Hii ni kwa wana-CHADEMA tu

Nashukuru mpaka sasa post haijaingiliwa na 'kirusi' (mamluki)...
Naunga mkono hoja :jambo la msingi ni kuwashukuru waliopigia chama,kuendeleza elimu ya uraia na kufungua matawi zaidi hasa vijijini,...one thing for sure hata wenyewe wanatambua japo hawataki kukubali hadharani ccm inakoelekea cko.
 
Naunga mkono, lakin pamoja na kurudi kuwashukuru hao elf 22, uongozi wa chama pia uweke mikakati madhubuti ya kujiimalisha vijijini
 
Bonge ya idea ila 2washukulu sana wale wamama na wazee waliojitokeza kupigia cdm kura kusema ukweli vijana wanaiangusha cdm cku za kupiga kura mie kwa mtazamo wangu tuwaimize vijana kujiandikisha kadi za kupigia kura.
 
Elimu ya uraia ni muhimu sana sio kwa Igunga au Tabora tu bali kwa Tanzania nzima, hasa maeneo ya vijijini kwa ile mikoa ya pembezoni na iliyo nyuma kimaendeleo na kielimu.
 
Mimi ninatoka mkoa mmoja wa kusini ambao kwa ujumla hauna uelewa kabisa wa elimu ya uraia na nadhani huu moto wa mageuzi haujafikia wananchi wengi sana. So kwa mkakati ambao mtoa hoja ameuwasilisha hapa, nipo tayari kuhamasisha wananchi wa vijijini na pia naomba support ya viongozi wa chama kwenda kuwasha moto huko vijijini. CCM inakera jamani kushika nchi, tupambane kuitokomeza.
 
Kila mtu ajaribu kuwa balozi wa kusambaza elimu,, si kila kazi wafanye viongozi wa chama. Hawana uwezo wa kuwafikia wananch wote.
 
Mkuu umetoa wazo zuri. Kusema kweli kwa hizo kura walizopata CDM ni nyingi na inaonyesha jinsi kinavyokubalika. Ukizingatia kwamba mwaka 2010 CDM haikusimamisha mgombea lakini sasa imesimamisha na kupata kura zote hizo ni jambo zuri na linaonyesha jinsi CDM inavyokubalika. Pia uchaguzi huu umeonyesha kitu kimoja kwamba CDM imekubalika mijini sasa kazi iwe ni kujipenyeza kwa nguvu huko vijijini wakati huohuo ikiendelea kujitanua mijini. Pia CDM ijitahidi kujiepusha na vurugu kwa sababu watu wa vijijini wanaogopa sana mambo ya vuru. Uza sera na toa elimu ya uraia kwa hoja.
 
Jamani humu janmvini kuna watu ambao wako karibu na viongozi wa cdm. Kwa nini wazo hili lisifikishwa ili tuanze kufanyia kazi? Hatuwezi kukalia kubofya tu keyboard bila vitendo. Kwa vile wengi wetu hapa kazi yetu ni strategy zaidi kuliko operation ya, tunahitaji kusupport operation za chadema maana zinagharama kuliko hii kazi yetu ya kupanga strategy. Naamini tunaweza kufanya kitu na hata vizazi vyetu waje kujivunia mchango wetu wa kuleta mabadiliko haya muhimu. Kwa wapenzi wachadema walivyowengi hata tukichangia kidogokidogo itatosha kuendesha operation ya elimu huko vijijini.

Tunataka ile namba ya kutuma neno 'CHADEMA' iwekwe hapa na kiongozi wa chadema watu tuanze kuchangia na tuwe tunatumiwa msg ya kutukumbusha kutoa kila mwisho wa mwezi. Maana watakuwa na database ya namba zote zilizowahi kuchangia.

Pia tuwe tunahamasisha hata vijana wenzetu ambao hawako JF waweze kujiunga hapa ili waweze kupata mwamko wakuchangia.
 
Naunga mkono hoja ila wasiwasi wangu ni tatizo la uongozi kwenye chama chetu. Wengi wao wanaonekana wako kipesa zaidi.
 
Chadema sasa sio chama maskini. kama imeweza kushindana kigharama na CCM katika uchaguzi huu ina maana kuwa sasa chadema ina uwezo wa kuanzisha ofisi zake katika hatua za chini yaani huko vitongojini, vijijini na kuwaajiri wanachama wa kuzisimamia ofisi hizo ili zitoe huduma kwa wananchi, na pia kuandikisha na kuwafuatilia wanachama wake. Huku vijijini hatuna viongozi wa nyumba kumi wa Chadema. mashauri yetu yanasikilizwa na viongozi wa nyumba kumi wa CCM. Maisha ya kawaida tunazungukwa na CCM; CDM tunaiona huko kwenye gazi za taifa tu.

Wengi tunaiangalia chadema kutokana na matatizo ya kitaifa lakini haya ya huku vijijini kwetu tunajikuta hatuna namna bali kuwaangukia CCM watuhudumie maana chadema hatupo. Mfano uchaguzi wa serikali za mitaa. huku vijijini hatuna chadema, CCM wanapita bila kupingwa.

Chadema sasa tubadilike hizo hela za ruzuku tuzitumie kujenga chama ngazi za chini, tusisubiri upepo wa uchaguzi tu.

CCM inashinda tu kwa sababu ya mtaji wa wanachama waaminifu. na kiukweli wanao wengi sana, Sisi chadema hatuna wanachama bali tuna wapenzi; ambao kwa bahati mbaya sana wengi wao si wapiga kura.

CCM huwa wanafanya sensa ya wapiga kura wao kila ifikapo karibu na uchaguzi. kwa kutumia wale viongozi wao wa nyumba kumi hupita nyumba hadi nyumba. kwanza huuluza kama wanafamilia ni wana CCM then wanawauliza kazi zao za chama then, kadi zao za kupiga kura. Takwimu hizo zinawasaidia kujua kuza za uhakika hata kabla ya kampeni. Kipindi cha kampeni wanakitumia kijalizia tu hizo kura za wanachama wao

Sisi chadema hatuna takwimu kama hizo. tunategemea hotuba zetu za kampeni tu na ushawishi wa muda mfupi. Hii haitotusaidia kamwe.

CHADEMA needs big revolution on its management and organization system.
 
Wazo zuri, CDM haitakiwi kukata tamaa, ni kupanga mikakati zaidi ya kusonga mbele. Mungu ibariki CHADEMA, mungu ibariki Tanzania
 
ucjali mkuu...tactic za ccm muda unavyozidi kwnda ndivyo wanavyozidi kuproof failure...ndio maana maujanja(hila) ni mengi...mi nadhani trend ya cdm ni nzuri tu ukilinganisha na watawala(sipendi kuwaita viongozi) wetu
 
Mawazo mazuri sana,natamani sana tuunganishe nguvu pamoja kimtandao.

Napendekeza tujigawe humu jamvini kimikoa. Tuweze kukutana tupange mikakati ya namna gani kutowapoteza wale waliotusuport na tufanyenini kwa wale ambao bado hawajaikubali Chadema.

Majukumu haya ni makubwa tusiwaachie viongozi peke yao.

Mimi niko tayari kwa mtu mwenye idea nzuri tuanzaje jambo hili.
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom