p_prezdaa
JF-Expert Member
- Apr 25, 2011
- 432
- 60
Jaman nina mpenzi wangu ambaye tunaishi mbali naye me niko mkoa mwingine na yeye mkoa mwingine tuliachana miaka minne iliyopta baada ya kucheza mechi za utotoni bila kujari kinga na kumasababishia ujauzito, uliperekea ajifungue mtoto wa kiume, Mwanzo alikuwa ataki hata kunisikia lakini jinsi siku zilivyoluwa zikienda akawa anapunguza ukali atimaye akanisamehe kwa yote na kukubali kuwa nami tena, Tatizo ni kwamba kama wiki mbili hivi zilizopita alikuwa akinibeep sana siku hiyo, lakini baadae nilipompigia akawa anakata simu, na baadae akanitumia sms kuwa anitaki na kunitukana japo sio matusi ya nguoni ila yalikuwa na kunikejeri, mpaka usiku akawa anaitumia sms za kunisisitiza kuwa anitaki tena, nami kwa upole nikaamua kuacha kumbembeleza na kukaa kimya. Asubuhi ilipofika akanipigia simu kama mara tatu sikupokea lakini, Baadae nikaamua kupokea baada ya kuona anapiga sana simu nilipopokea simu ikawa tofauti akawa anaongea kama awali tulivyokuwa na kuapiza kuwa ayuo tayari kunikosa kwa khali yoyote ile. Je ni Kweli huyu mtu ananipenda au ndo anataka niumiza mana mwenyewe nimemuuliza anasema alikuwa anajiraribu aone nitachukua aumuzi gani. Sasa hivi namuogopa sana mana anaweza nisababishia maumivu makali sana ya Moyo, je nifanyeje wadau I'm in hard time.........