Producer Enrico

Feb 6, 2024
40
50
PRODUCER ENRICO KUTOKA STUDIO ZA SOUND CRAFTERS.
_____________________

👉🏿Anaitwa Enrico figueiredo almaarufu enrico wa sound crafter's huyu ni mtayarishaji Muziki ( producer) mkongwe wa zamani, ameanza muziki tokea miaka ya 1990s..

Jamvi la ukwaju wa kitambo limebahatika kukutana nae na kuzungumza nae haya na yale kuhusu Tasnia ya Muziki wa "Bongo Fleva"

Tathimini yake kuhusu Muziki kwa ujumla Tangu miaka hiyo ya nyuma wakati wao wakifanya Kazi ya utayarishaji Muziki ( producer)

Enrico:"
Studio ya sound crafters ilianzishwa na mdogo wangu anaitwa Jason Mwaka 1994 .mimi kipindi hicho nilikuwa busy sana na shughuli za Nyimbo za Band mbalimbali za Muziki jijini Dar es Salaam.

Maana ya Soundcrafters kwa kiswahili ni "wahunzi sauti" Baadae mimi mwaka 1997 nikaendelea nayo hadi leo

Mdogo wangu jason ndiye aliyefanya Kazi na. Crew za Muziki zilizofanya miaka hiyo ya 1990s

👉🏿 Hard blasters crew ( h.b.c)

👉🏿 Deplowmatz (D.p.t)

Ukwaju wa kitambo:
Kwenye upande wa utayarishaji producer Gani ambaye alikuwa anakupa changamoto hadi kukufanya uongeze juhudi katika utengezaji midundo katika studio yako.

( Ulikuwa ukisikia Kazi zake unasema na wewe utengeneze kilichobora kuliko yenye)

Enrico:

" Kwenye ushindani tulikuwa mimi
Mika mwamba
Master jay
P funk majani

Sema mimi nilikuwa nawashinda kwa kurekodi Nyimbo za bendi na taarab walikuwa hawana uwezo huo

Live Band zote nilikuwa nafanya mpaka mchiriku kaswida ngoma za asili nk.

Nilichukua tuzo zote za mtayarishaji Bora wa Nyimbo za taarab enzi hizo

Kiukweli Nilipata tuzo zenye pesa na trophy siyo sawa na sasa wanapata trophy Fedha hamna


Niliwahi kuchukua mara tatu mfululizo mwaka 2013/14/15
Baada ya Hapo Tuzo
zikasitishwa mpaka majuzi wameanza tena chini ya basata

Mfano Bendi za sikinde iliyochukua tuzo juzi niliirekodi mimi Nyimbo Hizo.

Studio za kwanza tanzania daresalaam

Tfc ya serikali (tanzania film company)
Radio tanzania (club raha leo zilikuwa xinarekodi bendi live kabisa ukikosea unarudia)

Ndiyo zikafuata hizi daresalaam za watu binafsi

Mhutto magomeni
Bonny Luv- Mawingu Studio.
Don bosco- marlon linje
Soundcrafters- enrico/biz/ mac 2 b
Amit Mento-
Agies Record
Miika Mwamba- Fm Studio
Roy Bukuku - G Records.
Akili The Brain- Akili Records
P. Funk Majani- Bongo Records
Master Jay- Mj Records
Joshua Kameta - Kameta Studio
Said Comorien- alan mapigo- Metro Studio

Lakini kuna maproducers walipita katika studio hizi katika vipindi tofauti kama Marijani,Prof. Ludigo, Castro Ponela, na John Mahundi. Pia kuna wanamuziki walijaribu kuproduce kwa kipindi flani kama Marehemu Complex,Bodea na Soggy Dog Hunter.

Ila kuna Kizazi cha mwisho cha maproducer kabla hawajawa wengi kama mchele na studio kuongezeka kama bar za Sinza.... Hawa ni kama
Marco Chali wa Kama kawa Records. Dunga, producer Jonas (ukisikiliza ngoma za wakali kwanza utamsikia anatajwa), Downtown Records, Pasu kwa Pasu Records, na Active Record ya Producers Shakii toka kenya.

Hizo zote ilikuwa kabla ya 2008... Enzi hizi kila msanii lazima uje Dar ufuate studio nzuri....labda uende Zanzibar kulikuwa na Jupiter Records na Chuchu na studio yake ya Heartbeats Records.

Baada ya hapo ndiyo hawa tunao sasa

Ukwaju wa kitambo:

Unaizungumziaje kauli ya mr nice Kuhusu malalamiko aliyoyatoa kwa serikali na mamlaka inayohusika na masuala ya sanaa kiujumla kuwa kwanini style yake ya "tekeu style" haikutumika kama kiwakilishi cha aina ya Muziki ambao unapatikana Tanzania

Enrico:
" Takeu style ingeweza kupaa wakati ule Endapo kama ingetumika kama kiwakilishi cha aina ya Muziki inayopatikana Tanzania.

Maana Mr nice alikuwa anajulikana sana Afrika ya mashabiki hasa kenya & Uganda kupitia hiyo style .. kafanya show nyingi sana
Serikali ilikuwa imelala kwa kipindi hicho cha nyuma ila kwa mtazamo wangu naona kabisa mpaka sasa bado wamelala

Mataifa kama vile Kenya na uganda walisongesha style ya "kapuka beat"

Style ambayo alikuwa anaitumia msanii jose chameleone kutoka Uganda.

Vile vile Kenya wanathamanisha sana miziki ya Nyumbani ( wasanii wa Ndani )
siyo sisi wa Tanzania.

Hata show zinazofanyika kenya support ni kubwa kwa wasanii wanaotumbuiza katika Event Hizo
Watu huenda show mara kwa mara
Tofauti sana hapa Tanzania mpaka zifanyike show za fiesta ndio mashabiki wajitokeze kwa wingi.

Ukwaju wa kitambo:

"Unadhani ni kitu Gani kifanyaje ili kujenga msingi Dhabiti & Imara ya kuwawezesha wasanii , producers na wadau mbalimbali wa muziki ambao juhudi zao ndio zimefanya Muziki Huu kuwa Hapa ulipo..

Ili wasiishi maisha ya tabu na shidah mtaani Baada ya kupumzika shughuli Hizo za sanaa Hapa kwetu Tanzania.
Maana tumejionea Baadhi ya wasanii & producers wakiishi maisha ya shida wakati Mchango wao ulikuwa mkubwa sana katika tasnia hii ya Burudani ..

Na Kazi zao kwa ujumla zinatambulika vyema Tanzania nzima.

Mfano geez mabovu ,langa kileo & ngwea hawakustahili kutangulia mbele za Haki huku wakiwa na maisha duni..

Hali hii inatia huruma sana"

Enrico:

"Tatizo wa Tanzania Tunathamini sana kumleta msanii wa nje kumlipa pesa kibao wakati wa hapa hawapati kile wanachostahili ..

Lakini kwa sasa imebadilika kwa hawa wasanii wa sasa

Inapindi Serikali waone hili mirabaha ifanye kazi

zilipwe radio tv mabaa mabasi stendi maduka n.k

Hela ipo

Kila duka litoe buku 2 mfano
Tanzania nzima
Itakuaje..

Ukwaju wa kitambo:

"Vip mlikwisha wahi kuwaomba wahusika hasa serikali kukaa na kujadili kuhusu kupitia Kazi za sanaaa za ndugu zetu waliotangulia mbele za Haki , ili ziendelee kuzalishwa na kupelekwa sokoni na Fedha inayopatikana iwe kama shukurani kwa familia za ndugu zetu hao..

kama ilivyo kwa mataifa ya ulaya mfano Marehemu 2 pac shakur & michael jacksone

familia zao zinaendelea kunemeka ingawa wao hawapo Tena Duniani.

Enrico.

"Siyo hapa ila inaongelewa
Na hao walioingia wakina naibu waziri kazi wanayo
Maana nae ni sehemu ya tasnia hii ya Burudani.

Ukwaju wa kitambo:

'Changamoto kwa wasanii wadogo kutokupewi kipaumbele katika vituo vikubwa vya 📻 tofauti na zamani chanzo ni nini?

Nakumbuka zamani tulibahatika kusikiliza Kazi za wasanii wote bila kujali kipato nk..

Enrico:

Cha kwanza nikueleze jambo moja kwa kifupi Serikali haishauriki
Lakini Radio ni rushwa tubu ndio iliyotawala kwa sasa.
Mifumo mizuri Iliharibiwa siku nyingi sana.
Kwenye mataifa ya nje hamna hii kitu kabisa.

Ingawa kwa Sasa wanasema mziki ni biashara
Wakipiga pesa kwanza ndio wanakutoa kwa hiyo toa pesa upate pesa.

Tuombee tu kuwa Mungu yetu macho.

Ukwaju wa kitambo:

Vip kwa mtazamo wako unadhani "ladha halisi" ya Muziki wetu ni ipi ..

Kama mfano muziki aina ya hip hop chimbuko lake ni nchini Marekani.

Vile vile Muziki aina ya r.n.b chimbuko lake ni uingereza ila Hiki tunachoikiita "bongo Fleva" tunakitofautisha vipi na ladha ya Muziki kutoka nje! Hata kama nikifika ulaya nikisikia inapingwa katika kituo cha radioni nasema Yes " Am from Tanzania" na kujivunia hii ni ladha au Fleva kutoka kwetu Tanzania

Enrico:

Kuna kitu kinabuniwa serikalini kupitia basata kuwa na sampo za kutengeneza miziki ya tanzania
Labda tutaenda huko kwingine
Kwa sasa ni taarab na singeli na mchiriku ndiyo zina tazamwa huko ulaya kama miziki yetu

Ukwaju wa kitambo:
Sawa nitafikisha ujumbe juu ya hilo vip kwa sasa bado unaendeleaa na shughuli za Muziki..

Kama ni ndio ni Kazi zipi umefanya kwa sasa..

Pia ulinijibu kuwa Gharama za kurekondi studio kwa kipindi hicho wasanii
Walitoa tsh. 20,000/=

Vip kwa upande wa mauzo ya Album mlipofikisha Kazi za wasanii sokoni.
maana kuna hii inshu ya wadosi vipi kwa upande wako na wasanii ambao ulifanikiwa kufanya nao Kazi kuna changamoto yoyote mlipitia Enzi Hizo kwenye inshu ya mauzo ya Album

Enrico:

Tulikuwa tunapewa oda na wadosi nilikuwa nalipwa changu kwanza kabla ya kufanya Kazi..
Malipo ambayo tunakuwa tumekwisha kubaliana kupitia mikataba baina yao na mimi..

Sikuwa nataka kufanya kazi ya kutojua malipo yake kwanza.

Mara nyingi nilikuwa nalipwa ndiyo nafanya kazi

Ukiachilia nilikuwa nawasaidia wengi free pia Wasanii wachanga

Ukwaju wa kitambo:

"Kwa upande wako ni msanii yupi ambaye amepita katika mikono yako hadi Leo unajivunia unasema Hapa "yes"

Msanii ambaye ulimuonyesha njia ( kwa kifupi kafika kwako ajui chochote kuhusu Muziki)

Ila ulimpa somo hadi Leo unajivunia kwa hilo.

Enrico:

Wapo wengi sana siwezi wamaliza
Wote, maana wasanii wa zamani Wengi walianzia hapa kwangu katika studio za sound crafters kisha wakaibiwa na record lebo zingine kama mj record & Bongo record.

Maana mimi ni sehemu ya wamiliki wa studio za mwanzo kabisa Hapa Bongo kwahiyo wasanii Asilimia kubwa walikuja "sound crafters" kurekondi Kazi zao.

🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥.

Eeeh hayo ni maneno ya producer kutoka studio za sound crafters "ENRICO" moja ya watayarishaji wakongwe Nchini Tanzania.

Vip kuhusu Mtazamo wake kuhusu Muziki wa Bongo Fleva..

"Kwamba Muziki wa sasa ni kama big g "

Maneno haya yanaukweli wowote...

Ebu #funguka..

😃😃😃😃😃😃😃😃

Kwa stori kali za kitambo na za kijanja karibu whatsApp.

Nicheki
📞+255767542202

UKWAJU WA KITAMBO
#tunakurudisha_kaleee!!!
 

Attachments

  • FB_IMG_1709975192088.jpg
    FB_IMG_1709975192088.jpg
    31.8 KB · Views: 6

Similar Discussions

Back
Top Bottom