wengi ni wa maneno tu humu,,, vitendo zeronaunga mkono 100%
wengi ni wa maneno tu humu,,, vitendo zero
Naunga mkono hoja ila wasiwasi wangu ni tatizo la uongozi kwenye chama chetu. Wengi wao wanaonekana wako kipesa zaidi.
wengi ni wa maneno tu humu,,, vitendo zero
Chadema sasa sio chama maskini. kama imeweza kushindana kigharama na CCM katika uchaguzi huu ina maana kuwa sasa chadema ina uwezo wa kuanzisha ofisi zake katika hatua za chini yaani huko vitongojini, vijijini na kuwaajiri wanachama wa kuzisimamia ofisi hizo ili zitoe huduma kwa wananchi, na pia kuandikisha na kuwafuatilia wanachama wake. Huku vijijini hatuna viongozi wa nyumba kumi wa Chadema. mashauri yetu yanasikilizwa na viongozi wa nyumba kumi wa CCM. Maisha ya kawaida tunazungukwa na CCM; CDM tunaiona huko kwenye gazi za taifa tu.
Wengi tunaiangalia chadema kutokana na matatizo ya kitaifa lakini haya ya huku vijijini kwetu tunajikuta hatuna namna bali kuwaangukia CCM watuhudumie maana chadema hatupo. Mfano uchaguzi wa serikali za mitaa. huku vijijini hatuna chadema, CCM wanapita bila kupingwa.
Chadema sasa tubadilike hizo hela za ruzuku tuzitumie kujenga chama ngazi za chini, tusisubiri upepo wa uchaguzi tu.
CCM inashinda tu kwa sababu ya mtaji wa wanachama waaminifu. na kiukweli wanao wengi sana, Sisi chadema hatuna wanachama bali tuna wapenzi; ambao kwa bahati mbaya sana wengi wao si wapiga kura.
CCM huwa wanafanya sensa ya wapiga kura wao kila ifikapo karibu na uchaguzi. kwa kutumia wale viongozi wao wa nyumba kumi hupita nyumba hadi nyumba. kwanza huuluza kama wanafamilia ni wana CCM then wanawauliza kazi zao za chama then, kadi zao za kupiga kura. Takwimu hizo zinawasaidia kujua kuza za uhakika hata kabla ya kampeni. Kipindi cha kampeni wanakitumia kijalizia tu hizo kura za wanachama wao
Sisi chadema hatuna takwimu kama hizo. tunategemea hotuba zetu za kampeni tu na ushawishi wa muda mfupi. Hii haitotusaidia kamwe.
CHADEMA needs big revolution on its management and organization system.