Kibona
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 1,023
- 652
Nafurahi kuwa watu wengi wana uchungu na nchi. Mawazo mengi ya wanachadema yanaonyesha tatizo kubwa ni vijana kutopiga kura na ufahamu mdogo wa watu vijijini. Tukumbuke kuwa ule utaratibu wa kuchangia kwa neno CHADEMA umeuwawa na ccm baada ya kuyatisha makampuni ya simu. Sasa wazo langu ni kuwa kwanza tutambue kuwa matatizo yaliyotuangusha igunga yapo kila jimbo, hivyo ili tukabiliane nayo tufanye operation kitaifa. Chadema iendelee na operation Sangara maana ilionesha mafanikio makubwa. Pili chama kianzishe program za kufungua ofisi za matawi vijijini; hii ni kazi kubwa na inahitaji pesa kwahiyo hapa wanachama tujifunge mkanda. Zifunguliwe accounts katika kila benki lakini zisimamiwe na Chadema makao makuu, halafu uwekwe utaratibu wa chama kutoa riport kila baada ya miezi mitatu ambazo zitawekwa ktk mitandao ya kijamii, na media zingine. Utaratibu huu unaonekana mgumu lakini unawezekana maana ndivyo walivyofanya wafuasi wa Obama; watu walikuwa wanachangia hata dola 5 lakini riporti zilikuwa zinaonesha kila hela iliyochangwa na projected budget. Ikifanyika hivyo basi CCM inaweza hata kujitoa 2015 kwa kuogopa aibu.