Hii tabia ya maneno tata ya wasanii wa Singeli sio sawa

Kichangiri

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
331
670
Kumekuwa na tabia ya wasanii wa singeli kuimba kauli tata na watu kuchukulia poa.

Mfano unakuta mwanaume anaimba “mume wa mtu sumu ila kwangu mtamu” hivi hii iko sawa kweli?

Kwanini mamlaka husika wasikemee hili?
 
Hiyo ni sanaa mkuu. Wana uhuru wa kuimba, kufanya ni kitu tofauti.

Labda kuwekwe mfumo zisipigwe redioni muda fulani, au zikiuzwa ziwe na labels kuonesha zina maudhui ya kikubwa.
 
Nilikuwa nikifikiri jamii nyingine wanajali maadili kama jamii niliyotoka,unashangaa watoto hawana heshima Kwa wazazi wao na wazazi wao hata hawakemei kumbe ndiyo jamii Yao ilivyo. Hata mamlaka za nchi haziwezi kusimamia maadili Kwa sababu nao pia ni miingoni Kwa jamii.
 
Kumekuwa na tabia ya wasanii wa singeli kuimba kauli tata na watu kuchukulia poa.
Mfano unakuta mwanaume anaimba “mume wa mtu sumu ila kwangu mtamu” hivi hii iko sawa kweli?
Kwanini mamiaka husika wasikemee hili?
Hiyo ni sanaa, nisawa na Joti anavyo vaa wigs... kwani ndio analiwa..🤔
Labda tuseme tu kwaujumla kuna baadhi ya sanaa zipigwe marufuku kwaajili ya kunusuru new generations..
 
Nilikuwa nikifikiri jamii nyingine wanajali maadili kama jamii niliyotoka,unashangaa watoto hawana heshima Kwa wazazi wao na wazazi wao hata hawakemei kumbe ndiyo jamii Yao ilivyo. Hata mamlaka za nchi haziwezi kusimamia maadili Kwa sababu nao pia ni miingoni Kwa jamii.
Umetoka jamii ipi?
 
Kweli ndugu. Kuna sehemu unapita unakuta katoto kanafanya kitu unajiuliza hivi ingekuwa kwetu si angekuwa hospital sahivi😁
 
Kumekuwa na tabia ya wasanii wa singeli kuimba kauli tata na watu kuchukulia poa.

Mfano unakuta mwanaume anaimba “mume wa mtu sumu ila kwangu mtamu” hivi hii iko sawa kweli?

Kwanini mamlaka husika wasikemee hili?
Mkuu unataka wakaimbe kwaya?
 
kuna moja anasema "nakupenda wewe na huyo bwana wako"nilisikia mahali nilishanga sana
 
Kumekuwa na tabia ya wasanii wa singeli kuimba kauli tata na watu kuchukulia poa.

Mfano unakuta mwanaume anaimba “mume wa mtu sumu ila kwangu mtamu” hivi hii iko sawa kweli?

Kwanini mamlaka husika wasikemee hili?
Sasa wewe unalalamikia hilo? Sie wanyaji tunaikubali sana ile kauli ya Dulla Makabila ya Mchungaji kwenda motoni na mlevi kwenda peponi! Yaani inatupa amani sana tunapokuwa kwa "Mama Muuza"!
 
Hiyo haina tabu. Sio sawa na mtoto wa kiume kusifia kuwa mwanaume ni mtamu kwake
 
" nakupenda wewe na huyo bwana wako" Jamani huu si ushoga huu?
 
Aisee kuna nyimbo ukizisikiliza unabaki unatafakari kwa umakini

20230114_003317.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom