Hii ni kwa wana-CHADEMA tu

Account za cdm kulingana na tovuti yake: www.chadema.or.tz
NBC Corporate Branch (Local currency) 011103010075
NBC Samora Branch (Foreign currency) 012105019310
Pia kuna ile ya kutuma neno CHADEMA kwenda 15710 ambayo ni Ths 350/= kwa sms.
Nashauri CDM ifungue pia account katika NMB na CRDB kwani hizo ndio benki wanazomudu walalahoi.

Asante mkuu. Lakini ni muhimu tujuwe kuwa Majamba wananufaika mno na katiba mbovu tuliyonayo. Ni jukumu letu kudai kuandikwa kwa katiba mpya ambayo italeta Tume Huru ya Uchaguzi, Mahakama huru, Bunge huru na uhuru wa vyombo vya habari.
 
asante mkuu. Lakini ni muhimu tujuwe kuwa majamba wananufaika mno na katiba mbovu tuliyonayo. Ni jukumu letu kudai kuandikwa kwa katiba mpya ambayo italeta tume huru ya uchaguzi, mahakama huru, bunge huru na uhuru wa vyombo vya habari.

ndugu yangu hapo ndipo cdm hawawezi sijui kuna agenda gani? Kwanini kama wanaogopa wapishe watu wenye confidence zao nashangaa tundu lissu kabla ya kuwa mbunge tuliishaongea sana hilo lakini sasa kimyaaa! Kama hamtaweza hilo jiandaeni kuwa ccm c
 
Asante dada yangu, wazo zuri na muda wa utekelezaji pia ni muafaka. Ukombozi wa Tz utaletwa na wanachi wake na CDM kina ridhaa ya umma kufikisha.

Upo uzi mwingine pia wenye mawazo yakufanana so tuchangie na kufanikisha. nihesabu mimi miongoni mwa wachangiaji wa mwanzo na wwa kudumu ktk hili.

Hongera
 
Mama kubwa hiyo inaweza kuwa moja ya mikakati mnayoweza kuitumia kuongeza uungwaji mkono wa chama chenu na inaweza kuwasaidia KIDOGO kwenye uchaguzi ujao. Inabidi muelekeze nguvu zenu kwenye kudai katiba mpya itakayoandaa mazingira yanayotoa fursa sawa kwa vyama vyote. Kwa sasa hamuwezi kuishinda CCM ambayo inatumia dola kubaki madarakani.

CCM wana tume ya uchaguzi, wana wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wakurugenzi wa halmashauri za miji na wako chini ya ofisi ya waziri mkuu, wana polisi, wana usalama wa taifa, na wana uhakika wa kuwatumia mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ambao wote ni makada wa CCM lakini wanagharimiwa na serikali kuwakampenia CCM. kumkukeni kuwa wakuu wa mikoa na wilaya, ambao ni makada wa CCM, ndio wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama wa maeneo yao. Kwa kutumia kofia hiyo wanaweza kabisa kutoa maelekezo kwa maofisa wa polisi, usalama wa taifa na jeshi kuhusu kuwasaidia kweye uchaguzi.

Mfumo wa sasa wa kikatiba na kisheria uliandaliwa na Hayati Nyerere kuhakikisha kuwa CCM Inatawala milele. Msipofanikiwa kuubadilisha mfumo huo ili kuwapa fursa sawa na CCM, kamwe hamuwezi kushinda uchaguzi nchi hii. Mtapata majimbo machache ambayo wananchi wake wameamka kisiasa na wanauwezo wa kudai na kusimamia haki zao. Huku kwingine mtaishia kuyasikia kwenye redio tu.

Rafiki, u r very right. Elimu ya uraia kila pembe ya nchi iende sambamba na mafunuo ya katiba ilivyo haramu.
Madai ya katiba mpya yafike mpaka vijijini. Haya ni mapambano makubwa kuliko yale ya mwanzo ya kudai uhuru toka kwa wazungu pekee, sasa hivi ni dhidi ya ndugu zetu wakishrikiana na wazungu!


Ushindi ni lazima na saa ya ukombozi ni sasa.
 
Back
Top Bottom