Heche na Nape katika kipindi cha medani za siasa na uchumi cha star tv

heche swali ni nani anstahili anapaswa kulipa kodi
Heche anaanza kwa kusema patriotism inaanza kufa pale mtu amelipa kodi na huduma za kijamii hazifanyiwi kazi ''ufisadi'' kamtaja Jeeatu Patel na kusema watu wakifanyiwa mema watu wa watalipa kodi na ni jukumu la kila mtu kulipa kodi
Pia anasemea misaha mikubwa ya kodi ktk makampuni ya dhahabu ni hasara kwa serikali, hawanunui chochote hapa ndani
 
Nilikuwa sijawahi kumuona huyu Heche, kumbe ni pumba hivi eti anaongelea uchumi hana lolote ananyoosha mikono hovyo na magwanda yake
 
Ndo kipindi kimeanza hoja ndo zinaumia make uchambuzi ni mkali,Heche anamwambia Nape kabla hajawa hapa alipo vijana walimpenda sana lakini sahvi wanamchukia
 
Mods kama mada yangu iko tayari pengine naomba uipeleke kuunganisha. Nape anatetea kuwa watu walipe kodi ndo watapata maendeleo,misamaha ya kodi /grace period kwa wageni inazungumzika. Heche anasema Nape amebadilika hamtetei mnyonge baada ya kupata cheo. Wanaendelea na mjadala.
 
Nape bwana, eti wakolon hawakuacha barabara za lami, wao wamejenga lami, kwa hiyo uchumi umekua. Hapa nadhani haelewi tatizo la msingi
 
Mods kama mada yangu iko tayari pengine naomba uipeleke kuunganisha. Nape anatetea kuwa watu walipe kodi ndo watapata maendeleo,misamaha ya kodi /grace period kwa wageni inazungumzika. Heche anasema Nape amebadilika hamtetei mnyonge baada ya kupata cheo. Wanaendelea na mjadala.

nape anasema uchumi umekua wakoloni awajaacha lami,ivo kwa sasa afadhali. Anatoa mfano kuwa unaweza kutoa bidhaa delicate toka dsm kwenda tarime kwa barabara ikiwa salama. Katoa mfano tv. Kwa ujumla mada haivutii!
 
nape kaulizwa je tumbane mgeni zaidi kuliko mzawa? Jibu kila mtu alipe kodi na suala la misamaha ya kodi kwa makampuni ya dhahabu na grace period kwa makampuni ya kigeni anajitetea ansema Nape ni yule yule wa Masasi hajabadalika na bado anapiga vita ufisadi na anauchukuia
uchumi unakua mf. Wakoloni hawakuacha lami sasa kuna km nyingi za lami, unaepusha gharama nyingi sana ktk uchumi ila changamoto ni speed ya kuleta maendeleo ndo maana kuna mpango wa 2025. So uchumi sio static.
 
nape kwa miezi 8 Masasi kulikuwa na ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho ameacha 5 vinajengwa, anajisfia kuongeza mapato ya Masasi. Tatizo watu wanakwepa kodi. Na yeye alidhibiti ukwepaji kodi wa korosho Masasi. Na yeye alitia watu ndani kwa kutopalilia korosho, ansema hiyo ni mifani michache ya utendaji kazi ila watu nao wafanye bidii. Anasema vitambulisho vya utaifa ni suluhisho kwa wakwepa kodi mfano kenya

Haaa ahaa kumbe Nape anajinadi yeye siyo CCM?! Naona hizo ni sera za binafsi anaongelea labda chama hakina sera
 
Heche kaponda kukua kwa uchumi kuwa haundeni na 50yrs za ccm,karudia mfano wa mch.msigwa kuwa Tz ni sawa na mtoto wa miaka 15 ila anacheza mchezo wa mtoto wa miaka 2,hatuwezi kumsifia.
 
Waungwana fuatilia hoja, Nape na Heche wanatoa hoja zao Star Tv sasa hivi.... Nape anasema ni yuleyule (wa enzi zile za kupinga kuuzwa jengo la UVCCM) na kwa mba hajabadilika, nahisi ameona watu wanamnshangaa kama Nape wa sasa hivi ni yuleyule au kabadilika!

Heche anasema viongozi wa CCM wananwakejeli wananchi masikini, huku wakijisifu kuwa uchumi unakua kwa kasi, anasema jujuzi spika amewatukana watu wa kariakoo... alipowataka wabunge wasijilinganishe na watu wa kariakoo... anajiuliza 'sijui watu wa kariakoo wakoje?' labda wanakejeliwa kwa sababu ya umasikini wao? wakiwezeshwa uchumi wao ukakua hawataweza kukejeliwa hivi..
 
Heche: kuna vitu vimefanyika ila huwezi kulinganisha na muda 50 yrs rasilimali zilizotumika na muda haziendani na muda na gharama matatizo ni kama mgawo wa umeme tatizo ni muda na maendeleo. Anauliza je hizo lami ni za aina na ubora gani? hivi ndi vitu vinavyoudhi wananchi pamoja ubadhirifu ktk serikali. Hili la mpango ni kauli mbiu tu kama zingine za kilimo. Tatizo la posho la wabunge anasema souce ni gap kati ya walio nacho na wasio nacho
 
Nilikuwa sijawahi kumuona huyu Heche, kumbe ni pumba hivi eti anaongelea uchumi hana lolote ananyoosha mikono hovyo na magwanda yake
Heche anaongea mambo ya msingi sana, hizi zako ndio pumba
 
Nape: Anazungumza sana statistics za kwenye makaratasi and is very good at it

Heche: Anazungumzia Uhalisia wa Mtanzania wa Kwawaida and is very good at
 
Back
Top Bottom