Heche na Nape katika kipindi cha medani za siasa na uchumi cha star tv

Huyu Nape mpuuzi sana. Hatuongelei Tanganyika/Tanzania ya sasa na ya mkoloni. Tunaongea utendaji wa walio madarakani in relation to the progress on the ground. Malaysia na Singapore tumepata Uhuru around the same time, Nape anaweza kulinganisha maendeleo ya Tanzania na Malaysia leo hii? Na akumbuke Malaysia hawana hata nusu ya rasilimali zilizopo Tanzania. Hizo barabara za lami anazoongelea ni zipi? mashimo kila kona. 2015 is too far, we need to get rid of these moroons!
 
Nape na Kasumba ile ile ya Kum attack Dr. Slaa Personally ( Dr. Slaa ameleta Damage kubwa sana CCM)
 
Nape: anaulizwa kuhusu vipaumbele vya taifa. Anajibu: bajeti imegawanywa kwa uzito wake. Tz tuna awanu nne za uongozi, vipaumbele vya awamu ya kwanza si vya leo. Anasema yeye hana tatizo na vipaumbele,yeye anadai ubadhirifu ndo mkubwa. Halmashauri zinapata hati chafu. Kasema pia madiwani wetu wana uwezo mdogo,katoa mfano halmashauri ya singida,mambo anayaongoza mkurugenzi badala ya madiwani. Anadai wakati mwingne wananchi wanaburuza,hawasikilizwi.
 
swali je serikali halina vipaumbele vinavyoleweka? Vipaumbele vigawanywe kwa uzito. Ndo maana ktk kila awamu kulikuwa na kitu kilichoendelea zaidi, yeye hana shida na vipaumbele bali tatizo ni rasilimali na wizi ktk mashirika ya umma na halmashauri wakati kamati za bunge hizi ziko kwa wapinzani na mbona ndio zina malalamiko kasema bora hata mrema slaa alshindwa kabisa. Kasema pia uelewa wa madiwani ni tatizo wengine wamemwachia halmashauri mkurugenzi. Pia anaelezea wizi ktk ujenzi wa miradi ya halmashauri na hayo ndo matatizo ya vipaumbele vinavyoanzia
 
Nape na Kasumba ile ile ya Kum attack Dr. Slaa Personally ( Dr. Slaa ameleta Damage kubwa sana CCM)
namuona anavyojikanyaga, kamsifia Mrema, alafu hapo hapo anatuambia kwamba, anapiga mikwara ya kwenda polisi. Nani anayehitaji mikwara? Inawezekana naye alikuwa anapiga mikwara habari ya mapacha watatu.
 
Heche anasema mawaziri wanaungana na wezi kuiba. Nape anasema kuwa mbona kuna mawaziri wamepelekwa mahakamani tayari?
 
Nape anarusha mpira kwa kamati za hesabu za serikali ambazo zimekuwa zikiongozwa na wapinzani, anawataja Cheyo, Slaha, Zito na sasa Mrema... kwamba huko ndiko wamekuwa wakiona madudu lakini hakuna nafuu licha ya kuyaonesha...

Heche anajibu.. serikali na CCM wametengeneza mazingira fulani ya kulinda wezi na kwamba ndiyo maana kelele za kamati hizo hazijazaa matunda. anaongeza kwamba almost kila mtu ni mwizi kwenye serikali kibaya zaidi hasa wale wanaopaswa kuchukua hatua, kuanzia waziri mkuu, waziri, wakurugenzi... sasa hapo hunategemea wenyeviti wa kamati wafanye nini, kama wanatoa recomendation kwa hao hao wezi
 
Nape kamati zinazoongozwa na upinzi maeneo yao kumekuwa na ubadhilifu mkubwa. Huyu kweli kilaza
 
ktk suala la wizi ktk mashirika ya umma na halmashauri heche anasema tatizo ni jinsi ya kuwawajibisha hao watendaji wabovu mf madiwani hawawezi kumtoa hata afsa kilimo mapendekezo ya hizo kamati hazifanyiwi kazi
 
Hii Kauli anayoitumia sana Nape kwamba"HILI LINAZUNGUMZIKA"linaniudhi sana huku nikukosa msimamo na kauli ya woga kabisa.
 
Heche anasema madiwani wasibezwe,wanafanya kazi ila ma Dc ndo wanaharibu. Katoa mfano gari ya halmashauri ya Tarime iligongwa ikagotengenezwa kwa sh.25 milioni. Madiwani wakapiga kelele hawakusikilizwa,sasa diwani afanyeje?
 
Nape bana kila jambo LINAZUNGUMZIKA itabidi tuanze kumuita Mzee wa LINAZUNGUMZIKA
 
Back
Top Bottom