ukweli ama mantiki. lakini pia inamjenga mtu kutafakari na kujiuliza uliza mambo mbalimbali ni kitu kizuri na kinafundishika sijui kwa nini mnaona hakifundishiki. nakuhakikishia wale waliobahatika kusoma masomo hayo wanaweza kukueleza utofauti walionao sasa kulinganisha na walivyokuwa kabla hawajasoma falsafa. mimi nimebahatika kusoma mambo mengi ya falsafa na kupitia kazi za wanafalsafa wengi kwa kweli imenibadilisha. sibishani eti kwa sababu nabishana nasikiliza kwa makini, natafakari, najenga hoja. na nakubali kukosolewa na kueleweshwa lakini natafakari haya wanayonipa watu kwa kina kabla ya kuyachukua. hata mitazamo katika masuala mbalimbali ya kijamii nayaona katika mtazamo tofauti kabisa. na katika falsafa kuna mambo mengi sanaaaaaaaaaaa.
 
IL,

shule inakufanya uwe organized and systematic, but the ability to think critically is yours naturally. Visit a remote area in Tanzania where formal education is in short supply and ask people there questions about their world. They might surprise you with their answers and how they draw their conclusions. However, the same people wouldn't be well versed to answer world events such as the election in America because they have no knowledge or use of it.

Nilisoma nje ya Tanzania katika nchi ambayo CHESS ni mchezo wa taifa. They believe that playing chess improves ones ability to think critically. In my classes, many examples were revolving around the game of chess. Being a person who didn't play chess, I had tough life and they probably thought I was the dumbest person in my class. I wasn't.

Wanafunzi watanzania hawana waalimu mashuleni na masomo hayafundishwi ipasavyo. Hivyo sioni sababu ya kuzua issue ya critical thinking wakati knowledge hawana.

kiongozi,
si lazima uwe na knowledge ndio ufundishwe falsafa mana yenyewe inakupa misingi ya wewe kupata hiyo knowledge, na yenyewe yaweza kuwa ni knowledge tosha. mfn. mwalimu anawafundisha watoto jinsi ya kutambambua kauli zilizo jengwa vizuri na zikawa na utata ndani yake unaoweza kuzua matatizo ya uelewa ama utekelezaji, sasa hapa mwanafunzi haitaji kuwa ana PHD ya chochote kujengwa kuwa mzuri katika hilo. falsafa ndio msingi wenyewe wa ufahamu na uelewa wa mambo.
mfn mtu anasema bila woga wanawake wote ni wavivuwavivu, kama mtu amejengwa kujiuliza ataanza kuhoji na kuchanganua na akaja na majibu yake.
isipokuwa sasa ukiwa na uelewa mkubwa wa mambo, well informed unaweza kuwa mzuri zaidi katika falsafa. kujenga hoja mbalimbali.
 
Ukishapanua uwezo wako wa kufikiri, hata katika kilimo cha maembe mwanga hesabu hutaiacha
Maamuzi sahihi zaidi yanakuja baada ya uwezo wa kufikiri na kuchambua mazingira kimamilifu
Na hesabu husaidia katika hilo

hivi kweli mwanakijiji kama hisabati ni kitu muhimu namna hivyo kwa nini ihitajike mpaka iandikiwe ndio watu waone umuhimu wake? any way ukiandika usisahau kutukumbusha namna tunavyotumia calculus kwenye kilimo cha umwagiliaji huku mfindi.
 
Nilichotaka kufanya ni kile waChina, Wajapan walichofanya. Kutafsiri vitabu muhimu katika lugha zao hili kila mtu apitie. Kwa sasa hivi uzee umeingia na sina muda wa kutosha. Hivyo ninawaachia kizazi kipya cha bongo flava kuendeleza.

For minute there nilidhani unataka kutafsiri kazi muhimu za fasihi kwa Kiswahili ili kitanua usomaji wa fasihi kwa Kiswahili mbali na faida nyengine.

Nilidhani tukae tusubiri kuona vitabu vyenye majina haya kwenye tovuti yako "Kosa na Adhabu", "Kaka Karamazov", "Sanaa ya vita", "Kisa cha Miji Miwili", "Wanawake wadogo"... :)

Kuhusu vitabu vya hesabati, sijui vya primary schools, ila vya sekondari vina majibu yameandikwa nyuma. Ni kweli kuwa havionyeshi njia ya kufikia majibu hayo, ila majibu yapo.
 
mkuu zakumi,
sasa nafikiri unaanza kukubaliana na mimi kuwa cha msingi katika hesabu ni kule kufikiri anakojengwa mtu fikra nzito iliyozama katika kutafuta ufumbuzi. ndio cha msingi zaidi.

Nope. Kwanini katika mfumo wa kiingereza mwalimu anataka kuficha vitu ambavyo tayari vimevumbuliwa? Cha kushangaza ni kuwa mwalimu mwenyewe hajavumbua chochote kipya?

Katika shule za Tanzania, mwalimu anakupa reference zaidi ya 10 kwenye somo moja na hujui kwenye mtihani maswali yatatoka wapi.

Marekani, Nchi za Ulaya ya kati na mashariki, Nchi za Asia, vitu vyote viko nje nje. Unaambiwa katika somo hili tunatumia kitabu hiki na kila kitu kitatoka humo humo.

Critical thinking hipo lakini inai-overrate.
 
For minute there nilidhani unataka kutafsiri kazi muhimu za fasihi kwa Kiswahili ili kitanua usomaji wa fasihi kwa Kiswahili mbali na faida nyengine.

Nilidhani tukae tusubiri kuona vitabu vyenye majina haya kwenye tovuti yako "Kosa na Adhabu", "Kaka Karamazov", "Sanaa ya vita", "Kisa cha Miji Miwili", "Wanawake wadogo"... :)

Kuhusu vitabu vya hesabati, sijui vya primary schools, ila vya sekondari vina majibu yameandikwa nyuma. Ni kweli kuwa havionyeshi njia ya kufikia majibu hayo, ila majibu yapo.

Literature isn't my strength. Hisabati ni somo ambalo mwanafunzi mwenye juhudi anaweza kujisomea mwenyewe. Lakini hutunzi wa vitabu vya hisabati Tanzania doesn't take advantage of our ability to think critically naturally.

Nilipokuwa Tanzania wanafunzi walikuwa wanalalamika kuwa equations zenye variables x, y, etc hazina maana katika maisha yao. Wanasoma kujibu mitihani ili waendelee mbele. Lakini wanashindwa ku-correlate wanachosoma na mazingira yao.
 
kiongozi,
si lazima uwe na knowledge ndio ufundishwe falsafa mana yenyewe inakupa misingi ya wewe kupata hiyo knowledge, na yenyewe yaweza kuwa ni knowledge tosha. mfn. mwalimu anawafundisha watoto jinsi ya kutambambua kauli zilizo jengwa vizuri na zikawa na utata ndani yake unaoweza kuzua matatizo ya uelewa ama utekelezaji, sasa hapa mwanafunzi haitaji kuwa ana PHD ya chochote kujengwa kuwa mzuri katika hilo. falsafa ndio msingi wenyewe wa ufahamu na uelewa wa mambo.
mfn mtu anasema bila woga wanawake wote ni wavivuwavivu, kama mtu amejengwa kujiuliza ataanza kuhoji na kuchanganua na akaja na majibu yake.
isipokuwa sasa ukiwa na uelewa mkubwa wa mambo, well informed unaweza kuwa mzuri zaidi katika falsafa. kujenga hoja mbalimbali.

IL,

Correct me if am wrong. Inaonyesha umepata mafanikio makubwa katika elimu. Na masomo kama logic, falsafa, na critical thinking yamekufanya uelewe kujenga hoja vizuri.

Hivyo kwa mtazamo wako, ni lazima watanzania tupitie njia kama yako hili tuweze kujenga hoja.
 
Literature isn't my strength. Hisabati ni somo ambalo mwanafunzi mwenye juhudi anaweza kujisomea mwenyewe. Lakini hutunzi wa vitabu vya hisabati Tanzania doesn't take advantage of our ability to think critically naturally.

Nilipokuwa Tanzania wanafunzi walikuwa wanalalamika kuwa equations zenye variables x, y, etc hazina maana katika maisha yao. Wanasoma kujibu mitihani ili waendelee mbele. Lakini wanashindwa ku-correlate wanachosoma na mazingira yao.

Nadhani hapo ndipo kwenye mzizi wa tatizo hili. Walimu wengi hawafundishi kwa kuelezea nadharia zenyewe na namna unavyoweza kuzitumia katika maisha ya kila siku, badala yake wanafundisha namna ya kujibu maswali ya kwenye mtihani.

Hata mifano inayotumiwa kuelezea nadharia hizo wakati mwengine inakosa uhalisia wa mazingira yaliyomzunguka mwanafunzi. Walimu wanakosa ubunifu wakati wa kutumia vitabu vya kufundishia na kukosa kuvijenga kuendana na mazingira yaliyomzunguka mwanafunzi.

Naamini tatizo lipo kwenye aina ya walimu wanaopelekwa huko mashuleni. Mwalimu wa shule ya msingi ni yule aliyefeli (almost) Form four. Anafundishwa kidogo, anakabidhiwa darasa. Hatuwezi kutarajia maajabu kutoka kwa walimu hawa hususan wanapotakiwa kufundisha wanafunzi 80 kwenye darasa moja.

Mimi nilikuwa home-schooled (almost kwa primary school) na nadharia zote za hisabati zilikuwa customized wakati wa kuzieleza kuendana na interests zangu na vitu ninavyovijua vyema, hivyo ilikuwa rahisi sana ku-relate na maisha ya kila siku. Na kuweza ku-relate na maisha ya kila siku, kulinifanya niwe na interest na hisabati.

Ninachotaka kusema ni kuwa, interest na uelewa wa mtoto kwa somo la hisabati unachangiwa na mambo mengi, ikiwemo walimu, vitabu na mazingira ambayo kimsingi kwa Tanzania katika yote hayo tumepwaya sana.
 
ni kweli nimepata mafanikio mazuri kutokana na hayo mambo, na imenisaidia si tu kujenga hoja vizuri, bali imenipa busara, hekima, heshima, na kuwa na mipango mizuri katika maisha yangu ya kila siku, si hayo tu imenijenga kuwa mdadisi mfuatiliaji na mtekelezaji mzuri na wa umakini wa mipango yangu. imenijenga kuwasoma watu kuwaelewa watu na kuishi na watu kwa namna ya busara. and never to take things for granted.

si lazima watanzania wapitie njia kama yangu ila ni muhimu kama inawezekana,( na inawezekana) mafanikio sio jambo nilitakalo mimi tu ni kitu watu wote wanatamani kukipata.
 
Nadhani hapo ndipo kwenye mzizi wa tatizo hili. Walimu wengi hawafundishi kwa kuelezea nadharia zenyewe na namna unavyoweza kuzitumia katika maisha ya kila siku, badala yake wanafundisha namna ya kujibu maswali ya kwenye mtihani.

Hata mifano inayotumiwa kuelezea nadharia hizo wakati mwengine inakosa uhalisia wa mazingira yaliyomzunguka mwanafunzi. Walimu wanakosa ubunifu wakati wa kutumia vitabu vya kufundishia na kukosa kuvijenga kuendana na mazingira yaliyomzunguka mwanafunzi.

Naamini tatizo lipo kwenye aina ya walimu wanaopelekwa huko mashuleni. Mwalimu wa shule ya msingi ni yule aliyefeli (almost) Form four. Anafundishwa kidogo, anakabidhiwa darasa. Hatuwezi kutarajia maajabu kutoka kwa walimu hawa hususan wanapotakiwa kufundisha wanafunzi 80 kwenye darasa moja.

Mimi nilikuwa home-schooled (almost kwa primary school) na nadharia zote za hisabati zilikuwa customized wakati wa kuzieleza kuendana na interests zangu na vitu ninavyovijua vyema, hivyo ilikuwa rahisi sana ku-relate na maisha ya kila siku. Na kuweza ku-relate na maisha ya kila siku, kulinifanya niwe na interest na hisabati.

Ninachotaka kusema ni kuwa, interest na uelewa wa mtoto kwa somo la hisabati unachangiwa na mambo mengi, ikiwemo walimu, vitabu na mazingira ambayo kimsingi kwa Tanzania katika yote hayo tumepwaya sana.

mkuu,
uko sahihi kabisa.
 
Literature isn't my strength. Hisabati ni somo ambalo mwanafunzi mwenye juhudi anaweza kujisomea mwenyewe. Lakini hutunzi wa vitabu vya hisabati Tanzania doesn't take advantage of our ability to think critically naturally.

Nilipokuwa Tanzania wanafunzi walikuwa wanalalamika kuwa equations zenye variables x, y, etc hazina maana katika maisha yao. Wanasoma kujibu mitihani ili waendelee mbele. Lakini wanashindwa ku-correlate wanachosoma na mazingira yao.

unaona kiongozi wangu, hesabu inapofanywa ni namba zisizo na maana zaidi ya formular na kukariri haziwezi kuwa msaada kwa wanaozitumia.
lazima lengo linalofanywa watu wafundishwe hesabu lijulikane na lile lengo likishaeleweka watumiaji wa masomo hayo wanaweza kuhama katika namba na kutumia mbinu hizo wanazozitumia katika namba kufanya mambo mengine.
cha msingi katika hesabu ni kule kutafakari na mbinu zitumikazo kutafuta majibu zikitumiwa vizuri na kuzama katika mtumiaji basi anaweza kutumia katika maisha yake ya kila siku.
 
nafikiri zaidi ya yote tuliyoyaonge masomo mengi yanavyofundishwa hapa kwetu ni kukopi na komeza na kutapika kwa ajili ya mitihani. hili ni kosa kubwa sana. ndio maana waajiri wanalalamika kuwa watu wanatoka chuoni hawana kitu si kweli hawana ila wameshasahau kutokana na usomaji wa kukariri akimaliza pepa usiku muulize chochote hana kashatema katika mtihani na kamalizana nalo. hapa mtu huyu hawezi kuwa mbinifu wala mtu wa kutafakari na kutumia ujuzi na uelewa wake katika maisha yake ya kila siku.
sasa tukibadili mfumo huu na kuwa na mfumo wa kuelewa na sio kuangalia A's basi taifa litabadilika.
 
Back
Top Bottom