Tuoe wanawake wasio na tamaa wapo

iamriq_arthur

JF-Expert Member
May 1, 2021
377
884
Ni muda sasa sjahudhuria humu jamvini, leo nina habari ya kuwakumbusha vidume wenzangu.

Juzi Bimkubwa amenipa card yake ya Bank nikamtolee kiasi cha pesa.

Nimefika nikamkuta wakala mdada akanikaribisha vizuri kabisa, nilikuwa natoa Tsh laki tisa nilipomaliza sms haikurudi kumbe mtandao ulikuwa unasumbua, ikabidi niondoke nirudi mpaka home...

...nikamuelekeza bimkubwa kuwa mtandao unasumbua, akaniambia "vuta muda kidogo alafu nenda tena mana hiyo pesa ni ya muhimu inahitajika leo

Kweli bana muda ulipopita kidogo nikatoka tena mpaka kwa wakala ila nilipoenda sasa ni kwa wakala mwingine sio yule dada wa mwanzo.

Nilivyofika nikatoa pesa ikakubali, nikamrudishia mama pesa vake.

Sasa jana napita zangu road nasikia mtu amekazana kunita "we mkaka we mkaka" nikajisemea moyoni
"naitwa mimi au mtu mwingine?" Nageuka akaninyooshea mkono "yes wewe njoo" nikasema
...ohoo jina limetoka nini?.

Nafika pale ananiambia "we sindo mkaka ulie kuja kutoa pesa jana" nikamjibu "ndio kunatatizo?" akajibu
"hapana angalia salio kwenye account yako"

Ikabidi nimcheki bimkubwa aangalie salio kwenye account yake ya Bank.

Baada ya kuangalia ase akawa amepiga simu akiwa anahema namuuliza vipi ananambia account yake inasoma elfu kumi na tatu wakati jana mpaka mida ananipa nikamtolee pesa ilikuwa na Milioni mbili kasoro na nilikuwa nimetoa laki tisa tu!.

Sasa hapo karoho kakaanza kudunda...

...ikabidi nimjibu yule dada wakala sasa.

Akatabasamu kisha akasema "jana ulipojaribu kutoa ile pesa sms haikurudi mtandao ulikuwa unasumbua lakini ile pesa badae ilitoka ikanifikia" nilichoka nikaishiwa nguvu kabisa.

Basi akachukua ile pesa akanipatia nikaona aibu ...nikamuachia elfu tano ya vocha aise alikuwa muaminifu asiye na mfano kwa hali yenyewe ya sasa angekuwa mtu mwingine ilikuwa imetoka hiyo na nisingetambua pesa ilipotea vipi.

(Hawa ndio wanawake wa kuoa sasa ukimuachia pesa ya matumizi pale nyumbani pesa ikibaki..)
 
Someni vzuri bango ina sasa Bi mkubwa kupitia kadi yake pesa imetoka mara X 2? Yaani 1.8 million??
 
Usubir nn muoe au ndiyo mambo yako ya Miso misondo unatuletea hapa
Sisi tuoe moto ukituwakia uanze kutucheka?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom